data:post.body UFAHAMU UGONJWA WA NYAMA ZA MACHO NA MATIBABU YAKE.(PTERYGIUM) ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

UFAHAMU UGONJWA WA NYAMA ZA MACHO NA MATIBABU YAKE.(PTERYGIUM)

Ptyerigium ni nini?
Huu ni ugonjwa wa macho ambao huja kwa kuota kwa nyama eneo la mbele kabisa la jicho kitaalamu kama conjuctiva, nyama hiyo huota kuelekea katikati ya jicho ambapo kuna sehemu nyeusi ya jicho kwa jina la pupil.
                                                   
Hali hii huweza kumuogopesha mgonjwa na kufikiri kwamba ameugua saratani lakini ile sio saratani, katika hali isiyokua ya kawaida, uvimbe ule ukiwa mkubwa sana huweza kupunguza uwezo wa jicho kuona vizuri.
ugonjwa huu unaweza kuathiri jicho moja au yote mawili kwa mpigo, japokua huu sio ugonjwa hatari sana lakini unaweza kukuletea usumbufu wa kuona vizuri na muonekano wako usiwe mzuri.

nini chanzo cha tatizo hili?
 • kupigwa na jua muda mrefu
 • macho makavu
 • vumbi na upepo machoni.
dalili zake ni zipi?
 • hisia za kitu machoni
 • macho kuwasha
 • macho mekundu
 • kushindwa kuona vizuri
 • macho kuwasha.

matibabu yake ni yapi?
ukiwa na tatizo hili hauhitaji matibabu yeyote, lakini unaweza kupewa dawa za kuweka matone jichoni kupunguza usumbufu wa dalili.
lakini nyama zikiwa kubwa sana kuanza kuzuia kuona basi utafanyiwa upasuaji mdogo kuziondoa.

jinsi ya kuzuia ugonjwa huu
hakikisha unavaa miwani za kujizuia na mwanga mkali wa jua mara kwa mara.                                                                   STAY ALIVE
                                           DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                         0769846183/0653095635

Maoni 7 :

 1. Habari gani kiupele kinachoota nje ya ukuta wa jicho namaanisha kwenye mzunguko wa nje ya mboni

  JibuFuta
 2. Asante kwasomo

  JibuFuta
 3. Asante Kwa ufafanuzi doctor

  JibuFuta
 4. Unapatikana wapi? Nina shida hiyo pia kama dawa ni shilingi ngapi?

  JibuFuta
 5. Elimu nzuri nimependa

  JibuFuta
 6. Kwa kweli umenitoa hofu snaa kwa hili ahsnate doctor

  JibuFuta
 7. Asante sana ume nitoa shake na hofu 🙏

  JibuFuta