data:post.body UFAHAMU UGONJWA WA AKILI NA MATIBABU YAKE.(SCHIZOPHRENIA) ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

UFAHAMU UGONJWA WA AKILI NA MATIBABU YAKE.(SCHIZOPHRENIA)

schizophrenia ni nini?
Huu ni ugonjwa mbaya sana wa akili ambao huharibu au kubadilisha mfumo wa kuwaza, kutafsiri mambo, hisia na tabia ya mtu.
Ni ugonjwa ambao umeathiri zaidi ya watu milion 21 dunia nzima, ugonjwa huu huathiri uwezo wa kiuchumi na kielemu wa watu wengi sana.
Watu wenye ugonjwa huu wa akili huweza kufa mapema sana kuliko watu wengine kutokana na magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kuzuilika kama moyo, kisukari na kadhalika.
Ubaguzi, kutengwa na talaka kwa wagonjwa ni mkubwa sana dunia nzima hasa nchi zinazoendelea kama afrika.

chanzo cha ugonjwa huu ni nini?
Tafiti hazijaweza kugundua chanzo halisi cha ugonjwa huu, lakini muingiliano kati ya vinasasaba au gene na mazingira tunayoishi unaweza ndio kua chanzo cha ugonjwa huu.
watu ambao wako kwenye hatari kubwa ya kuugua ugonjwa huu ni watu ambao wana ndugu wagonjwa, msongo mkubwa wa mawazo hasa watu wanaoishi mjini, matatizo ya ubongo yakuzaliwa nayo au ya kuugua ukubwani.


dalili za ugonjwa huu ni kama ifuatavyo.

 • Kuona na kusikia vitu ambavyo wenzako hawavioni wala kusikia.
 • Kuamini vitu ambavyo havipo mfano mgonjwa anaweza kuamini kwamba yeye ni raisi wa nchi, hana kiungo fulani, anapendwa sana, anasalitiwa na mpenzi wake au kuna watu wanataka kumuua.
 • Tabia ambazo sio za kawaida kama kutembea tembea hovyo, kucheka bila sababu, kua mchafu mchafu na kuwa tofauti na siku zote.
 • Kuongea vitu ambavyo havipo au haviendani na maada husika.
 • Tofauti ya hisia na muonekano yaani mgonjwa anaweza kucheka wakati ana huzuni.
 • Kujitenga na watu.
 • Kukaa kimya muda mrefu na kukaa sehemu moja.
vipimo gani hufanyika?
hakuna kipimo cha moja kwa moja ambacho kinaweza kugundua ugonjwa huu lakini baadhi ya vipimo hufanyika ili kujiridhisha kwamba hakuna ugonjwa mwingine umeingilia, mfano
 • kipimo cha malaria
 • kipimo cha ukimwi
 • kipimo cha kaswende
 • wingi wa damu
 • mkojo
 • choo
 • kipimo cha uwezo wa ubongo i.e EEG
MATIBABU
Hakuna dawa za moja kwa moja za kumaliza ugonjwa huu lakini zipo dawa ambazo mtu anatakiwa atumie ili aweze kuishi maisha  ya kawaida kama watu wengine.
dawa hizo ni kama haloperidol, chlorpromazine, olanzapine, respiredone, na clozapine.
dawa hizi hutolewa kulingana na hali ya mgonjwa na zinatakiwa zitumike maisha yake yote na kwa wagonjwa ambao wanashindwa kuvumilia dawa za kumeza basi zipi sindano za kuchoma mara moja kwa mwezi kwa jina la fluphenazine.
matibabu mengine ambayo sio ya dawa yanahusiana na kumsaidia mgonjwa kutumia dawa, kumpa ushirikiano, ushauri na kumsaidia mahitaji yake.
wagonjwa wengi hufa mapema kwa kukosa ushirikiano na kutengwa na ndugu.
Nchi ambazo hazijaendelea wagonjwa hawa hawapati matibabu kabisa hivyo kuishi katika hali mbaya zaidi.
Usihangaike na waganga wa kienyeji, hakuna dawa ya kutibu kabisa tatizo hili, ila zipo dawa za kutuliza.

                                                              STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                 0769846183/0653095635
         

0 maoni:

Chapisha Maoni