data:post.body FAHAMU TATIZO LA MSONGO WA MAWAZO NA MATIBABU YAKE. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

FAHAMU TATIZO LA MSONGO WA MAWAZO NA MATIBABU YAKE.

Msongo wa mawazo ni tatizo kubwa na linalokua sana hasa kwenye dunia ya sasa hivi, waathirika wengi wakiwa vijana na watu wazima  kutokana na tatizo kubwa la ajira, matatizo ya mahusiano, kufiwa  na wapendwa na matatizo mbalimbali ya kimaisha ambayo yako nje ya uwezo wao.
wanawake hua wanakua na msongo wa mawazo sana kuliko wanaume.
                                                                   
Tafiti zinaonyesha kwamba zaidi ya watu milioni mia tatu duniani wana msongo mkubwa mkubwa wa mawazo na baadhi yao huhitaji matibabu na kulazwa kabisa.
Msongo wa mawazo huchangia sana watu kujiua, zaidi ya watu laki nane hujiua kila mwaka kutokana na tatizo la msongo wa mawazo.
Bahati mbaya sio tatizo la kipaumbele kwa nchi za kiafrika kwani sisi waafrika mara nyingi tunapambana na magonjwa ambayo yanaonekana sio ya kisaikolojia.
Msongo wa mawazo huja na dalili mbalimbali na zifuatazo ni dalili kuu ambazo huonekana kwa mgonjwa wa tatizo hilo.
kukosa hamu ya kufanya chochote;  mtu mwenye msongo wa mawazo anakua hatamani kufanya chochote, hata kama kitu hicho kinafurahisha watu wengine yeye anakua hawezi kukifurahia, unaweza kuliona hilo kwa kumuangalia tu bila kumuuliza chochote.
kutokua na furaha muda wote; mtu kama huyu anakua hana furaha, muda mwingi anakua na huzuni na kulia mara kwa mara na kukosa matumaini kabisa ya maisha, hii humfanya mtu ashindwe kufanya shughuli yeyote ya kimaendeleo au kikazi.
mabadiliko ya uzito; kupungua uzito mwingi sana bila kufanya diet au mazoezi yeyote ni dalili ya msongo wa mawazo sababu ya kushindwa kula lakini pia baadhi ya watu huongezeka uzito kipindi hiki kwani msongo wao wa mawazo huwafanya wale chakula kingi ili wajisikie afadhali.
kukosa usingizi; watu wenye msongo wa mawazo hua hawapati usingizi kabisa, anaweza kukaa kitandani masaa mengi sana bila usingizi na akaja kupata usingizi kukiwa kunakaribia asubuhi, hichi ni kitu amabacho kinaweza kumfanya mtu ashindwe kufanya shughuli zake za kila siku.
mawazo ya kujiua; wagonjwa wengi wenye msongo wa mawazo hua wanajiona hawana thamani ya kuishi, hivyo kichwani mwao wanakua na mawazo ya kujiua japokua wanaweza kushindwa kutekeleza mipango yao lakini mawazo hayo yapo na ikitokea mawazo hayo yakaendelea muda mrefu mtu anaweza akaamua kujiua.
uchovu na kuishiwa nguvu; mtu mwenye msongo wa mawazo anakua anaishiwa nguvu za kufanya kazi, anaweza kushindwa hata kunyenyua kitu ambacho ana uwezo wa kukibeba kila siku.
kushindwa kufikiri vizuri; mtu mwenye msongo wa mawazo hawezi kufanya kazi yeyote inayohitaji akili sana kufanya kazi, kwani uwezo wake wa kufikiri unakua chini sana.
kujihisi hana thamani; watu wenye msongo wa mawazo hujihisi hawana thamani kabisa na wakati mwingine husikia sauti ambazo zinamwambia kwamba yeye hana thamani na ni bora ajiue tu kwani kuwepo duniani ni kikwazo kikubwa.
kufanya mambo taratibu; mtu mwenye msongo wa mawazo hawezi kufanya kazi kwa haraka kama watu wa kawaida, anaweza akakaa sehemu moja na kujisahau kwa muda mrefu sana.
mara nyingi hufanya shughuli zake kama mtu ambaye ni mgonjwa.

matibabu yasio na dawa.
hakuna matibabu ya moja kwa moja ya msongo wa mawazo zaidi ya kukubaliana na hali uliyokua nayo na kuamini kwamba sio wewe peke yako lakini kila binadamu hupitia matatizo katika maisha yake ya kila siku.
kama matatizo yako yana suluhisho basi tafuta suluhisho, kama ni ugonjwa usiopona, kuvunjika kwa mahusino au vifo vya wapendendwa  au tatizo lingine lolote lile basi kubaliana na hali, waone washauri wakusaidie jinsi ya kuendelea na maisha yako.

matibabu ya dawa;
Kuna dawa mbalimbali ambazo hutumika kwa ajili ya kupunguza maumivu ya msongo wa mawazo, zinaweza kua kupunguza maumivu ya msongo wa mawazo na kupunguza dalili zake.
dawa hizi haiwezi kuondoa matatizo yako lakini sinaweza kukusaidia kujisikia vizuri, dawa hizo ni kama amitriptyline na  paroxetine.
                                                               
                                                                       STAY ALIVE

                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                          06539095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni