data:post.body FAHAMU CHANZO CHA MAKOVU MAKUBWA NA MATIBABU YAKE.[KELOIDS] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

FAHAMU CHANZO CHA MAKOVU MAKUBWA NA MATIBABU YAKE.[KELOIDS]

Keloid  ni nini?
kwa kawaida ngozi ikiumia kinakuja kidonda kwanza kisha baadae kovu linakuja kufunga kidonda, sasa katika hali isiyo ya kawaida mwili huweza kutengeneza kovu kubwa sana na kubadilisha muonekano wa mgonjwa.
                                               
kovu hili au keloid huweza kua kubwa kuliko hata kidonda chenyewe na mara nyingi hutokea kifuani, begani, sikioni,  na mashavuni japokua huweza kutokea sehemu yeyote ya mwili.
Japokua makovu haya hua hayana madhara yeyote lakini yanaweza kuharibu muonekano na urembo wa mtu.

dalili za kovu la keloid.

  • uvimbe mkubwa sehemu ilipokua kidonda
  • uvimbe mweusi kwa mtu mweusi au mwekundu kwa mtu mweupe.
  • kuwasha
  • maumivu sehemu hiyo ikiguswa
  • kuendelea kuongezeka muda unavyozidi kwenda.
nini chanzo cha keloid?
  • kuungua
  • chunusi
  • kutoboa sikio
  • makovu ya surua
  • kovu la chanjo
  • kovu la upasuaji wa hospitali.
  • kidonda cha ajali yeyote
  • kuchora tattoo.
  • kung'atwa na mdudu.
Tafiti za chuo kimoja nchini marekani kwa jina la American otheopatic college of demartology zinaonyesha kwamba asilimia 10% duniani wanapata makovu haya, huku idadi ya wanaume na wanawake wanaopata makovu haya ikilingana.
Watu weusi, watu wa asia, walatino, watu chini ya miaka 30 na wajawazito wana hatari sana ya kupata tatizo hili.
Tatizo la keloid lina chembechembe za urithi, yaani ukiwa na wazazi wenye tatizo hili basi na wewe una hatari kubwa ya kupata tatizo hili.

lini upate matibabu?
mara nyingi keloid haihitaji matibabu ila kama inakukera unaweza kwenda hospitali kutafuta matibabu, lakini pia ukuaji  mkubwa wa keloid inaweza kua dalili za saratani ya ngozi.

vipimo gani hufanyika hospitali?
dakatari anaweza kuigundua keloid kwa kuingalia tu bila kipimo chochote lakini pia daktari anaweza kuchukua sehemu ya nyama na kwenda kuipima kuhakikisha kwamba sio kansa ya ngozi.

matibabu ya keloid ni yapi?
kuna matibabu mbalimbali ya keloid kama ifuatavyo.
corticosteroids ; hizi ni dawa ambazo hutolewa kwa awamu kadhaa kupunguza uvimbe, kitaalamu dawa hizi ni ant inflamatory hivyo huzuia inflamation au uvimbe unayoletwa na mwili. mfano triamnisolone
upasuaji;  hii ni njia ya kukata na kuondoa nyama yote japokua uwezekano wa kurudi ni asilimia mia.
laser therapy; hii ni mionzi inayoweza kuliondoa kovu hilo taratibu japokua inachukua muda kumaliza tatizo.
pressure; watu ambao wanafahamu kwamba wana matatizo haya wanashauriwa kufunga vidonda vyao na kwa vitambaa ili kuzuia keloid kuota.

mwisho; matibabu ya keloids ni magumu sana kwani ina tabia ya kurudi hata baada ya matibabu, ni vema kukaa mbali na urembo wowote unaohusu kutoboa ngozi yako na kujilinda na vidonda mbalimbali.
                                                                     STAY ALIVE
                                              DR,KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                     
                                                            0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni