data:post.body Februari 2019 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

FAHAMU SHERIA INAYORUHUSU MGONJWA KUSAIDIWA KUFA NA DAKTARI.(EUTHANASIA)

Euthanasia ni nini?
Huu ni utaratibu ambao unamruhusu mgonjwa ambaye ameugua kwa muda mrefu ugonjwa ambao hautibiki na sasa amechoka anataka aondolewe maumivu yake na apumzike kwa kifo.mfano ukimwi, saratani, au kopooza.


sio utaratibu halali kwa nchi zote dunia lakini nchi nyingi za ulaya pamoja na baadhi ya majimbo ya  marekani wanaruhusu utaratibu huu.

Historia
Euthanasia ilianza kutumika zamani sana nchini ugiriki na roma, mmea wa conium ambao ulikua na sumu kali sana ulitumika kuwahisha vifo vya watu wengi ambao walihitaji huduma hii.
utaratibu huu ulisapotiwa na socretes na pilato miaka ya zamani sana na kuonekana moja ua utaratibu bora zaidi wa kuzuia mateso ya wagonjwa ambao mara nyingi hukaa kitandani kusubiri kifo.
baadhi ya nchi zimepinga sana utaratibu huu kwa misingi ya kidini na misingi ya haki za binadamu.
Nchini Tanzania hakuna utaratibu huu, hivyo kisheria kitu kama hii hairusiwi.

Aina za authanasia
kuna aina kuu mbili za utaratibu huu
active eunathasia; hii na aina ambayo dawa ya kuua ambayo ina sumu kali sana hutolewa kwa mgonjwa, lakini dawa hii inaua taratibu bila maumivu.
passive eunathasia; huu ni utaratibu ambao mgonjwa hapewi sumu lakini matibabu ambayo alikua anapewa yanasitishwa mfano mashine ya kupumua inatolewa na dawa zote  alizokua anapewa zinasimamishwa.

dawa zinazotumika kufanya euthanasia.

  1. sodium theopental;  hii ni dawa ya usingizi ambayo inatumika hata kwenye hospitali za kawaida, lakini hapa hutolewa kwa dozi kubwa sana kumfanya mgonjwa alale usingizi ndani ya sekunde 30, pia dawa hii pia hupunguza uwezo wa kupumua wa mgonjwa.
  2. pancuronium bromide; hii ni dawa ya pili kutolewa ambayo hufanya kazi kwenye mishipa ya fahamu na kumfanya mgonjwa kupooza na kushindwa hata kuinua kidole, dawa hii hufanya kazi mwili mzima hasa kwenye kifua na kumfanya mgonjwa ashindwe kupumua.
  3. pottasium chloride; hii ni dawa ya mwisho kutolewa ambayo huongeza sana kiasa cha madini ya potashiamu kwenye damu na kusababisha moyo kusimama kitaalamu kama cardiac arrest, kifo huweza kutokea kwenye dawa ya pili au dawa ya tatu.

watu maarufu waliokubali kufa kwa euthanasia.
Piergiorgio welbly: Huyu jamaa alikua muandika mashairi maarufu nchini Italia, aligunduliwa na ugonjwa wa mascular dystrophy akiwa na miaka 17, ugonjwa ambao ulimfanya apooze na kushindwa kupumua mwenyewe.
mwaka 2006 alipewa haki ya kufa kwa eunathasia baada ya kuteseka kwa muda mrefu lakini kanisa lilimpinga sana na kumyima mazishi ya kikanisa.

Karen Ann; Akiwa na miaka 22 alianguka mlangoni kwao baada ya kutoka kwenye sherehe ambapo alikunywa pombe na baadhi ya madawa ya kulevya.
Alipopelekwa hospitali ilionekana ubongo wake ulikua umeshaharibika sana kitaalamu kama brain dead.
wazazi wake waliomba atolewe vifaa vinavyomsaidia kuishi lakini alifariki rasmi miaka kumi baadae.
Hugo clouds; huyu alikua kiongozi wa filamu na muandishi wa vitabu huko Ubeligiji ambaye alitikisa sana na kupata tuzo nyingi sana kipindi cha uhai wake.
aliugua ugonjwa wa kusahau sana kitaalamu kama  alzheimer's disease ambapo mgonjwa anaweza akasahau mpaka wazazi wake.
Hali ilivyokua mbaya sana aliomba kufa ili afe na heshima yake.

vinayak damodar; huyu alikua mwanasiasa wa kihindi ambaye alikua mmoja wa wapambanaji wa uhuru.
miaka mingi baadae aliugua ugonjwa ambao haukutajwa na alitakiwa kumeza dawa kila siku, baadae
alikataa dawa na chakula mpaka akafariki.



Terri Schiavo; ni moja kati ya wamarekani maarufu amabao walioPATA huduma hii,.
mwaka 1990 alipata mshituko wa moyo ambao uliharibu sana ubongo wake, alikaa hospitali miaka kumi ndipo mme wake akamsaidia kupata kifo kisheria.
                                                                               


STAY ALIVE.

DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0769846183/0653095635

FAHAMU TATIZO LA MSONGO WA MAWAZO NA MATIBABU YAKE.

Msongo wa mawazo ni tatizo kubwa na linalokua sana hasa kwenye dunia ya sasa hivi, waathirika wengi wakiwa vijana na watu wazima  kutokana na tatizo kubwa la ajira, matatizo ya mahusiano, kufiwa  na wapendwa na matatizo mbalimbali ya kimaisha ambayo yako nje ya uwezo wao.
wanawake hua wanakua na msongo wa mawazo sana kuliko wanaume.
                                                                   
Tafiti zinaonyesha kwamba zaidi ya watu milioni mia tatu duniani wana msongo mkubwa mkubwa wa mawazo na baadhi yao huhitaji matibabu na kulazwa kabisa.
Msongo wa mawazo huchangia sana watu kujiua, zaidi ya watu laki nane hujiua kila mwaka kutokana na tatizo la msongo wa mawazo.
Bahati mbaya sio tatizo la kipaumbele kwa nchi za kiafrika kwani sisi waafrika mara nyingi tunapambana na magonjwa ambayo yanaonekana sio ya kisaikolojia.
Msongo wa mawazo huja na dalili mbalimbali na zifuatazo ni dalili kuu ambazo huonekana kwa mgonjwa wa tatizo hilo.
kukosa hamu ya kufanya chochote;  mtu mwenye msongo wa mawazo anakua hatamani kufanya chochote, hata kama kitu hicho kinafurahisha watu wengine yeye anakua hawezi kukifurahia, unaweza kuliona hilo kwa kumuangalia tu bila kumuuliza chochote.
kutokua na furaha muda wote; mtu kama huyu anakua hana furaha, muda mwingi anakua na huzuni na kulia mara kwa mara na kukosa matumaini kabisa ya maisha, hii humfanya mtu ashindwe kufanya shughuli yeyote ya kimaendeleo au kikazi.
mabadiliko ya uzito; kupungua uzito mwingi sana bila kufanya diet au mazoezi yeyote ni dalili ya msongo wa mawazo sababu ya kushindwa kula lakini pia baadhi ya watu huongezeka uzito kipindi hiki kwani msongo wao wa mawazo huwafanya wale chakula kingi ili wajisikie afadhali.
kukosa usingizi; watu wenye msongo wa mawazo hua hawapati usingizi kabisa, anaweza kukaa kitandani masaa mengi sana bila usingizi na akaja kupata usingizi kukiwa kunakaribia asubuhi, hichi ni kitu amabacho kinaweza kumfanya mtu ashindwe kufanya shughuli zake za kila siku.
mawazo ya kujiua; wagonjwa wengi wenye msongo wa mawazo hua wanajiona hawana thamani ya kuishi, hivyo kichwani mwao wanakua na mawazo ya kujiua japokua wanaweza kushindwa kutekeleza mipango yao lakini mawazo hayo yapo na ikitokea mawazo hayo yakaendelea muda mrefu mtu anaweza akaamua kujiua.
uchovu na kuishiwa nguvu; mtu mwenye msongo wa mawazo anakua anaishiwa nguvu za kufanya kazi, anaweza kushindwa hata kunyenyua kitu ambacho ana uwezo wa kukibeba kila siku.
kushindwa kufikiri vizuri; mtu mwenye msongo wa mawazo hawezi kufanya kazi yeyote inayohitaji akili sana kufanya kazi, kwani uwezo wake wa kufikiri unakua chini sana.
kujihisi hana thamani; watu wenye msongo wa mawazo hujihisi hawana thamani kabisa na wakati mwingine husikia sauti ambazo zinamwambia kwamba yeye hana thamani na ni bora ajiue tu kwani kuwepo duniani ni kikwazo kikubwa.
kufanya mambo taratibu; mtu mwenye msongo wa mawazo hawezi kufanya kazi kwa haraka kama watu wa kawaida, anaweza akakaa sehemu moja na kujisahau kwa muda mrefu sana.
mara nyingi hufanya shughuli zake kama mtu ambaye ni mgonjwa.

matibabu yasio na dawa.
hakuna matibabu ya moja kwa moja ya msongo wa mawazo zaidi ya kukubaliana na hali uliyokua nayo na kuamini kwamba sio wewe peke yako lakini kila binadamu hupitia matatizo katika maisha yake ya kila siku.
kama matatizo yako yana suluhisho basi tafuta suluhisho, kama ni ugonjwa usiopona, kuvunjika kwa mahusino au vifo vya wapendendwa  au tatizo lingine lolote lile basi kubaliana na hali, waone washauri wakusaidie jinsi ya kuendelea na maisha yako.

matibabu ya dawa;
Kuna dawa mbalimbali ambazo hutumika kwa ajili ya kupunguza maumivu ya msongo wa mawazo, zinaweza kua kupunguza maumivu ya msongo wa mawazo na kupunguza dalili zake.
dawa hizi haiwezi kuondoa matatizo yako lakini sinaweza kukusaidia kujisikia vizuri, dawa hizo ni kama amitriptyline na  paroxetine.
                                                               
                                                                       STAY ALIVE

                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                          06539095635/0769846183

UFAHAMU UGONJWA WA AKILI NA MATIBABU YAKE.(SCHIZOPHRENIA)

schizophrenia ni nini?
Huu ni ugonjwa mbaya sana wa akili ambao huharibu au kubadilisha mfumo wa kuwaza, kutafsiri mambo, hisia na tabia ya mtu.
Ni ugonjwa ambao umeathiri zaidi ya watu milion 21 dunia nzima, ugonjwa huu huathiri uwezo wa kiuchumi na kielemu wa watu wengi sana.
Watu wenye ugonjwa huu wa akili huweza kufa mapema sana kuliko watu wengine kutokana na magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kuzuilika kama moyo, kisukari na kadhalika.
Ubaguzi, kutengwa na talaka kwa wagonjwa ni mkubwa sana dunia nzima hasa nchi zinazoendelea kama afrika.

chanzo cha ugonjwa huu ni nini?
Tafiti hazijaweza kugundua chanzo halisi cha ugonjwa huu, lakini muingiliano kati ya vinasasaba au gene na mazingira tunayoishi unaweza ndio kua chanzo cha ugonjwa huu.
watu ambao wako kwenye hatari kubwa ya kuugua ugonjwa huu ni watu ambao wana ndugu wagonjwa, msongo mkubwa wa mawazo hasa watu wanaoishi mjini, matatizo ya ubongo yakuzaliwa nayo au ya kuugua ukubwani.


dalili za ugonjwa huu ni kama ifuatavyo.

  • Kuona na kusikia vitu ambavyo wenzako hawavioni wala kusikia.
  • Kuamini vitu ambavyo havipo mfano mgonjwa anaweza kuamini kwamba yeye ni raisi wa nchi, hana kiungo fulani, anapendwa sana, anasalitiwa na mpenzi wake au kuna watu wanataka kumuua.
  • Tabia ambazo sio za kawaida kama kutembea tembea hovyo, kucheka bila sababu, kua mchafu mchafu na kuwa tofauti na siku zote.
  • Kuongea vitu ambavyo havipo au haviendani na maada husika.
  • Tofauti ya hisia na muonekano yaani mgonjwa anaweza kucheka wakati ana huzuni.
  • Kujitenga na watu.
  • Kukaa kimya muda mrefu na kukaa sehemu moja.
vipimo gani hufanyika?
hakuna kipimo cha moja kwa moja ambacho kinaweza kugundua ugonjwa huu lakini baadhi ya vipimo hufanyika ili kujiridhisha kwamba hakuna ugonjwa mwingine umeingilia, mfano
  • kipimo cha malaria
  • kipimo cha ukimwi
  • kipimo cha kaswende
  • wingi wa damu
  • mkojo
  • choo
  • kipimo cha uwezo wa ubongo i.e EEG
MATIBABU
Hakuna dawa za moja kwa moja za kumaliza ugonjwa huu lakini zipo dawa ambazo mtu anatakiwa atumie ili aweze kuishi maisha  ya kawaida kama watu wengine.
dawa hizo ni kama haloperidol, chlorpromazine, olanzapine, respiredone, na clozapine.
dawa hizi hutolewa kulingana na hali ya mgonjwa na zinatakiwa zitumike maisha yake yote na kwa wagonjwa ambao wanashindwa kuvumilia dawa za kumeza basi zipi sindano za kuchoma mara moja kwa mwezi kwa jina la fluphenazine.
matibabu mengine ambayo sio ya dawa yanahusiana na kumsaidia mgonjwa kutumia dawa, kumpa ushirikiano, ushauri na kumsaidia mahitaji yake.
wagonjwa wengi hufa mapema kwa kukosa ushirikiano na kutengwa na ndugu.
Nchi ambazo hazijaendelea wagonjwa hawa hawapati matibabu kabisa hivyo kuishi katika hali mbaya zaidi.
Usihangaike na waganga wa kienyeji, hakuna dawa ya kutibu kabisa tatizo hili, ila zipo dawa za kutuliza.

                                                              STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                 0769846183/0653095635
         

UFAHAMU UGONJWA WA NYAMA ZA MACHO NA MATIBABU YAKE.(PTERYGIUM)

Ptyerigium ni nini?
Huu ni ugonjwa wa macho ambao huja kwa kuota kwa nyama eneo la mbele kabisa la jicho kitaalamu kama conjuctiva, nyama hiyo huota kuelekea katikati ya jicho ambapo kuna sehemu nyeusi ya jicho kwa jina la pupil.
                                                   
Hali hii huweza kumuogopesha mgonjwa na kufikiri kwamba ameugua saratani lakini ile sio saratani, katika hali isiyokua ya kawaida, uvimbe ule ukiwa mkubwa sana huweza kupunguza uwezo wa jicho kuona vizuri.
ugonjwa huu unaweza kuathiri jicho moja au yote mawili kwa mpigo, japokua huu sio ugonjwa hatari sana lakini unaweza kukuletea usumbufu wa kuona vizuri na muonekano wako usiwe mzuri.

nini chanzo cha tatizo hili?
  • kupigwa na jua muda mrefu
  • macho makavu
  • vumbi na upepo machoni.
dalili zake ni zipi?
  • hisia za kitu machoni
  • macho kuwasha
  • macho mekundu
  • kushindwa kuona vizuri
  • macho kuwasha.

matibabu yake ni yapi?
ukiwa na tatizo hili hauhitaji matibabu yeyote, lakini unaweza kupewa dawa za kuweka matone jichoni kupunguza usumbufu wa dalili.
lakini nyama zikiwa kubwa sana kuanza kuzuia kuona basi utafanyiwa upasuaji mdogo kuziondoa.

jinsi ya kuzuia ugonjwa huu
hakikisha unavaa miwani za kujizuia na mwanga mkali wa jua mara kwa mara.



                                                                   STAY ALIVE
                                           DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                         0769846183/0653095635

FAHAMU CHANZO CHA MAKOVU MAKUBWA NA MATIBABU YAKE.[KELOIDS]

Keloid  ni nini?
kwa kawaida ngozi ikiumia kinakuja kidonda kwanza kisha baadae kovu linakuja kufunga kidonda, sasa katika hali isiyo ya kawaida mwili huweza kutengeneza kovu kubwa sana na kubadilisha muonekano wa mgonjwa.
                                               
kovu hili au keloid huweza kua kubwa kuliko hata kidonda chenyewe na mara nyingi hutokea kifuani, begani, sikioni,  na mashavuni japokua huweza kutokea sehemu yeyote ya mwili.
Japokua makovu haya hua hayana madhara yeyote lakini yanaweza kuharibu muonekano na urembo wa mtu.

dalili za kovu la keloid.

  • uvimbe mkubwa sehemu ilipokua kidonda
  • uvimbe mweusi kwa mtu mweusi au mwekundu kwa mtu mweupe.
  • kuwasha
  • maumivu sehemu hiyo ikiguswa
  • kuendelea kuongezeka muda unavyozidi kwenda.
nini chanzo cha keloid?
  • kuungua
  • chunusi
  • kutoboa sikio
  • makovu ya surua
  • kovu la chanjo
  • kovu la upasuaji wa hospitali.
  • kidonda cha ajali yeyote
  • kuchora tattoo.
  • kung'atwa na mdudu.
Tafiti za chuo kimoja nchini marekani kwa jina la American otheopatic college of demartology zinaonyesha kwamba asilimia 10% duniani wanapata makovu haya, huku idadi ya wanaume na wanawake wanaopata makovu haya ikilingana.
Watu weusi, watu wa asia, walatino, watu chini ya miaka 30 na wajawazito wana hatari sana ya kupata tatizo hili.
Tatizo la keloid lina chembechembe za urithi, yaani ukiwa na wazazi wenye tatizo hili basi na wewe una hatari kubwa ya kupata tatizo hili.

lini upate matibabu?
mara nyingi keloid haihitaji matibabu ila kama inakukera unaweza kwenda hospitali kutafuta matibabu, lakini pia ukuaji  mkubwa wa keloid inaweza kua dalili za saratani ya ngozi.

vipimo gani hufanyika hospitali?
dakatari anaweza kuigundua keloid kwa kuingalia tu bila kipimo chochote lakini pia daktari anaweza kuchukua sehemu ya nyama na kwenda kuipima kuhakikisha kwamba sio kansa ya ngozi.

matibabu ya keloid ni yapi?
kuna matibabu mbalimbali ya keloid kama ifuatavyo.
corticosteroids ; hizi ni dawa ambazo hutolewa kwa awamu kadhaa kupunguza uvimbe, kitaalamu dawa hizi ni ant inflamatory hivyo huzuia inflamation au uvimbe unayoletwa na mwili. mfano triamnisolone
upasuaji;  hii ni njia ya kukata na kuondoa nyama yote japokua uwezekano wa kurudi ni asilimia mia.
laser therapy; hii ni mionzi inayoweza kuliondoa kovu hilo taratibu japokua inachukua muda kumaliza tatizo.
pressure; watu ambao wanafahamu kwamba wana matatizo haya wanashauriwa kufunga vidonda vyao na kwa vitambaa ili kuzuia keloid kuota.

mwisho; matibabu ya keloids ni magumu sana kwani ina tabia ya kurudi hata baada ya matibabu, ni vema kukaa mbali na urembo wowote unaohusu kutoboa ngozi yako na kujilinda na vidonda mbalimbali.
                                                                     STAY ALIVE
                                              DR,KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                     
                                                            0653095635/0769846183

HAYA NDIO MADHARA YA KUTUMBUA CHUNUSI.

chunusi ni nini? 
hivi ni vipele vinavyotokea usoni, kifuani na mgongoni sababu ya kubadilika kwa mfumo wa kutengeneza mafuta wa ngozi, hali hii husababishwa na kutengenezwa kwa mafuta mengi chini ya ngozi kuliko kawaida na kuziba kwa vinyweleo vya ngozi.
                                                                  

imekua ni jadi kwa watu wengi kupenda kuzitumbua chunusi pale ambapo zinakua zimekua kubwa na wakati mwingine hata zikiwa ndogo.
lakini kimsingi kuna madhara makubwa sana ya tabia hii kwenye ngozi yako na afya ya mwili wako wote kiujumla kwa ujumla kama ifuatavyo.
kuacha makovu meusi; kwa kawaida chunusi ikipona yenyewe hua haichi alama yeyote lakini ukianza kuikamua na kuisugua basi unatengeneza kidonda kidogo ambacho baadae kitapona kwa kaucha kovu.
makovu ya usoni yanaleta muonekano mbaya sana kwani usoni ni sehemu ambayo inaonekana sana kukiko sehemu zote za mwili.

uwezekano wa kuondoa makovu haya ni mgumu na hata ukiwezekana ni kwa kutumia dawa za gharama kubwa na wengine huamua kujichubua kabisa.
maumivu makali; chunusi huambatana na maumivu makali ikianza kutumbuliwa na chunusi ambazo zinakua mbele kidogo ya masikio husababisha maumivu makali ya kichwa zikitumbuliwa.
hii inaweza kumfanya mtu akawa mgonjwa sana na kushindwa kuendelea na shughuli zake.
                                                          

homa ya uti wa mgongo; japokua hii hutokea mara chache sana lakini ni hatari na inaweza kumuua mtu, usoni kuna mishipa ya damu ambayo huko ndani huungana na mishipa mingine ya damu na kufika kwenye ubongo.
sasa ukitumbua chunusi bakteria wanaweza kusambaa na kupita kwenye damu mpaka kwenye ubongo.
ugonjwa huu ni hatari na huua watu sana.

kuharibu muonekano hapo hapo;  kwa kawaida chunusi ambayo haionekani vizuri huvimba zaidi ukijaribu kuitumbua, hii itakufanya uonekane una chunusi nyingi kuliko kawaida na kukunyima kujiamini mbele za watu.

mwisho: kutumbua chunusi sio njia bora ya kupambana nazo kama tulivyoona hapo juu, hivyo kama unataka kujua matibabu mazuri ya chunusi soma hapa http://www.sirizaafyabora.info/2014/08/ufahamu-ugonjwa-wa-chunusi-na-matibabu.html

                                                       STAY ALIVE

                                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                            0653095635/0769846183