data:post.body HUU NDIO UMRI SAHIHI WA MWANAMKE KUBEBA MIMBA.[UTAFITI] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HUU NDIO UMRI SAHIHI WA MWANAMKE KUBEBA MIMBA.[UTAFITI]

Shukrani kwa njia za uzazi wa mpango siku hizi wanawake wanaweza kuamua wakae muda gani kabla ya kuamua kuzaa.
                                                                         
kusubiri muda sahihi wa kuzaa ni vizuri kiuchumi na kisaikolojia  lakini kuna madhara yake kwani uwezo wa kubeba mimba huendelea kupungua kadri mwanamke anavyozidi kua mkubwa.
hivyo wakati mwingine kama kweli unahitaji mtoto maishani mwako na huoni uwezekano wa kumpata mume wa kukuoa na umri unazidi kwenda ni vema kufanya maamuzi magumu  ya kuzaa hata kama hiyo ndoa haijaja.
kukosa mme maishani ni kawaida lakini kukosa watoto inaweza kuleta msongo mkubwa wa mawazo maishani na kukufanya uzeeke peke yako nyumbani.

kuzaa kipindi cha miaka 20
hichi ni kipindi cha kilele cha mwanamke kubeba mimba ambacho wanawake wanakua na uwezo mkubwa sana wa kubeba mimba hasa kwanzia miaka 18 mpaka 25, ni kipindi ambacho tunasema kizazi kinakua na sumaku kwani ukigusa tu ni mimba.
kipindi hiki mwanamke anakua na mayai mengi sana na sio rahisi kupata matatizo ya uzazi kama kifafa cha mimba, kushindwa kuzaa kawaida au kisukari cha mimba na mengine mengi.
lakini pia mwanamke anakua bado mwili wake unaweza kuchoma mafuta kwa kasi sana kiasi kwamba hata akizaa huweza kupungua mwili ndani ya muda mfupi wakati mwingine bila hata mazoezi wa diet yoyote.
ukichunguza wanawake waliozaa wakiwa bado wadogo sana utagundua wengi wao hawakunenepeshwa na uzazi na tafiti zinaonyesha kwamba watoto bora kabisa huzaliwa kipindi hiki,

kuzaa kipindi cha miaka 30
uwezo wa mwanamke kuzaa huanza kupungua akifikisha miaka 32, akifikisha miaka 35 uwezo wa kuzaa unazidi kupungua kwa kasi sana.
wanawake huzaliwa na zaidi ya mayai milion moja lakini kipindi hiki mwanamke hukadiriwa kubakisha mayai 25000 tu ambayo yanakua yamepungua ubora.
hivyo uwezekano wa kubeba mimba akishiriki tendo la ndoa kwa miezi mitatu mfululizo ni kama asilimia 12 tu.
matatizo wakati wa kujifungua na kuzaa watoto wenye matatizo mbalimbali huongezeka mwanamke akifikisha miaka 35.
kwa nchi zilizoendelea watu wa umri huu wakibeba mimba, vipimo vingi hufanyika na kama mtoto akikutwa ana tatizo basi mama hushauriwa kutoa mimba.
vifafa vya mimba, mimba kuharibika, kuzaa kwa upasuaji, mtoto kufia tumboni, kisukari cha mimba na matatizo mengine mengi hutokea wakati huu.
matatizo mengine ya kuzaa kipindi hiki ni kunenepa sana kwani uwezo wa mwili kuchoma mafuta unakua umepungua sana.

kuzaa kipindi cha miaka 40.
kipindi hiki uwezo wa mwanamke kuzaa ni kama asilimia saba tu, matatizo ya uzazi kama kuzaa mtoto aliyekufa, uzito mdogo, kifafa cha mimba, mtoto ambaye ana matatizo ya kiakili au kimwili, kisukari na kifafa cha mimba huongezeka sana.
kwa nchi za afrika ambapo teknolojia ni ndogo sana huu sio muda sahihi wa kuzaa lakini kwa nchi ambazo zimeendelea sana wanaweza kupambana na matatizo yatakayojitokeza.
kama ilivyo kipindi cha miaka 30, kipindi hiki wanawake hunenepa zaidi na zaidi wakizaa.

mwisho;
kibailojia akimaliza uzazi akiwa na miaka 25 anakua amefanya jambo la msingi sana  lakini kulingana na mabadiliko ya hali ya maisha na uchumi ni vizuri kumaliza uzazi ukiwa na miaka 30.
unaweza kwenda zaidi mpaka miaka 35 lakini matatizo yapo mengi kama nilivyoainisha.

                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                              0653095635/0769846183



0 maoni:

Chapisha Maoni