data:post.body Januari 2019 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

UFAHAMU UGONJWA WA MACHO MEKUNDU NA MATIBABU YAKE.(CONJUCTIVITIS)

Conjuctivitis ni nini?
huu ni ugonjwa unaohusiana na kushambuliwa kwa sehemu ya mbele ya jicho kitaaalamu kama conjuctiva.
Huu ni moja ya magonjwa ambayo yanaongoza kusababisha macho mekundu kwa wagonjwa wengi.

nini chanzo cha ugonjwa huu?

  • bacteria
  • virusi
  • aleji mbalimbali.
ugonjwa unaweza kuambukizwa?
kama ugonjwa umesababishwa na aleji sio rahisi kuambukizwa lakini kama nia bacteria au virusi basi ugonjwa unaweza kusambaa kwa kasi sana hasa maeneo ya shule.
mara nyingi ugonjwa huanza na jicho moja lakini huambukia jicho lingine pale mtu anapofikicha macho yote na kuhamisha wadudu jicho moja kwenda lingine.
lakini pia unaweza kuambukizwa kwa kuchangia taulo, miwani au nguo ambazo zinafika machoni.

dalili za ugonjwa ni zipi?
wakati mwingine dalili za ugonjwa huweza kutegemea chanzo cha ugonjwa wenyewe kama ni bacteria, virusi au aleji lakini kuna dalili za ujumla kama zifuatazo.
  • usaha kutoka machoni
  • macho kuvimba
  • kutoka majimaji usoni
  • kusikia kama mchanga machoni.
  • macho kuwasha kama ni aleji.

matibabu ni yapi?
  • dawa ya kuweka machoni kwa jina la chlorampenicol itumike kutwa mara tatu kwa muda wa siku tano.
  • kama kuna dalili za aleji basi kuna dawa inaitwa sodium cromoglyacate ambayo mara nyingi hutumika kutwa mara mbili au mara tatu.
jinsi ya kuzuia ugonjwa huu
  • epuka kuchangia taulo au miwani na mgonjwa.
  • nawa uso  na kuosha mikono na sabuni mara kwa mara.
  • kaa mbali na vitu vinavyokupa aleji.
                                                             STAY ALIVE

                                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                0769846183/0653095635

UFAHAMU UGONJWA WA JIPU LA MACHO NA MATIBABU YAKE.(STYE)

STYE ni nini?
huu ni ugonjwa wa macho ambao huwapata watu wengi sana katika kipindi cha maisha yao yaani angalau mara moja au mara mbili.
huu ni uvimbe wa jipu ambao hutokea kwenye sehemu ya jicho na kuleta maumivu makali.
                                               

chanzo cha ugonjwa huu ni nini?
ugonjwa huu husababishwa na bacteria ambao hushambulia sehemu ya macho inayohusika na kutengeneza majimaji ya kulainisha macho kitaalamu kama gland of zeis.
pamoja na bacteria kusababisha hali hii ukosefu wa maji ya kutumia, kutokula mlo kamili, kusugua macho na mikono, kushuka kwa kinga ya mwili na kukosa usingizi wa kutosha huongeza uwezekano wa kuugua ugonjwa huu.
ugonjwa huu sio hatari lakini una usumbufu mkubwa ambao unaweza kufanya kushindwa kufanya shughuli zako kwa amani.


dalili za ugonjwa huu ni zipi?

  • uvimbe sehemu ya juu au chini ya jicho.
  • maumivu makali sana ya jicho hasa ukiinama,
  • jicho kua jekundu
  • kushindwa kuangalia mwanga wa jua.
  • kutokwa na machozi
  • kuhisi kama mchanga jichoni.
matibabu ya asili;
mara nyingi ugonjwa huu hupona wenyewe bila matibabu yeyote ndani ya siku 7 mpaka 14, lakini kama unataka kupona haraka basi chukua maji ya moto kisha kanda kila siku mara moja sehemu ambayo ina uvimbe na jipu linaweza kupotea bila hata kuiva.
watu wenye ugonjwa huu hawashauriwi kupaka  urembo wowote make up, mafuta ya losheni usoni au kuweka urembo wowote machoni.

matibabu ya kisasa
meza dawa za antibayotiki kama amoxicillin kutwa mara tatu ndani ya siku tano mpaka saba lakini pia unaweza ukatumia dawa za matone.
lakini pia meza panadol au diklopa kutwa mara tatu kupunguza maumivu ya jicho.
kwa matibabu haya ugonjwa unaweza ukaisha wenyewe na kama usipoisha basi inabidi uende hospitali ukapasuliwe ili kuondoa usaha wote.
matibabu ya upasuaji yanapedekezwa kwa jipu lililoiva au kwa mgonjwa ambaye ugonjwa unamrudia mara kwa mara.

jinsi ya kuzuia 
  • usichangie vifaa vya kuoga kama taulo.
  • usichangie vifaa vya kupaka urembo kama make up.
  • nawa mikono na oga kila siku.
  • hakikisha umenawa urembo wote wa macho kabla ya kulala.
  • kula mlo kamili kuweka kinga yako vizuri.

                                                                STAY ALIVE
                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO  
                                                    0769846183/0653095635

SABABU 10 KWANINI WANAWAKE HUWASALITI WAPENZI WAO(SAIKOLOJIA)

Japokua wanaume wengi ndio wanaonekana sana kusaliti ndoa zao au mahusiano yao kuliko wanawake siku hizi wanawake pia wanasaliti ndoa zao au mahusiano yao pia.
Tangu mwaka 1990 tafiti zinaonyesha kwamba idadi ya wanawake wanaosaliti mahusiano yao umeongezeka kwa asilimia arobaini lakini idadi ya wanaume wanaosaliti ndoa zao imebaki ileile, kitu ambacho kinazua maswali mengi.
                                                               
wanawake wa siku hizi wana mtazamo sawa na wanaume linapokuja swala la ngono, na huweza kuchepuka mara moja au mbili kwa mwezi au mara moja kila mwezi.
kuna aina ya wanawake ambao hawawezi kua na mwanaume mmoja kwani hawawezi kupata kila wanachotaka maishani kwa kua na mwanaume mmoja tu.
lakini pia baadhi ya wanawake kusaliti mahusiano yao ni sehemu ya maisha yao, yaani wakivutiwa sehemu hawawezi kujidhibiti hisia zao hivyo huamua kulala na hao watu tu ili kupata mambo mapya.
lakini kwa ujumla mara nyingi sana wanawake huenda nje ya ndoa kama kuna vitu fulani vimeanza kukosekana ndani ya ndoa au mahusiano tofauti na wanaume ambao kiukweli huwezi kuwazuia hata kama kila kitu kipo. zifuatazo ni sababu kuu...
kukosa mawasiliano; hata kama unaishi na mwanamke nyumba moja, mawasililiano ni muhimu sana baina yenu, ni vizuri kujua nini kinaendelea kwenye maisha yake kwani anaweza kua ana dukuduku na wewe hutaki kusikiliza lakini pia mahusiano ya mbali kwa kiasi kikubwa yakiwa na mawasiliano yanamfanya mwanamke ahisi kama yuko na mwanaume sehemu moja, lakini mawasiliano yakiwa mabovu yaani kupitisha siku bila kuongea kabisa inamvuta mwanamke kutamani mahusiano mengine.
kisasi; wanawake ni watu wa visasi sana hasa wakitendwa vibaya, au ukiwasaliti wakajua. wanaweza kujifanya wamekubaliana na hali baada ya kuombwa msamaha lakini wakaliweka moyoni na siku moja watakulipa tu.
na sio kwamba atalipiza kisasi kwa kua wewe umelala na mwanamke mwingine tu ila anaweza kulipiza sababu hukumjali, hukukumbuka siku yake ya kuzaliwa, hukukumbuka siku ya wapendanao au siku yake yeyote muhimu.
kutoridhika na tendo la ndoa; wanaume wengi hudhani kwamba wanawake hua hawajisikii kufanya tendo la ndoa mara nyingi kitu ambacho sio kweli.
wanawake pia wana hamu sana ya tendo la ndoa kama wanaume lakini tofauti na sisi wanaume, wao hawajali sana umelala naye mara ngapi kwa siku au umepiga mishindo mingapi ulipokua kitandani.
wanawake wanajali ubora wa tendo la ndoa.
mwanamke anaweza akalala na mume wake mara tatu au nne kwa wiki na akaridhika lakini mwnamke anayelala na mwanume wake kila siku na mishindo minne kila siku asiridhike na akaenda nje.
kimsingi kama unaona unashindwa kumridhisha mwanamke wako kabla ya ndoa ni vizuri ukabadilisha mawazo ukatafuta ambaye unamuweza kwani bila hivyo utasaidiwa sana.
mwanaume kua na wivu sana; kuna wanaume wanawaendesha sana wanawake zao, yaani atapiga simu kila mara na kutaka kuongea na rafiki zake ili kuhakikisha mwanamke wake yupo salama.
lakini hii sio njia nzuri, kisaikolojia binadamu ukimbana sana ndio unamtengenezea mazingira ya kutoroka.
mwanamke huyu atakusaliti ili kukuonyesha kwamba pamoja na mitego yako yote wewe humuwezi, hivyo muache mwanamke huru kama sio msaliti wala hawezi kukusaliti.
kutojiamini; wanawake wanapenda kuambiwa kwamba ni wazuri na wamependeza, sasa ikitokea unakaa na mwenza wako miezi kadhaa bila kumsifia afu akaanza kusifiwa na watu wengine basi anaweza kuamua kulala na huyo anayemsifia kwani ndio mtu anayemfanya ajisikie vizuri.
lakini pia umri ukishamtupa mkono mwanamke halafu akawa kwenye mahusiano ambayo anahisi ndoa inachelewa sana anaweza kuanza kwenda nje kubahatisha mtu ambaye anaweza akamuoa.
ugumu wa maisha; wazungu wanasema kwamba 'everyone has a price' yaani kila mtu ana bei yake ambayo anaweza kununulika.
sasa katika kipindi fulani kigumu sana cha maisha mtu anaweza akatokea akamwambia mpenzi wako au mke wako kwamba nataka kulala na wewe kisha ntakupa fedha kiasi fulani.
sasa akiwa amekabwa sana na shida anaweza kuwaza, kwani kulala mara moja na huyu mtu kutabadilisha nini?
na hapo ndipo usaliti unapoanza.
mfano ni wanawake wachache sana wanaweza kukataa milion moja mpaka kumi kwa tendo la saa moja tu.
kutegemea makubwa kwenye mahusiano; mwanamke anaweza kuingia kwenye mahusiano akiwa na mategemeo makubwa sana ya kimapenzi au ya kiuchumi lakini baadae akagundua kwamba hivyo vitu haviwezekani.
lakini pia hakuna mwanaume ambaye anaweza kuonyesha mapenzi yaleyale kwa miaka yote, kuna kipindi mapenzi lazima yapungue kidogo japokua hayataisha kabisa.
hiii inatoa nafasi ya mwanamke kwenda nje ya ndoa kujaribu kuyapata yale aliyoyategemea.
kukosa vitu vidogo vidogo kwenye mahusiano; unaweza ukamfanyia vitu vikubwa sana mwanamke lakini akakusaliti sababu kuna viti vidogo vidogo sana havipati ambavyo anahisi kwamba haumpendi ndio maana hauvifanyi.
unaweza kumnunulia gari ila siku moja akapata pancha akakupigia ukashindwa kwenda kwa wakati sababu ya kazi zimekubana.
akitokea mwanaume mpya akamsaidia kubadilisha tairi ataonekana muhimu sana kuliko wewe uliyenunua gari.,
presha ya marafiki; mara nyingi tabia huwavuta watu pamoja na kua marafiki, ukiona mwanamke wako ana marafiki ambao wana tabia za undangaji au ni watu wa kutafuta mabwana usifikiri wamekutana na mke wako bahati mbaya, kuna uwezekano mkubwa mke wako pia ni mwenzao.
hata kama mke wako hafanyi hivyo basi ipo siku moja atawafuata.
kuchoshwa na mahusiano; tukiacha unafiki, ndoa za zamani zilidumu sababu ya misingi ya uvumilivu na kumuogopa mungu lakini mioyo ya binadamu ilikua radhi kwenda nje.
sasa kwa dunia hii ya sasa ambayo hofu ya mungu haipo wala uvumilivu hakuna ni rahisi sana mtu aliyemchoka mwenza wake kwenda nje kutafuta ladha nyingine.
mwisho; hakuna mtu anayeweza kusiamama na kudai yeye amemdhibiti mwanamke wake, pamoja kwamba unaweza kufanya yote lakini mwisho wa siku maamuzi hubaki mikononi mwake.
wanawake ambao wanamjua mungu sana hawaendi nje sababu ya kuogopa dhambi sio kwamba mioyo yao imeridhika na wewe.

                                                         STAY ALIVE

                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                             0653095635/0769846183

UKIONA HIZI DALILI UJUE MWANAMKE WAKO ANAKUSALITI.(SAIKOLOJIA)

Usaliti sio kitu kigeni kwenye dunia ya mahusiano, tafiti zinaonyesha kati ya watu wanne waliko kwenye mahusiano basi mmoja wao anamsaliti mwenzake.
unaweza kuona jinsi gani tatizo la usaliti ni kubwa sana kiasi kwamba linaweza kuhatarisha mahusiano mengi.                                                         
                                                                       
swala la kiafya ni muhimu zaidi kuliko kuharibika kwa mahusiano kwani magonjwa mengi ya kuambukizwa kama ukimwi hupata upenyo sehemu kama hizi.
makala ya leo ntazungumzia dalili za wanawake wanaosaliti kwani zinakua tofauti kidogo na zile za wanaume lakini pia makala ijayo ntazungumzia upande wa wanaume.
Asilimia kubwa ya wanawake husaliti wenza wao kwenda kutafuta mapenzi ndio maana usaliti ukishaanza kutoka kwa mwanamke basi mahusiano hayo huenda yamefika mwisho lakini pia baadhi ya wanawake wachache husaliti kwa sababu za kuongeza kipato, ndio maana utakuta mwanamke anajiuza lakini kuna mtu anampenda sana. japokua kila siku anabadilisha wanaume.
zipo sababu zingine nyingi lakini ntaziongelea makala zijazo.
sasa kama uko kwenye mahusiano na mwanamke muda mrefu au hata muda mfupi na dalili hizi zikaanza kujitokeza basi ujue mtu huyo anakusaliti, anaweza asionyeshe zote lakini kama unaziona kua makini.
Anaficha simu yake; mwanamke anayekusaliti mara nyingi akija kwako  kwanza atakua hapendi kukaa sehemu ambayo wewe unaona kioo cha simu yake akiwa anachati, pili simu yake mara nyingi itakua haina sauti na baadhi ya simu atakua hazipokei kwa madai kwamba watu wanamsumbua.
lakini kitu cha msingi kabisa hata ukitishia kuchukua simu yake atabadilika sana na huenda akakuzuia hata kama unataka kupiga simu kutumia simu yake.
kipindi hiki kutakua kuna namba moja ambayo anawasialiana nayo sana lakini kwa siri sana kwani anashindwa kuchati kwa uhuru mbele yako.
muda mwingi watu hawa watakwambia kwamba kila mtu asishike simu ya mwenzake lakini hizo ni sababu za kujilinda, wapenzi wa kweli hawafichani chochote kile.
anajishtukia sana; kwa hali ya kawaida ukimpigia simu mtu ukamuuliza yuko wapi atakupa jibu rahisi sana kwamba niko sehemu fulani lakini mwanamke msaliti hawez kujibu swali hilo kirahisi, ataanza kukuuliza kwanini unamuuliza hilo swali? kwani kuna nini?
lakini pia atakua anakwepa maswali yeyote kutoka kwako ili asiweze kujichanganya kwenye maelezo yake.
huenda anahisi umemona sehemu ambayo sio kawaida au umeambiwa kitu wakati wewe hujui lolote.
hataki tena mahaba na wewe; mwanamke huyu ataanza kukupa sababu mbalimbali za kutoshiriki tendo la ndoa na wewe, kumkumbatia au kumbusu.
anaweza kuanza kua bize sana, kusingizia uchovu sana au kujifanya mgonjwa au kutokua na hamu kabisa ya tendo la ndoa wakati wewe unafahamu kwamba ni mtu ambaye kwa miaka yote alikua ni mpenzi wa hivyo vitu lakini leo ghafla havitaki tena.
wakati mwingine unaweza kushiriki naye tendo la ndoa lakini hatakua pale kihisia na mwisho wa siku itaonekana humridhishi.
kumbuka yule anayekusaliti kwa mambo ya pesa sehemu hii ya mahaba inaweza isibadilike kabisa.
ratiba za siri; mtu ambaye ulikua unajua ratiba zake vizuri kwa muda mrefu lakini siku hizi anaanzisha safari ambazo hazikuwepo, anafanya mambo ya siri sana ambayo wewe mwenyewe kama mpenzi wake unajua alitakiwa akushirikishe.
wanawake ni watu ambao wanapenda sana kuwahusisha wanaume wao na mambo wanayofanya ili kupata ushauri hivyo ukiona hakuulizi kitu ujue kuna tatizo.
yuko bize sana; huenda mwanzoni ulikua una uwezo wa kumshtukiza mkatoka kwenda kula au kwenda kutembea sehemu lakini siku hizi hataki mambo hayo.
anataka chochote mnachotaka kufanya mpange siku kadhaa kabla ili aweze kujua ni muda gani wa kutumia na wewe na muda gani wa kwenda kwa wanaume wengine.
hataki kuzungumzia ndoto zenu; mara nyingi mwanamke huyu hataki kusikia habari zenu wewe na yeye kuhusu maisha ya baadae, atakua hataki kuzungumzia kwani yeye hajioni akiwa na wewe.
wanawake ni watu ambao wanapenda sana kua siriazi na mahusiano mpaka ndoa hivyo ukiona hakuulizi chochote ujue hauko peke yako tena wewe ndio mwanaume wa pembeni.
anakutuhumu kwamba unamsaliti; mwanamke huyu anakua ana hofu kubwa kwamba huenda utamgundua, hivyo kuepusha shari hili ni kukutuhumu sana wewe huku akiwataja wanawake ambao huenda ni wafanyakazi wenzako au ni rafiki zako tu kwamba unatoka nao.
hii ni njia ya kufanya ili kukupoteza wewe ushindwe kuoana mambo yake.
anataka kua peke yake kwa muda(break); mara nyingi wanawake hua hawapendi kukaa bila mahusiano ndio maana ukiachana naye leo utasikia wiki ijayo kapata mpenzi mpya.
sasa ukisikia mwanamke anakwambaia kwamba anatake break kwa muda basi hana uhakika kama yuko tayari kuachana na wewe hivyo anaenda kujaribu mahusiano mapya na kwasababu wewe utakua sio mpenzi wake kipindi hicho basi utakua huna uwezo wa kumuuliza chochote.
mabadiliko ya muonekano wake: mara nyingi mkizoeana sana kwenye mahusiano mnakua hamtumii muda mwingi kutaka kuonyeshana mionekano yenu.
mara nyingi mwanamke akipata mwanaume mpya anaweza akaanza kuvaa nguo za ndani ambazo sio za kawaida yaani zile zinazomuonyesha vizuri, hata uvaaji wake  wa nje unaweza kubadilika sana ili kumuonyesha huyo mwanaume mpya.
anakukwepa wewe na jamaa zako;  mara nyingi anakua hataki tena kutumia muda mwingi akiwa na wewe, huenda alikua anakupigia simu mara kwa mara ili muonane lakini siku hizi anakwambia ukae tu na marafikiki zako lakini pia kama ulikua umemtambulisha kwa ndugu zako na rafiki zako atakua anawakwepa kwasababu ya mambo anayoyafanya na anajua nyinyi hamuendi popote ili siku mkiachana hao watu wasimsumbue.
anakwepa macho yako; macho ni kioo cha roho ya binadamu, mtu akishindwa kukuangalia usoni basi kuna siri anaificha na anajiona msaliti kwa kinachoendelea.
hawezi kukuambia kwamba anakupenda; kwenye hatua za mwisho kabisa neno "nakupenda" anashindwa kulitamka kwa amani kwani hamaanishi tofauti na mwanzo ambapo alikua anakukumbusha mara kwa mara jinsi gani anakupenda.
mwisho; mwanamke akishaanza kukusaliti hakuna unachoweza kufanya kumrudisha, ukiona dalili hizi basi jiandae kisaikolojia kwa ajili ya maumivu ya kuachana, inaweza kua ngumu kukubaliana na ukweli lakini kuachana naye ni suluhisho ambalo hutalijutia baadae.

                                                       STAY ALIVE

                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO.
                                              0653095635/0769846183

gggg

hhhh

HUU NDIO UMRI SAHIHI WA MWANAMKE KUBEBA MIMBA.[UTAFITI]

Shukrani kwa njia za uzazi wa mpango siku hizi wanawake wanaweza kuamua wakae muda gani kabla ya kuamua kuzaa.
                                                                         
kusubiri muda sahihi wa kuzaa ni vizuri kiuchumi na kisaikolojia  lakini kuna madhara yake kwani uwezo wa kubeba mimba huendelea kupungua kadri mwanamke anavyozidi kua mkubwa.
hivyo wakati mwingine kama kweli unahitaji mtoto maishani mwako na huoni uwezekano wa kumpata mume wa kukuoa na umri unazidi kwenda ni vema kufanya maamuzi magumu  ya kuzaa hata kama hiyo ndoa haijaja.
kukosa mme maishani ni kawaida lakini kukosa watoto inaweza kuleta msongo mkubwa wa mawazo maishani na kukufanya uzeeke peke yako nyumbani.

kuzaa kipindi cha miaka 20
hichi ni kipindi cha kilele cha mwanamke kubeba mimba ambacho wanawake wanakua na uwezo mkubwa sana wa kubeba mimba hasa kwanzia miaka 18 mpaka 25, ni kipindi ambacho tunasema kizazi kinakua na sumaku kwani ukigusa tu ni mimba.
kipindi hiki mwanamke anakua na mayai mengi sana na sio rahisi kupata matatizo ya uzazi kama kifafa cha mimba, kushindwa kuzaa kawaida au kisukari cha mimba na mengine mengi.
lakini pia mwanamke anakua bado mwili wake unaweza kuchoma mafuta kwa kasi sana kiasi kwamba hata akizaa huweza kupungua mwili ndani ya muda mfupi wakati mwingine bila hata mazoezi wa diet yoyote.
ukichunguza wanawake waliozaa wakiwa bado wadogo sana utagundua wengi wao hawakunenepeshwa na uzazi na tafiti zinaonyesha kwamba watoto bora kabisa huzaliwa kipindi hiki,

kuzaa kipindi cha miaka 30
uwezo wa mwanamke kuzaa huanza kupungua akifikisha miaka 32, akifikisha miaka 35 uwezo wa kuzaa unazidi kupungua kwa kasi sana.
wanawake huzaliwa na zaidi ya mayai milion moja lakini kipindi hiki mwanamke hukadiriwa kubakisha mayai 25000 tu ambayo yanakua yamepungua ubora.
hivyo uwezekano wa kubeba mimba akishiriki tendo la ndoa kwa miezi mitatu mfululizo ni kama asilimia 12 tu.
matatizo wakati wa kujifungua na kuzaa watoto wenye matatizo mbalimbali huongezeka mwanamke akifikisha miaka 35.
kwa nchi zilizoendelea watu wa umri huu wakibeba mimba, vipimo vingi hufanyika na kama mtoto akikutwa ana tatizo basi mama hushauriwa kutoa mimba.
vifafa vya mimba, mimba kuharibika, kuzaa kwa upasuaji, mtoto kufia tumboni, kisukari cha mimba na matatizo mengine mengi hutokea wakati huu.
matatizo mengine ya kuzaa kipindi hiki ni kunenepa sana kwani uwezo wa mwili kuchoma mafuta unakua umepungua sana.

kuzaa kipindi cha miaka 40.
kipindi hiki uwezo wa mwanamke kuzaa ni kama asilimia saba tu, matatizo ya uzazi kama kuzaa mtoto aliyekufa, uzito mdogo, kifafa cha mimba, mtoto ambaye ana matatizo ya kiakili au kimwili, kisukari na kifafa cha mimba huongezeka sana.
kwa nchi za afrika ambapo teknolojia ni ndogo sana huu sio muda sahihi wa kuzaa lakini kwa nchi ambazo zimeendelea sana wanaweza kupambana na matatizo yatakayojitokeza.
kama ilivyo kipindi cha miaka 30, kipindi hiki wanawake hunenepa zaidi na zaidi wakizaa.

mwisho;
kibailojia akimaliza uzazi akiwa na miaka 25 anakua amefanya jambo la msingi sana  lakini kulingana na mabadiliko ya hali ya maisha na uchumi ni vizuri kumaliza uzazi ukiwa na miaka 30.
unaweza kwenda zaidi mpaka miaka 35 lakini matatizo yapo mengi kama nilivyoainisha.

                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                              0653095635/0769846183