data:post.body HIZI NDIO NJIA KUMI ZA KUISHI NA UGONJWA WA PRESHA BILA KUTUMIA DAWA. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HIZI NDIO NJIA KUMI ZA KUISHI NA UGONJWA WA PRESHA BILA KUTUMIA DAWA.

Wagonjwa wengi na baadhi ya madaktari huamini kwamba unapokutwa na ugonjwa wa shinikizo la damu au presha kitu cha kwanza ni kumeza dawa kisha mengine yatafuata, kitu ambacho sio kweli.
Mfumo wa maisha una mchango mkubwa sana kwenye tatizo la ugonjwa wa presha kuliko hata kumeza dawa.
                                                                           

ukiweza kuishi aina fulani ya maisha baada ya kuugua presha, basi unaweza usitumie dawa kabisa au ukachelewa kuanza dawa, cha msingi uwe na kipimo cha presha nyumbani kwako ili kila siku uhakikishe kweli presha iko sawa.
yafuatayo ni mambo muhimu ambayo unaweza kufanya na ukaishi bila kutumia dawa.
punguza uzito; kuongezeka kwa uzito hua kunaenda sambamba na kuongezeka kwa presha, tafiti zinaonyesha kwamba kila kilo unayopunguza inapungua na mmhg moja ya presha.
lakini sio uzito tu, angalia kiuno chako, hakikisha kiuno chako kinakua kwenye ukubwa sahihi kulingana na vipimo vya afya.
wanaume wana hatari ukubwa, kiuno kikizidi sentimita 102 na wanawake wana hatari ukubwa wa kiuno ukizidi sentimita 89.
fanya mazoezi mara kwa mara; kufanya mazoezi angalau nusu saa kwa siku tano za wiki itakuunguzia presha ya damu kwa kiasi kikubwa sana.
ni vizuri kua mvumilivu na kufuata ratiba yako kwa makini kwani kuacha mazoezi kutairudisha presha pale ilipokua mwanzo.
mazoezi kama kukimbia, kutembea na kuruka kamba ni muhimu sana kwa wagonjwa hawa.
kula vizuri; ulaji wa vyakula bora vya kiafya unaweza kupunguza presha kwa mpaka kwa 10mmhg.
hakikisha unakula mtunda, mboga za majani, vyakula asilia ambavyo havijakaangwa na mafuta mengi bila kusahau kupunguza au kuacha kabisa kula nyama nyekundu na maziwa yake.
punguza ulaji wa chumvi; kula chumvi kwa kiasi kidogo sana kunaweza kukupunguzia presha kwa 5 mpaka 6 mmhg kama presha yako iko juu.
epuka vyakula vya kusindikwa na kukaanga ambavyo huhifadhiwa kwa chumvi nyingi, epuka vyakula vya mahotelini ambavyo navyo hupikwa na chumvi nyingi.
pika vyakula nyumbani na uweke kiasi kidogo sana cha chumvi na kama huwezi tafuta chumvi maalumu kwa wagonjwa wa presha ambazo zinapatikana kwenye maduka ya madawa na supermarket.
punguza unywaji wa pombe; pombe inaweza kukupunguzia presha au kukuongezea presha kulingana na unywaji wako mwenyewe.
bia mbili kwa siku kwa mwanaume na moja kwa wanawake zenye kiwango cha kawaida cha ulevi au alcohol au mvinyo glasi moja kwa siku inaweza kua na faida sana na kupunguza presha.
lakini unywaji wa pombe mkubwa kupitiliza hapo unafanya presha ipande lakini pia huzuia dawa za presha kufanya kazi vizuri.
acha sigara; ukivuta sigara presha yako ya damu inaongezeka saa chache tu unapoanza kuvuta, na ukiacha kuvuta presha yako inashuka ndani ya muda mchache.
watu wanaoacha sigara huweza kuishi miaka mingi na kujizuia kuugua magonjwa ya moyo ukilinganisha na watu ambao hushindwa kuacha sigara.
achana na kawaha; kahawa ni kinywaji ambacho bado watafiti wanaamini kwamba kinaongeza presha ya damu, japokua inasemekana presha hiyo hupanda zaidi kwa watu ambao wanakunywa mara moja moja kuliko wanaokunywa kila siku.
lakini kama wewe ni mgonjwa wa presha, jaribu kunywa kikombe cha kahawa kisha pima presha baada ya nusu saa.
kama presha inapanda achana na kahawa.
epuka msongo wa mawazo; ni kweli kila binadamu ana msongo mkubwa wa mawazo hasa kwenye mambo ya mahusiano, fedha, kazi na familia.
kuwaza sana hakuwezi kubadilisha kabisa hali yako ya kifedha, kitu unachoweza kufanya ni kukubali kwamba changamoto za maisha ni kawaida na kukubaliana nazo.
ongeza juhudi kupambana na yale unayoweza kupambana nayo, yale usioyaweza achana nayo.
fuatilia presha yako; kama una uwezo nunua kipimo ukae nacho ndani, kama huna uwezo angalau uwe unapima mara mbili au mara tatu kwa wiki kwenye kituo chochote cha afya.
haya mambo niliyotaja hapo juu yakianza kufanya kazi presha itaanza kushuka sana hivyo ni vizuri kumuona daktari ili akupunguzie dozi au aukuahishe dawa kabisa chini ya uangalizi maalumu.
pata sapoti; hakikisha ndugu zako au watu wako wa karibu wana kukumbusha mambo yote muhimu ambayo yanahusika kama mazoezi, chakula na kadhalika.
kama hupati sapoti hii basi tafuta wagonjwa wa presha wakupe moyo na kukusaidia jinsi ya kumbana na hali hii.

                                                                    STAY ALIVE
                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                           
                                                          0653095635/0769846183

   



0 maoni:

Chapisha Maoni