data:post.body Desemba 2018 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

JINSI YA KUONDOA KITU KILICHOKWAMA PUANI KWA MTOTO UKIWA NYUMBANI.

Mara nyingi watoto wadogo hua na tabia ya kujiingizia vitu puani wakati wa michezo, hii huleta taharuki sana kwa mama au walezi wa mtoto yule na kuwafanya waaache shughuli zao kukimbilia hospitali, kwa watu wazima hua ni bahati mbaya.

mara nyingi vitu ambavyo vinaingia kwenye pua la mtoto ni mbegu kama za maharage, njegere, au vyuma na plastiki za mduara mdogo.
mara nyingi sana pua moja ndio linaathirika kwani mtoto mwenyewe akishagundua hicho kitu hakitoki anaanza kulia au anabadilika ghafla.
dalili ni kama kupiga chafya sana. kutoka na kamasi nyingi au damu kidogo.

matibabu ya nyumbani.
hakikisha unakiona kitu kilichoingia, kama ni kitu chenye ncha kali basi hicho hakifai kutolewa nyumbani lakini kama sio kitu chenye ncha kali basi nunua kalamu yenye mrija, ondoa mrija wa ndani ubakize bomba.
sasa chukua bomba ingiza kidogo na upulize kwa nguvu kwenye lile pua ambalo halijaingiliwa na kitu, puliza kwa nguvu hata mara nne au mara tano.
inategemea na umbali kilipofika, ila kama kiko mwanzoni kitatoka mara moja na kama kipo juu kidogo kitakua kinashuka kila ukipuliza.
kwa mtu mzima anaweza kuziba pua zima na kupenga kamasi tu na kitu kikatoka lakini watoto hua hawawezi.
onyo; kama kitu kimeingia afu hakionekani usijaribu njia hii, nenda hospitali.

matibabu ya hospitali
kule kuna vifaa maalumu vya kuondoa vitu kama hivyo, mgonjwa atatolewa bila kumpa hata dawa ya usingizi.

jinsi ya kuzuia
kwa mtoto anayetambaa muweke mbali na kitu chochote ambacho unakiona kinaweza kupita puani kwake.
hata kama amefika umri wa kutembea muonye kutoweka kitu chochote mdomoni au puani ambacho sio chakula.

                                                                      STAY ALIVE

                                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                            0653095635/0769846183

FAHAMU CHANZO CHA KUOZA MENO NA MATIBABU YAKE.[DENTAL CARIES]

Kuoza meno ni nini?
hili ni tatizo ambalo husababishwa na bacteria kujificha ndani ya sehemu za meno kisha kumwaga tindikali ambayo huenda kuondoa madini ambayo yapo kwenye meno na kufanya meno kuanza kupungua ukubwa na kutoboka.
kitaalamu bacteria ambao wanaishi kwa kula sukari au wanga mdomoni ndio hutengeneza tindikali ambayo huharibu meno.
mdomoni mwa binadamu kuna kiwango cha tindikali{pH] kwanzia 6.2 mpaka 7 ambayo huongezeka pale mtu anapoanza kutumia sukari, soda, biskuti, chocolate au vyakula vya wanga kwani bacteria huanza kazi ya kutengeneza tindikali kila unapokula milo hiyo.
kiwango cha tindikali kikiwa kingi sana mdomoni basi tindikali huanza kutoboa matundu kwenye meno na hapo ndio chanzo cha meno kuanza kuharibika.
kama tatizo hili lisipowahiwa basi jino litashambuliwa mpaka kwenye mzizi na kitakacho baki itakua kuling'oa tu.

watu gani wako kwenye hatari ya kuharibika meno?
  • ulaji wa vyakula vya wanga
  • ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi.
  • kutopiga mswaki kwa wakati.
  • kurithi kwa wazazi.
dalili za ugonjwa huu ni kama ifuatavyo...

  • hatua ya kwanza ya ugonjwa; meno yanakua yametoboka kidogo sana na hapa hua hakuna dalili kabisa ambayo mgonjwa ataisikia.
  • hatua ya pili ya ugonjwa; hapa meno yanakua yametoboka zaidi na mgonjwa huanza kusikia dalili za maumivu kwa mbali sana hasa akila vyakula vyenye sukari sana.
  • hatua ya tatu ya ugonjwa; meno yanatoboka zaidi na kipindi hiki maumivu hua makali mgonjwa akila chakula cha moto sana au cha baridi sana.
  • hatua  ya nne ya ugonjwa;  jino kwa sasa limetoboka sana na maumivu hua ni makali mno kiasi kwamba ikifika usiku mtu hawezi kulala na hata akimeza dawa za maumivu hizi ndogo ndogo bado maumivu hayaishi.
  • hatua ya tano ya ugonjwa; hii ni hatua ambayo jino limekua limechimbika sana na kuleta jipu sehemu ya eneo la jino, maumivu ni makali sana na homa huwa juu.
matibabu

matibabu ya meno hutegemea sana hatua ya kuharibika ambayo meno yamefikia kama ifuatavyo.
hatua ya kwanza na ya pili; haihitaji matibabu lakini mgonjwa anashauriwa kuacha kutumia vyakula vyenye sukari na wanga sana kisha hushauriwa kupiga mswaki kila baada ya mlo ili kuonoda mabaki ya vyakula mdomoni.
hatua ya tatu; hii ni hatua ambayo jino limetoboka na na maumivu yanakua makali kwa kunywa maji ya baridi ya ya moto sana.
huu ni muda muafaka wa kuziba jino hili.
hatua ya nne; hii ni hatua ambayo maumivu ni makali sana hasa usiku na mgonjwa kushindwa kulala kitaalamu kama pulpitis.
matibabu pekee ni kuondoa sehemu ya ndani ya jino iliyoharibika kisha kuijaza kitaalamu kama root canal, lakini sababu sehemu nyingi hawafanyi matibabu haya ya root canal wengi huishia kung'olewa jino.
hatua ya tano; hii ni hatua ambayo mtu anapata jipu la kwenye jino, matibabu yanayohusika hapa ni kuliodoa jino na kufanya upasuaji mdogo kuondoa usaa.

jinsi ya kuzuia kuharibika kwa meno.

  • punguza ulaji wa sukari na vyakula vya wanga.
  • piga mwaki kila baada ya mlo.
  • muone daktari wa meno akuchunguze angalau mara nne kwa mwaka.

                                                  STAY ALIVE


                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                  0753095635/0769846183


,

HIZI NDIO NJIA KUMI ZA KUISHI NA UGONJWA WA PRESHA BILA KUTUMIA DAWA.

Wagonjwa wengi na baadhi ya madaktari huamini kwamba unapokutwa na ugonjwa wa shinikizo la damu au presha kitu cha kwanza ni kumeza dawa kisha mengine yatafuata, kitu ambacho sio kweli.
Mfumo wa maisha una mchango mkubwa sana kwenye tatizo la ugonjwa wa presha kuliko hata kumeza dawa.
                                                                           

ukiweza kuishi aina fulani ya maisha baada ya kuugua presha, basi unaweza usitumie dawa kabisa au ukachelewa kuanza dawa, cha msingi uwe na kipimo cha presha nyumbani kwako ili kila siku uhakikishe kweli presha iko sawa.
yafuatayo ni mambo muhimu ambayo unaweza kufanya na ukaishi bila kutumia dawa.
punguza uzito; kuongezeka kwa uzito hua kunaenda sambamba na kuongezeka kwa presha, tafiti zinaonyesha kwamba kila kilo unayopunguza inapungua na mmhg moja ya presha.
lakini sio uzito tu, angalia kiuno chako, hakikisha kiuno chako kinakua kwenye ukubwa sahihi kulingana na vipimo vya afya.
wanaume wana hatari ukubwa, kiuno kikizidi sentimita 102 na wanawake wana hatari ukubwa wa kiuno ukizidi sentimita 89.
fanya mazoezi mara kwa mara; kufanya mazoezi angalau nusu saa kwa siku tano za wiki itakuunguzia presha ya damu kwa kiasi kikubwa sana.
ni vizuri kua mvumilivu na kufuata ratiba yako kwa makini kwani kuacha mazoezi kutairudisha presha pale ilipokua mwanzo.
mazoezi kama kukimbia, kutembea na kuruka kamba ni muhimu sana kwa wagonjwa hawa.
kula vizuri; ulaji wa vyakula bora vya kiafya unaweza kupunguza presha kwa mpaka kwa 10mmhg.
hakikisha unakula mtunda, mboga za majani, vyakula asilia ambavyo havijakaangwa na mafuta mengi bila kusahau kupunguza au kuacha kabisa kula nyama nyekundu na maziwa yake.
punguza ulaji wa chumvi; kula chumvi kwa kiasi kidogo sana kunaweza kukupunguzia presha kwa 5 mpaka 6 mmhg kama presha yako iko juu.
epuka vyakula vya kusindikwa na kukaanga ambavyo huhifadhiwa kwa chumvi nyingi, epuka vyakula vya mahotelini ambavyo navyo hupikwa na chumvi nyingi.
pika vyakula nyumbani na uweke kiasi kidogo sana cha chumvi na kama huwezi tafuta chumvi maalumu kwa wagonjwa wa presha ambazo zinapatikana kwenye maduka ya madawa na supermarket.
punguza unywaji wa pombe; pombe inaweza kukupunguzia presha au kukuongezea presha kulingana na unywaji wako mwenyewe.
bia mbili kwa siku kwa mwanaume na moja kwa wanawake zenye kiwango cha kawaida cha ulevi au alcohol au mvinyo glasi moja kwa siku inaweza kua na faida sana na kupunguza presha.
lakini unywaji wa pombe mkubwa kupitiliza hapo unafanya presha ipande lakini pia huzuia dawa za presha kufanya kazi vizuri.
acha sigara; ukivuta sigara presha yako ya damu inaongezeka saa chache tu unapoanza kuvuta, na ukiacha kuvuta presha yako inashuka ndani ya muda mchache.
watu wanaoacha sigara huweza kuishi miaka mingi na kujizuia kuugua magonjwa ya moyo ukilinganisha na watu ambao hushindwa kuacha sigara.
achana na kawaha; kahawa ni kinywaji ambacho bado watafiti wanaamini kwamba kinaongeza presha ya damu, japokua inasemekana presha hiyo hupanda zaidi kwa watu ambao wanakunywa mara moja moja kuliko wanaokunywa kila siku.
lakini kama wewe ni mgonjwa wa presha, jaribu kunywa kikombe cha kahawa kisha pima presha baada ya nusu saa.
kama presha inapanda achana na kahawa.
epuka msongo wa mawazo; ni kweli kila binadamu ana msongo mkubwa wa mawazo hasa kwenye mambo ya mahusiano, fedha, kazi na familia.
kuwaza sana hakuwezi kubadilisha kabisa hali yako ya kifedha, kitu unachoweza kufanya ni kukubali kwamba changamoto za maisha ni kawaida na kukubaliana nazo.
ongeza juhudi kupambana na yale unayoweza kupambana nayo, yale usioyaweza achana nayo.
fuatilia presha yako; kama una uwezo nunua kipimo ukae nacho ndani, kama huna uwezo angalau uwe unapima mara mbili au mara tatu kwa wiki kwenye kituo chochote cha afya.
haya mambo niliyotaja hapo juu yakianza kufanya kazi presha itaanza kushuka sana hivyo ni vizuri kumuona daktari ili akupunguzie dozi au aukuahishe dawa kabisa chini ya uangalizi maalumu.
pata sapoti; hakikisha ndugu zako au watu wako wa karibu wana kukumbusha mambo yote muhimu ambayo yanahusika kama mazoezi, chakula na kadhalika.
kama hupati sapoti hii basi tafuta wagonjwa wa presha wakupe moyo na kukusaidia jinsi ya kumbana na hali hii.

                                                                    STAY ALIVE
                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                           
                                                          0653095635/0769846183

   



KWA MARA YA KWANZA MWANAMKE ALIYEWEKEWA KIZAZI CHA MAMA ALIYEFARIKI AJIFUNGUA

Huko nchini brazili katikati ya jiji la sao paul yametokea maajabu makubwa katika mapinduzi ya  sayansi kwa mara ya kwanza kabisa duniani.
                                                                   
katika majaribio 39 ambayo yameshawahi kufanyika ya kuchukua vizazi vya wanawake walioko hai na kuvipandikiza kwa wanawake wengine ambao wana matatizo ya uzazi, ni watoto 11 tu ambao walipatikana huku wengine 28 waliowekewa vizazi wakishindwa kabisa kupata watoto kwa mimba kushindwa kuingia kabisa au mimba kuharibika.
lakini pia kumekua na utafiti ambao wanawake 10 waliwekewa vizazi vya watu ambao ni wafu lakini wote hawakufanikiwa kupata watoto.
leo hii huko nchini brazili mtoto wa kwanza amezaliwa baada ya kizazi cha mwanamke ambaye alikua amefariki kupandikizwa kwa mwanamke mwingine.

kazi ilifanyika vipi?
mama mmoja mwenye umri wa miaka 40 ambaye alikua na watoto watatu alifariki baada ya kuvuja damu kwenye ubongo wake, ndani ya muda mfupi viungo vyake ikiwemo mfuko wa uzazi vilihifadhiwa,
mwanamke ambaye alizaliwa na tatizo la kizazi chake kushindwa kuumbika vizuri tangu utotoni alifanyiwa upasuaji na kuwekewa kizazi hichi cha mama mfu.
baadae mayai  ya mwanamke huyu mzima yalichukuliwa na kuchanganywa na mbegu za mme wake huko maabara kisha kuhifadhiwa vizuri.
baada ya wiki sita mwanamke huyu alianza kupata hedhi kama kawaida na alipofika wiki ya saba yai lake ambalo lilihifadhiwa, likiwa limeritubishwa tayari liliwekwa ndani ya kizazi chake.

matokeo
baada ya miezi tisa ya mimba kama kawaida, mtoto wa kike mwenye kilo mbili na nusu alizaliwa kwa upasuaji akiwa hai.
haya ni maendeleo mkubwa sana kwani katika viungo ambavyo ni ngumu kupata ni kizazi hasa kutoka kwa watu ambao wako hai.

                                                                 STAY ALIVE
                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                          
                                                    O769846183/0653095635

HAWA NDIO MAPACHA WASIOWEZA KUAMBUKIZWA UKIMWI, WANAOTENGENEZWA CHINA.

CRISPR ni nini?
hili ni neno la kibailogia linalomaanisha uwezo wa kubadili vinasasaba au gene ya viumbe hai vya aina yoyote kwa ajili ya lengo fulani la faida za kimaisha.
                                                                     
CRISPR iligunduliwa nchini marekani mwaka 2012 na mtaalamu wa bailojia profesa Jennifer Doudna ambaye alikua akifanya tafiti ya jinsi ambavyo bacteria wanaweza kujikinga na kushambukiwa na virusi.

nini kimetokea china?
Baada ya wataalamu hawa kuitangaza teknolojia hii, nchi nyingi duniani zimekua zikiitumia teknolojia hii kubadili vinasasaba vya wanyama na mimea mbalimbali kwa ajili ya kupata ubora mkubwa zaidi kuliko ule wa mwanzo.
Sasa huko nchini china wataalamu kwa mara ya kwanza wamefanya kitu hicho kwa mapacha ambao bado hawajazaliwa.

mtaalamu huyo kutoka china ameondoa vinasasaba kwa jina la CCR5 ambavyo hutumika na virusi vya ukimwi kama njia ya kuingia kwenye seli nyeupe za damu na kuushambulia mwili.
Kwa maana nyingine hata virusi vikiingia ndani ya mtu, vitashindwa kuingia ndani ya seli za damu kwa ajili ya kuushambulia mwili hivyo baada ya muda vitakufa kwa kukosa virutubisho.
hivyo tunategenegemea kwa mara ya kwanza kabisa kuzaliwa kwa binadamu ambao hawawezi kupata ukimwi kwa njia yeyote ile.
mpaka sasa hivi kuna wazazi zaidi wameshajitolea kubeba mimba kwajili ya utafiti huu.

kwanini dunia inampinga?
wataalamu mbalimbali duniani wamepinga sana teknolojia hii kutumika kwa binadamu kwani inaenda kinyume na makubaliano ya umoja wa mataifa ambayo hayaruhusu vinasasaba vya binadamu kuchezewa kwa aina yeyeote ile ili kutunza kizazi cha binadamu halisi.
Dunia ina hofu kwamba yeknolojia hii itaondoa usawa wa kibinadamu.
watu watakua wana uwezo wa kuamua kuzaa mtoto wa urefu wanaotaka, mwili wanaotaka, na rangi wanayotaka.
Mwisho wa siku hata magonjwa ya aina fulani yatakua hayawahusu binadamu wengine.
Hii italeta aina mpya ya binadamu ambao hawajawahi kutokea na wengine watatumika vitani kama silaha kwa nchi zilizoendelea.
Teknolojia hii italeta watu wakubwa au giants ambao siku za usoni wanaweza wakatubadilikia wakaangamiza vizazi halisi vya binadamu.
Historia ya dunia kibiblia inaonyesha kwamba waliwahi kutokea binadamu wakubwa sana ambao walileta shida sana duniani lakini baadae waliangamizwa wakati wa nuhu na inasemekana mpaka leo kuna mabaki ya binadamu waliowahi kua wakubwa sana.

                                
nini faida ya teknolojia hii?
Teknolojia hii ikitumika vizuri inaweza kuondoa magonjwa yote ya kurithi kwenye ukoo, magonjwa ya saratani, kuzuia unene, na magonjwa yote ambaukizi ambayo yamekosa dawa, kwani wanasayansi watakua na uwezo wa kutengeneza binadamu imara yaani kama ku update version za binadamu mpya.
tatizo ni kwamba, teknolojia hii haitaweza kudhibitiwa na itaweza kuleta maafa makubwa duniani au kuleta magonjwa mapya ambayo yalikua yanazuiliwa na vinasasaba ambavyo tunaviondoa sasa hivi.


                                                                STAY ALIVE 

                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0653095635/0769846183