data:post.body Novemba 2018 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

HIZI NDIO SABABU ZINAZOPELEKEA MWANAUME KUA SHOGA.

Swala la ushoga limeleta mijadiliano mikali sana kwenye nchi mbalimbali huku nchi zingine zikiwaunga mkono mashoga, wakati huo huo nchi zenye misimamo mikali ya kidini zikiwapa adhabu kali za vifungo vya gerezani.
                                                                 
mashoga hupingwa sana na dini mbalimbali za kikikristo na kiislam, dini hizo zikidai kwamba wanachokifanya ni chukizo mbele za mungu na wataishia motoni.
lakini pia mashoga hupingwa sana na kwenye nchi za afrika ambazo zina maadili yao amabyao hayaamini kwenye ushoga tofauti na nchi zilizoendelea ambazo ubaguzi wa mashoga hauna nguvu sana.
baadhi ya nchi zilizoendelea mashoga ni kundi maaalumu ambalo hupewa vipaumbele hata kwenye ufadhili wa kusoma vyuo vikuu.

msimamo wa kitaalamu kuhusu mashoga ukoje?
kitengo cha madaktari wa akili huko nchini marekani kinachofahamika kama THE AMERICAN PSYCHIATRIC  ASSOCIATION ilikua ikiwatambua mashoga wote au watu wote wenye mahusiano na jinsia moja kama wagonjwa wa akili.
lakini mwaka 1970 kitengo hichi kiliacha kuwatambua watu hawa kama wagonjwa wa akili sababu waliweza kuendelea na shughuli zao za kikazi kama kawaida kama watu wengine bila msaada wowote hivyo waliona hakuna haja ya kuwatambua watu hawa kama wagonjwa wa akili.
lakini bado swali linakuja, je kwanini mtu anaamua kua shoga? tafiti mbalimbali zilizofanyika zilikuja na majibu yafuatayo.
Genetics; mwaka 1990 utafiti ulifanyika na ambao ulikuja na majibu kwamba chromosome X ambayo inatoka kwa mama kwenda kwa mtoto wa kiume hua inakua imebeba vinasasaba tofauti tofauti ambavyo vinaweza kumfanya mtoto huyu wa kiume akawa shoga.
tafiti hii iligundua kuwepo kwa vinasasaba hivi kwenye asilimia hamsini mpaka sitini ya mashoga waliofanyiwa utafiti.
sababu kibailojia;  tafiti zingingine mpya zinasema kwamba kuna mabadiliko ya homoni ambayo yanatokea kwenye mfuko wa uzazi wa mama kabla mtoto hajazaliwa.
mabadiliko haya huathiri ubongo wa mtoto kwa njia ambayo haijafahamika na kumfanya atoke akiwa na tabia hizi za kushiriki mapenzi ya jinsia moja.
kitaalamu mwanaume akiwa kwenye mfuko wa uzazi anakua na vinasasaba vya kiume yaani XY lakini anakua na maumbile ya kike mpaka wiki sita ambapo homoni za kiume huingilia kati na kuanza kumtengenezea maumbile ya kiume, lakini homoni hii ikipata shida kidogo mtu anaweza akatoka na maumbile ya kiume lakini hajakamikika.
ushahidi kwamba mwanaume alikuwa mwanamke kabla ni uwepo wa matiti kwa mwanaume ambayo hayana kazi, na kufanana sana kwa kazi kati ya kinembe na uume.
mazingira; baadhi ya tafiti zinaamini kwamba mazingira ambayo mtoto anakuziwa yanaweza kumfanya awe shoga.
yaani kutunzwa na mama muda mwingi na kua na baba mkali ambaye hana muda na mtoto, kuishi na dada zake tu bila kuwepo watoto wengine wa kiume, kuanza kuingiliwa kinyume na maumbile akiwa mtoto mdogo, kuona swala la ushoga kwenye TV na kulichukulia kawaida, kutokemewa kwa tabia za kishoga akiaanza kuzionyesha utotoni na  umaskini wa kipato.
lakini pia baadhi ya watu hua mashoga sababu ya kuiga mambo au kujaribu kila kitu ujanani.
kuna watu ambao ukiwaona mtaani hawana dalili hata moja ya ushoga kimuonekano lakini ni mashoga.
mfano ukiangalia soko la mitindo au modeling Tanzania lina watu wengi sana wa mapenzi ya  jinsia moja ambao kwa hali ya kawiada ni rahisi kujua kwamba hawa watu wanafanya mambo haya kama kwa kuigana au kulazimika kufanya hivyo sababu ya shida sio kwamba walizaliwa hivo.
lakini pia baadhi ya tafiti zilikuja kupinga hoja kwamba watoto waliozaliwa kwenye mazingira ya kishoga hua mashoga kwani kuna watu wengi ambao wamelelewa na wapenzi wa jinsia moja lakini wakakua na kutojihusisha na mambo hayo ya ushoga na pia kuna wazazi ambao wamezaa watoto mashoga japokua wao sio jinsia moja.
baadhi ya mashoga walihojiwa wanasema kwamba wao walizaliwa wa kiume japokua moyoni walijihisi wa kike.
walipambana sana ili wasiingie kwenye tabia hiyo ya jinsia moja kwa kutafuta wapenzi wa kike na hata kujaribu kushiriki tendo la ndoa na wanawake lakini hawakupata hisia zozote huko na baadae walaiamua kukubaliana na hali zao za jinsia moja.
mwisho; wataalamu wanaamini kwamba asilimia kubwa ya watu ambao ni mashoga hawakua vile kwa kuamua lakini kwa kuwepo kwa sababu mbalimbali za kibailojia, mabadiliko ya homoni, na mazingira waliyokulia.
japokua baadhi ya tabia za kishoga kwa baadhi ya mashoga zingeweza kuzuiliwa kwa kuzikemea tabia hizi, hasa zinazosababishwa na mazingira.

                                                               STAY ALIVE...

                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                  0769846183/0653095635

TAFITI MPYA:KUNYWA MAJI YA BARIDI SANA KUNASAIDIA KUPUNGUZA UZITO NA KITAMBI.

Ni wazi kwamba watu wengi sana wanafahamu kwamba kunywa maji ya uvuguvugu hasa wakati wa asubuhi kunasaidia sana kupunguza uzito kwa kuongeza joto la mwili na kuongeza kasi ya uchomaji wa mafuta mwilini.
                                                               
na hii njia imekua ikitumika kwa miaka mingi sana na baadhi ya watu wamekua wakiongeza na limao ili kupata matokeo zaidi.
lakini pia watu walikua wakiyaogopa maji ya baridi sana kwa kuamini kwamba yanagandisha mafuta tumboni na kuongeza kitambi.
lakini tafiti mpya hivi karibuni zimeonyesha tofauti na watu walivyokua wanafikiria mwanzo.

tafiti mpya zinasemaje?
maji ya baridi sana au yenye barafu kabisa yanasaidia kupunguza uzito zaidi kwani maji yakiingia tumboni yakiwa ya baridi sana, mwili unalazimika kutumia nguvu za ziada kuyachemsha yawe katika kiwango kinachohitajika na mwili kabla ya kuanza kuyatumia.
sio kwamba maji ya uvuguvugu hayasaidii tena lakini tafiti zinaonyesha maji ya baridi sana ni bora zaidi kuliko ya uvuguvugu.
lakini pia tafiti hizo zinaongeza kwamba sio kwenye kunywa tu lakini hata utafiti uliofanyika kwa watu wanao ogelea kwenye maji ya baridi sana huweza kupungua uzito haraka kutokana na njia hiyo hiyo.

nini cha kufanya?
hii ni habari njema hasa kwa watu ambao wanashi maeneo ya joto, kwani walikua wakilia sana kunywa maji ya uvuguvugu kipindi cha joto kali.
sasa hivi wanaweza kunywa maji ya baridi sana bila wasiwasi wa kuhisi kwamba watanenepa zaidi.

                                                                     STAY ALIVE

                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                          0769846183/0653095635  

HIZI NDIO NJIA ZINAZOTUMIKA KUBADILI JINSIA (TRANSGENDER)

Watu wengi duniani ambao ni wa jinsia fulani hua wanahisi kwamba walizaliwa na jinsia ile kimakosa hivyo wanatamani wangezaliwa na jinsia tofauti.
                                                     
           
Baadhi yao hukubaliana na hali yao lakini wengine huamua kuchukua hatua ya kujibadilisha jinsia ili wawe tofauti na mwanzo.
Inakadiriwa kwamba zaidi ya watu laki saba nchini marekani walibadilisha jinsia baada ya kutoridhika na jinsia zao za mwanzo.
Ukishabadilisha jinsia, unaruhusiwa kubadilisha jina na jinsia yako kwenye vyeti vyako vya kuzaliwa na vitambulisho vyako vyote.
zifuatazo ni hatua za kitaalamu zinazofuata kubadilisha jinsia.

hatua ya kwanza; kupimwa akili.
kabla ya kuanza hatua za kitatbibu za kubadilisha jinsia, madaktari bingwa wa mambo ya akili na saikolojia hukaa na mgonjwa ili kujua kweli kwamba ana tatizo la kisaikolojia ambalo linamfanya ahisi kwamba yeye hafai kua jinsia fulani.
kitaalamu ugonjwa huu unaitwa gender dysphoria.
baada ya hapo wataalamu hawa watakwambia hatua ambazo utapitia ili ubadilishe jinsia yaani kwanzia dawa mpaka upasuaji wa kubadilisha viungo vya uzazi.
watakwambia madhara yote ambayo huambatana na hatua utakazo pitia ili kufika huko lakini mwisho watahitaji kujua watu ambao watakua pamoja na wewe na kusapoti mabadiliko hayo kwani kila mtu akikupinga utaishi kwa shida sana.

hatua ya pili; matibabu ya homoni
homoni hizi ndio hatua ya kwanza kabisa ya kubadilisha maumbile ya mtu,  hubadilisha maumbile ya kike kua ya kiume au maumbile ya kiume kua ya kike.
wanawake ambao wanataka kua wanaume huanza kutumia homoni za kiume kitaalamu kama adrogens ambazo ndio huanza kuwabadilisha kua wanaume kwa kufanya yafuatayo.

  • huongeza misuli
  • kuleta sauti nzito
  • kuleta manyonya kwenye ngozi
  • kuongeza ukubwa wa kinembe.
wanaume ambao wanataka kubadilisha jinsia na kua wanaume hutumia homone za kike ambazo zinaweza kubadilisha maumbile yao yakawa ya kike mfano oestrogen.
dawa hizo 
  • hupunguza homoni za kiume aina ya testosterone mwilini.
  • hupunguza manyoya kwenye ngozi.
  • kuongeza matiti.
  • kugawanya mafuta ya mwili.
mabadiliko huanza mapema ndani ya mwezi mmoja na huweza kufika hatua ya mwisho kabisa ndani ya miaka mitano.
mfano mwanaume anayaetaka kua mwanaumke mpaka matiti yatokee  huchukua miaka mitatu mpaka mitano.
matumizi ya dawa hizi yana madhara mbalimbali kama magonjwa ya moyo, ugumba, damu kuganda, na kadhalika hivyo ni vizuri kufanya vipimo mbalimbali wakati wa kuanza dawa ilikuona kama mwili unaenda vizuri na dawa hizo.
wakati mwingine watumiaji wa dawa hupata msongo wa mawazo kutokana na kutokua na uhakika wa kitu ambacho wameamua hivyo ni vizuri kutembelea wataalamu wa ushauri.

hatua ya tatu; upasuaji
Hii ni hatua ya  mwisho kabisa wa kubadilisha baadhi ya viungo ambavyo haviwezi kubadilika kwa matumizi ya homoni tu.
Lakini asilimia sabini na tano ya watu ambao hujibadilisha jinsia zao hawapendi kufanya upasuaji kutokana na gharama kubwa sana pamoja na madhara ambayo hayawezi kubadilika baada ya kutoa maamuzi.
viungo kama matiti ya wanawake, uume kwa wanaume, korodani, kizazi na mirija ya uzazi ya kike huweza kuondolewa.
wanaume hufanyiwa upasuaji na kuwekewa uke lakini pia wanawake hufanyiwa upasuaji na kuwekewa uume.
upasuaji wa kuweka uke hua una matokeo mazuri lakini upasuaji wa kuweka uuume mpya kitaalamu kama phalloplasty hauna matokeo mazuri sana ndio maana wanawake wengi wanaotaka kua wanaume hawapendi kufanya upasuaji huo.

je unaweza kurudi kwenye jinsia yako ya zamani baada ya kubadilika?
baadhi ya watu waliojibadilisha jinsia hujutia maamuzi yao hivyo huamua kurudi kwenye jinsia zao za zamani.
mabadiliko ambayo yanafanywa na homoni mara nyingi yanaweza kurudi kama mwanzo iwapo ukiacha dawa japokua tafiti zinaonyesha kuna mabadiliko ambayo huletwa na homoni za kiume kwa wanawake yanaweza yasirudi kama mwanzo.
baadhi ya watu wamefanikiwa kurudi katika hali zao za zamani japo sio kwa asilimia mia moja.
Mabadiliko ya upasuaji hayawezi kurudi kama mwanzo.

                                                                
                                                          STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                             0769846183/0653095635