data:post.body VIPIMO FEKI VYA UKIMWI NI JANGA LA AFRIKA ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

VIPIMO FEKI VYA UKIMWI NI JANGA LA AFRIKA

Katika vita dhidi ya ukimwi hapa Afrika, kumekua na changamoto nyingi ikiwemo watu kupuuzia elimu ya kujikinga na ukimwi, kutokuwepo kwa dawa za kutosha za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi na watu kutojitokeza kabisa kupima ukimwi.
                                                                       

kulingana na muongozo wa shirika la afya duniani(WHO), mgonjwa hatakiwi kupewa majibu ya kua ameathirika na ukimwi mpaka apimwe na vipimo vya aina tofauti ambavyo vinahakikisha kweli ana maambukizi ya ukimwi.
shirika la doctor without borders(MSF) lilifanya utafiti  na kugundua kwamba vipimo havifanani nguvu hivyo kuleta makosa katika utoaji wa majibu na msisitizo mkubwa ukiwa katika watu ambao wanapewa majibu kwamba wameathirika wakati hawajaathirika kitaalamu kama false positive.
Ni kweli kuna baadhi ya watu ambao wanaweza kua na ukimwi vipimo vikaoneyesha hawana kitaalamu kama false negative lakini ni asilimia ndogo sana.

mtu kupewa majibu ya ukimwi kwamba ameathirika wakati hajaathirika huweza kuleta msongo mkubwa wa mawazo, maumivu ya kihisia na kuvunjika kwa mahusiano.

ushahidi wa hili ni upi?
Damu ilikusanywa kutoka kwa wagonjwa 2785 wa ukimwi ambao walikua wanahudhuria katika kliniki  mbalimbali za nchini kenya, uganda, congo, guinea na cameroon.
damu hiyo ilihifadhiwa vizuri na kutumwa ubeligiji kwa ajili ya vipimo vya ukimwi ili kuweza kuhakiki kama kweli wale watu ni wagonjwa wa ukimwi.
kati ya watu 2785 ambao damu zao zilichukuliwa, watu 1474 walikua hawana ukimwi na  watu 1306 pekee ndio walikua na virusi vya ukimwi kweli.
kwa maana nyingine hawa watu 1474 wamekua wakimeza dawa za ukimwi kwa muda wote huo kimakosa.

nchini Tanzania hali ikoje?
Hakuna tafiti kama hii iliyofanyika na kutangazwa rasmi nchini kwetu kuhusu hili lakini nitoe rai kwa wizara ya afya na wadau wengine wa afya kuliangalia swala hili kwa makini sana sababu kenya na uganda ni majirani zetu na sidhani kama teknolojia tunazotumia zimeachana mbali sana na teknolojia za kwao.
huenda na sisi tunatoa dawa kwa watu ambao sio wagonjwa.

                                                               STAY ALIVE
                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                       0769846183/0653095635

0 maoni:

Chapisha Maoni