data:post.body HIVI NDIO VYAKULA 5 MUHIMU ZAIDI KWA WAGONJWA WA SIKO SELI. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HIVI NDIO VYAKULA 5 MUHIMU ZAIDI KWA WAGONJWA WA SIKO SELI.

katika matibabu ya ugonjwa wa siko seli, mara nyingi nguvu nyingi zinawekwa kuhakikasha mgonjwa hapungukiwi na damu wala hapati maumivu makali ya mara kwa mara kwani hivyo ndio vyanzo vikuu vinavyosababisha vifo kwa wagonjwa hawa kwa kusababisha kufeli kwa baadhi ya viungo muhimu kama vigo, maini, mapafu na ubongo.
sasa kama wewe ni mama au baba una mgonjwa huyu ndani basi vyakula vifuatavyo visikose nyumbani kwako.
5.nyama nyekundu; nyama hii ina kiwango kikubwa sana cha madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa mgonjwa wa huyu kwa ajili ya kuongeza kiasi cha damu mwilini.
kimsingi nyama nyekundu ina madini ya chuma mengi zaidi kuliko nyama  ya samaki na kuku. ule weupe wa nyama ya kuku na samaki ni taarifa ya kiasi kidogo cha madini ya chuma kilichomo.
Sijasema asile kuku wala samaki lakini nyama nyekundu ya ngombe na mbuzi ni muhimu zaidi.
Hivyo hakikisha hakosi nyama nyekundu angalau mara mbili kwa wiki huku ukimchanganyia na samaki na kuku siku zingine.
                                                     

4.matembele; hii ni mboga ya majani inayopatikana sehemu mbalimbali nchini kwetu, mboga hii ina kijani nzito kuliko mboga nyingi..
ukijani huu unaonyesha wingi wa madini ya folic acid ndani yake. Mboga zote za rangi ya kijani kama mchicha, chinese, kisamvu zina madini haya lakini matembele ndio kiboko yao.
folic acid ni muhimu sana kwa mgonjwa huyu kwani huungana na madini ya chuma kutengeneza seli nyekundu za damu ambazo ni muhimu sana kwa mgonjwa lakini pia ni husaidia kupunguza kiasi cha lehemu au cholestrol kinachopatikana kwenye ulaji nyama nyekundu.
                                                   
3.machungwa; haya ni jamii ya matunda ambayo yana kiasi kikubwa sana cha vitamin C. kazi ya vitamin hii ni kuusaidia mwili kuchukua madini ya chuma ambayo yanapatikana kwenye nyama unayokula.Hivyo hata ukimpa mtoto nyama  nyingi kiasi gani bila matunda unapoteza muda tu.
lakini pia matunda haya yana kemikali kitaalamu kama ant oxidant ambazo ni kinga ya mwili hasa kuzuia madhara ya ambatanayo na ulaji wa nyama nyekundu kama saratani, magonjwa nyemelezi na magonjwa ya moyo.

2.dagaa; dagaa zina kiasi kikubwa sana cha madini ya kashiamu kuliko kiwango kinachopatikana kwenye samaki.
sababu kubwa ni kwamba ukila dagaa unakula na mifupa yake ambayo ina kashiumu nyingi sana kuliko ukila samaki kwani sio rahisi kula samaki na mifupa yake.
wagonjwa hawa wanahitaji kashium nyingi kwa ajili ya kuimarisha mifupa yao, kusaidia mishipa ya fahamu na husaidia kuganda kwa damu haraka pale unapopata kidonda lakini pia dagaa zina madini ya chuma na huweza kua mbadala kwa watu ambao kununua nyama ni ngumu kwao.
kumbuka, kuvuja damu kidogo tu kwa mgonjwa huyu ni hatari na huweza kuleta kifo.
                                                      
        
 1.maji ya kunywa; asilimia sabini ya mwili wa binadamu ni maji tu, ni bora mgonjwa wa siko seli ashinde na kulala njaa kuliko kushinda na kulala bila kunywa maji.
maji ni muhimu sana kwa wagonjwa hawa kwani husaidia kusambaza seli zake sehemu mbalimbali za mwili bila kukwama.
mgonjwa huyu akikosa maji ya kutosha, seli za damu hukwama kwenye mishipa ya damu na kuanzisha maumivu makali sana au sickle cell crisis.
hivyo mgonjwa huyu akishinda na kulala bila kunywa maji basi majibu yake utayaona hapohapo kuliko kushinda na kulala njaa kwani damu haiwezi kupungua ghafla.
                                                                           

5.mwisho; kama mzazi wa mgonjwa wa siko seli basi ni vizuri ukawekeza kwenye elimu kujifunza kuhusu wagonjwa hawa ili uwe na elimu ya kutosha na kuweza kuwasaidia.
mgonjwa huyu anaweza kuishi maisha marefu kama watu wengine na tafit zinaonyesha mwanaume anaweza kuishi mpaka miaka 60 wakati mwanamke anaweza kuishi miaka 68.


                                                              STAY ALIVE
                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                             0653095635/0769846183
                              







0 maoni:

Chapisha Maoni