Pesa ni muhimu sana kwenye maisha ya binadamu kwani ndio mfumo ambao umewekwa ili kuendesha shughuli zetu za kila siku na kila mtu ana wajibu wa kuzitafuta pesa hizi kwa bidii sana ili aweze kuishi maisha mazuri
lakini pesa hizi ukizitafuta bila kua makini basi utazipata pesa unazotaka lakini utakuwepo kitandani huwezi hata kuamka sababu ya afya yako kuharibiwa na shughuli zako.
yafuatayo ni mambo ambayo yanaweza kujaribu afya yako sababu ya utafutaji wa pesa.
kutopata usingizi wa kutosha; binadamu anatakiwa alale masaa saba mpaka nane kwa usiku lakini utasikia watafutaji wa pesa hawalali usiku na mchana wanafanya kazi, utakuta mtu mmoja ana kazi tatu kwa kisingizio cha kutafuta pesa.
hali hii huleta msongo wa mawazo, hatari ya magonjwa ya moyo, kushuka kinga ya mwili, kunenepa na kuongeza hatari ya ugonjwa wa kisukari.
hivyo, pamoja na kutafuta hela kumbuka usingizi ni muhimu.
kutokula vizuri na kwa wakati; mifumo mingi ya kazi inawafanya watu wengi wale chakula kile kile kila siku labda chipsi, ugali na wali bila matunda na mboga za majani za kutosha, lakini pia watu hawa wakati mwingine hula kwa kuchelewa sana au kula mlo mmoja kwa siku.
kuna watu hawali vizuri kwa kubana pesa ili waishi maisha mazuri baadae, naomba nikwambie kwamba maisha ni haya haya....bana pesa kwenye mambo yote lakini ukila vibaya au usipokula kwa wakati unaharibu afya.
magonjwa ya kutoabukiza kama kisukari, presha na moyo husababishwa na ulaji mbaya wa vyakula.
kutopumzika au likizo; watu waliweka kwamba binadamu anatakiwa apumzike baada ya kazi sio wajinga, wanafahamu madhara ya kufanya kazi mfulululizo bila kupumzika.
utakuta watu wanafanya kazi siku saba kwa wiki huku wakidai wanatafuta pesa lakini pia hakuna kipindi cha mwaka ambacho wanapumzika.
hata serikali imeweka likizo kwa wafanyakazi wake na ilo hua sio ombi ni lazima uende likizo kwani pamoja na kukujenga kiafya, likizo inaongeza uzalishaji wako kazini.
kutofanya uchunguzi wa afya; binadamu ana magonjwa mengi sana ambayo yanamsakama lakini watu wengi sana hawaendi kufanya uchunguzi wakidhani eti wanabana pesa na wengi wao huenda pale wakiwa wanaumwa tu bila kujua kwamba gharama za matibabu hua ni kubwa sana kuliko kutibiwa.
kuna magonjwa kama saratani, ambayo yasipoonekana mapema huwezi kupona hata uende wapi na hizo pesa unazozitafuta utaziacha.
Steve Jobs ambaye alikua anamiliki kampuni ya apple aligunduliwa na saratani ya koo lakini alipuuza upasuaji ambao madaktari walimshauri afanye.
mwisho wa siku alikua kitandani akijutia mambo aliyofanya kwenye maisha yake.
kutopata matibabu sahihi; moja ya watu ambao ni wagumu sana linapokuja swala la kulipia gharama za matibabu ni waafrika, sio lwamba wote hawana pesa lakini wako tayari kutoa ngombe kwa mganga wa kienyeji lakini sio sh 20000 hospitali.
katika mambo ambayo unatakiwa uyape kipaumbele basi ni swala lako la kiafya, hili halina mbadala.
ukikwepa unajikomoa mwenyewe, hizo pesa unazotafuta utazipata na kuzifurahia ukiwa na afya sio ukiwa mgonjwa, poteza pesa zote upone na utaanza upya.
kutofanya mazoezi; watu wengi huanza shughuli zao saa kumi na moja alfajiri na kurudi nyumbani saa tano au saa sita usiku.huku wakikwambia kwamba hawana muda na mazoezi.
naomba nikwambie kwamba kama hupati muda wa mazoezi basi magonjwa kama kisukari, moyo na presha yatapata muda na wewe. na shughuli zako zitakua zimeishia hapo.
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0653095635/0769846183
0 maoni:
Chapisha Maoni