data:post.body JINSI YA KUHESABU CALORIE ZA CHAKULA KUPUNGUZA UZITO AU KUONGEZA UZITO.. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

JINSI YA KUHESABU CALORIE ZA CHAKULA KUPUNGUZA UZITO AU KUONGEZA UZITO..

Kimsingi kuna njia nyingi sana za kupunguza au kuongeza uzito, kikubwa ni muhusika mwenyewe kukaa na kuangalia ni njia gani rahisi kwake kupungua uzito.
unaweza kupungua uzito kwa kufanya mazoezi au kupunguza ulaji wa chakula au unaweza ukatumia njia zote mbili kama unaweza.

calorie ni nini?
calorie ni nguvu ambayo inapatikana kwenye chakula tunachokula kila siku, ili binadamu akae kwenye uzito alonao sasa hivi inabidi calorie anazotumia kwa siku kwenye chakula zilingane na calorie ambazo anazitoa nje kwenye shughuli zake za kila siku.

unatumia vipi njia hii?
kwa hali ya kawaida binadamu asipofanya kazi yeyote ile kwa siku anapungua calorie 2000 ambazo zinatumika wakati wa kupumua, kukojoa,kumeng'enya chakula na shughuli zingine za ndani ya mwili.
 hivyo ukitaka uzito wako usipungue kula calorie 2000 kwa siku, ukitaka upungue kula calorie 1500 au 1000 kwa siku, ukitaka uongezeke kula zaidi calories 2000 kwa siku.
kila chakula ambacho tunakula kina idadi fulani ya calories ambazo zimo kwenye chakula husika ambazo zinaweza kuhesabika, hivyo unaweza ukaamua kwamba asubuhi ule calories kadhaa, mchana calories kadhaa na usiku calories kadhaa.

njia hii hupunguza uzito kiasi gani?
ukiweza kula calorie 1000 kwa siku utapungua kilo moja kwa wiki, ukiweza kula calories 1500 kwa siku utapungua nusu kilo kwa wiki.
inategemea na uwezo wako wa kuhimili chakula lakini kula calories 1500 kwa siku ni rahisi na unaweza kugawa calorie 500 kwa kila mlo.
njia hii haingalii umekula chakula usiku sana au mchana.

utajuaje chakula hichi kina calories kadhaa?
kila chakula limeandikwa calories zake mtandaoni kwa mfano chapati moja ina calories 110, chai ya rangi kama ukiweka vijiko vitatau vidogo ni calories 50.
hivyo ukila chapati mbili na chai asubuhi umekula calories 270.
kwa hesabu hizo ni kazi kwako kuangalia mara nyingi hua unakula chakula gani ili uweze kuhesabu calories zake na uweze kuhesabu.
zifuatazo ni idadi za calories kwenye vyakula vingi vya kiafrika.
  • maziwa kikombe kimoja-calories 50
  • yai-calories 90
  • kikombe cha wali uliopikwa-calories 200
  • ndizi mbivu-calories 105
  • chungwa-calories 62
  • ugali-calories 180
  • parachichi-calories 240
  • kiazi kitamu(saizi ya ngumi ya mtu mzima)-calories 280
  • slesi ya mkate-calories 53.
  • sambusa-calories 190
  • kuku mzima-calories 1430
  • nyama ya ngombe- calories 2500
  • nyama ya nguruwe-calories 2420
  • soda-calories 150
  • beer-calories 153 ( inategemea na ukubwa wa beer lakini nyingi zimeandikwa kwenye lebo ya  chupa husika, light beer hua zina calories kidogo zaidi) 
  • supu ya kawaida-theluthi ya kilo-312 calories
 huo ni mfano wa vyakula mbalimbali lakini kama una vyakula vingine unapendelea kula uaweza kuingia google ukapata calories zake kisha ukajumlisha kupata wingi unaotaka mwenyewe.

mwisho; kwa kutumia njia hii unaweza kuongezeka au kupunguza uzito bila kufanya mazoezi yeyote yale kama uko bize na mambo mbalimbali na ukifanya mazoezi utapungua zaidi kama unahitaji, kumbuka kama unajiona sasa hivi wewe ni mnene sana au mwembamba sana, tambua kwamba huo uzito haukupungua au kuongezeka kwa siku moja ila ilichukua muda mrefu sema wewe ulikua huoni hivyo hata kupungua au kuongezeka kunataka muda.
kama ukiongezeka nusu kilo kwa wiki ni kilo mbili kwa mwezi, kama ukipungua nusu kilo kwa wiki ni unapungua kilo mbili kwa wiki.

                                                                  STAY ALIVE

                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                              0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni