data:post.body JE BINADAMU ANAWEZA KUISHI MUDA GANI BILA KULA WA KUNYWA? ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

JE BINADAMU ANAWEZA KUISHI MUDA GANI BILA KULA WA KUNYWA?

Binadamu anahitaji maji na chakula iliaweze kuishi, 60% ya mwili wa binadamu ni maji matupu na vingine vilivyobaki ndio misuli, mafuta, mifupa na viungo mbalimbali.
kumekua na ubishani mwingi ni muda gani binadamu anaweza kuishi bila kula na kumekua na majibu ya tafiti mbalimbali kutoka kwa uzoefu wa watu walikofa sababu ya kutokula.
                                                                   

Mahatma Gadhi aliyekua mwanaharakati wa India wakati wa kudai uhuru aliwahi kukaa wiki tatu bila kula huku akinywa maji lakini hii haimaanishi kwamba yeye ndio kipimo sahihi cha watu wote.

ukweli ni upi?
tafiti nyingi zinaamini kwamba binadamu mwenye afya ya kawaida akipewa maji tu anaweza kuishi wiki nne mpaka nane bila kufa lakini pia binadamu ambaye ni mnene sana akipewa maji anaweza kuishi mpaka miezi 6 huku mwili wake ukichoma mafuta na kutumia kama chanzo cha nguvu.
lakini kwa jinsi watu wengi wasivyotarajia, binadamu akipewa chakula akanyimwa maji basi ana uwezo wa kuishi siku nne mpaka siku saba tu kwani maji ni muhimu sana kwa binadamu kuliko hata chakula.

kitu gani husababisha kifo mtu akikosa chakula?
binadamu akikosa chakula kwa muda fulani mwili huanza kutumia mafuta kutengeneza nguvu kwa ajili ya kutumia, baadae mafuta yakiisha mwili huanza kutumia misuli kutengeneza nguvu na hapa ndipo viungo maalumu kama moyo hushindwa kuendelea na kazi na kusimama.

                                                            STAY ALIVE
                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                           0769846183/0653095635

                                    
 
 

Maoni 3 :

 1. Tumeuliza anaweza kuishi siku ngapi bila Maji wa chakula
  Mnajibu vingine

  Nawewe Dokta pita Huku

  JibuFuta
 2. Kwa kweli jibu limetolewa tofauti kabisa.
  Dr nyoosha maelezo tu.

  JibuFuta
 3. Majibu ayaja toshereza mtu asipo kula Wala kunywa ataishi siku ngapi

  JibuFuta