data:post.body Septemba 2018 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

JE BINADAMU ANAWEZA KUISHI MUDA GANI BILA KULA WA KUNYWA?

Binadamu anahitaji maji na chakula iliaweze kuishi, 60% ya mwili wa binadamu ni maji matupu na vingine vilivyobaki ndio misuli, mafuta, mifupa na viungo mbalimbali.
kumekua na ubishani mwingi ni muda gani binadamu anaweza kuishi bila kula na kumekua na majibu ya tafiti mbalimbali kutoka kwa uzoefu wa watu walikofa sababu ya kutokula.
                                                                   

Mahatma Gadhi aliyekua mwanaharakati wa India wakati wa kudai uhuru aliwahi kukaa wiki tatu bila kula huku akinywa maji lakini hii haimaanishi kwamba yeye ndio kipimo sahihi cha watu wote.

ukweli ni upi?
tafiti nyingi zinaamini kwamba binadamu mwenye afya ya kawaida akipewa maji tu anaweza kuishi wiki nne mpaka nane bila kufa lakini pia binadamu ambaye ni mnene sana akipewa maji anaweza kuishi mpaka miezi 6 huku mwili wake ukichoma mafuta na kutumia kama chanzo cha nguvu.
lakini kwa jinsi watu wengi wasivyotarajia, binadamu akipewa chakula akanyimwa maji basi ana uwezo wa kuishi siku nne mpaka siku saba tu kwani maji ni muhimu sana kwa binadamu kuliko hata chakula.

kitu gani husababisha kifo mtu akikosa chakula?
binadamu akikosa chakula kwa muda fulani mwili huanza kutumia mafuta kutengeneza nguvu kwa ajili ya kutumia, baadae mafuta yakiisha mwili huanza kutumia misuli kutengeneza nguvu na hapa ndipo viungo maalumu kama moyo hushindwa kuendelea na kazi na kusimama.

                                                            STAY ALIVE
                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                           0769846183/0653095635

                                    
 
 

HII NDIO SABABU BAADHI YA WATU WANAKULA SANA LAKINI HAWANENEPI.

Kila mtu hua ana ushahidi wa kua na rafiki yake ambaye hata ale chakula kiasi gani hawezi kunenepa, lakini wewe binafsi unahisi ukila kidogo tu unanenepa kupindukia na unashindwa kuelewa ni kitu gani kinasababisha hivyo.
Kimsingi ni kwamba asilimia 60 mpaka 70  ya unene au wembamba wa mtu unategemea urithi wa kibailojia kutoka kwa wazazi na mababu zake.(genetics)
lakini pia watafiti wanaongeza kwamba mambo mengine kama mazoezi na chakula tunachokula kinachangia uzito au muonekano wa miili yetu kwa asilimia 30 mpaka 40.
hivyo ukiwa unafanya mazoezi na kufanya diet kumbuka kwamba unapambana na asilimia 30 mpaka 40 tu, na zingine zilizobaki zinaamuliwa na genes zako.
watafiti wameshagundua genes ambazo zinaamua ukubwa wa miili yetu lakini mpaka leo hawaelewi genes hizo zinafanya kazi vipi, kama ukichunguza vizuri utagundua kuna baadhi ya ukoo watu ni wanene watupu wakati koo zingine ni wembamba watupu.

chanzo ni nini?
mwili wa binadamu una aina mbili za mafuta yaani mafuta meupe na mafuta ya kahawia, kimsingi mafuta ya kahawia ambayo yanapatikana shingoni na mgongoni kwa juu yana kiasi kikubwa cha mitochondria[sehemu ya mwili inayochuma chakula kutengeneza nguvu].
sasa kwa tabia hii ya mafuta kuchoma chakula kutengeneza nguvu hufanya watu ambao wana mafuta haya kuendelea kua wembamba na kuonekana vijana miaka yote.
hivyo kitaalamu mafuta haya tunaita mafuta mazuri  kwani husaidia kuchoma chakula badala ya kuhifadhi mafuta.
mtoto akiwa mdogo anakua na mafuta ya kahawia mengi sana na ndio maana watoto wadogo huweza kula sana bila kunenepa na mafuta haya yanaendelea kupungua kadri mtoto anavyozidi kukua LAKINI mafuta meupe au white adipose tissue hayana uwezo kama mafuta ya kawahia.
mafuta meupe yana mitochondria kidogo na hufanya kazi ya kuhifadhi zaidi kuliko kuchoma, mafuta haya yanakua mengi zaidi mtu anavyokua mtu mzima na hayasaidii kuchoma chakula ili kupunguza uzito.
mafuta haya hupatikana karibia sehemu zote za mwili wa binadamu kama tumboni, makalioni, hips na sehemu mbalimbali.
watu weye mafuta meupe mengi hua wanene sana kutokana na asili ya mafuta haya kutochoma chakula sana kutengeneza joto.
sasa baadhi ya watu wana mafuta ya kahawia mengi zaidi kuliko meupe, watu hawa hawanenepi hata wale nini kwani miili yao huchoma chakula sana kutengeneza nguvu na joto.
watu wenye hii bahati ya kuzaliwa na mafuta mengi ya kahawia hua hawangaiki na swala la uzito kwenye maisha yao.

jinsi gani unaweza kuongeza mafuta ya kahawia mwilini? 
kama unaona watu wengi kwenye ukoo wenu ni wanene, inawezekana kwenu kuna asili ya unene hivyo una mafuta mengi meupe.

mafuta ya kahawia yanaweza kuongezwa kwa kufanya mazoezi, kukaa sehemu yenye baridi kali ili kuulazimisha mwili kutengeneza joto, kula matunda ya apple, kupata usingizi wa kutosha, na kutojishindisha njaa kwa kula kwa kiasi.

                                                                  STAY ALIVE     
                                               
                                           DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0769846183/0653095635



FAHAMU KIFO CHA MAJI KINAVYOTOKEA NA JINSI YA KUJIOKOA.[IMMERSION DEATH]

Vifo vya maji sio vigeni kuviona au kuvisikia kwenye maisha yetu, vifo hivi ni moja ya vifo vibaya sana ambavyo mwanadamu yeyote asingependa kuvipitia kwenye maisha yake.
                                                                   

sio kila mtu anayekutwa kwenye maji anakua alikufa sababu ya maji, kuna wengine walikufa kabla hawajatumbukia kwenye maji na wengine waliuawa na magonjwa ambayo walikua nayo tangu zamani hasa magonjwa ya moyo.
ukiwa na tatizo la  moyo ukatumbukia kwenye maji ule uchovu mdogo tu wa kupambana na maji utasababisha moyo kusimama.

mtu anakufaje akiingia kwenye maji?
mtu akitumbukia kwenye maji anazama kidogo sababu ya uzito wake pamoja na kasi ya mvutano kitaalamu kama force of gravity lakini baada ya sekunde chache hurudi juu ya maji sababu ya uasili wa mwili kuelea.(boyancy).
kama akitumbukia kwenye maji ya baridi sana atavuta hewa kwa nguvu sababu ya mshtuko wa mwili ambao unatokea.(reflex from skin stimulation).
mtu huyu anaweza kushikilia pumzi kwa dakika chache lakini baada ya muda hewa ya carbondioxide itamzidia mwilini mwake na atajikuta anaanza kupumua na kuvuta maji kwenye mapafu yake.
kadri mtu huyu anavyozidi kulia kuomba msaada na kupambana ndio anavyozidi kuvuta maji mengi zaidi.
anaweza kutapika lakini anavyozidi kupambana ndio anazidi kuzama zaidi kwenye maji.
kuzama na kuibuka kwenye maji huendelea mpaka mtu anapata degedege na kupoteza fahamu ndani ya maji.
mtu akishapoteza fahamu hawezi kujiokoa tena na kifo kitamkuta hapa.
mara nyingi watu hupoteza fahamu kwanzia dakika ya tatu mpaka ya kumi ambapo ubongo hukosa hewa kiasi kwamba hauwez kupona hata mtu akikolewa muda huo.(irrevesible brain damage).

kifo kwenye maji ya yasiyo na chumvi.
maji ya mtoni na ziwani hua na chumvi kidogo kama 0.6% hivi, mtu akifa huvuta maji haya kwa kiasi kikubwa na kupitia mapafu huingia ndani ya damu.
ndani ya dakika moja damu inakua imeshachanganyikana na damu zaidi ya lita mbili na nusu, baada ya dakika tatu maji huzidi zaidi.
hii hufanya moyo kuzidiwa na kushindwa kusukuma kiasi kikubwa cha maji kilichoingia.
hii husababisha moyo kusimama na kuleta kifo.
                                                               


kifo kwenye maji ya chumvi.
kiasi kikubwa cha chumvi iliyoko kwenye maji huingia kwenye damu kupitia mapafu, muhanga hufariki kwa kukosa hewa safi ya oxygen.

nini cha kufanya?
jukumu la kulinda maisha lipo mikononi mwako, kama una shughuli zako ambazo zinakufanya upite kwenye maji hakikisha unamiliki life jacket yako kwenye begi ambayo utaivaa kila siku wakati wa kupita kwenye chombo hicho.
ukitumbukia kwenye maji na life jacket kitakachoweza kukuua na wanyama wa majini au njaa kitu ambacho sio rahisi.
kumbuka ukitumbukia kwenye maji ya baridi kali sana unaweza ukafa kwa sababu ya baridi kama jinsi watu wengi walivyokufa baada ya meli ya TITANIC kuzama.
wengi wao walikua na life jackets lakini bahari ya atlantic kazikazini ni baridi sana kiasi kwamba ukitumbukia unakufa ndani ya dakika 30.

                                                                      STAY ALIVE

                                                   DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                         0769846183/0653095635


                                                       

HUU NDIO UMRI AMBAO NGUVU ZA KIUME ZINAANZA KUPUNGUA KWA MWANAUME.

Tafiti mpya zinaonyesha kwamba kadri umri unavyozidi kwenda mbele lazima kila mwanaume atakutana uso kwa uso na tatizo la kuishiwa nguvu za kiume.
                                                                               

Tafiti hii iliwekwa wazi mwaka 2003 kwenye jarida la issue of Annals of Internal Medicine, ilionyesha kwamba tatizo hili lipo sana kwa watu wazima sana ukilinganisha na umri mdogo na nguvu za kiume hupungua ghafla baada ya miaka 50 na kuendelea kupungua zaidi na zaidi.

kuishiwa nguvu za kiume ni nini?
kuishiwa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kuusimamisha uume wako vizuri na kwa muda mrefu ili kuweza kushiriki tendo la ndoa na kuridhika wewe na mpenzi wako.
mwanzoni madaktari walidhani ni tatizo la kisaikolojia tu na msongo wa mawazo lakini tafiti hizo zinaonyesha kwamba asilimia 90 ya wahannga ni zaidi ya miaka 50.

utafiti ulifanyika wa watu gani?
utafiti huu ulifanyika kwa wataalamu wa afya 31000 wenye umri wa miaka 53 mpaka 90 ambao walijitolea kufanyiwa utafiti huu na waliambiwa waseme nguvu zao za kiume kama ni nzuri, mbaya au mbaya sana.
lakini pia watafiti waliangalia vigezo vingine kama unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara na mazoezi.

majibu ya utafiti yako vipi?
majibu yalionyeshwa kwamba asilimia kubwa ya wanaume zaidi ya miaka 50 walionyesha kupungukiwa nguvu za kiume huku asilimia kidogo sana ya watu wenye umri huu wakionyesha kua na nguvu zao za kiume kama kawaida.
wanaume  wenye umri mkubwa ambao hufanya mazoezi, ambao sio wanene na kutovuta sigara walionekana kupungukiwa na hatari hii kwa asilimia 30.
nchini marekani tu zaidi ya watu milion 20 walionekana kuishiwa nguvu za kiume kitu ambacho hupunguza uwezo wa kujiamini kwa wanaume wengi.

                                                                     STAY ALIVE


 

HUU NDIO UMRI AMBAO MBEGU ZA KIUME ZINAANZA KUPOTEZA UBORA WAKE.

Inafahamika kwamba mwanaume anaweza kuzalisha mwanamke kwa kipindi chote cha maisha yake kwani mwanaume aliyerekodiwa kumpa mwanamke mimba akiwa na umri mkubwa kabisa alikua na miaka 96.                                                    

Lakini linapokuja swala la kubeba mimba salama na kuzaa watoto salama umri wa mwanaume ni muhimu sana kama jinsi umri wa mwanamke ulivyo muhimu, kama una mpango wa kuzaa ni vizuri kuzaa mapema sana ili kuepuka matatizo ambayo yanatokana na umri mkubwa.
baadhi ya magonjwa ya watoto kama kua bubu, magonjwa ya akili na baadhi ya saratani husababishwa na mwanaume kua na umri mkubwa.

ubora wa mbegu unapungua mtu akiwa na miaka mingapi?
Kadri umri unavyozidi kua mkubwa uwezo wa mwanaume kumpa mwanamke mimba unazidi kupungua, mwanaume akifikisha miaka 40 uwezo wa kumpa mwanamke mimba ndio unaanza kupungua rasmi.
kipindi hiki mwanaume humpa mwanamke mimba kwa shida sana na hata akifanikiwa uwezekano wa mimba kuharibika hua mkubwa sana.
sio kwamba wanaume wote wenye umri zaidi ya miaka 40 watapata shida hizi lakini hichi ni kipindi cha bahati nasibu sana hivyo kama una mpango wa kubeba mimba na kuzaa basi hakikisha unafanya maamuzi mapema.

nini cha kufanya?
kuna baadhi ya wanaume huchelewa kuoa kwasababu mbalimbali ambazo zinakua nje ya uwezo wao lakini kumbuka hakuna mahusiano kati ya ndoa na kuzaa kwenye dunia ya sasa.
unaweza kuanza uzazi hata kama huna uwezo wa kugharamia harusi au hauko tayari kwa sasa kuingia kweye majukumu hayo lakini ukafuga ndoa baadae lakini mtoto hasubiri.
lakini pia kama tayari ndio umri sahihi wa kuzaa umeshakutupa mkono na una nia ya kupata watoto basi ni vizuri mimba hiyo ifuatiliwe kwa makini sana huku ikifanyiwa vipimo mbalimbali ili kujua kama mtoto mtarajiwa ana tatizo lolote na kama tatizo likionekana basi hatua ichukuliwe mapema.

                                                                        STAY ALIVE

                                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO\
                                                                     0653095635/0769846183

JINSI YA KUHESABU CALORIE ZA CHAKULA KUPUNGUZA UZITO AU KUONGEZA UZITO..

Kimsingi kuna njia nyingi sana za kupunguza au kuongeza uzito, kikubwa ni muhusika mwenyewe kukaa na kuangalia ni njia gani rahisi kwake kupungua uzito.
unaweza kupungua uzito kwa kufanya mazoezi au kupunguza ulaji wa chakula au unaweza ukatumia njia zote mbili kama unaweza.

calorie ni nini?
calorie ni nguvu ambayo inapatikana kwenye chakula tunachokula kila siku, ili binadamu akae kwenye uzito alonao sasa hivi inabidi calorie anazotumia kwa siku kwenye chakula zilingane na calorie ambazo anazitoa nje kwenye shughuli zake za kila siku.

unatumia vipi njia hii?
kwa hali ya kawaida binadamu asipofanya kazi yeyote ile kwa siku anapungua calorie 2000 ambazo zinatumika wakati wa kupumua, kukojoa,kumeng'enya chakula na shughuli zingine za ndani ya mwili.
 hivyo ukitaka uzito wako usipungue kula calorie 2000 kwa siku, ukitaka upungue kula calorie 1500 au 1000 kwa siku, ukitaka uongezeke kula zaidi calories 2000 kwa siku.
kila chakula ambacho tunakula kina idadi fulani ya calories ambazo zimo kwenye chakula husika ambazo zinaweza kuhesabika, hivyo unaweza ukaamua kwamba asubuhi ule calories kadhaa, mchana calories kadhaa na usiku calories kadhaa.

njia hii hupunguza uzito kiasi gani?
ukiweza kula calorie 1000 kwa siku utapungua kilo moja kwa wiki, ukiweza kula calories 1500 kwa siku utapungua nusu kilo kwa wiki.
inategemea na uwezo wako wa kuhimili chakula lakini kula calories 1500 kwa siku ni rahisi na unaweza kugawa calorie 500 kwa kila mlo.
njia hii haingalii umekula chakula usiku sana au mchana.

utajuaje chakula hichi kina calories kadhaa?
kila chakula limeandikwa calories zake mtandaoni kwa mfano chapati moja ina calories 110, chai ya rangi kama ukiweka vijiko vitatau vidogo ni calories 50.
hivyo ukila chapati mbili na chai asubuhi umekula calories 270.
kwa hesabu hizo ni kazi kwako kuangalia mara nyingi hua unakula chakula gani ili uweze kuhesabu calories zake na uweze kuhesabu.
zifuatazo ni idadi za calories kwenye vyakula vingi vya kiafrika.
  • maziwa kikombe kimoja-calories 50
  • yai-calories 90
  • kikombe cha wali uliopikwa-calories 200
  • ndizi mbivu-calories 105
  • chungwa-calories 62
  • ugali-calories 180
  • parachichi-calories 240
  • kiazi kitamu(saizi ya ngumi ya mtu mzima)-calories 280
  • slesi ya mkate-calories 53.
  • sambusa-calories 190
  • kuku mzima-calories 1430
  • nyama ya ngombe- calories 2500
  • nyama ya nguruwe-calories 2420
  • soda-calories 150
  • beer-calories 153 ( inategemea na ukubwa wa beer lakini nyingi zimeandikwa kwenye lebo ya  chupa husika, light beer hua zina calories kidogo zaidi) 
  • supu ya kawaida-theluthi ya kilo-312 calories
 huo ni mfano wa vyakula mbalimbali lakini kama una vyakula vingine unapendelea kula uaweza kuingia google ukapata calories zake kisha ukajumlisha kupata wingi unaotaka mwenyewe.

mwisho; kwa kutumia njia hii unaweza kuongezeka au kupunguza uzito bila kufanya mazoezi yeyote yale kama uko bize na mambo mbalimbali na ukifanya mazoezi utapungua zaidi kama unahitaji, kumbuka kama unajiona sasa hivi wewe ni mnene sana au mwembamba sana, tambua kwamba huo uzito haukupungua au kuongezeka kwa siku moja ila ilichukua muda mrefu sema wewe ulikua huoni hivyo hata kupungua au kuongezeka kunataka muda.
kama ukiongezeka nusu kilo kwa wiki ni kilo mbili kwa mwezi, kama ukipungua nusu kilo kwa wiki ni unapungua kilo mbili kwa wiki.

                                                                  STAY ALIVE

                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                              0653095635/0769846183

MAMBO 6 AMBAYO HUHARIBU AFYA YAKO WAKATI WA KUTAFUTA PESA.

Pesa ni muhimu sana kwenye maisha ya binadamu kwani ndio mfumo ambao umewekwa ili kuendesha shughuli zetu za kila siku na kila mtu ana wajibu wa kuzitafuta pesa hizi kwa bidii sana ili aweze kuishi maisha mazuri
                                                                    
lakini pesa hizi ukizitafuta bila kua makini basi utazipata pesa unazotaka lakini utakuwepo kitandani huwezi hata kuamka sababu ya afya yako kuharibiwa na shughuli zako.
yafuatayo ni mambo ambayo yanaweza kujaribu afya yako sababu ya utafutaji wa pesa.
kutopata usingizi wa kutosha; binadamu anatakiwa alale masaa saba mpaka nane kwa usiku lakini utasikia watafutaji wa pesa hawalali usiku na mchana wanafanya kazi, utakuta mtu mmoja ana kazi tatu kwa kisingizio cha kutafuta pesa.
hali hii huleta msongo wa mawazo, hatari ya magonjwa ya moyo, kushuka kinga ya mwili, kunenepa na kuongeza hatari ya ugonjwa wa kisukari.
hivyo, pamoja na kutafuta hela kumbuka usingizi ni muhimu.
kutokula vizuri na kwa wakati; mifumo mingi ya kazi inawafanya watu wengi wale chakula kile kile kila siku labda chipsi, ugali na wali bila matunda na mboga za majani za kutosha, lakini pia watu hawa wakati mwingine hula kwa kuchelewa sana au kula mlo mmoja kwa siku.
kuna watu hawali vizuri kwa kubana pesa ili waishi maisha mazuri baadae, naomba nikwambie kwamba maisha ni haya haya....bana pesa kwenye mambo yote lakini ukila vibaya au usipokula kwa wakati unaharibu afya.
magonjwa ya kutoabukiza kama kisukari, presha na moyo husababishwa na ulaji mbaya wa vyakula.
kutopumzika au likizo; watu waliweka kwamba binadamu anatakiwa apumzike baada ya kazi sio wajinga, wanafahamu madhara ya kufanya kazi mfulululizo bila kupumzika.
utakuta watu wanafanya kazi siku saba kwa wiki huku wakidai wanatafuta pesa lakini pia hakuna kipindi cha mwaka ambacho wanapumzika.
hata serikali imeweka likizo kwa wafanyakazi wake na ilo hua sio ombi ni lazima uende likizo kwani  pamoja na kukujenga  kiafya, likizo inaongeza uzalishaji wako kazini.
 kutofanya uchunguzi wa afya; binadamu ana magonjwa mengi sana ambayo yanamsakama lakini watu wengi sana hawaendi kufanya uchunguzi wakidhani eti wanabana pesa na wengi wao huenda pale wakiwa wanaumwa tu bila kujua kwamba gharama za matibabu hua ni kubwa sana kuliko kutibiwa.
kuna magonjwa kama saratani, ambayo yasipoonekana mapema huwezi kupona hata uende wapi na hizo pesa unazozitafuta utaziacha.
Steve Jobs ambaye alikua anamiliki kampuni ya apple aligunduliwa na saratani ya koo lakini alipuuza upasuaji ambao madaktari walimshauri afanye.
mwisho wa siku alikua kitandani akijutia mambo aliyofanya kwenye maisha yake.
kutopata matibabu sahihi; moja ya watu ambao ni wagumu sana linapokuja swala la kulipia gharama za matibabu ni waafrika, sio lwamba wote hawana pesa lakini wako tayari kutoa ngombe kwa mganga wa kienyeji lakini sio sh 20000 hospitali.
 katika mambo ambayo unatakiwa uyape kipaumbele  basi ni swala lako la kiafya, hili halina mbadala.
ukikwepa unajikomoa mwenyewe, hizo pesa unazotafuta utazipata na kuzifurahia ukiwa na afya sio ukiwa mgonjwa, poteza pesa zote upone na utaanza upya.
kutofanya mazoezi; watu wengi huanza shughuli zao saa kumi na moja alfajiri na kurudi nyumbani saa tano au saa sita usiku.huku wakikwambia kwamba hawana muda na mazoezi.
naomba nikwambie kwamba kama hupati muda wa mazoezi basi magonjwa kama kisukari, moyo na presha yatapata muda na wewe. na shughuli zako zitakua zimeishia hapo.

                                                                        STAY ALIVE

                                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                                0653095635/0769846183



UFAHAMU UGONJWA WA UTUMWA WA NGONO NA MATIBABU YAKE(SEX ADDICTION)

Utumwa wa ngono ni nini?
huu ni ugonjwa wa akili  unaoambatana na tabia ya kua na hamu sana ya ngono, kufanya ngono mara  kwa mara na mtu mmoja au  watu tofauti bila kuridhika.
ni tatizo ambalo linawapata watu wa jinsia zote yaani wanawake na wanaume lakini wanaume ni waathirika zaidi.


mwanadada kutoka uingereza kwa jina la rebecca anasema kwamba "nilikua nafanya ngono mara tano kwa siku bila kuridhika hata kidogo"

nini dalili za ugonjwa huu?
kwa kipindi cha miezi 6 mgonjwa anakua na dalili zifuatazo
  • mgonjwa hupata hamu za kufanya ngono mara kwa mara bila kuridhika na kujikuta akishiriki mpaka mara tano au kumi kwa siku kwa kulala na wanawake/wanaume  au kupiga punyeto.
  • muda wa kufanya ngono au punyeto unaingiliana na kufanya shughuli zingine muhimu za kimaendeleo.
  • hamu ya ngono huambatana na hali fulani za kimaisha kama msongo wa mawazo, wasiwasi, na au kujisikia raha sana.
  • mgonjwa hujikuta akianza kupambana na hali hiyo ili aache kufanya ngono au punyeto lakini bado hawezi.
  • mgonjwa hushiriki ngono hata na watu mbalimbali bila kuwaza kuhusu madhara ambayo yanaweza kumtokea kwa kufanya hivyo.
  • hali ya kufanya ngono mara kwa mara inamchosha sana muhusika. 
  • kua kwenye mahusiano na watu wengi.
  • ngono zembe.
  • kununua malaya
  • ngono kwa njia ya simu. 
 Tafiti mbalimbali zimeonyesha mahusiano makubwa kati ya msongo wa mawazo na hali hii, majibu yakionyesha kwamba watu wenye msongo wa mawazo huingia zaidi kwenye tatizo la kufanya ngono sana au kujichua  ili kujaribu kusahau matatizo yao.

chanzo cha ugonjwa huu ni nini?
kimsingi chanzo kikuu cha ugonjwa huu wa akili hakifahamiki, ileweke kwamba ngono ni jambo la kawaida na baadhi ya watu hupenda kufanya ngono na watu mbalimbali ili kupata ladha mbalimbali lakini pale mtu anapoanza kufanya ngono sana kiasi cha kushindwa kujizuia na kuanza kupata madhara mbalimbali ya kiuchumi na kijamii sababu hiyo basi huyo ni mtumwa wa ngono yaani sex addict.


matibabu ya tatizo hili ni nini?
hakuna matibabu ya moja kwa moja kwa tatizo hili lakini njia zifuatazo zimeonekana kusaidia kupona kwa tatizo hili.
tafuta chanzo cha kinachopelekea tatizo kua kubwa zaidi; sababu mbalimbali huambatana na tatizo hili kuendelea kua kubwa yaani ile hali ya mgojwa kupata hamu ghafla, inaweza kuchangiwa na kuangalia video za ngono, kujifungia ndani muda mwingi, kutokua na kazi ya kufanya.
msongo wa mawazo; jaribu kutafuta chanzo cha msongo wa mawazo na jinsi gani unaweza kulitatua tatizo hili, huenda unafikiri kufanya ngono na kujichua kutakusahaulisha matatizo yako lakini sio kweli.
jifunze tabia mpya za kukufanya uwe bize; ingia kwenye vikundi  vya mazoezi, ngoma, kuchora, kuogelea au hobby nyingine yeyote ambayo unahisi inaweza kukusaidia kua bize na mambo yako.
dawa; kikundi cha dawa za serotonin reuptake inhibitors husaidia kupunguza hamu ya ngono na kukufanya uishi maisha ya kawaida tu.

                                                                   STAY ALIVE

                                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                      0653095635/0769846183

JE NI KWELI MTU ANAWEZA AKAFA NA KUFUFUKA?

Jana imetokea taharuki nchini Tanzania huko mkoani kigoma baada ya binti mmoja aliyekua amethibitika kufariki katika hospitali ya baptist kuamka tena na kua mzima baada ya kurudishwa nyumbani kwa ajili ya mazishi.
maswali mengi yamezuka kutoka kwa wananchi na wataalamu baada ya hali hii, wengine wakidhani ni imani za kishirikina huku wengine wakimtupia lawama daktari kwamba huenda utaalamu wake ulikua finyu.

je ukweli ni upi?
kitaalamu mtu akishakufa kabisa hawez kurudi tena kwenye uhai kwani ubongo huanza kuharibika ndani ya dakika tano tu baada ya kufariki huku viungo vingine vilivyobaki vikiendelea kuharibika taratibu ndani ya masaa machache baada ya kifo chake, hivyo kwa hali yeyote mtu aliyekua imesemekana amekufa afu akarudi kwenye uhai basi ujue huyo alikua hajafa.

kitu gani kinatokea mpaka watu wanahisi mtu amekufa wakati bado yuko hai?
hii hali kitaalamu inaitwa suspended animation, ni hali ambayo hutokea  pale ambapo moyo, ubongo na mfumo wa upuaji huanza kufanya kazi kwa kiwango cha chini sana ambacho hukaribia hali ya kifo kabisa lakini unakua hujafa rasmi.
kiwango hicho cha ufanyaji wa kazi wa viungo kinaweza kushindwa kugundulika kwa hali ya kawaida au kwa vipimo vya kawaida ambavyo vimapatikana kwenye hospitali zetu  na kama hauko makini sana kama daktari anaweza ukathibitisha kifo.
hali hii huweza kutokea baada ya kupewa dawa za usingizi kabla ya upasuaji, mshituko wa moyo, ugonjwa kipindupindu, sumu(narcotics), joto kali sana, kuumia kwa kichwa, au kwa mazoezi ya yoga.
tofauti kati ya kifo na hali hii ni kwamba mtu anaweza akarudi kwenye hali yake ya kawaida iwapo akipewa matibabu ya kushtua moyo kitaalamu kama  cardio pulmonary resuscitation au anaweza akaamka mwenyewe.
hivyo kimsingi tunasema hali hii ni ya karibu kabisa na kifo lakini bado kifo hakijatokea rasmi.
watu wengi wa aina hii huweza kuota ndoto za ajabu au kuona maluweluwe na baadae wakaja kuhadithia kwamba walimuona yesu kitu ambacho sio kweli.

je kuna matukio kama haya ambayo yameshawahi kutokea?
 ndio, kuna watu wengi sana ambayo yametokea ya watu koenekana kufufuka lakini ni machache sana ambayo yamerekodiwa mpaka sasa kama ifuatavyo.
  • mwaka 1999 daktari wa sweeden kwa jina la Ana Bagenholm alitumbukia kwenye ziwa la barafu na kukaa kwa dakika 40 huku moyo wake ukiwa umesimama na baadae aliokolewa ubongo wake ukiwa mzima kabisa na akaishi tena.
  • mwaka 2006  Mitsutaka Uchikosh ambaye ni mjapani alipoteza fahamu na kukaa sehemu yenye baridi kali kwa siku 24 bila kula wala kunywa akiwa kwenye hali ya herbanation yaani katikati ya uhai na kifo.
  • mwaka 2001 mtoto Erica nordby alikaa masaa mawili bila mapigo ya moyo huku joto laki likishuka mpaka nyuzi joto 16 kama mfu wakati joto la binadamu wa kawaida ni nyuzi joto 37.
                         
                                                        STAY ALIVE 

                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                              0653095635/0769846183