data:post.body KIASI GANI CHA POMBE KINAWEZA KIKAKUUA? ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

KIASI GANI CHA POMBE KINAWEZA KIKAKUUA?

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa habari, utakua umeshasikia vifo vingi ambavyo hua vinatokea kwenye mashindano ya kunywa pombe.
                                                                       
mwili wa binadamu una kiasi ambacho ukifika huwez kuendelea kuvumilia pombe yaani utakufa tu.
ripoti za umoja wa mataifa zinasema kwamba kila mwaka watu milion 3 hufariki kwa sababu ambazo zinasababishwa na unywaji wa pombe...yaani kwa pombe yenyewe au ajari na madhara mengine ya unywaji wa pombe.
kutokana na wingi wa matangazo ambayo yanaisifia pombe basi vijana wengi hua hawaamini kitu hichi na kuhisi kwamba ni sheria tu ambazo zinawekwa ili kuwanyima uhuru wa kunywa pombe.

kiasi gani cha pombe kinatakiwa kiafya?
kimsingi mwanaume anatakiwa anywe unit mbili za pombe kama bia mbili hivi au  glass moja ya wine au robo glass ya pombe kali.
mwanamke anatakiwa anywe unit moja sawa na nusu ya vitu nilivyotaja hapo kwa mwanaume.
kunywa zaidi ya hapo hakuwezi kukuua hapo hapo ila ni hatari kiafya.

kiasi gani cha pombe ambacho kinaua?
kabla mtu hajafa mara nyingi hupoteza fahamu au kutapika sana na kuishiwa maji mwilini, wakati mwingine kufa kwa pombe sio kwa kunywa pombe siku nzima au wiki nzima,mtu anaweza kufika bar akaizifakamia pombe nyingi ndani ya dakika 15 au 30 zikamuua.
sasa kitaalamu gramu 300 za pombe zinaweza kukuua, hii ni sawa na bia 30 za kawaida, lita moja ya pombe kali kama spirit na chupa nne za wine.
japokua kuna watu wachache sana wanaweza wakaponea hospitali kwa kunywa kiasi kikubwa cha pombe kama hichi au wengine walevi wa siku nyingi sana wanaweza wasife lakini uwezekano wa kufa ni mkubwa mno.
na ikitokea mlevi ameacha pombe kabisa halafu akazirudia kama baada ya mwaka mmoja na kunywa kiasi kile kile cha zamani wakati anacha basi uwezekano wa kufa ni mkubwa sana kwani mwili unakua haujazoea kama hapo mwanzo.
ni vizuri kunywa pombe taratibu ndani ya muda mrefu ili ukiona zimekukamata sana uweze kuacha kwanza.
lakini ile tabia ya kuzinywa nyingi haraka, zikianza kazi mwilini unaweza usiamke tena.

                                                               STAY ALIVE
                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
          
                                                         0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni