data:post.body HII NDIO DAWA YA MBADALA WA P2 AMBAZO ZINAUZWA BEI RAHISI. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HII NDIO DAWA YA MBADALA WA P2 AMBAZO ZINAUZWA BEI RAHISI.

Dawa ya P2 imekua maarufu sana kwa matumizi ya wanawake wengi ambao wanaitumia kwa ajili ya kutaka kuzuia mimba baada ya tendo la ndoa.
                                                                                          

dawa hii haina tofauti na zile zinazomezwa kila siku kwenye uzazi wa mpango ila tofauti yake ni kiwango cha dawa,  ambapo hii p2 inakua na miligram nyingi kuliko dawa za uzazi wa mpango za kawaida.

P2 inatumikaje?
ili iweze kufanya vizuri inatakiwa imezwe angalau ndani ya siku tatu baada ya kushiriki tendo la ndoa bila kutumia kinga.

kwanini nazungumzia mbadala wa P2?
dawa hizi ni gharama sana kwa watu wenye uwezo wa chini, dozi huuzwa kwanzia shilingi 5000 mpaka 10000, na ikitokea ukajisahau tena utaingia gharama tena, kitu ambacho ni kigumu kidogo.

mbadala wa p2 ni upi?
kuna dawa zinitwa microgynon ambazo hutumika kumezwa kila siku kama njia ya uzazi wa mpango lakini pia zinatumika kama njia ya kuzuia mimba kama vile p2.
dawa hizi zinauzwa shilingi 500 mpaka 1000 inategemea na sehemu uliyonunua.

inatumika vipi?
nunua vidonge vya microgynon ambavyo vinakua 28 kwenye packet, chukua vidonge vinne kunywa kisha baada ya saa 12 meza vingine vinne na hapo utakua tayari uko salama.

pakua/download  app yetu hapa uwe wa kwanza kila siku kuona makala zetu kwenye simu yako http://www.tiny.cc/sirizaafyabora kisha share na marafiki.


                                                                  STAY ALIVE

                                   DR,KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                       0653095635/0769846183

Maoni 3 :

 1. Habari kiongozi.
  nimependa sana mada hii. naomba kujua hii dawa m badala wa p2 pia naweza kutumia hata baada ya masaa 12 au hata 24 baada ya tendo? kama p2 au ni hapo hapo baada ya tendo naomba kujibiwa tafadhali

  JibuFuta
  Majibu
  1. unaweza kutumia ndani ya masaa 72 ada ya sex.

   Futa
 2. Izo dawa unaweza kutumia banda ya sex

  JibuFuta