data:post.body FAHAMU JINSI YA KUCHELEWESHA SIKU ZAKO ZA HEDHI WAKATI HUZIHITAJI. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

FAHAMU JINSI YA KUCHELEWESHA SIKU ZAKO ZA HEDHI WAKATI HUZIHITAJI.

kuchelewesha siku za hedhi ni nini?
hii ni hali ya kuzuia siku zako za hedhi kutoka kwa muda fulani mpaka utakapokua tayari kuzipata.
                                                                   
kwanini wanawake hucheewesha siku hizi za hedhi?
sababu mbalimbali huchangia wanawake kuchelewesha siku zao za hedhi kama ifuatavyo..

 • siku hizo kuangukia kipindi ambacho yuko bize sana mfano kipindi cha mitihani au majukumu fulani.
 • maumivu makali ya hedhi ambayo yanaweza kuzuia shughuli muhimu unayotaka kufanya mwezi huo.
 • siku hizo za hedhi kutaka kutokea wakati wa honey moon baada ya ndoa kitu ambacho kikapoteza raha ya siku ile muhimu.
 • siku za hedhi kutaka kutokea kipindi ambacho mpenzi wako anayeishi  mbali sana anafika kuja kukuona.
 • kutaka kutokea kipindi wewe ni mgonjwa na maumivu ya hedhi yatakufanya uzidiwe kabisa.
njia gani hutumika kuchelewesha hedhi?

dawa za norethisterone hutumika kuzuia hedhi kwa kuzuia ukuta wa kizazi kutoa damu siku ya hedhi inapofika, dawa hii ina kiasi kikubwa cha homone ya progesterone ambayo ni maalumu kwa kazi hiyo.

jinsi ya kutumia.
siku tatu kabla ya kuanza kuona siku zako za hedhi, meza kidonge kimoja kutwa mara tatu na kisha endelea na dozi mpaka utakapokua tayari kupata hedhi.
siku ukiacha kutumia dawa, utakaa siku mbili mpaka tatu ndio utaanza kuona damu za hedhi.

watu gani hawaruhusiwi kumeza dawa hizi?
 • wajawazito
 • wanaonyonyesha
 • wenye kisukari
 • saratani mbalimbali
 • wenye matatizo ya kuganda kwa damu
 • maumivu makali ya kichwa[migraine headache]
 • kutokwa na damu ovyo sehemu za siri  na chanzo chake hakifahamiki.
onyo; dawa hizi hazitumiki kuzuia mimba na usitumie mara kwa mara kama dawa zingine, ni vizuri kutumia mara chache.

                                                              STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                 0653095635/0769846183

                          

0 maoni:

Chapisha Maoni