data:post.body JE NI KWELI POMBE KALI ZINASAIDIA KUKATA MAFUTA NA KUPUNGUZA UZITO? ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

JE NI KWELI POMBE KALI ZINASAIDIA KUKATA MAFUTA NA KUPUNGUZA UZITO?

Sehemu nyingi mtaani utasikia watu wanene wanaambiwa kwamba 'kunywa pombe fulani kali ili uweze kukata mafuta', na watu wengi kweli hufuata ushauri huo kwa kuamini kwamba bia inanenepesha sana hivyo ni bora kunywa pombe kali sana kama konyagi na wenzake ili kupungua uzito.                                                               
                                                                       
mtazamo huu unatumika na watu wengi sana na hakuna mtu ambaye ameshawahi kusimama kwa ajili ya kulizungumizi hili.

je ni kweli pombe kali inapunguza uzito?
jibu la moja kwa moja ni HAPANA, hizi ni imani tu ambazo watu wamejijengea...NI KWELI pombe kali mara nyingi hua hazina ngano au wanga hata kidogo kama maji vile hivyo kila mtu alitegemea pombe hizi ziweze kupunguza uzito.
lakini ukweli ni kwamba pombe kali hupunguza kasi ya mwili wako kuchoma mafuta na sukari hivyo kukunenepesha zaidi.
katika hali ya kawaida maini ya binadamu ambaye hajanywa pombe hufanya kazi ya kuchoma mafuta ili kutengeneza nguvu za kufanya kazi, lakini inapotokea umekunywa pombe yeyote basi mwili hauwezi kuhifadhi pombe hiyo kama jinsi inavyohifadhi vyakula vingine na itaanza kupambana kuondoa pombe mwilini.
wakati maini yanapambana kuondoa pombe mwilini basi shughuli zote za kuchoma mafuta inabidi zisimame ili pombe itoke mwilini.
sasa kama wewe ni mnywaji wa mara kwa mara maana yake wewe utakua unanenepa tu, na hasa tabia ya kunywa pombe kali na chakula ndio inaongeza unene maradufu kwani mafuta ya  chakula yanahifadhiwa moja kwa moja bila kufanywa chochote..
lakini pia baada ya muda mrefu maini yatachoka na kasi ya kuchoma mafuta itapungua zaidi hata kama ukiacha kunywa pombe.
hivyo kama na wewe ni moja ya watu wanao amini kwamba pombe kali inapunguza uzito na unatumia njia hiyo basi unapoteza muda na uanze kutafuta njia mbadala, kama unataka kupungua na soma hapa http://www.sirizaafyabora.info/2015/08/kama-umeshindwa-kabisa-kutoa-kitambi-na.html
na kama umeamua kunywa basi kunywa kwa ajili ya starehe zakp binafsi sio kwa ajili ya kupunguza kitambi na unene.

                                                                             STAY ALIVE

                                                   DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                
                                                                0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni