magonjwa yasio ya kuambukiza ni yapi?
haya ni magonjwa ambayo humuathiri mtu mmoja mmoja kutokana na mfumo wake wa maisha na hayawezi kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine mfano shinikizo la damu, kisukari, saratani, na magonjwa ya moyo.
haya ni magonjwa ambayo humuathiri mtu mmoja mmoja kutokana na mfumo wake wa maisha na hayawezi kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine mfano shinikizo la damu, kisukari, saratani, na magonjwa ya moyo.
- magonjwa haya yanaua watu milioni 41 kila mwaka duniani sawa na 70% ya vifo vyote duniani kwa ujumla.
- ugonjwa wa moyo unaongoza kwa kuua, ukifuatiwa na saratani, magonjwa ya kifua na kisukari.
- haya magonjwa manne ni chanzo kikuu cha asilimia 80% ya vifo vinavyotokea kwenye umri mdogo.
- magonjwa haya huua zaidi watu kwenye nchi ambazo zinaendelea.
nini chanzo cha magonjwa haya?
uvutaji wa sigara; uvutaji wa sigara moja kwa moja au kuishi nawavuta sigara ni moja ya vyanzo vikuu vya magonjwa yasioambukiza hasa saratani za aina mbalimbali zikiwemo zile za mapafu na mlango wa uzazi.
kutofanya mazoezi; watu wengi shughuli zao za kila siku sio za kutokwa jasho, ni zile za kukaa tu...hali hii huwafanya watu kutojishughulisha na mazoezi kabisa huku kundi kubwa la watu likidhani kwamba mazoezi ni kwa ajili ya watu wanene tu kitu ambacho sio kweli.
magonjwa kama saratani, magonjwa ya moyo na kisukari husababishwa na kutofanya mazoezi.
kunywa pombe sana; unywaji wa pombe katika kiasi fulani una faida mwilini lakini unywaji huo unapopitiliza kiasi, huambatana na madhara makubwa sana ya kiafya ikiwemo kuharibika kwa maini kitaalamu kama liver cirhosis, magonjwa ya moyo, saratani na kisukari.
kula vibaya; ninaposema kula vibaya simaanishi kutokula vyakula vizuri hapana, ila ni tabia ya kutokula mlo kamili.watu wengi siku hizi hupendelea vyakula vya kisasa kama chipsi, biskuti, keki, baga, soseji, soda na kadhalika ambavyo kimsingi madhara yake ni makubwa mno kuliko faida.
ulaji wa sukari na vyaku;a vyenye sukari ni hatari sana kiafya.
matumizi makubwa ya chumvi; zaidi ya vifo milioni 4 kila mwaka vinasbabishwa na matumizi makubwa sana ya chumvi kwenye chakula chetu kitu ambacho huongeza presha ya damu kwenye miili yetu.
uzito uliopitiliza; unene ni hatari sana kwa afya ya moyo, na mwili wote kwa ujumla...kua mnene tu ni moja ya hatari kubwa ya kushambuliwa na magonjwa haya.
kiwango kikibwa cha cholestrol mwilini; tafiti nyingi zinaonyesha kwamba kuna watu wengi ambao wanaonekana ni wazima kwa macho lakini wana kiwango kikubwa sana cha cholestrol au lehemu mwilini kitu ambacho kinawapa hatari kuugua magonjwa haya.
0 maoni:
Chapisha Maoni