data:post.body Julai 2018 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

ZIFAHAMU FAIDA 10 ZA KULA NYAMA NYEUPE

Nyama nyeupe ni ipi?
hii ni nyama ambayo ikichinjwa inakua na rangi nyeupe kabla ya kupikwa mfano halisi ni nyama ya kuku, bata, mbuni, ndege wote na samaki aina zote.
nyama nyekundu ni ipi?
hii ni nyama ambayo ikichinjwa inakua na rangi nyeupe kabla ya kupikwa, mfano ni nyama za wanyama wote kama nguruwe, mbuzi, ng'ombe, na kadhalika.
katika makala zangu zilizopita niwahi kuzungumzia madhara ya nyama nyekundu hivyo kama hukusoma pitia hapa, http://www.sirizaafyabora.info/2015/08/haya-ndio-madhara-nane-madhara-ya-kula.html

kumekua na mijadala na maswali mengi kutaka kujua faida hasa za nyama hii nyeupe ukilinganisha na ile nyekundu naleo ntazitaja faida hizo kwa kifupi..

  • upatikanaji wa virutubisho muhimu vya siku kwani nyama nyeupe ina mafuta kidogo, vitamin, protini na nguvu kwa ajili ya shughuli za kila siku.
  • nyama hizi zina amino acid nyingi ambayo ni muhimu kwa ujenzi wa seli za binadamu na ukuaji wa nywele kwa ujumla.
  • nyama hizi zina mafuta kidogo sana ambayo sio hatari kwa afya ya moyo na mfumo mzima wa mwili wa binadamu.
  • nyama samaki ina kemikali inayoitwa omega 3 ambayo haitengenezwi na miili yetu lakini ni muhimu sana kwa kupunguza kiasi cha lehemu au cholestrol mwilini.
  • nyama ya kuku ina kiasi kikubwa cha selemium ambayo ina kazi ya kuzuia saratani mbalimbali kwenye miiili yetu.
  • nyama nyeupe ni nzuri sana kama ikitumika kama sehemu ya diet kwa ajili ya kupunguza uzito kwani ni laini na mwili unaimeng'enya kirahisi sana.
  • samaki ina vimelea ambavyo ni muhimu sana kwa ajli ya kuzuia tatizo la kusahau sana uzeeni ambalo tafiti zimeonyesha kwamba nyama nyekundu huchangia kwa tatizo hili,
  • kiasi cha phosphorus kipatikanacho kwenye samaki ni muhimu sana kwa ajili ya kusaidia macho yaendelee kuona vizuri.
  • nyama nyeupe inaweka kiwango cha sukari mwilini katika hali nzuri sana na inaweza kuwafaa sana wagonjwa wa kisukari.
  • nyama hii haikai sana tumboni ukilinganisha na ile ya mayai hivyo huweza kuzuia tatizo la saratani ya utumbo ambalo ni kubwa sana kwa watumiaji wa nyama nyekundu.

                                                                     STAY ALIVE

                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                                        0653095635

JE? NI KWELI KWAMBA MAZIWA NDIO DAWA YA SUMU ZOTE?

Watanzania wengi kama sio wote wanafahamu kwamba mtu akinywa sumu basi matibabu ya haraka ni maziwa.
hichi ni kitu ambacho kimetulea na mpaka leo tunafanya hivyo katika maisha yetu ya kila siku yaani akitokea mtu amekunywa sumu basi matibabu yake ni maziwa.
bahati mbaya katika matibabu haya sidhani kama kuna mtu ambaye ameshawahi kuchunguza na kuangalia matokeo ya matibabu ya hao watu wanaokunywa maziwa kama ni mazuri au mabaya.

ukweli ni upi?
kiukweli maziwa sio dawa ya sumu, yaani nafasi ya maziwa kwenye kutumika mtu akinywa sumu haina tofauti kubwa sana na maji ya kunywa.
sumu pekee ambayo mtu anaweza kunywa kisha maziwa au maji yakamsaidia ni tindikali tu ambayo inaweza kupunguzwa nguvu na maziwa.[acid vs base].

sumu zingine vipi?
sumu zingine zote unazofahamu wewe hazisaidiwi kwa chochote na maziwa, yaani kitu pekee ambacho unaweza kumsaidia mtu aliyekunywa sumu za aina tofauti ni kumpeleka hospitali haraka.
hii ni kwasababu kwamba sumu karibia zote hua zina dawa yake maalumu hospitali ambayo kazi yake ni kupambana na sumu uliyotumia kitaalamu kama antidote.
                                                             
lakini pia hata kama dawa ya sumu uliyotumia haipo hospitali, wao wanafahamu njia gani wanaweza kukusaidia  kuindoa sumu ikiwa bado iko tumboni kabla haijasambaa mwilini,[gastric lavage] sio njia hizi za kienyeji za kutapisha watu ambazo zina madhara zaidi kwa mgonjwa.

mfano wa sumu zingine ambazo maziwa hayawezi kusaidia ni..

  • sumu ya panya
  • sumu ya mafuta ya taa.
  • sumu ya oyaga
  • sumu ya dawa
  • sumu za wanyama
  • sumu za chakula
  • sumu za bacteria mbalimbali
  • sumu zingene zote unazozijua wewe.
                                                                   STAY ALIVE

                                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                           0653095635/0769846183


JE NI KWELI HAIRUHUSIWI KUNYWA MAZIWA NA DAWA?

Tangu tukiwa wadogo tulikua tukiambiwa kwamba dawa huharibiwa na maziwa iwapo zikitumika pamoja.
                                                               
mimi binafsi nilipata tabu kidogo kwani baba yangu alikua daktari na alikua akinipa dawa na maziwa na hata nilikua nikimuuliza kuhusu madai ya watu mtaani alikua hanipi jibu.
lakini baada ya kwenda chuo cha udakaktari kuna mambo ambayo nimejifunza na kuelewa kuhusu swala hili la maziwa na dawa.

je dawa zote  zinamalizwa nguvu na maziwa?
jibu la hapa ni ndio na hapana, kiukweli ni kwamba ni dawa chache sana ambazo zinaingiliana na matumizi ya maziwa na dawa nyingi sana hazina shida na maziwa.
maziwa yana madini ya calcium ambayo ndio yanafanya baadhi ya dawa zikatae kwenda na unywaji wa maziwa.
mfano dawa za magnesium ambazo hutumika mara nyingi na watu ambao wana madonda ya tumbo au ambao wanasikia matumbo yao yamejaa gesi haitakiwi kutumika na maziwa kwani madini ya magnesium na calcium hupambana ili  kumeng'enywa na mwili hivyo ukinywa maziwa dawa haitafanya kazi vizuri.
mfano mwingine ni dawa za jamii ya tetracyline kama doxycyline ambayo ikitumika na maziwa haifanyi kazi vizuri yaani hupungua nguvu.
lakini dawa nyingi zilizobaki huwa hazina shida.

je kuna faida ya kunywa maziwa na dawa?
baadhi ya dawa zinafanya kazi vizuri zikimezwa na maziwa, mfano hai ni dawa ya mseto ya malaria ambayo ili ifanye kazi vizuri inatakiwa iambatane na vyakula vya mafuta kama maziwa, nyama au maparachichi hivyo kutumia dawa hii na maziwa ni bora zaidi kuliko kumeza na maji.
dawa zingine za maumivu kama diclofenac, diclopa, ibuprofen, meloxicam, peroxicam [ambazo zipo kwenye kundi la non steroidal ant inflamatory drugs], ni nzuri zaidi zikitumika na maziwa kuliko maji kwani zina tabia ya kuchubua utumbo na kusababisha madonda ya tumbo.

nini cha kufanya?
ni vizuri ukawa makini wakati unapewa dawa hospitaini ili kufuata maelekezo, kama wewe ni muoga wa dawa chungu unaweza kuinywa na soda, juice au hata maziwa.
tusikariri tu kwamba kila dawa inamalizwa nguvu na maziwa...mimi binafsi sijawahi kunywa dawa kwa maji tangu nimezaliwa.

                                                  STAY ALIVE
                           DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                            0653095635/0769846183 

JE? NI KWELI MAZIWA YANASAFISHA MAPAFU BAADA YA KUVUTA HEWA CHAFU?

Katika mazingira ya kitanzania sio ajabu kusikia kwamba mtu ambaye ametoka sehemu yenye vumbi sana, hewa chafu sana au kuvuta sigara anaambiwa anywe maziwa ili yaingie ndani yasafishe mapafu.
ni kitu ambacho kila mtu amekua amekisikia tangu utotoni na kukifuata bila kuhoji kwa undani ili kupata ufumbuzi.                                       

ukweli ni upi?
kimsingi hakuna mahusiano kati ya maziwa na kusafisha mapafu, lakini pia maziwa yana kirutubisho kinaitwa casomorphin ambacho kimeonekana kutengeneza utando au kamasi kwenye utumbo wa binadamu lakini pia wataalamu wamewahi kutest maabara na kugundua kwamba utando huo unatokea kwenye mapafu pia.
sasa katika hali ya kawaida huwezi kuongeza utando kwenye mapafu na kutegemea kwamba vumbi ndio litatoka, zaidi ndio litaganda kabisa huko.
baaadhi ya vyakula ambavyo havishauriwi kabisa kwa watu wenye magonjwa ya mapafu ya muda mrefu ni maziwa.
kwa mantiki hii hakuna sababu ya kuendelea kuamini kwamba maziwa yanasafisha mapafu.

nini cha kufanya ili usafishe mapafu baada ya kutoka sehemu yenye uchafu sana?
kunywa maji mengi kuongeza mzunguko wa damu mwilini lakini pia kaa sehemu yenye uwazi yenye hewa safi na mapafu yako yataanza kua safi yenyewe lakini pia fanya mazozi ya kuvuta pumzi kwa nguvu na kuiachia.
         
                                                      STAY ALIVE
                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                      0760846183/0653095635

JE NI KWELI POMBE KALI ZINASAIDIA KUKATA MAFUTA NA KUPUNGUZA UZITO?

Sehemu nyingi mtaani utasikia watu wanene wanaambiwa kwamba 'kunywa pombe fulani kali ili uweze kukata mafuta', na watu wengi kweli hufuata ushauri huo kwa kuamini kwamba bia inanenepesha sana hivyo ni bora kunywa pombe kali sana kama konyagi na wenzake ili kupungua uzito.                                                               
                                                                       
mtazamo huu unatumika na watu wengi sana na hakuna mtu ambaye ameshawahi kusimama kwa ajili ya kulizungumizi hili.

je ni kweli pombe kali inapunguza uzito?
jibu la moja kwa moja ni HAPANA, hizi ni imani tu ambazo watu wamejijengea...NI KWELI pombe kali mara nyingi hua hazina ngano au wanga hata kidogo kama maji vile hivyo kila mtu alitegemea pombe hizi ziweze kupunguza uzito.
lakini ukweli ni kwamba pombe kali hupunguza kasi ya mwili wako kuchoma mafuta na sukari hivyo kukunenepesha zaidi.
katika hali ya kawaida maini ya binadamu ambaye hajanywa pombe hufanya kazi ya kuchoma mafuta ili kutengeneza nguvu za kufanya kazi, lakini inapotokea umekunywa pombe yeyote basi mwili hauwezi kuhifadhi pombe hiyo kama jinsi inavyohifadhi vyakula vingine na itaanza kupambana kuondoa pombe mwilini.
wakati maini yanapambana kuondoa pombe mwilini basi shughuli zote za kuchoma mafuta inabidi zisimame ili pombe itoke mwilini.
sasa kama wewe ni mnywaji wa mara kwa mara maana yake wewe utakua unanenepa tu, na hasa tabia ya kunywa pombe kali na chakula ndio inaongeza unene maradufu kwani mafuta ya  chakula yanahifadhiwa moja kwa moja bila kufanywa chochote..
lakini pia baada ya muda mrefu maini yatachoka na kasi ya kuchoma mafuta itapungua zaidi hata kama ukiacha kunywa pombe.
hivyo kama na wewe ni moja ya watu wanao amini kwamba pombe kali inapunguza uzito na unatumia njia hiyo basi unapoteza muda na uanze kutafuta njia mbadala, kama unataka kupungua na soma hapa http://www.sirizaafyabora.info/2015/08/kama-umeshindwa-kabisa-kutoa-kitambi-na.html
na kama umeamua kunywa basi kunywa kwa ajili ya starehe zakp binafsi sio kwa ajili ya kupunguza kitambi na unene.

                                                                             STAY ALIVE

                                                   DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                
                                                                0653095635/0769846183

HIVI NDIO MAGONJWA YASIO YA KUAMBUKIZA YANAVYOIMALIZA DUNIA KWA SASA.

magonjwa yasio ya kuambukiza ni yapi?
haya ni magonjwa ambayo humuathiri mtu mmoja mmoja kutokana na mfumo wake wa maisha na hayawezi kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine mfano shinikizo la damu, kisukari, saratani, na magonjwa ya moyo.


  • magonjwa haya yanaua watu milioni 41 kila mwaka duniani sawa na 70% ya vifo vyote duniani kwa ujumla.
  • ugonjwa wa moyo unaongoza kwa kuua, ukifuatiwa na saratani, magonjwa ya kifua na kisukari.
  • haya magonjwa manne ni chanzo kikuu cha asilimia 80% ya vifo vinavyotokea kwenye umri mdogo.
  • magonjwa haya huua zaidi watu kwenye nchi ambazo zinaendelea.
nini chanzo cha magonjwa haya?

   uvutaji wa sigara; uvutaji wa sigara moja kwa moja au kuishi nawavuta sigara ni moja ya vyanzo vikuu vya magonjwa yasioambukiza hasa saratani za aina mbalimbali zikiwemo zile za mapafu na mlango wa uzazi.
kutofanya mazoezi; watu wengi shughuli zao za kila siku sio za kutokwa jasho, ni zile za kukaa tu...hali hii huwafanya watu kutojishughulisha na mazoezi kabisa huku kundi kubwa la watu likidhani kwamba mazoezi ni kwa ajili ya watu wanene tu kitu ambacho sio kweli.
                                                                         
magonjwa kama saratani, magonjwa ya moyo na kisukari husababishwa na kutofanya mazoezi.
kunywa pombe sana; unywaji wa pombe katika kiasi fulani una faida mwilini lakini unywaji huo unapopitiliza kiasi, huambatana na madhara makubwa sana ya kiafya ikiwemo kuharibika kwa maini kitaalamu kama liver cirhosis, magonjwa ya moyo, saratani na kisukari.
                                                                         
kula vibaya; ninaposema kula vibaya simaanishi kutokula vyakula vizuri hapana, ila ni tabia ya kutokula mlo kamili.watu wengi siku hizi hupendelea vyakula vya kisasa kama chipsi, biskuti, keki, baga, soseji, soda na kadhalika ambavyo kimsingi madhara yake ni makubwa mno kuliko faida.
ulaji wa sukari na vyaku;a vyenye sukari ni hatari sana kiafya.
hali hii hushusha kinga ya mwili na kushambuliwa na magonjwa kama saratani.
                                                                 
matumizi makubwa ya chumvi; zaidi ya vifo milioni 4 kila mwaka vinasbabishwa na matumizi makubwa sana ya chumvi kwenye chakula chetu kitu ambacho huongeza presha ya damu kwenye miili yetu.                           
                                          
uzito uliopitiliza; unene ni hatari sana kwa afya ya moyo, na mwili wote kwa ujumla...kua mnene tu ni moja ya hatari kubwa ya kushambuliwa na magonjwa haya.
                                                               
kiwango kikibwa cha cholestrol mwilini; tafiti nyingi zinaonyesha kwamba kuna watu wengi ambao wanaonekana ni wazima kwa macho lakini wana kiwango kikubwa sana cha cholestrol au lehemu mwilini kitu ambacho kinawapa hatari kuugua magonjwa haya.
                                                                     


utajikinga vipi na magonjwa haya?
ni rahisi, epuka vyanzo vyote vilivyotajwa hapo juu na utakua salama.




STAY ALIVE........