data:post.body KWANINI KIFO CHA PACHA MMOJA KILISABABISHA KIFO CHA PACHA MWINGINE?.[forensic medicine] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

KWANINI KIFO CHA PACHA MMOJA KILISABABISHA KIFO CHA PACHA MWINGINE?.[forensic medicine]

Jana nchi yetu imepigwa na pigo zito baada ya vifo vya wasichana wawili maarufu kwa jina la mariam na consolata ambao walikua wamejizolea umaarufu kwa kuungana sehemu ya tumbo na kifua kwenda chini lakini pia juhudi zao na ndoto zao za kusoma mpaka chuo kikuu na kua walimu.
                                                                   
hivi karibuni inasemekana mmoja wao aliugua sana mpaka akalazwa hospitalini, mpaka sasa hivi sijafahamu yule mgonjwa alikua anasumbuliwa na ugonjwa gani lakini yule mwenzake alikua ni mzima kabisa.
baadhi ya picha zinaonyesha aliyekua ni mgonjwa aliwekewa mashine ya oxygen kabla ya kifo chake hivyo huenda alikua na tatizo la moyo au kifua.
baada ya kifo cha pacha wa kwanza zilipita dakika kumi kisha yule pacha mwingine pia akfariki kitu ambacho kimeacha maswali mengi kwa watu kwamba inakuaje yule ambaye sio mgonjwa na yeye amefariki?

mfumo wa mapacha hawa ukoje?
kitaalamu mapacha wale walikua wameungana maeneo ya tumbo na kifua  kitaalamu kama thoracopagus, mapacha wa aina hii huweza kua na miguu miwili, mitatu au minne lakini kwa upande wa juu kila moja hujitegemea kwa kila kitu kwanzia  mfumo wake wa chakula, moyo wake na ubongo wake.
lakini hawa watu wanachangia sehemu za haja kubwa na haja ndogo na kitu kingine cha msingi zaidi wanachochangia ni mfumo wa damu kitaalamu kama circulatory sytem.
yaani japokua kila mtu ana moyo wake damu ya upande mmoja huweza kwenda kwa mtu mwingine kutokana na maungio yao.

nini kinaweza kua chanzo cha kifo cha pacha mwingine?
binadamu wa kawaida hua anakua na lita nne na nusu mpaka tano na nusu za damu kwenye mwili wake hivyo kwakua wale walikua wameungana wanaweza walikua wanachangia kama lita kumi za damu.
baada ya kifo cha pacha wa kwanza moyo wake ulisimama kufanya kazi kabisa, hivyo moyo mmoja uliobaki ndio ulitakiwa uendelee kusukuma damu yeto iliyobaki kitu ambacho kwa hali ya kawaida hakiwezekani.
hii ilipekea kitu kinaitwa kitaalamu kama cardiac overload yaani moyo wa pacha aliyebaki hai ulizidiwa kusukuma damu ya pache mwenzake hivyo na wenyewe ukasimama na kupelekea kifo cha pacha wa pili.
katika hali ya kawaida hakuna binadamua anaweza kuongezewa lita tano za damu akapona, hata hospitali ukiwa umepungukiwa damu kiasi gani unaweza kuongezewa nusu lita tu ndani ya masaa 24, lakini hata ukitakiwa kuongezewa maji kwa mgonjwa aliyeishiwa maji mwilini basi unaongezewa kwa vipimo maalumu.

nini kingeweza kuokoa maisha ya pacha mwingine?
huenda hakuna mtu aliyekua amejipanga kwa kifo cha pacha huyo mmoja, labda walikua wanajua angepona tu.
lakini kwa nchi zilizoendelea na ambao wanakua wako tayari kwa vifaa vya kisasa kabisa, ungefanyika upasuaji wa haraka sana wa kuwatenganisha kabla damu ya pacha aliyekua amefariki haijaingia kwa pacha aliyekua hai.
hii ndio njia pekee ambayo ingeweza kumokoa mwenzake lakini mpaka sasa hivi hatuwezi kumlaumu mtu yeyeote ila kuwaombea wapumzike kwa amani.

                                                                    STAY ALIVE

                                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                      0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni