Kipindi kimoja cha televisheni maarufu kama THE BIGGEST LOSER ambacho hukusanya watu wanene zaidi na kukaa nao ili kuwasaidia kupunguza uzito kiliwahi kuonyesha kwamba zaidi ya asilimia 80 ya watu wanene waliofanikiwa kupunguza uzito walijikuta wakirudi kwenye uzito ule ule wa zamani baada ya mwaka mmoja.
hali hii inawapa msongo mkubwa wa mawazo na kuwafanya wakate tamaa kabisa ya kupungua, tafiti mbalimbali zimefanyika kutafuta kwanini watu wengi wakipungua hurudi kwenye uzito wa zamani au kuongezeka zaidi ya mwanzo...maelezo yafuatayo yalitolewa.
mabadiliko ya homoni; watafiti wamegundua kwamba mtu akipungua uzito kuna mabadiliko ya homoni ambayo yanaweza kumfanya aweze kunenepa tena.
homoni ya leptin ambao hutoa taarifa pale unapokua umeshiba hupungua sana wakati homoni ya ghrelin ambayo huleta njaa kali inaongezeka.
kwa maana hiyo mtu anakula sana kwani hata akishiba hapati taarifa lakini pia homoni zake za njaa ziko juu sana.
watafiti wanashauri ni bora watu hawa kutumia virutubisho au dawa za kupunguza hamu ya kula baada ya kupungua uzito ili wasinenepe kama zamani.
kutobadilika tabia; watu wengi wanashindwa kuelewa kwamba mfumo wao wa maisha wa zamani ndio uliowafanya wanenepe hivyo mambo ambayo wamefanya wapungue sasa hivi wanatakiwa waendelee nayo kama mfumo wao mpya wa maisha.
yaani kula kwa uangalifu, kufanya mazoezi, kunywa maji mengi, kupata usingizi wa kutosha na kadhalika.
hivyo ni vizuri kuendeleza tabia hizi mpya ambazo baada ya muda utaziozoea na kuishi maisha ya kawaida.
sasa watu hufikiri kwamba ukishapungua ndio basi unaweza kuendelea na maisha yako ya zamani kitu ambacho sio kweli.
kutopima uzito; mara nyingi hakuna mtu anagundua kwamba anaongezeka unene, mpaka watu wamwambie vipi mbona unanenepa sana ndio atakimbilia kwenye mzani.
inashauriwa sana kununua mzani wako mwenyewe na kukaa nao ndani ili ukiona imeongezeka hata kilo moja unachukua hatua haraka.
watu wengi wakishapungua uzito wanafikiri kazi imeisha sasa naweza kuendelea kuisha navyotaka, kitu ambacho sio kweli.
kutotulia na diet moja; kuna watu wanapungua na kuongezeka uzito mara kwa mara sababu ya kusikiliza kila ushauri wa kupungua uzito.
matokeo yake anajikuta ana diet nyingi sana ambazo hawezi kwenda nazo kwa mpigo na kujikuta anapoteza uelekeo, anakata tamaa na kuona haiwezekani na kunenepa kama mwanzo.
kama kuna diet imekupa matokeo mazuri basi endelea nayo, achana na kupotezwa na watu.
uwepo wa sumu za mwili; mwili wa binadamu huhifadhi sumu kwenye mafuta, sasa mafuta yakianza kuisha sumu zile huanza kurudi kwenye damu.
hivyo mwili ukiona hatari ya kuzidiwa na sumu hizi unaweza kutengeneza mafuta mapya ili kujilinda, hivyo baadhi ya tafiti zinashauri kwamba kupunguza uzito kuendane na programu za kuondoa sumu mwilini kama mazoezi, maji mengi, kuacha kula vya kula vyenye sumu nyingi kama mikaango, sukari, soda huku ukijikita kwenye vyakula asili, kunywa maji mengi, au kutumia virutubisho vya kuondoa sumu mwilini vya asilia au vya kununua.
programu za kupunguza uzito; sasa hivi sokoni kuna bidhaa nyingi sana za kupunguza uzito, ni kweli bidhaa nyingi hufanya kazi kwani zimetengenezwa kumfanya mtumiaji kula chakula au calories kidogo sana kwa siku.
zikitumika muda mrefu mtu huweza kupunguza mpaka kilo 40..
tatizo ya bidhaa hizi ni kwamba hazikufundishi utaishi vipi baada ya kuacha kutumia bidhaa hizi na matokeo yake miezi michache tu baada ya kumaliza programu hizi watu hurudi mwanzo na kua uzito uleule au kuongezeka zaidi.
ni vizuri watu wanaopungua kwa bidhaa hizi kujifunza ni jinsi gani wataishi bila kunenepa tena bila kutumia bidhaa hizi.
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0653095635/0769846183

0 maoni:
Chapisha Maoni