data:post.body Juni 2018 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
 • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

LIFAHAMU TATIZO LA KUTOKWA NA DAMU NYINGI SANA WAKATI WA HEDHI NA MATIBABU YAKE.

menorahgia ni nini?
hili ni tatizo la kutokwa na damu nyingi sana na kwa muda mrefu kipindi cha sili za hedhi, baadhi ya wanawake husumbuliwa na tatizo hili kitu ambacho huwakosesha amani na kushindwa kufanya shughuli zao za kawaida,
                                                                         

dalili za tatizo hili..

 • kujaza pedi moja damu ndani ya saa moja kwa muda wa saa kadhaa.
 • uhitaji wa kutumia pedi mbili kuzuia damu ya hedhi.
 • kuamka usiku ili kubadilisha pedi.
 • kutokwa damu zaidi ya wiki moja.
 • kushindwa kufanya shughuli zako sababu ya damu nyingi.
 • dalili za upungufu wa damu kama kuchoka sana, kushindwa kupumua vizuri na uchovu.
                                         chanzo cha tatizo hili.
magonjwa mbalimbali yanaweza kupelekea tatizo hili, ni vizuri kufanya uchunguzi wa kina ili kujua chanzo halisi cha tatizo hili ili kufanya matibabu ya uhakika.
tatizo la homoni; ili mwanamke akae kwenye mzunguko sahihi ambao unaeleweka lazima viwango vya homoni za oestrogen na progesterone viwe katika kiwango sahihi.
homoni hizi zikiwa kwenye kiwango ambacho sio sahihi damu nyingi huanza kutoka na kupelekea tatizo hili.
matatizo ya ovary; kama ovary zako zikishindwa kutoa mayai siku za hatari[anaovulation], mwili wako hauwezi kutoa homoni ya progesterone na hii huweza kupelekea kutokwa na damu nyingi sana siku ya hedhi.
uvimbe ndani ya kizazi;  uvimbe wowote ndani ya kizazi huweza kusababisha damu kutoka nyingi sana, mfano polyps, saratani  kizazi, fibroids.
kuharibika kwa mimba; wakati mwingine mwanamke anaweza kupata mimba bila kujua, akahisi labda siku zake zimechelewa tu lakini baadae akaona siku zake zinatoka na damu nyingi na mabonge.
hiii ni dalili kwamba mimba imeharibika na sio hedhi ya kawaida.
matatizo ya kuvuja damu ya kurithi; baadhi ya magonjwa ya kurithi ambayo husababisha damu kutoka nyingi kuliko kawaida pale mtu anapokua amejikata, pia huweza kupelekea tatizo hili.
mfano haemophilia diseases.
dawa; baadhi ya dawa za homoni[dawa za uzazi wa mpango], dawa za maumivu mfano [aspirini, diclofenac ] na dawa za kulainisha damu kama warfin huweaza kuleta tatizo hili.
baadhi ya magonjwa;  baadhi ya magonjwa ya figo na maini huweza kuleta tatizo hili.

                                                vipimo vinavyoweza kufanyika..

 • kipimo cha damu; kipimo hichi hufanyika ili kupima uwezo wa damu kuganda ili kuhakikisha kama mgonjwa ana matatizo uwezo wa damu kushindwa kuganda anapokua ameumia lakini pia huangalia kama umepata upungufu wa damu mwilini.
 • pap smear; hichi ni kipimo cha mlango wa uzazi kuangalia kama kuna dalili za magonjwa ya saratani.
 • biopsy; hichi nikipimoambacho sehemu ya nyama ya mlango wa uzazi au ndani ya kizazi huchukuliwa kwenda kupima kuangalia kama kuna saratani imeanza.
 • utrasound; hichi ni kipimo cha kuangalia sehemu za uzazi kama kizazi, mirija ya uzazi, mayai na mlango wa uzazi.
                                                                         matibabu
matibabu ya kuvuja damu nyingi kipindi cha hezi hutegemea na chanzo cha ugonjwa husika, baadhi ya matibabu yatolewayo ni kama ifuatavyo..
non steroidal ant inflamatory drugs; mfano wa dawa hizi ni ibuprofen, na naproxaten...dawa hizi hupunguza kiasi cha damu kinachotoka na kupunguza maumivu makali ya siku za hedhi,
dawa za uzazi wa mpango; dawa hizi za zina homoni ambazo huweza kurekebisha tatizo  la kutokwa damu nyingi kipindi cha hezi.
kitanzi; kitanzi cha uzazi wa mpango hupunguza ukubwa wa ukuta wa kizazi[endometrium] na kupunguza wingi wa damu.
tranexanamic acid; hupunguza kiasi cha damu siku za hedhi lakini imezwe siku za hedhi tu.

                                                       matibabu mengine
kama matibabu hayo juu yakishindikana kuna matibabu mengine huweza kutolewa kupambana na hali hi kama ifuatavyo.
dilatation and curratage; hii ni njia ya kusafisha sehemu za siri kwa kutumia vifaa maalumu, mara nyingi hufanyika mimba inapokua imeharibika na baadhi ya nyama hazijatoka.
uterine artery embolization; kwa akina mama ambao wa uvimbe kwenye vizazi vyao ambavyo vinatoa damu, mshipa wa damu unaopeleka damu kwenye kizazi huweza kufungwa ili kuzuia hali hiyo.
myomectomy; huu ni upasuaji unaofanyika kuondoa uvimbe[fibroids[ ndani ya kizazi kwa mwanmke ambaye anatokwa na damu nyingi sana kwasababu ya kua na uvimbe huo.
endometrial ablation; huu ni upasuaji wa kuondoa sehemu ya ndani kabisa ya kizazi ambayo inahusika na kuvuja damu wakati wa hedhi.
hysterectomy; huu ni upasauji wa kuondoa kizazi, unaweza kutoa kizazi tu au kutoa kila kitu yaani kizazi, mlango wa uzazi, mrija ya uzazi na mayai.

                                                                   STAY ALIVE

                                   DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                               0653095635/0769846183


KIFAHAMU CHANZO CHA KUNENEPA TENA BAADA YA KUPUNGUA UZITO.[REBOUND WEGHT GAIN]

Kipindi kimoja cha televisheni maarufu kama THE BIGGEST LOSER ambacho hukusanya watu wanene zaidi na kukaa nao ili kuwasaidia kupunguza uzito kiliwahi kuonyesha kwamba zaidi ya asilimia 80 ya watu wanene waliofanikiwa kupunguza uzito walijikuta wakirudi kwenye uzito ule ule wa zamani baada ya mwaka mmoja.
                                                                    
hali hii inawapa msongo mkubwa wa mawazo na kuwafanya wakate tamaa kabisa ya kupungua, tafiti mbalimbali zimefanyika kutafuta kwanini watu wengi wakipungua hurudi kwenye uzito wa zamani au kuongezeka zaidi ya mwanzo...maelezo yafuatayo yalitolewa.
mabadiliko ya homoni; watafiti wamegundua kwamba mtu akipungua uzito kuna mabadiliko ya homoni ambayo yanaweza kumfanya aweze kunenepa tena.
homoni ya leptin ambao hutoa taarifa pale unapokua umeshiba hupungua sana wakati homoni ya ghrelin ambayo huleta njaa kali inaongezeka.
kwa maana hiyo mtu anakula sana kwani hata akishiba hapati taarifa lakini pia homoni zake za njaa ziko juu sana.
watafiti wanashauri ni bora watu hawa kutumia virutubisho au dawa za kupunguza hamu ya kula baada ya kupungua uzito ili wasinenepe kama zamani.
kutobadilika tabia; watu wengi wanashindwa kuelewa kwamba mfumo wao wa maisha wa zamani ndio uliowafanya wanenepe hivyo mambo ambayo wamefanya wapungue sasa hivi wanatakiwa waendelee nayo kama mfumo wao mpya wa maisha.
yaani kula kwa uangalifu, kufanya mazoezi, kunywa maji mengi, kupata usingizi wa kutosha na kadhalika.
hivyo ni vizuri kuendeleza tabia hizi mpya ambazo baada ya muda utaziozoea na kuishi maisha ya kawaida.
sasa watu hufikiri kwamba ukishapungua ndio basi unaweza kuendelea na maisha yako ya zamani kitu ambacho sio kweli.
kutopima uzito; mara nyingi hakuna mtu anagundua kwamba anaongezeka unene, mpaka watu wamwambie vipi mbona unanenepa sana ndio atakimbilia kwenye mzani.
inashauriwa sana kununua mzani wako mwenyewe na kukaa nao ndani ili ukiona imeongezeka hata kilo moja unachukua hatua haraka.
watu wengi wakishapungua uzito wanafikiri kazi imeisha sasa naweza kuendelea kuisha navyotaka, kitu ambacho sio kweli.
kutotulia na diet moja; kuna watu wanapungua na kuongezeka uzito mara kwa mara sababu ya kusikiliza kila ushauri wa kupungua uzito.
matokeo yake anajikuta ana diet nyingi sana ambazo hawezi kwenda nazo kwa mpigo na kujikuta anapoteza uelekeo, anakata tamaa na kuona haiwezekani na kunenepa kama mwanzo.
kama kuna diet imekupa matokeo mazuri basi endelea nayo, achana na kupotezwa na watu.
uwepo wa sumu za mwili; mwili wa binadamu huhifadhi sumu kwenye mafuta, sasa mafuta yakianza kuisha sumu zile huanza kurudi kwenye damu.
hivyo mwili ukiona hatari ya kuzidiwa na sumu hizi unaweza kutengeneza mafuta mapya ili kujilinda, hivyo baadhi ya tafiti zinashauri kwamba kupunguza uzito kuendane na programu za kuondoa sumu mwilini kama mazoezi, maji mengi, kuacha kula vya kula vyenye sumu nyingi kama mikaango, sukari, soda huku ukijikita kwenye vyakula asili, kunywa maji mengi, au kutumia virutubisho vya kuondoa sumu mwilini vya asilia au vya kununua.
programu za kupunguza uzito; sasa hivi sokoni kuna bidhaa nyingi sana za kupunguza uzito, ni kweli bidhaa nyingi hufanya kazi kwani zimetengenezwa kumfanya mtumiaji kula chakula au calories kidogo sana kwa siku.
zikitumika muda mrefu mtu huweza kupunguza mpaka kilo 40..
tatizo ya bidhaa hizi ni kwamba hazikufundishi utaishi vipi baada ya kuacha kutumia bidhaa hizi na matokeo yake miezi michache tu baada ya kumaliza programu hizi watu hurudi mwanzo na kua uzito uleule au kuongezeka zaidi.
ni vizuri watu wanaopungua kwa bidhaa hizi kujifunza ni jinsi gani wataishi bila kunenepa tena bila kutumia bidhaa hizi.

                                                          STAY ALIVE

                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                             0653095635/0769846183

ZIFAHAMU SEHEMU 9 ZA MWILI WAKO AMBAZO UNAWEZA KUZIUZA PESA NYINGI SANA.

Kwa upande wa fedha, mwili wako una gharama kubwa kuliko unavyofikiria...watu wanaweza kulipa mabilioni ya pesa tu kununua sehemu ya mwili wako.
                                                                         
   
mara nyingi watu hutoa sehemu zao za mwili kuwapa wengine bure kabisa kiubinadamu  lakini kuna wengine huamua kuuza kwa faida.
nchi zilizoendelea kama marekani, uingereza, ujerumani, canada na kadhalika biashara hii inafanyika sana.
na kama unataka kujua thamani ya viungo mbalimbali vya mwili wako basi soma hapa.
mbegu za kiume; mbegu za kiume ni mali sana, huuzwa mpaka shilingi laki tatu za kitanzania kwa kupeleka sample moja ambayo ni kama milioni moja na laki mbili hivi kwa mwezi.
vigezo vya kuchangia mbegu; umri kwaniza miaka 20 mpaka 39, urefu wa futi tano na nchi saba kwenda juu, uweze kupeleka mbegu angalau mara nne kwa mwezi ndani kwa miezi sita au mwaka mfulululizo, usikae mbali na kituo cha kutoa mbegu, utoe historia ya ukoo wako na uwe umemaliza degree moja ya chuo kikuu.
plasma; kama ushawahi kushuhudia damu inaganda na kujitenga sehemu mbili yaani maji maji na na sehemu ya damu iliyoganda.
sasa ili sehemu ya majimaji ndio inaitwa plasama, plasma hutumika kutibu magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya kuvuja damu sana kitaakamu kama haemophilia.
                                                     
sample moja ya damu unaweza kulipwa kwanzia elfu sitini mpaka laki moja na ishirini.
nywele; sasa hivi nywele za binadamu zina soko sana duniani kote na zinauzwa kwa bei kubwa sana.
kama ukiweza kutunza nywele zako zikawa ndefu sana bila kuwekewe kemikali ambazo zinaweza kuharibu ubora wake basi unaweza kuuza kwanzia milion mbili kwenda juu.
                                                   
yai la mwanamke; yai la mwanamke mara nyingi hutolewa moja kila mwezi ili liweze kurutubishwa kwa ajili ya kupata mtoto.
kutokana na na shughuli ambayo mwanamke anaipitia ili yai liweze kutoka yaani ikiwemo kuchomwa sindano za homoni na kazi ya kulitoa yai husika.
yai moja huuzwa shilingi milioni 17.
                                       
kizazi chako; kupitia njia ya kitaalamu kama surrogacy yaani mwanamke anawekewa yai la mwanamke mwingine ambalo limerutubishwa ili ambebee mimba mwanamke mwenzake  na akishajifungua anawakabidhi wazazi halisi wa mtoto.
inasemekana mchezaji maarufu christian ronaldo alifanya kitu kama hicho ndio maana mama wa mtoto wake hafahamiki, lakini pia msanii maarufu kanye west na mke wake wamefanya kitu kama hicho.
Gharama ya kufanya hivyo ni shilingi milion hamsini mpaka mia moja za kitanzania,
                                                           
uboho[bone marow]; baadhi ya majimbo nchini marekani hua ni kosa kufanya biashara hii lakini
kulingana na uhitaji mkubwa biashara hii hufanyika hasa kwa wagonjwa wa saratani ya damu na siko seli.
shughuli ya kutoa uboho huu huambatana na maumivu makali sana lakini ukifanikiwa kutoa unaweza kulipwa mpaka milioni kumi kwa mpigo.

ngozi yako; watu maarufu au wenye ushawishi fulani katika jamii wanaweza kuuza sehemu ya ngozi zao zipakwe tatoo kwa ajili ya kutangaza biashara fulani.
mwanamke mmoja mchezaji kwenye kasino kubwa nchini marekani alilipwa milioni 20 kwa kuchora tattoo ya kampuni moja nchini humo lakini pia mtaalamu mmoja wa computer nchini humo alilipwa milioni 70 kwa kazi hiyo hiyo.

majaribio ya mwili wako mzima; watafiti mbalimbali duniani kabla ya kuzitoa dawa zao kwa ajili ya matumizi ya watu mbalimbali kwanza hupenda zijaribiwe.
kazi ya kujaribu dawa hizi ili kujua zinafaa au hazifai kwa matumizi huweza kufanywa na watu ambao hujitoa na kulipwa angalau milioni mbili kwa kila dawa wanayopewa kumeza.
                                                                 
figo; kitaalamu binadamu anaweza kuishi na figo moja tu, japokua atahitaji kua makini na mfumo wa maisha yake ili asiweze kuharibu hiyo figo iliyobaki.
nchini marekani figo inaweza kuuzwa mpaka shilingi milioni 550 zakitanzania.
                                                                 


moyo na maini: hivi ni ambavyo unaweza kuuza lakini pesa wakala watu waliobaki wewe ukiwa umekufa ni moyo ambao ni bilion mbili za kitanzania ukifuatiwa na maini ambayo ni bilioni moja ya kitanzania,


                                                                   STAY ALIVE 

                                  DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0769846183/0653095635

HIVI NDIO KONDOMU INAVYOWEZA KUPOTEA UKENI.

kondomu hutumika kuzuia magonjwa mbalimbali ya ngono ikiwemo ukimwi pamoja na kuzuia mimba, pamoja na faida zake hizi kondomu hua kuna madhara madogo madogo ambayo huweza kutokea iwapo mtu akizitumia.
madhara haya madogo madogo hayakufanye uache kuitumia condomu kwani madhara ya kutotumia kondomu ni makubwa zaidi.
wakati wa tendo la ndoa kondomu inaweza ikapotea ndani ya uke na isionekane kabisa, hii inaweza kuleta mshtuko mkubwa kwa wahusika na kuhisi hali ya hatari imefika.
vitu gani husababisha kondomu kupotea ndani ya uke?

 • kutumia kondomu ambazo ni kubwa sana kuliko saizi ya uume wako.
 • kupasuka kwa kondomu ambako ni sababu ya kutumia kondomu zilizokwisha muda wake au kupatwa kwa joto sana.
 • kutoivaa vizuri mpaka mwanzo kabisa ya uume.
 • kutoishika vizuri wakati wa kuchomoa.
 • kuchelewa kuichomoa baada ya tendo.
je inaweza kupotea kabisa isipatikane tena?
hapana kondomu haiwezi kuingia ndani ya mlango wa uzazi, hivyo kama unaona imepotea basi lazima ipo katikati ya uke na mlango wa uzazi hivyo usipate wasiwasi kabisa kwamba kuna shida yeyote itatokea.

nifanyaje condom ikipotea ndani ya uke?
kondom ikiingia ndanin unaweza usiisikie iko sehemu gani hivyo wewe mwanamke jaribu kuingiza vidole vyako viwili mpaka ndani kabisa ya uke kisha ikamate na kuitoa nje, ukiona umeshindwa basi mwambie mpenzi wako ajaribu kuitoa kwani yeye anakua na nafasi nzuri zaidi ya kuitoa na wakati huo jaribu kusimama, kuweka mguu mmoja kwenye kiti, na kuchuchumaa.
kama ukishindwa kabisa nenda hospitali ambapo wahudumu wa afya wataitoa kondomu hiyo kirahisi sana na ni vizuri kuchukua na dawa za kuzuia mimba na magonjwa mengine kwani kuna uwezekano mkubwa mbegu za kiume zimemwagika ndani. 

                                                           STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                      0653095635/0769846183

JINSI UNAVYOWEZA KUPUNGUZA UZITO KWA KULA VYAKULA VYA MAFUTA.[ketogenic diet]

Dunia nzima iliaminishwa zamani kwamba watu wanaonenepa ni wanaokula vyakula vya mafuta, kitu ambacho kimeonekana sio kweli baada ya tafit nyingi za hivi karibuni.
                                                             
kimsingi uzito unaongezwa na ulaji mkubwa wa vyakula vya wanga na sukari kwa ujumla lakini ulaji wa vyakula vya mafuta unasababisha kupungua uzito na sio kuongezeka.

ketogenic diet ni nini?
hii ni diet ambayo inakua na asilimia 75% ya vyakula vya mafuta, asilimia 20 vyakula vya protini huku asilimia tano tu ndio vyakula vya wanga.
hii ina maana kwamba badala ya kula sahani moja ya wali na samaki au nyama kidogo basi unakula sahani moja ya nyama na wali kidogo au ugali mdogo sana na wakati mwingine unaweza kula nyama tupu au samaki tupu mboga za majani na matunda.
kimsingi hii ni moja ya njia pekee mtu anaweza kupungua uzito bila kufanya mazoezi kabisa.

ketogenic diet inafanya vipi kazi?
kwa kawaida mwili wa binadamu hutumia glucose kutoka kwenye vyakula vya wanga na sukari kukupa nguvu, na glucose ikibaki hubadilishwa kua mafuta na kuhifadhiwa sehemu mbalimbali za mwili.
sasa unapokula vyakula vya mafuta kwa wingi inafika hatua wanga ni kidogo mwilini, mwili unaanza kutumia mafuta mwilini mwako ili kutengeneza nguvu.
hali hii kitaalamu inaitwa  ketosis yaani kunakua kumetengenezwa vitu ambavyo vinaitwa ketones sababu ya uchomaji wa mafuta mwilini.
ukitaka kujua umeingia kwenye ketosis nenda kapime mkojo na utaambiwa kuna ketone bodies kwenye mkojo wako na hiyo ni dalili nzuri.
ukiendelea na diet hii mwili utandelea kuchoma mafuta kutengeneza nguvu na ndipo hapo uzito wako unaanza kupungua kwa kasi sana.
lakini pia diet hii inakufanya ujisikie kushiba muda wote na kukosa hamu ya kula kwani mafuta yanakaa sana tumboni hii itakufanya usile  sana tofauti na ulaji wa vyakula vya wanga ambao unamfanya muhusika apende zaidi kula kwani hamu yake ya kula inaongezeka.
mwanzoni diet hii inaweza kua ngumu kidogo kwa kujisikia umeshiba lakini huna nguvu za kutosha lakini hali hii itaisha.

faida zingine za ketogenic diet ni zipi?
ketogenic diet imeanza kutumika kutibu magonjwa mengine mbalimbali kama ifuatavyo
magonjwa ya moyo; diet hii inapunguza cholestrol au lehemu mbaya mwilini, kupunguza sukari na mafuta mwilini na kukufanya uwe na afya bora zaidi.
kifafa; tafiti zinaonyesha kwamba diet hii inapunguza sana mgonjwa wa kifafa kuanguka mara kwa mara na kumfanya aishi masiha ya kawaida.
kisukari; diet hii huwasaidaia wagonjwa wa kisukari kupungua uzito, kushusha kiasi cha sukari  na homoni ya insulini mwilini, hali hii hufanya uwezo wa insulini kufanya kazi huongezeka.
taiti zilizofanyika zimegundua kwamba kati ya watu 24 wenye kisukari waliotumia diet hii basi 7 kati yao waliacha dozi kabisa na 92% walipunguza dozi ya dawa.
lakini pia wengi wao walipungua uzito kwa kilo 11.
chunusi; diet hii huondoa kabisa chunusi na kuiacha ngozi yako kama ya mtoto mdogo.
alzheimers disease;  huu ni ugonjwa wa mfumo wa ubongo ambao humfanya mgonjwa kusahau kila kitu, huweza kupata nafuu kwa diet hii.
ajali ya kichwa; watu waliopoteza fahamu kwa kuumia kichwani huweza kupata nafuu haraka kwa kuanzishiwa diet hii.
polycystic ovarian syndrome; wagonjwa wenye uvimbe kwenye mayai ya uzazi huweza kupata nafuu kwa diet hii kwani hupunguza sana kiasi cha insulini mwilini.
parkinston disease; huu ni ugonjwa wa kutetemeka mikono sababu ya matatizo ya kwenye ubongo na mishipa ya fahamu, huweza kupata nafuu kwa diet hii.

vyakula gani vya kutumia ukitaka kufuata diet hii?

 • nyama
 • samaki
 • mayai
 • maparachichi
 • karanga na korosho
 • mboga za majani
 • siagi
 • mafuta ya kula ya asili.
 • maziwa
vyakula gani vya kuepuka?
 • vyakula vyote vya sukari mfano keki,soda, ice cream, pipi, jojo na kadhalika
 • wali, tambi, ugali, 
 • maharage,njegere
 • viazi vitamu,chipsi,ndizi
 • punguza mafuta ya kutengeneza viwandani mfano mayonise na mengine ya kula
 • pombe; kwani nyingi zina wanga wa kukuondoa kwenye diet
 • sugar free diet; hivi ni vyakula na vinywaji ambavyo vimetengenezwa kiwandani bila sukari lakini vina sugar alcohol ambayo sio nzuri. mfano pepsi diet au coca zero.
 • matunda yote yenye sukari mfano machungwa,embe, ndizi, tikiti maji, chenza  na kadhalika.
 • asali
madhara gani madogomadogo unapoanza diet hii?
ukianza diet hii unaweza kua unapata njaa wakati mwingine hivyo jitahidi kunywa maji mengi, kuishiwa nguvu, mafua, kukosa usingizi, kushindwa kufanya mazoezi, na akili kushindwa kufanya kaz kwa makini.
kupunguza madhara haya unatakiwa ule vyakula vya wanga kidogo na diet hio kwa wiki chache za kwanza mpaka utakapozoea hali hii.

je hutakiwi kula tena vyakula nilivyokataza?
mwanzoni hutakiwi uvile kabisa na kama ukila iwe kwa kiasi kidogo sana kama unaona unaishiwa nguvu lakini baada ya miezi mitatu unaweza kula chakula kama sasa hivi kwenye siku maalumu kabda harusi au sherehe fulani lakini unarudi haraka kwenye diet yako.


kuna madhara ya diet hii?
watu wengi huchanganya ketoacidosis ambayo ni hali ya hatari kwa watu wenye sukari na ketosis ambayo ni kawaida kabisa kwa binadamu wa kawaida hivyo hakuna madhara yeyote.

mfano wa mpangilio wa chakula.
asubuhi; yai moja,mbili hata tano ya kuchemshwa au kukaangwa na maziwa ambayo hayana sukari.
mchana; nyama ya ngombe au dagaa au kuku au samaki,parachichi na mboga za majani.
usiku kabla ya saa moja; nyama au dagaa au  kuku au samaki, mboga za majani.

NB; huo juu ni mfano tu, unaweza kuchanganya vyakula unavyopenda kulingana na vyakula unavyovipata kwako, kama hauli chakula kingine chochote unaweza kula hata mayai 15 kwa siku. yaani matano asubuhi, mtano mchana matano jioni.
mfumo wa ulaji wa kiafrika wa kula wanga zaidi ndio chanzo kikuu cha unene katika nchi zetu hata ulaya.


                                                                  STAY ALIVE

                                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                      0653095635/0769846183

HATIMAYE UGONJWA WA SIKOSELI WAPATA TIBA YA KUDUMU.[GENE THERAPY]

Kwa miaka mingi ugonjwa wa sikoseli umekua tishio na mateso kwa wahanga na wanafamilia wa watu wanaoumwa ugonjwa huu.
ugonjwa huu wa kurithi kama tunavyofahamu hua hauna dawa ya kuutibu kabisa ila dawa za kupunguza makali.
wanasayansi wamekaa na kuumiza sana vichwa kwa miaka mingi kupata mwarobaini wa tatizo hili ambalo linawasumbua sana vichwa.
miaka ya hivi karibuni kumetokea ugunduzi ambao umelenga kupunguza magonjwa mengi duniani na kuwafanya binadamu kua imara zaidi kitaalamu kama gene therapy.
sisi wote tunatambua kwamba magonjwa yote hushambulia binadamu kulingana na uimara wa yeye alivyoumbwa yaani genes.
kuna watu ni wepesi sana kuugua na wengine ni wagumu sana kuugua na hii ni sababu ya gene ambazo tunarithi kutoka kwa wazazi wetu.
gene therapy ni teknolojia iliyojipanga kubadisha au kuzifuta gene ambazo sio imara na kuweka zile ambazo ni imara.
hivyo tunategemea vizazi vijavyo vitakua na gene imara kupambana na magonjwa ambayo yanatutesa sana sasa hivi kutokana na unyonge wetu wa kimaumbile.

teknolojia hii inatumika vipi kwa wagonjwa wa sickle cell?
sasa teknolojia hii itatumika kulingana na chanzo cha ugonjwa husika, hivyo kwa upande wa sikoseli ugonjwa ambao mifupa kitaalamu kama bone marrow inayotengeneza seli ambazo katika mazingira fulani ya kukosa hewa ya oxygen ya kutosha hubadilika shepu na kua kama mundu au mwezi..
basi mgonjwa huyu atabadilishiwa vitengeneza damu au bone marrow hizo na kuwekewa zile nzima ambazo zinatoa seli nzima.

kazi hii inafanyika vipi?
kwanza mgonjwa hupewa dawa za kuua bone marrow zake kitaalamu kama chemotherapy, baada ya hapo bone marrow zake zote ambazo zinatoa seli za sikoseli zinakua zimekufa kisha huwekewa bone marrow mpya kutoka kwa mtu ambaye anakua amejitolea kumchangia, [mara nyingi mtu huyu anatakiwa awe ndugu yake wa tumbo moja na baba mmoja ambaye ni mzima na damu yake inafanana na ndugu yake mgonjwa].
bone marrow hizi huingizwa kupitia mishipa ya damu kama jinsi mtu anavyoongezewa damu ya kawaida na baada ya hapo hizo bone marrow mpya zinaanza kutengeneza seli mpya na mgonjwa anakua amepona kabisa.

kazi hii inachukua muda gani?
kazi hii huweza kuchukua wiki kadhaa mpaka miezi, mgonjwa anatakiwa aendelee kuwepo karibu na wataalamu ambao wamefanya hiyo kazi yaani transplant team ili wamfuatilie kwa muda mrefu na kuangalia kama kuna madhara anapata ili yaweze kutibika.
timu hii ikishajiridhisha kama mgonjwa amepona unaweza kurushusiwa kwenda nyumbani.

kuna ushahidi wa hichi kitu?
march 3 mwaka 2017 jarida la new england journal of medicine liliandika kwamba mgonjwa wa kwanza wa duniani hatimaye amepona kabisa sikoseli, kazi hiyo ilifanyika nchini ufaransa ambapo matibabu yalianza mvulana huyo akiwa na miaka 13 na alipofikisha miaka 15 alikua hana dalili zozote za ugonjwa huu kwa vipimo na dalili hivyo aliachishwa dawa zote za sikoseli.
"tangu amefanyiwa matibabu hajaonyesha dalili yeyote ya kuugua, hajaongezewa damu, maumivu yameisha na anacheza michezo shuleni na hii inatupa uhakika kwamba mtoto huyu amepona kabisa" alizungumza Dr.Philipe Leboulch ambaye ni profesa wa medicine katika chuo kikuu cha paris.
baada ya hapo nchi mbalimbali zilianza kuripoti kufanikiwa kwa kitu hicho na kuleta matumaini kwa wagonjwa hawa.

nini madhara ya matibabu haya?
kutokana na madhara ya matibabu haya mara nyingi wanashauri yatumike kwa mgonjwa ambaye ugonjwa unamsumbua sana.
madhara kama kutokwa na damu nyingi, matibabu kufeli na ugonjwa kurudi, na kifo huwezi kutokea hivyo ukiamua matibabu haya lazima uwe tayari kwa lolote.
japokua wataalamu wanaamini miaka ijayo wataweza kupunguza madhara haya kutokana na tafiti zinazoendelea.

ni wapi unaweza kupata huduma hii?
huduma hii hupatikana nchi zilizoendelea kama south africa, marekani, india, ufaransa na kadhalika na gharama yake huanzia shilingi milioni mia saba mpaka bilioni moja na milioni mia mbili, inategemea na nchi au hospitali.
 lakini hapa nchini kwetu hakuna huduma hii.
tunategemea mabadiliko ya teknolojia yataleta mapinduzi ya matibabu huko mbeleni na huenda huduma hizi zitaweza kuwafikia maskini wa nchi za kiafrika ambao ndio wahanga wakuu kwa gharama ndogo miaka ijayo.

                                                          STAY ALIVE

                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                               [0653095635/0769846183]
KWANINI KIFO CHA PACHA MMOJA KILISABABISHA KIFO CHA PACHA MWINGINE?.[forensic medicine]

Jana nchi yetu imepigwa na pigo zito baada ya vifo vya wasichana wawili maarufu kwa jina la mariam na consolata ambao walikua wamejizolea umaarufu kwa kuungana sehemu ya tumbo na kifua kwenda chini lakini pia juhudi zao na ndoto zao za kusoma mpaka chuo kikuu na kua walimu.
                                                                   
hivi karibuni inasemekana mmoja wao aliugua sana mpaka akalazwa hospitalini, mpaka sasa hivi sijafahamu yule mgonjwa alikua anasumbuliwa na ugonjwa gani lakini yule mwenzake alikua ni mzima kabisa.
baadhi ya picha zinaonyesha aliyekua ni mgonjwa aliwekewa mashine ya oxygen kabla ya kifo chake hivyo huenda alikua na tatizo la moyo au kifua.
baada ya kifo cha pacha wa kwanza zilipita dakika kumi kisha yule pacha mwingine pia akfariki kitu ambacho kimeacha maswali mengi kwa watu kwamba inakuaje yule ambaye sio mgonjwa na yeye amefariki?

mfumo wa mapacha hawa ukoje?
kitaalamu mapacha wale walikua wameungana maeneo ya tumbo na kifua  kitaalamu kama thoracopagus, mapacha wa aina hii huweza kua na miguu miwili, mitatu au minne lakini kwa upande wa juu kila moja hujitegemea kwa kila kitu kwanzia  mfumo wake wa chakula, moyo wake na ubongo wake.
lakini hawa watu wanachangia sehemu za haja kubwa na haja ndogo na kitu kingine cha msingi zaidi wanachochangia ni mfumo wa damu kitaalamu kama circulatory sytem.
yaani japokua kila mtu ana moyo wake damu ya upande mmoja huweza kwenda kwa mtu mwingine kutokana na maungio yao.

nini kinaweza kua chanzo cha kifo cha pacha mwingine?
binadamu wa kawaida hua anakua na lita nne na nusu mpaka tano na nusu za damu kwenye mwili wake hivyo kwakua wale walikua wameungana wanaweza walikua wanachangia kama lita kumi za damu.
baada ya kifo cha pacha wa kwanza moyo wake ulisimama kufanya kazi kabisa, hivyo moyo mmoja uliobaki ndio ulitakiwa uendelee kusukuma damu yeto iliyobaki kitu ambacho kwa hali ya kawaida hakiwezekani.
hii ilipekea kitu kinaitwa kitaalamu kama cardiac overload yaani moyo wa pacha aliyebaki hai ulizidiwa kusukuma damu ya pache mwenzake hivyo na wenyewe ukasimama na kupelekea kifo cha pacha wa pili.
katika hali ya kawaida hakuna binadamua anaweza kuongezewa lita tano za damu akapona, hata hospitali ukiwa umepungukiwa damu kiasi gani unaweza kuongezewa nusu lita tu ndani ya masaa 24, lakini hata ukitakiwa kuongezewa maji kwa mgonjwa aliyeishiwa maji mwilini basi unaongezewa kwa vipimo maalumu.

nini kingeweza kuokoa maisha ya pacha mwingine?
huenda hakuna mtu aliyekua amejipanga kwa kifo cha pacha huyo mmoja, labda walikua wanajua angepona tu.
lakini kwa nchi zilizoendelea na ambao wanakua wako tayari kwa vifaa vya kisasa kabisa, ungefanyika upasuaji wa haraka sana wa kuwatenganisha kabla damu ya pacha aliyekua amefariki haijaingia kwa pacha aliyekua hai.
hii ndio njia pekee ambayo ingeweza kumokoa mwenzake lakini mpaka sasa hivi hatuwezi kumlaumu mtu yeyeote ila kuwaombea wapumzike kwa amani.

                                                                    STAY ALIVE

                                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                      0653095635/0769846183

HIVI NDIO JINSI MWANAUME ANAVYOWEZA KUNASA KWENYE UKE WA MWANAMKE.[PENIS CAPTIVUS]

Watu wengi ambao hua wanasikia kwamba mwanaume amenasa kwenye uke wa mwanamke hua wanadhani labda kuna mambo ya kishirikina yamehusika hasa kama ni mme au ni mke wa mtu kitu ambacho hua sio kweli.
tatizo la uume kunaswa kwenye uke sio hadithi au imani kama watu wanavyofikiri, ila ni tatizo la kweli kabisa ambalo limewapata watu wachache sana tangu dunia kuumbwa.
hali hiyo huweza kuaibisha sana hasa pale ambapo inatakiwa kwenda hospitali kupata msaada.

nini kinasababisha uume kunasa kwa mwanamke?
kwa hali ya kawaida uume ukiwa ndani ya uke wa mwanamke huendelea kupata damu nyingi ili uendelee kua na nguvu ya kushiriki tendo la ndoa.
lakini pia mwanamke akifika kileleni misuli ya uke hujikunja sana kiasi kwamba mwanaume unaweza kuisikia hali ile kwa muda wa sekunde kadhaa na baadae kuachia.
katika hali ambayo sio ya kawaida misuli ya uke wa mwanamke huendelea kubana sana na uume kuendelea kusimama.
hali husababisha uume kushindwa kutoka kabisa na kujikuta watu wakipelekwa hospitali kuomba msaada wa kimatibabu.

je kuna ulazima sana wa kwenda hospitali hali hii ikitokea?
hali hii ikitokea mara nyingi wapenzi hupaniki sana na kupaniki kule hufanya hali ile iendelee kua mbaya zaidi.
lakini kawa waki relax na kutuliza mawazo na kuanza kufikiria mambo mengine basi hali ile huweza kuisha kabisa bila matibabu yeyote.

watu wangapi wamepatwa na hali hii?
historia inaonyesha ni watu wachache sana ambao wameshapatwa na hali hii, kimsingi wanyama hasa mbwa wamekua wakipata tatizo hili kuiko viumbe wengine wowote wale.
japokua uwezekano wa mtu kupata hali hii na mtu wake wakati wa tendo la ndoa ni mdogo sana lakini sio kwamba haiwezekani kabisa kutokea.
Mwaka 1980 Dr.Brendan Musgrave aliandika ripoti muhimu kwenye jarida la british medical journal kwamba kwa uzoefu wake mwenyewe akiwepo hospitali ya royal isle aliwahi kuona hali hii.
Anasema "nakumbuka niliona ambulance ikileta mke na mme waliokua honeymoon wakiwa wameshikana kwenye machela moja, bahati nzuri tuliweza kuwasaidia".
Mwaka 2016 hali kama hii pia ilionekana kenya ambapo inadaiwa kwamba muhisika mmoja alikua mke wa mtu, watu hawa walichukuliwa na kupelekwa kwa waganga wa kienyeji ambapo inasemekana walifanikisha kuwatenganisha.
Nchini china mzee mmoja mtu mzima alinasa kwenye uke wa mwanamke anyejiuza kisha akapata mshutuko wa moyo na kufariki hapohapo, mwanamke huyo ilibidi apelekwe hospitali ili kuweza kunasuliwa kutoka kwenye mwili huo.

matibabu gani hufanyika hospitali?
Mara nyingi watu hawa hupewa dawa za usingizi na za kulegeza misuli[muscle relaxant] na baada ya muda hurudi katika hali ya kawaida.
hakuna ushahidi wa hali hii kuhusika na mambo ya kishirikina, ila ni kitu ambacho kina maelezo ya kitaalamu kabisa ya kujieleza.

jinsi gani ya kuzuia hali hii?
kama nilivyosema hapo mwanzo, wahusika wanatakiwa wa relax baada ya hali hii kutokea na kusubiri kwa muda fulani.
na hali hii huweza kuisha yenyewe, japokua ndio hivyo kwa akili ya kawaida watu wanashindwa kurelax hali hii haiwezi kuisha yenyewe kwani watu wengi wanakua wameshachangayikiwa muda huo.


                                                               STAY ALIVE

                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO   
                                                          0653095635/0769846183