data:post.body LIFAHAMU TATIZO LA MIMBA KUPITILIZA MUDA WAKE..[POST TERM PREGNANCY] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

LIFAHAMU TATIZO LA MIMBA KUPITILIZA MUDA WAKE..[POST TERM PREGNANCY]

kawaida mimba ya binadamu inatakiwa ibebwe kwa wiki 37 mpaka 42 TU, mwanamke anayezidisha wiki ya 42 bila kuzaa tunaita kitaalamu kama post term pregnancy yaani mimba imepitiliza muda halali wa kuzaliwa.
                                                                           
aina mbili za watoto hua tumboni kwa njia hizi.
aina ya kwanza; mtoto anakua taratibu kiasi kwamba muda wa kuzaliwa unafika lakini yeye bado hajakomaa yaani bado anakua.
aina ya pili; mtoto anakua kwa wakati lakini ikifika muda wa kuzaliwa anakua amekomaa tumboni na kuendelea kukua zaidi.
aina zote hizi za mimba kuchelewa huambatana na vifo vya watoto tumboni na hatari ya kuzaa kwa uapasuaji.

chanzo cha mimba kuchelewa kuzaliwa ni nini?
kuhesabu tarehe vibaya; watu wengi wenye matatizo haya hua na historia ya kuhesabu siku zao vibaya na kutoa taarifa ambazo sio sahihi clinic.
utakuta mimba iko kawaida tu na muda wake lakini kwasababu mama alitoa tarehe ambayo sio ya kweli basi anaonekana mimba yake imechelewa.
tatizo ya kurithi; baadhi ya familia ni kawaida kwa vizazi vyote kujikuta vinakua na mimba za kupitiliza hivyo ukiona mimba yako ukiona imepitiliza ni vizuri ukaulizia kwa wazazi na ndugu zako kama hicho kitu hua kinatokea mara kwa mara kwenye ukoo husika.
mimba nje ya kizazi; mimba chache sana hutungwa nje ya kizazi na kukua mpaka kua kubwa kabisa, lakini mimba hizi haziwez kuzaliwa kwa kawaida kwasababu mtoto anakua eneo ambalo haliwezi kupata uchungu hasa kwenye eneo la tumbo la chakula kitaalamu kama abdominal cavity, sasa mimba ya aina hii huweza kuzaliwa kwa upasuaji tu.
mambo mengine yanayoweza kusababisha mimba ikachelewa kuzaliwa ni unene wa mama mjamzito, mtoto wa kiume tumboni na mimba ya kwanza.

  vipimo vinavyofavyika kugundua kama mimba imepitiliza

  • uchunguzi kutokwa kwa daktari.[history and physical examination]
  • vipimo vya utrasound.
  • kuhesabu tarehe vizuri.
  • x ray kuangalia ukomavu wa mifupa ya mtoto.
  matibabu yanayofanyika.
ikishathibitika kwa vipimo kwamba mimba imepitiliza tumboni na bado haijazaliwa, mama huanzishiwa dawa za uchungu ili aweze kuzaa kwa njia yakawaida lakini kama ikionekana mtoto ni mkubwa sana au nyonga ya mama ni ndogo sana kupitisha mtoto basi mama hufanyiwa upasuaji.

     madhara ya mimba kuchelewa kuzaliwa.
  • mtoto kufia tumboni
  • mtoto kukomaa sana akiwa tumboni.i.e kuota kucha, nywele na  ngozi kavu.
  • baba kumkana mtoto kwa kuhisi mimba haikua yake.
  • mama kupata wasiwasi sana
  • matatizo ya uzazi kama kuvuja damu sana baada ya kuzaa.                                                                                                                                                                                                                                                                        STAY ALIVE                                                                                                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO                                                                                                O653095635/0769846183                              

Maoni 3 :