data:post.body LIFAHAMU TATIZO LA KUTEGUKA KWA BEGA NA MATIBABU YAKE. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

LIFAHAMU TATIZO LA KUTEGUKA KWA BEGA NA MATIBABU YAKE.

kuteguka kwa bega ni tatizo linalotokea mara nyingi kwenye ajali mbalimbali na michezo hasa ya vijana, hutokea pale moja ya mfupa wa bega unapojitoa kwenye sehemu yake.
bega linaweza kuteguka kwa mbele au kwa nyuma na mara nyingi hali hii hutokea mtu anapokua ameanguka.
                                                                       
kuvunjika kwa mbele hutokea zaidi yaani kwa 95% kuliko kuteguka kwa nyuma ambayo hutokea chini ya asilimia 5%.
kuteguka kunaweza kua kidogo pale mfupa unapokua umejitoa kabisa kwenye jointi au kidogo pale mfupa unapokua umejiondoa kidogo kwenye jointi.

                                                 dalili za kuteguka bega

  • maumivu makali kuhamisha mkono.
  • kuweka mkono mbali na mwili kwani kuusogeza karibu yako kunauma sana.
  • kona ya bega kuchongoka badala ya kua mviringo.
  • ganzi
  • kutosikia mfupa ndani ya jointi kwa kupapasa.
                                                                      

                                                 vipimo vinavofanyika

      x-ray; hii hupigwa kwa upande wa mbele na pembeni kwa mtu ili kuonyesha mfupa ulivyofunjika na hata kama kuna punje za mifupa zimetoka ziweze kuonekana vizuri.
    vipimo vingine kama utrasound, mri  na ct scan huweza kupima kuangalia mifupa japokua utrasound sio nzuri sana kwa upande huu.

                                                              matibabu
kitu cha kwanza kabisa ni kuurudisha mfupa kwenye mahali pake kwa kutumia njia mbalimbali za kitaalamu ambazo ni vizuri zikafanyika na watu wenye utaalamu wa afya na sio mtu yeyote.
ukimkuta mtu ameteguka bega usijaribu kurudisha mwenyewe kwani unaweza kuvunja kabisa, hivyo muweke vizuri kwenye kiti au machela bila kulisumbua bega kisha mpeleke hospitali.
                                                                  
akifika hospitali madaktari wataurudisha mkono kwenye sehemu yake baada ya kumpa dawa ya usingizi au maumivu na kama ikishindikana kuurudisha basi upasuaji utafanyika ili kuurudisha.
baada ya kuuweka sawa, mgonjwa hufungwa bandeji maalumu ili kuutuliza mkono ukae sawa kwa muda wa wiki 3 mpaka 6.
kabla ya kufungwa bandeji hakikisha bega lako halina nganzi ili kue na uhakika kama bega limekaa sehemu sahihi.
baada ya wiki ya sita mgonjwa anaweza kuanza kuufanyia mazoezi madogo madogo.
 tatizo hili hupenda kujirudia sana kwa watu ambao wameshateguka kwa mara ya kwanza hivyo ni vema kua makini sana na shughuli zako.
 
                                                               STAY ALIVE

                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                     0653095635/0769846183

Maoni 1 :

  1. Naomba kuuliza, ni mazoezi gani unatakiwa kufanya kwa mtu aliyevunjika bega na kiganja cha mkono baada ya week 3 au 4 za matibabu? Je inachukua muda mgonjwa kutosikia maumivu kabisa? na baada ya muda uliotegemewa kutosikia maumivu mgonjwa akasikia, tafsiri yake ni nin?

    JibuFuta