data:post.body JE UTOAJI WA MIMBA UNASABABISHA VIPI UGUMBA KWA MWANAMKE? ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

JE UTOAJI WA MIMBA UNASABABISHA VIPI UGUMBA KWA MWANAMKE?

kwa makala mbalimbali nimekua nikipost hapa kwamba utoaji wa mimba una madhara makubwa sana na ni vizuri kuzuia mimba kwa njia salama za uzazi wa mpango kuliko kuzitoa.
ni kweli kuna wanawake wameshawahi kutoa mimba lakini baadae wakapata watoto lakini wapo waliotoa mimba moja pia na mpaka leo wanalilia mtoto.
                                                                     
kuna watu wengi wamekua wakiniuliza mara kwa mara ni jinsi gani utoaji wa mimba unaweza kusababisha ugumba.

leo ntalijibu swali hilo kama ifuatavyo.......
kuharibika kwa kuta ya ndani ya uzazi; kati ya kuta za uzazi ambazo ni tatu ipo kuta moja ya ndani sana ambayo inaitwa kitaalamu kama endometrium, kuta hii ndio inayohusika kulishika yai ambalo limerutubishwa ili liweze kukua na kua mtoto baadae.
sasa wakati wa kutoa mimba wataalamu huikwangua kuta hii ili iachie yai lilorutubishwa na kwa bahati mbaya ukikwanguliwa sana hii kuta hutoka kabisa au kuharibika.
kuta hii ikishatoka huwezi kupata mimba hata uende wapi.
kushambuliwa na bacteria baada ya mimba kutoka; wakati mwingine mimba inaweza kutoka salama bila tatizo lolote lakini bacteria hushambulia kizazi kwasababu baada ya mimba kutoka kinakua kwenye hatari kubwa ya kushambuliwa.
ni kweli watu hutumia dawa za antibayotiki kuzuia bacteria hawa lakini wakati mwingine bacteria hawa hua na nguvu zaidi kuzishinda dawa na matokeo yake mtu huugua magonjwa sugu ya kizazi kitaalamu kama pelvic inflamatory infection ambayo huleta ugumba baadae.
kutolewa kizazi; wakati mwingine wakati ya kazi ya kutoa mimba kizazi huweza kutoboka, hii ni hali ya hatari sana na kama mtu anatolewa mimba maeneo ambayo hakuna chumba kikibwa cha upasuaji anaweza akafa kwa kuvuja damu nyingi sana.
kizazi kikitoboka inatakiwa mgonjwa afanyiwe upasuaji wa haraka ili kukishona na kama kiko vibaya sana huweza kuondolewa kabisa.

                                                                  STAY ALIVE

                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                    0653095635/0769846183
                             

0 maoni:

Chapisha Maoni