data:post.body Mei 2018 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

JE UTOAJI WA MIMBA UNASABABISHA VIPI UGUMBA KWA MWANAMKE?

kwa makala mbalimbali nimekua nikipost hapa kwamba utoaji wa mimba una madhara makubwa sana na ni vizuri kuzuia mimba kwa njia salama za uzazi wa mpango kuliko kuzitoa.
ni kweli kuna wanawake wameshawahi kutoa mimba lakini baadae wakapata watoto lakini wapo waliotoa mimba moja pia na mpaka leo wanalilia mtoto.
                                                                     
kuna watu wengi wamekua wakiniuliza mara kwa mara ni jinsi gani utoaji wa mimba unaweza kusababisha ugumba.

leo ntalijibu swali hilo kama ifuatavyo.......
kuharibika kwa kuta ya ndani ya uzazi; kati ya kuta za uzazi ambazo ni tatu ipo kuta moja ya ndani sana ambayo inaitwa kitaalamu kama endometrium, kuta hii ndio inayohusika kulishika yai ambalo limerutubishwa ili liweze kukua na kua mtoto baadae.
sasa wakati wa kutoa mimba wataalamu huikwangua kuta hii ili iachie yai lilorutubishwa na kwa bahati mbaya ukikwanguliwa sana hii kuta hutoka kabisa au kuharibika.
kuta hii ikishatoka huwezi kupata mimba hata uende wapi.
kushambuliwa na bacteria baada ya mimba kutoka; wakati mwingine mimba inaweza kutoka salama bila tatizo lolote lakini bacteria hushambulia kizazi kwasababu baada ya mimba kutoka kinakua kwenye hatari kubwa ya kushambuliwa.
ni kweli watu hutumia dawa za antibayotiki kuzuia bacteria hawa lakini wakati mwingine bacteria hawa hua na nguvu zaidi kuzishinda dawa na matokeo yake mtu huugua magonjwa sugu ya kizazi kitaalamu kama pelvic inflamatory infection ambayo huleta ugumba baadae.
kutolewa kizazi; wakati mwingine wakati ya kazi ya kutoa mimba kizazi huweza kutoboka, hii ni hali ya hatari sana na kama mtu anatolewa mimba maeneo ambayo hakuna chumba kikibwa cha upasuaji anaweza akafa kwa kuvuja damu nyingi sana.
kizazi kikitoboka inatakiwa mgonjwa afanyiwe upasuaji wa haraka ili kukishona na kama kiko vibaya sana huweza kuondolewa kabisa.

                                                                  STAY ALIVE

                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                    0653095635/0769846183
                             

LIFAHAMU TATIZO KUTEGUKA MKONO NA MATIBABU YAKE.

kuteguka kwa jointi ya mkono ni moja ya ajali ambazo zinatokana na kupata ajali michezoni au kuanguka katika shughuli mbalimbali.
mara nyingi huhitaji nguvu nyingi sana kuteguka kwa mkono huu na huambatana na maumivu makali sana....                                                                 
kuteguka kwa mkono huweza kutokea kwa mbele ya mkono[anterior dislocation], au nyuma ya mkono[posterior dislocation].

 dalili za kuteguka kwa mkono.....

  • maumivu makali ya mkono
  • kupata ganzi ya mkono
  • kuvimba sehemu ya jointi.
  • kushindwa kabisa kuutumia mkono kufanya kazi.
 vipimo ambavyo vinapimwa ili kuhakikisha kama mkono umeteguka.
  • x ray
  • ct scan
  • mri
  • utrasound.
                           
   
matibabu ya kuteguka kwa mkono

mgonjwa hupewa dawa ya usingizi ili kutuliza maumivu kisha mkono hurudishwa katika sehemu yake kama mwanzo[closed reduction] na kama mkono ukishindwa kurudishwa kwa kawaida mgonjwa hutakiwa kupasuliwa na kurudishwa katika hali yake ya kawaida[open reduction].
                                                                 
baadae mkono hufungwa P.O.P kwa muda wa wiki nne kisha P.O.P hutolewa na kuanzishiwa matibabu ya taratibu.
                                                       
                    
                                                     
                                                     STAY ALIVE
                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                          0653095635/0769846183
                                                 



LIFAHAMU TATIZO LA KUTEGUKA MKONO NA MATIBABU YAKE..

kuteguka kwa jointi ya mkono ni moja ya ajali ambazo zinatokana na kupata ajali michezoni au kuanguka katika shughuli mbalimbali.
mara nyingi huhitaji nguvu nyingi sana kuteguka kwa mkono huu na huambatana na maumivu makali sana....                                                                   
kuteguka kwa mkono huweza kutokea kwa mbele ya mkono[anterior dislocation], au nyuma ya mkono[posterior dislocation].

 dalili za kuteguka kwa mkono.....

  • maumivu makali ya mkono
  • kupata ganzi ya mkono
  • kuvimba sehemu ya jointi.
  • kushindwa kabisa kuutumia mkono kufanya kazi.
 vipimo ambavyo vinapimwa ili kuhakikisha kama mkono umeteguka.
  • x ray
  • ct scan
  • mri
  • utrasound.
                             
   
matibabu ya kuteguka kwa mkono

mgonjwa hupewa dawa ya usingizi ili kutuliza maumivu kisha mkono hurudishwa katika sehemu yake kama mwanzo[closed reduction] na kama mkono ukishindwa kurudishwa kwa kawaida mgonjwa hutakiwa kupasuliwa na kurudishwa katika hali yake ya kawaida[open reduction].
                                                                   
baadae mkono hufungwa P.O.P kwa muda wa wiki nne kisha P.O.P hutolewa na kuanzishiwa matibabu ya taratibu.
                                                         
                    
                                                     
                                                     STAY ALIVE
                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                          0653095635/0769846183
                                                 


LIFAHAMU TATIZO LA KUTEGUKA KWA BEGA NA MATIBABU YAKE.

kuteguka kwa bega ni tatizo linalotokea mara nyingi kwenye ajali mbalimbali na michezo hasa ya vijana, hutokea pale moja ya mfupa wa bega unapojitoa kwenye sehemu yake.
bega linaweza kuteguka kwa mbele au kwa nyuma na mara nyingi hali hii hutokea mtu anapokua ameanguka.
                                                                       
kuvunjika kwa mbele hutokea zaidi yaani kwa 95% kuliko kuteguka kwa nyuma ambayo hutokea chini ya asilimia 5%.
kuteguka kunaweza kua kidogo pale mfupa unapokua umejitoa kabisa kwenye jointi au kidogo pale mfupa unapokua umejiondoa kidogo kwenye jointi.

                                                 dalili za kuteguka bega

  • maumivu makali kuhamisha mkono.
  • kuweka mkono mbali na mwili kwani kuusogeza karibu yako kunauma sana.
  • kona ya bega kuchongoka badala ya kua mviringo.
  • ganzi
  • kutosikia mfupa ndani ya jointi kwa kupapasa.
                                                                      

                                                 vipimo vinavofanyika

      x-ray; hii hupigwa kwa upande wa mbele na pembeni kwa mtu ili kuonyesha mfupa ulivyofunjika na hata kama kuna punje za mifupa zimetoka ziweze kuonekana vizuri.
    vipimo vingine kama utrasound, mri  na ct scan huweza kupima kuangalia mifupa japokua utrasound sio nzuri sana kwa upande huu.

                                                              matibabu
kitu cha kwanza kabisa ni kuurudisha mfupa kwenye mahali pake kwa kutumia njia mbalimbali za kitaalamu ambazo ni vizuri zikafanyika na watu wenye utaalamu wa afya na sio mtu yeyote.
ukimkuta mtu ameteguka bega usijaribu kurudisha mwenyewe kwani unaweza kuvunja kabisa, hivyo muweke vizuri kwenye kiti au machela bila kulisumbua bega kisha mpeleke hospitali.
                                                                  
akifika hospitali madaktari wataurudisha mkono kwenye sehemu yake baada ya kumpa dawa ya usingizi au maumivu na kama ikishindikana kuurudisha basi upasuaji utafanyika ili kuurudisha.
baada ya kuuweka sawa, mgonjwa hufungwa bandeji maalumu ili kuutuliza mkono ukae sawa kwa muda wa wiki 3 mpaka 6.
kabla ya kufungwa bandeji hakikisha bega lako halina nganzi ili kue na uhakika kama bega limekaa sehemu sahihi.
baada ya wiki ya sita mgonjwa anaweza kuanza kuufanyia mazoezi madogo madogo.
 tatizo hili hupenda kujirudia sana kwa watu ambao wameshateguka kwa mara ya kwanza hivyo ni vema kua makini sana na shughuli zako.
 
                                                               STAY ALIVE

                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                     0653095635/0769846183

LIFAHAMU TATIZO LA MIMBA KUPITILIZA MUDA WAKE..[POST TERM PREGNANCY]

kawaida mimba ya binadamu inatakiwa ibebwe kwa wiki 37 mpaka 42 TU, mwanamke anayezidisha wiki ya 42 bila kuzaa tunaita kitaalamu kama post term pregnancy yaani mimba imepitiliza muda halali wa kuzaliwa.
                                                                           
aina mbili za watoto hua tumboni kwa njia hizi.
aina ya kwanza; mtoto anakua taratibu kiasi kwamba muda wa kuzaliwa unafika lakini yeye bado hajakomaa yaani bado anakua.
aina ya pili; mtoto anakua kwa wakati lakini ikifika muda wa kuzaliwa anakua amekomaa tumboni na kuendelea kukua zaidi.
aina zote hizi za mimba kuchelewa huambatana na vifo vya watoto tumboni na hatari ya kuzaa kwa uapasuaji.

chanzo cha mimba kuchelewa kuzaliwa ni nini?
kuhesabu tarehe vibaya; watu wengi wenye matatizo haya hua na historia ya kuhesabu siku zao vibaya na kutoa taarifa ambazo sio sahihi clinic.
utakuta mimba iko kawaida tu na muda wake lakini kwasababu mama alitoa tarehe ambayo sio ya kweli basi anaonekana mimba yake imechelewa.
tatizo ya kurithi; baadhi ya familia ni kawaida kwa vizazi vyote kujikuta vinakua na mimba za kupitiliza hivyo ukiona mimba yako ukiona imepitiliza ni vizuri ukaulizia kwa wazazi na ndugu zako kama hicho kitu hua kinatokea mara kwa mara kwenye ukoo husika.
mimba nje ya kizazi; mimba chache sana hutungwa nje ya kizazi na kukua mpaka kua kubwa kabisa, lakini mimba hizi haziwez kuzaliwa kwa kawaida kwasababu mtoto anakua eneo ambalo haliwezi kupata uchungu hasa kwenye eneo la tumbo la chakula kitaalamu kama abdominal cavity, sasa mimba ya aina hii huweza kuzaliwa kwa upasuaji tu.
mambo mengine yanayoweza kusababisha mimba ikachelewa kuzaliwa ni unene wa mama mjamzito, mtoto wa kiume tumboni na mimba ya kwanza.

  vipimo vinavyofavyika kugundua kama mimba imepitiliza

  • uchunguzi kutokwa kwa daktari.[history and physical examination]
  • vipimo vya utrasound.
  • kuhesabu tarehe vizuri.
  • x ray kuangalia ukomavu wa mifupa ya mtoto.
  matibabu yanayofanyika.
ikishathibitika kwa vipimo kwamba mimba imepitiliza tumboni na bado haijazaliwa, mama huanzishiwa dawa za uchungu ili aweze kuzaa kwa njia yakawaida lakini kama ikionekana mtoto ni mkubwa sana au nyonga ya mama ni ndogo sana kupitisha mtoto basi mama hufanyiwa upasuaji.

     madhara ya mimba kuchelewa kuzaliwa.
  • mtoto kufia tumboni
  • mtoto kukomaa sana akiwa tumboni.i.e kuota kucha, nywele na  ngozi kavu.
  • baba kumkana mtoto kwa kuhisi mimba haikua yake.
  • mama kupata wasiwasi sana
  • matatizo ya uzazi kama kuvuja damu sana baada ya kuzaa.                                                                                                                                                                                                                                                                        STAY ALIVE                                                                                                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO                                                                                                O653095635/0769846183                              

NJIA RAHISI KUMI ZA KUPUNGUZA TUMBO BAADA YA KUJIFUNGUA.

baada ya kujifungua wanawake wengi hujikuta bado wana matumbo makubwa yaani wakati mwingine watu wasiokujua wanaweza wakahisi bado haujazaa, lakini ukweli ni kwamba inakuchukua miezi tisa kulivimbisha tumbo hilo hivyo hata kulipunguza huchukua muda fulani.
                                                                         
kwa kawaida kizazi kinachukua wiki mbili kurudi hali yake ya kawaida lakini mafuta yaliyoko eneo la tumbo yawezi kuondoka  kirahisi kama usipochukua hatua yeyote.
                                                                   
kitu gani kinafanya mwanamke apate tumbo baada ya kujifungua?
kwa kawaida mwanamke huongezeka kilo 12 akibeba mimba hii ni kutokana na uzito wa mtoto, uzito wa  kondo la nyuma na ulaji wa chakula ambao mtoto anauhitaji sana ili kukua lakini baada ya kujifungua mama  hupunguza kilo sita tu na  kilo sita zingine hubaki kama mafuta eneo la tumbo.

inachukua muda gani hasa kwa tumbo la uzazi kuondoka?
baadhi ya wazazi huchukua siku kadhaa, baadhi huchukua miezi kulingana na bidii ya mwanamke husika ya kulitoa tumbo baada ya kujifungua.

mambo ya kuzingatia ili kuliondoa tumbo la uzazi...
nyonyesha mtoto; kunyonyesha mtoto sio kuna ongeza kinga ya mtoto tu lakini kunasababisha kuongezeka sana kwa homoni ya oxytocin ambayo inahusika na kupunguza ukubwa wa kizazi na kuzuia homoni za uzazi ambazo zinahusika na kuongeza ukubwa wa kizazi wakati mwanamke ana mimba.
wanawake wengi wa siku hizi hawanyonyeshi kwa sababu za kiurembo lakini nakwambia wengi wao huishia kua wanene sana kwa kukosa faida hii.
vaa mkanda wa tumbo; hii ni njia ya kiasili na kizamani zaidi kwani imetumika kwa miaka mingi na watu wa rangi mbalimbali duniani.
mkanda wa tumbo husaidia kuikaza misuli ya tumbo na kuongeza kasi ya kupungua kwa ukubwa wa kizazi.
ukiwa unavaa mkanda wa tumbo au unafunga kitambaa chochote hakikisha haukazi sana au kulegeza sana ili uweze kupata matokeo mazuri.
kwa matokeo mazuri zaidi, mkanda huu uvaliwe kwa  wiki nne mpaka sita baada ya kujifungua.
fanya mazoezi; mazoezi husaidia sana kupunguza tumbo la uzazi, sio lazima kufanya mazoezi mazito sana lakini unaweza kutembea, kukimbia kidogo, kuruka kamba,cardio na kadhalika, na utapata matokea mazuri sana ndani ya muda mfupi,
fanya mazoezi angalau dakika 20 mpaka 30 kwa siku hasa pale mtoto anapokua amesinzia.
kula kwa uangalifu na epuka diet kali sana; wanawake wengi hupaniki baada ya kuzaa na  huanza kufunga kula na kuruka chakula ili wapungue haraka kitu ambacho sio kizuri kwako na kwa mtoto.
kipindi hiki bado unahitaji chakula cha kutosha ili uweze kupata maziwa mengi ya kumpa mtoto, hivyo punguza sana ulaji wa vyakula vya wanga kama ugali, mihogo, wali, ndizi na acha kabisa kula wanga ambao sio muhimu kama chips, sukari, biskuti, soda,maandazi, na fast food zote.
kula zaidi vyakula vya protein kama nyama, samaki, dagaa, maharage na karanga huku ukichanganya na mboga za majani na matunda kwa wingi.
kumbuka ni vizuri kula kidogo kidogo angalau mara sita kwa siku kuliko kula milo mitatu mizito.
pumzika; ni kweli mtoto hua anasumbua sana lakini mtoto akitulia na wewe pumzika ili upate usingizi wa kutosha.
kwa hali ya kawaida kama mama hupati usingizi mwili wako unakua katika hali ambayo sio ya kawaida, hali hii huvutia mafuta katikati ya tumbo na kukufanya uendelee kua mnene.

kunywa chai ya kijani[green tea]; majani haya yamejizolea umaarufu duniani kote kwani huondoa sumu mwilini na kusaidia sana kwenye uchomaji wa chakula kwenye mwili wa binadamu.
kwa kutumia majani ya chai haya kila siku hukusaidia sana kupunguza kitambi cha uzazi.
                                                         
kunywa maji ya uvuguvugu; kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi na hata mchana ukisikia kiu, unaweza kuchanganya na limao kidogo.
maji ya uvuguvugu huongeza kasi ya uchomaji wa mafuta ya mwili kwa kuongeza joto na kuondoa nje sumu ya mwili.
massage ya mwili; massage ni muhimu sana hasa zile sehemu ambazo zinaonekana zina mafuta sana maeneo ya tumboni.
massage pia husaida metabolism  au uunguzaji wa mafuta na ni vizuri ukaikafanyika hasa baada ya mazoezi.
epuka msongo wa mawazo; msongo wa mawazo humwaga homoni aina ya cortisol kwenye damu ya mtu, homoni hiii husababisha kuchoka  na kuongezeka uzito.
hakikisha mambo yako umeyapangilia vizuri na hata kama kuna kitu unaona kinakupa mawazo sana basi usikipe nafasi, amini matatizo yapo kwa kila mtu na yataisha tu.
kula mboga za majani nyingi; mboga za majani husaidia mmengenyo wa chakula, huondoa sumu ambazo zinajikusanya kwenye utumbo mkubwa, pia zina virutubisho vingi na uzito mdogo[calories] kiasi kwamba hata ukila nyingi haziwezi kukunenepesha...hii husaidia kupunguza uzito.
                                                                       
                                                             
mwisho;hakuna uzazi rahisi, mara nyingi ukijifungua lazima uongezeke uzito..hivyo ni wajibu wako kupambana na uzito huo mpaka urudi kwenye hali yako ya kawaida.
kuendelea kua mnene baada ya kujifungua kuna madhara mengine baadae ikiwemo kisukari, shinikizo a damu, ugonjwa wa moyo na uzazi mgumu wa mimba zijazo..

                                                               STAY ALIVE
                                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                        O653095635/0769846183