data:post.body UFAHAMU UGONJWA WA MKANDA WA JESHI NA MATIBABU YAKE.[HERPES ZOSTER] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

UFAHAMU UGONJWA WA MKANDA WA JESHI NA MATIBABU YAKE.[HERPES ZOSTER]

mkanda wa jeshi ni nini?
huu ni ugonjwa wa ngozi na mishipa ya fahamu unaosababishwa na virusi kwa jina la varicella-zoster, virusi hao ndio walewale wanaosababisha ugonjwa tetekuwanga.
kawaida baada ya mtoto kuugua tetekuwanga akiwa mdogo, virusi hivi hua havifi lakini vinabaki kwenye mishipa ya fahamu kwa miaka mingi sana.
siku ikitokea kinga ya mwili wako ikashuka kwa sababu ya umri mkubwa, kula vibaya chakula ambacho hakina kinga kwa mwili, matumizi ya dawa za saratani, na dawa za kushusha kinga ya mwili za jamii ya steroids,magonjwa kama saratani, virusi vya ukimwi na kisukari basi virusi hivi huamka upya na kukushambulia na kuleta mkanda wa jeshi.

dalili za mkanda wa jeshi.
ugonjwa huu hushambulia upande mmoja wa mwili tu ndio maana uliitwa mkanda wa jeshi kwa kiswahili...inaweza kua sura,shingo au mgongo mpka tumboni...kumbuka mkanda wa jeshi haupitilizi upande wa pili wa mwili.
uvimbe kama wa mtu aliyeungua na majimaji hutokea sehemu zilizo athirika huku ukiambatana maumivu makali sana kama ya moto na kuwasha.[moto wa mungu]
dalili zingine ni kama homa kali,kichwa kuuma, misuli kuuma, na kuchoka sana.

mkanda wa jeshi kwa wajawazito.
japokua sio kawaida kwa mama mjamzito kupata mkanda wa jeshi lakini anaweza kupata pia hasa akigusana na mgonjwa husika, hali hii ni hatari kwani husababisha kuathirika kwa mtoto aliyoko tumboni kwa kuzaliwa akiwa na matatizo ya kimaumbile.

jinsi ya kutambua ugonjwa huu
daktari mzoefu anaweza kuutambua ugonjwa huu bila vipimo kabisa na kwa hospitali ambazo zina vifaa vya kutosha majimaji ya upele ule huweza kupimwa ili kuhakikisha ni kweli ugonjwa ni wenyewe.

matibabu ya mkanda wa jeshi
ugonjwa huu hauna dawa, hua unaisha wenyewe ndani ya wiki mbili mpaka tatu..baadhi ya dawa hutolewa kupunguza maumivu makali na kupunguza muda wa kuugua.
dawa hizo ni kama acyclovir,ibuprofen, lidocaine cream na amitriptyline..
matibabu mengine ni kupumika nyumbani, kuweka barafu sehemu athirika kupunguza maumivu, kupaka calamine lotion kupunguza miwasho.

madhara ya mkanda wa jeshi;

  • maumivu makali baada ya kupona; hata baada ya kupona maumivu makali ya sehemu zilizoathirika huendelea na mgonjwa huweza kurudi hospitali kwa kudhani bado ugonjwa haujaisha..matibabu ya hali hii ni dawa mbalimbali za kupoza mfano amitriptyline..
  • upofu; mkanda wa jeshi unaotokea usoni huweza kuharibu kabisa cornea sehemu ya jicho ambayo ipo kama kioo na kumfanya mtu ashindwe kuona tena.
  • homa ya uti wa mgongo
  • kupooza kwa kwa upande mmoja uso na kupoteza uwezo wa kusikia upande mmoja.
  • makovu; baadhi ya watu hubaki na makovu makubwa kama vile waliwahi kuungua na moto.

jinsi ya kuzuia mkanda wa jeshi..

  • chanjo kwa watu wote ambao wako kwenye hatari ya kupata ugonjwa huu kama watoto, umri kwanzia miaka 60 na kwenda mbele, wagonjwa wa ukimwi, saratani na kisukari.
  • mgonjwa anatakiwa akae mbali na watu wengine kwani ugonjwa huu unaweza kuambukizwa.
                                                                           STAY ALIVE
                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                             0653095635/0769846183


0 maoni:

Chapisha Maoni