data:post.body UFAHAMU UGONJWA WA MALARIA NA MATIBABU YAKE. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

UFAHAMU UGONJWA WA MALARIA NA MATIBABU YAKE.

malaria ni moja ya magonjwa hatari zaidi kusini mwa jangwa la sahara ambao umeshambulia watu wengi sana eneo hilo.
tafiti zinaonyesha kwamba kila mwaka watu milion 300 mpaka milion 500 huugua malaria duniani kote na kati ya hao watumilion 1.1 mpaka milioni 2.7 hufa kwa ugonjwa huu kila mwaka.
kati ya vifo hivyo zaidi ya watu milion moja ni chini ya miaka mitano, hii huwakilisha robo ya vifo vyote vya watoto chini ya miaka mitano wanaokufa africa huuawa na ugonjwa wa malaria.
ugonjwa wa malaria ni chanzo kikuu cha homa kali,degedege, upungufu wa damu na vifo.

chanzo cha malaria
malaria huambukizwa na wadudu wa aina wanne wa plasmodium ambao huhamisha ugonjwa kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mtu ambaye sio mgonjwa.
wadudu hao ni plasmodium faciparum, plasmodium malariae,plasmodium vivax, plasmodium ovale.

dalili za malaria.
malaria ni ugonjwa unaoshambulia mfumo mzima wa mwili wa binadamu hivyo huja na dalili mbalimbali za mwili mzima kama ifuatavyo..
kuchoka sana
kichwa kuuma
homa kali
kuumwa jointi za mifupa.
kupoteza hamu ya kula
kizunguzungu

dalili za malaria kali ni kama.
upungufu wa damu
macho ya njano
degedege
kupoteza fahamu
kuchanganganyikiwa.
kutapika kila kitu
presha kushuka sana.

  • kumbuka sio kila mgonjwa atapata dalili zote, mwingine atapata dalili moja tu au mbili.


vipimo vinavyofanyika..
vipimo vya damu kitaalamu kama

  • blood smear; kipimo hiki hupima damu kwa kutumia darubini na kuangalia wadudu wa malaria ambao wamshambulia mwili, huchukua kama dakika 15 mpaka 30 kua tayari.
  • mrdt;kipimo cha haraka sana ambacho hutoa majibu ndani ya dakika tano.
matibabu ya malaria
1.dawa ya mseto wa malaria hutumika kutibu malaria ambayo sio kali sana na ndio dawa ya kwanza kutumika mgonjwa anapougua.

dozi ya dawa ya mseto ni kama ifuatavyo..
miezi mitatu mpaka miaka mitatu kidonge kimoja
miaka mitatu mpaka miaka nane vidonge viwili
miaka saba mpaka miaka kumi na mbili ni vidonge vitatu
miaka 12 na kuendelea ni vidonge vinne.

jinsi ya kutumia.
dawa hizi mgonjwa atazimeza mara sita kwa muda wa siku tatu..
dozi ya kwanza humezwa muda wowote, dozi ya pili baada ya saa nane, dozi ya tatu, ya nne, ya tano na sita kila baada ya saa 12.
hakikisha umetumia dawa zote na kumaliza dozi hata kama umepata nafuu kabla ya kumaliza dozi.
matumizi ya nyama, samaki na maziwa husaidia dawa kufanya kazi vizuri.

watu gani hawaruhusiwi kumeza dawa za mseto?
wajawazito miezi mitatu ya kwanza; hawa wakiugua wanatakiwa wameze vidonge vya kwinini kwani dawa ya mseto ina madhara kwa mimba changa kama hii.
watoto wadogo chini ya kilo tano; hawa hawana uwezo wa kupambana na dawa ya malaria hivyo wanatakiwa wapewe dawa ya kwinini.
watoto chini ya kilo tano wanaonyonya; mama wa watoto hawa hawatakiwi kutumia dawa za mseto kwani dawa hizo huweza kupita kwenye maziwa na kuathiri watoto.
dawa za SP au fansidar kwa sasa hazipo kwenye muongozo wa kutibu malaria hivyo zitumiwe na wajawazito tu kuzuia malaria.

2.dawa zingine zinazotumika dawa ya mseto ikishindwa ni kama kwinini vidonge na sindano, sindano za artusinate, sindano za arthmeter injection.

jinsi ya kuzuia malaria
hakikisha matumizi bora ya net iliyowekwa dawa.
safisha mapori na misitu karibu na nyumba
wagonjwa watibiwe haraka iwezekanavyo
matumizi ya dawa za kuzuia malaria kwa wageni wa nchi husika mfano doxycline.

                                                                    STAY ALIVE

0 maoni:

Chapisha Maoni