data:post.body KWANINI NI HATARI KUFUNGA CHAKULA KWENYE MIFUKO YA ALUMINIUM? ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

KWANINI NI HATARI KUFUNGA CHAKULA KWENYE MIFUKO YA ALUMINIUM?

ukipita mitaa mbalimbali ya nchi zinazoendelea kama Tanzania, utakutana na wapika chips wengi na wateja wao wakifunga chakula hicho kwenye mifuko fulani inayong'aa kwa jina la aluminium.
sasa tafiti zinaonyesha kwamba aluminium ile huvuja na kuhamia kwenye chakula cha mlaji kitu ambacho ni hatari kiafya.
                                               
kwenye nchi zinazoendelea miaka ya nyuma matumizi ya sufuria za madini ya shaba yalikua juu sana lakini siku hizi hali hiyo imepotea sababu ya kuingia kwa masufuria yenye aluminium kwa ndani ambayo ni bei rahisi na rahisi kuosha lakini yakiwa na maswali mengi kuhusu mahusiano yake kiafya.

                     MAHUSIANO KATI YA MIFUKO YA ALUMINIUM NA AFYA YA BINADAMU...
kitaalamu mwili wa binadamu unaweza kuondoa kiasi kidogo sana cha aluminium ndani ya mwili kama 2.4mg kwa siku kwa mtu mzima mwenye kilo 60.
sasa mtu mmoja anaweza kujikuta anapata aluminium nyingi sana kwenye mwili wake sababu ya kuwepo vitu vingi sana ambavyo vinaongeza aluminium ndani ya mwili wake kama chumvi, chai, masufuria, pafyumu za ngozi na dawa za hospitali.
ugonjwa wa alzheimers ni ugonjwa ambao unaharibu sana seli za kwenye ubongo na kumfanya mtu asahau kila kitu mpaka jina lake. wagonjwa wengi wa ugonjwa huu wamekutwa na kiasi kikubwa sana cha aluminium kwenye ubongo wao kitu ambacho kimezua maswali mengi kwamba ugonjwa huu unaweza kua na mahusiano mkubwa sana na matumizi ya aluminium.

                                                    NINI CHA KUFANYA?
mara nyingi aluminium hua inahamia kwenye chakula hasa chakula kikiwa cha moto sana na kikaa muda mrefu kabla ya kuliwa hasa wale wanaobeba kwenda kula nyumbani. ni vizuri kuepuka kabisa kuweka kwenye mifuko hiyo au kufunga kwenye karatasi.
lakini pia usiweke kwenye mifuko ya nylon moja kwa moja sababu ya hatari ya kupata saratani mbalimbali.
                                                           STAY ALIVE

0 maoni:

Chapisha Maoni