data:post.body UKIWA NA MAGONJWA HAYA HUWEZI KUPUNGUA UZITO HATA UFANYE NINI. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

UKIWA NA MAGONJWA HAYA HUWEZI KUPUNGUA UZITO HATA UFANYE NINI.

watu wengi huongezeka uzito na kunenepa sana sababu wanakula chakula kingi kuliko kazi wanazofanya kila siku yaani calories au nguvu wanazokula ni nyingi kuliko wanazochoma kwenye shughuli zao za kila siku.
                                                               
lakini pamoja na sababu hiyo kuna baadhi ya magonjwa ambayo ikitokea yakashambulia mwili wa mtu husika basi hawezi kupungua hata afanye mazoezi gani au ale chakula kidogo kiasi gani.
kuna watu wana magonjwa haya na wamekua wakipambana sana kupungua uzito bila mafanikio na huenda leo wakisoma makala hiziwanaweza kwenda kufanya vipimo ili kuhakiki kama kweli wana magonjwa haya au hapana.
hypothyrodism; huu ni ugonjwa ambao unasababishwa na kupungua kwa homoni[thyroxine na triidothyranine] ambazo zinahusika na kuendesha mfumo wa mwili kitaalamu kama metabolism, homoni hizi zikipungua mwilini,  uwezo wa mwili kufanya kazi na kuchoma mafuta mwilini unapungua kiasi kwamba hata mtu akila chakula kiasi kidogo vipi ataendelea kua mnene.
ugonjwa huu hupata watu wa rika na jinsia zote lakini mara nyingi zaidi huonekana kwa akina mama watu wazima.
ugonjwa huu hupunguzwa makali kwa kumeza dawa za homoni ambazo zinafanana na hizo ambazo zinakua zimepungua mwilini mfano vidonge vya levothyroxine.
ukitaka kujua kama una ugonjwa huu unafanya kipimo kinaitwa thyroid function test.                            kisukari; wagonjwa wa kisukari hutumia dawa za insulini kama moja ya matibabu ya ugonjwa huu, sasa madhara ya dawa hii ambayo hufanya kazi ya kuufanya mwili utumie sukari iliyoko kwenye damu  kupeleka kwenye seli ili kukupa wewe ni nguvu ni kukufanya upate njaa.
sasa njaa ile humfanya mgonjwa kula mara kwa mara na matokeo yake huongezeka sana uzito na kua mnene.
ni vizuri kukaa vizuri na daktari wako ili kujua ni kiasi gani hasa cha dawa kitakufaa ili njaa hii isikupate mara kwa mara.
umri; misuli ya mwili hufanya kazi kubwa ya kuchoma mafuta mwilini, kwa bahati mbaya misuli hii hupungua ukubwa kadri mtu anavyozidi kua mtu mzima na matokeo yake kumfanya mtu huyo kunenepa..
kama umeongezeka unene sasa hivi utagundua kwamba chakula kile kile ulichokila ukiwa kijana mdogo wa miaka 17 ndio hichohicho kinachokunenepesha sasa hivi ukiwa na miaka zaidi ya 25.
hivyo unashauriwa kupunguza wingi wa chakula unachokula kadri unavyozidi kukua na kuongeza kasi ya mazoezi ili kujenga misuli.
cushing syndrome; huu ni ugonjwa ambao husababishwa na kuwepo kwa kiasi kikubwa sana cha homoni za cortisol.
hali hii husababishwa na matumizi ya muda mrefu wa dawa aina ya steroid ambayo hutumika kupunguza makali ya magonjwa mbalimbali kama pumu, aleji na maumivu ya mifupa lakini pia ugonjwa huu huweza kuanza wenyewe bila matumizi ya dawa yeyote kwa kuota kwa uvimbe ndani ya mwili kama saratani ambao hutengeneza homoni hizi za cortisol.
sasa homoni ya cortisol husababisha mafuta kusambaa sehemu mbalimbali za mwili kama kifuani, usoni na tumboni.
unene huu hauwezi kuisha bila kuacha hizi dawa au kufanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe ambao unakua unatengeneza homoni hizi mwilini.
polystic ovarian syndrome; huu ni ugonjwa ambao una athiri mfumo wa kazi wa ovari za mwanamke ambazo hufanya kazi ya kutengeneza mayai ya kike.
ugonjwa huu huleta viuvimbe vidogovidogo vingi ambavyo vinakua vina maji ndani yake karibu na ovari za mwanamke.
dalili za ugonjwa huu ni kuongezeka uzito, kua na manyoya mengi mwilini, kupata hedhi ambazo hazieleweki na kushindwa kubeba mimba.
chanzo halisi cha ugonjwa huu hakifahamiki japakua umehusishwa na kuwepo kiwango kikubwa cha homoni za testosterone na insulin.
mgonjwa huyu huongezeka unene maeneo ya tumboni,,,na kadri uzito unavyozidi kuongezeka mwili unatengeneza homoni nyingi za insulini na kuongezeka unene zaidi.
matumizi ya dawa za uzazi wa mpango husaidia kuziweka sawa homoni za uzazi na kupunguza chunusi, na hatari ya kupata saratani ya kizazi.
mwisho; kama kweli umefanya juhudi kubwa ya kupungua uzito bila mafanikio huenda una magonjwa haya, ni vizuri kwenda kuhakisha kwamba hauna matatizo yeyote ya kiafya ambayo yanakufanya uwe mnene kabla ya kuanza shughuli ya kupunguza unene.
ukigundulika na magonjwa haya na kuanza matibabu basi unaweza kupungua uzito.

                                                         STAY ALIVE

                               DR,KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                              0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni