data:post.body FAHAMU JINSI SINDANO YA MATAKO IVYOWEZA KUKUACHA NA ULEMAVU WA MAISHA. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

FAHAMU JINSI SINDANO YA MATAKO IVYOWEZA KUKUACHA NA ULEMAVU WA MAISHA.

Sindano ya matako ni moja ya sindano ambazo zinachomwa sana, sidhani kama kuna mtu ambaye hajawahi kukutana na sindano hii tangu amezaliwa.
sindano hii hutumika kuingiza dawa mbalimbali za kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo maumivu, magonjwa kama malaria, kaswende, kisonono na mengine mengi.
                                                                 
baadhi ya dawa kama diclofenac na benzathine penicilin hazichomwi kwenye mishipa ya damu na njia pekee ya kuchomwa sindano hizi ni matakoni tu.
bahati mbaya kuna madhara makubwa sana ambayo unaweza kuyapata iwapo ukichomwa vibaya sindano hii.

hali hii hutokea vipi?
mshipa wa fahamu mkubwa kuliko yote kitaalamu kama sciatic nerve unapita katikati ya tako la binadamu ukitokea mgongoni kwenye kipande cha L4 na S3, mshipa huo unafanya kazi kwanzia mgongoni,takoni, pajani na sehemu zote za miguu.
sasa wakati wa kuchoma sindano mchomaji lazima ahakikishe mshipa huu wa fahamu hauguswi na sindano na ikitokea umeuchoma mshipa huu kuna uwezekano mkubwa sana wa kua kilema maisha yako yote.                                                       
hivyo kwa kawaida sindano hii inatakiwa ichomwe upande wa juu wa kulia wa tako au upper outer quadrant.

chanzo ni nini?
kutotulia wakati wa kuchomwa; ukiwa unachomwa sindano ni vizuri kutulia hata kama maumivu ni makali kiasi gani, hii itamfanya mchomaji aweze kuchoma sehemu ambayo ni sahihi.
kuchomwa na mtu ambaye sio mtaalamu; huko mtaani kuna watu wengi ni manesi ambao hawajasoma vyuo vinavyotambulika lakini wanachoma watu sindano kila siku..hii ni hatari sana na inaweza ikaleta madhara makubwa.

dalili za kwamba mshipa wa fahamu umeumia.

 • kupata ngazi kali kwenye upande uliochomwa sindano.
 • mguu kuishiwa nguvu na kulegea.
 • mguu kupinda kuliko kawaida.
 • mguu kuanza kupungua ukubwa sababu hautumiki tena.

vipimo vinavyofanyika kugundua hali hii.

 • magnetic resonant imaging
 • electromyography
matibabu
mishipa ya fahamu ikishaharibika hua haiwezi kupona, mara nyingi matibabu ya kujaribu kusaidia tu ndio yanaweza kutumika..
kitengo cha mazoezi kitaalamu kama physiotherapy ndio kitengo pekee ambacho kinaweza kumpa mgonjwa nafuu japokua huwezi kupona kabisa,

                                                                      STAY ALIVE

                                             DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                            0769846183/0653095635

Maoni 7 :

 1. Mm nimechomwa kwenye tako. Umeweka uvimbe kwa ndani. Ukiushika unasikia ni mkubwa kama ndimu

  JibuFuta
 2. Mm mwanangu kachomwa mguu mmoja anachechemea shida nini

  JibuFuta
 3. Mimi ni miezi miwili imepita tangu nichomwe sindano.nasikia maumivu makali nikijigusa au hata nikiwa nimekaa tu.jamani

  JibuFuta

 4. Je ulemav huo hutokea apo apo

  JibuFuta
 5. Mwanangu amechomwa sindano anamaumivu makali sana. Pia hawezi ata kusimama anamwaka mmoja msaada

  JibuFuta
 6. Mwanangu amechomwa sindano ya ya maralia kwenye paja toka achomwe sindano hiyo analia sana hawezikukaa wala kusimama usk anatokwa jasho sana msaada ndugu ata wa mawazo nipo kigoma 0621316402 naitaji msaada

  JibuFuta