data:post.body Machi 2018 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

SABABU 10 KWANINI MAZIWA YA NG'OMBE NI HATARI KWA AFYA YAKO.

historia ya dunia naonyesha kwamba hapo mwanzo binadamu alikula chakula ambacho kikitokana na mimea tu na kuishi miaka mingi sana, lakini hapo baadae binadamu alianza kula chakula kitokanacho na wanyama na hapo ndio ilikua mwanzo wa kuanza kupata magonjwa ambayo hapo mwanzo alikua hayapati na kupungua kwa umri wa kuishi.
viwanda vya maziwa na wawekezaji wakubwa wa biashara hii, huitangaza sana na kudai kwamba maziwa ni chanzo kikuu cha madini ya kashiamu mwilini hivyo watu wanywe sana, angalau glass tatu kwa siku lakini hakuna ambaye anasema madhara yake faida ya biashara hii ni kubwa sana na hata ukisema hauta sikika.
lakini ukweli uliopo kuhusu maziwa ni tofauti huo unaohubiriwa kwani pamoja kwamba maziwa yana kashiamu,  bado kashiamu hiyo ni ngumu kumeng'enywa na  mwilini ukilinganisha na ile ya mimea na huambatana na madhara makubwa ya kiafya ambayo ukiyaangalia kwa undani hutaona sababu ya kuondelea kunywa maziwa kwani unaweza kupata kashiamu hiyo kwenye vyakula vingine vya kawaida.
maziwa ya wanyama wote tunayokunywa yana madhara yafuatayo...
ugonjwa wa kisukari; madaktari wote wanafahamu na vitabu vyote vimeandika kwamba moja ya sababu ya kuugua kisukari hasa  kwa watoto wadogo ni uwepo wa proteni ya casein kwenye maziwa ambayo hufanya walinzi wa mwili kuushambulia mwili wenyewe kimakosa kwa kudhani kwamba unapambana na adui.
moja ya viungo vinavyoshambuliwa ni kongosho ambalo baadae  hushindwa kutengeneza homoni ya insulini kwa ajili ya kushusha au  kuweka sukari ya binadamu kwenye hali ya kawaida.
kuvunjika kwa mifupa; tafiti moja iliyofanyika nchini sweeden imeonyesha kwamba wanawake wanaokunywa maziwa sana wana hatari ya kuvunjika mifupa ukilinganisha na hawa wengine ambao hawanywi au wanaokunywa kidogo.
lactose intolerance; maziwa yana sukari ambayo inaitwa lactose, ili uweze kunywa maziwa haya lazima uwe na kemikali au enzyme  inayoitwa lactase mwilini mwako kwa ajili ya kumengenya maziwa haya..
baadhi ya watu hawana kabisa kemikali hii au huweza kua ndogo hata ukubwani na kukuletea matatizo kama kuharisha, tumbo kuvimba na kichefuchefu...hata hivyo maziwa ni moja ya vyakula vinavyo ongoza kwa aleji duniani.
kiwango kikubwa cha lehemu au cholestrol; mtaalamu mmoja wa afya aliwahi kusema kwamba maziwa ni nyama ambayo iko kwenye mfumo wa kimiminika na kwamba matatizo mengi yatokanayo na nyama ndio hayohayo yataokanayo na maziwa.
glasi moja ya maziwa in miligram 33 na lehemu au cholestrol ambazo ni hatari kiafya zikiwa nyingi mwilini.
saratani ya ovari; tafiti zingine nchini sweeden zimeonyesha kua wanawake wanaotumia glass mpaka nne za maziwa kwa siku wameugua zaidi saratani hiyo kuliko wanaokunywa kidogo au ambao hawanywi kabisa.
saratani hii haina dalili sana na mara nyingi hugunduliwa hatua za mwisho.
kunenepa sana; tafiti zinaonyesha kwamba unavyokunywa maziwa mengi zaidi ndio jinsi unavyozidi kunenepa sana.
tafiti hizi zilifanyiwa kazi kwa watoto na kugundua kwamba watoto waliokunywa maziwa mengi walinenepa sana na hata walioshauriwa wasinywe soda bali wanywe maziwa basi waliendelea kunenepa vile vile.
kushindwa kwa dawa za antibayotiki; ngombe wengi huchomwa antibayotiki kali na nyingi ili wasiugue magonjwa mbalimbali.
antibayotiki hizo huliwa na binadamu kwenye maziwa na kufanya ziuozoee mwili wa binadamu...katika hali hii mtu akiugua ugonjwa basi zile dawa ambazo tayari amezinywa kwenye maziwa hazitamsaidia.
kuongezeka kwa chunusi za ngozi; tafiti zinaonyesha kwamba utumiaji wa maziwa umeambatana sana kuugua kwa chunusi kwa wanawake na wanaume hasa wale ambao wanavunja ungo.
saratani ya tezi dume; tafiti zinaonyesha kuwepo kwa mahusiano makubwa kati ya unywaji wa maziwa na saratani ya tezi dume... hata wagonjwa wa saratani ya tezi dume ambao walipunguza maziwa kwenye chakula chao walionekana kupata nafuu.
magonjwa ya wanyama; binadamu ndio mnyama pekee ambaye anakunywa maziwa ya mnyama mwingine  mpaka ukubwani.
ukiangalia wanyama wote kama mbwa, mbuzi, ngombe, simba na kadhalika hakuna mnyama ambaye anakunywa maziwa ya mwenzake.
hata ndama mwenyewe kuna umri anafika anaacha kunywa maziwa kwani maziwa ni maalumu kwa ajili ya kumkuza tu, na ndio maana baada ya miaka miwili tu ngombe anakua ashakua mkubwa sana.
magonjwa mengi ambayo ngombe anaugua yanaweza kupita kwenye maziwa..jamii ya bacteria wanaosababisha kifua kikuu kitaalamu kama myobacterium bovis hupatikana kwenye maziwa ya ngombe na ni hatari sana kwa binadamu.

                                                                    STAY ALIVE

                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO.
                                                            0653095635/0769846183

TATIZO LA KUOTA MATITI KWA WANAUME NA MATIBABU YAKE.[GYNACOMASTIA]

GYNACOMASTIA ni nini?
huu ni ugonjwa wa kuvimba matiti kwa wanaume unaosababisha na mvurugiko wa homoni ndani ya mwili wa binadamu.
                                                                 
homoni za oetrogen zinapokua nyingi kwa wanaume kuliko zile homoni za progesterone, mgonjwa anaweza kuvimba matiti yote mawili au akavimba titi moja.
tatizo hili hutokea pia wakati wavulana wakiwa wanabalehe kutokana na mabadiliko ya homoni lakini baadae hali hii huisha yenyewe.
kimsingi tatizo hili sio hatari kwa maisha lakini hutia aibu na kuwafanya wahusika wakose raha kabisa.

dalili za ugonjwa huu.

  • kuvimba kwa matiti na kua makubwa kama ya kike.
  • maumivu kwenye matiti ukigusa sehemu hizo.
chanzo cha tatizo hili.........
kama nilivyosema hapo mwanzo kwamba tatizo hili ni mvurugiko wa homoni za uzazi, homoni hizi zinaweza kuvurugwa na vyanzo mbalimbali kama ifuatavyo.
mabadiliko ya kawaida ya mwili; watu wengi hudhani kwamba homoni za oestrogen ni za wanawake tu kitu ambacho sio kweli, homoni hizi pia wanaume wanazo lakini kwa kiasi kidogo sasa pale homoni hizi zinapokua nyingi kuliko za zile za progesterone hali hii hutokea na wavulana wengi hupitia hali hii wakati wa kubalehe.
matumizi ya dawa; dawa nyingi sana huweza kuleta tatizo hili kama ifuatavyo,
dawa za madonda ya tumbo i,e cimetidine, omeprazole
dawa za msongo wa mawazo i.e amitriptyline
dawa za kansai.e chemotherapy
dawa za moyo i.e nifedipine, amlodipine. digoxin
dawa za kuzuia kutapika i.e metoclopramide
dawa za ukimwi i.e efavirenz
dawa za kupunguza maji mwilini i.e spironalactone
antibayotic; metronidazole
matumizi ya vilevi; baadhi ya vilevi kama pombe,bangi, methadone,na heroin ni chanzo cha kuongezeka na kukua kwa matiti.
matatizo ya kiafya;  magonjwa kama utapiamlo, magonjwa ya maini, magonjwa ya figo,, umri mkubwa, unene na kadhalika.
dawa za miti shamba; baadhi ya dawa za mitishamba ambazo zina changia utengenezaji wa homoni hizi za oestrogen zimekua zikichangia kuongezeka kwa tatizo hili.

nini madhara ya tatizo hili?
tatizo hili halina madhara yeyote sema humfanya mushusika ajisikie vibaya sana na kupata aibu.

jinsi ya kugundua ugonjwa huu.
daktari atakuchukua maelezo na kukufanyia vipimo mbalimbali kuhakikisha tatizo hili, baadhi ya vipimo hufanyika ili kuhakikisha kwamba sio magonjwa mengine ambayo yanakuja na dalili za ugonjwa kama huo..magonjwa kama saratani ya matiti, jipu au unene huweza kuja na dalili kama hizi.
vipimo kama...
  • damu
  • mamogram
  • ct scan
  • mri
  • utrasound
  • biopsy 
matibabu ya tatizo hili..
mara nyingi tatizo hili huondoka lenyewe bila matibabu yeyote japokua huweza kuchukua muda mrefu, lakini ni vyema kuondoa chanzo au kutibu chanzo cha tatizo kama kikionekana kama nilivyotaja kwenye sababu ya tatizo hili.
baadhi ya dawa za kutibu kansa ya matiti kama tamoxifen,raloxefine,arimidex zimesaidia kutibu tatizo hili kwa baadhi ya wanaume japokua dawa hizi hazikutengenezwa kwa ajili ya kazi hiyo.
kama maziwa yakishindikana kutoka au kama mtu anataka kuyatoa haraka basi upasuaji huweza kufanyika kutibu matatizo haya kitaalamu kama mastectomy au liposuction.

                                                           STAY ALIVE

                                   DR,KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                            O653095635/0769846183

FAHAMU JINSI SINDANO YA MATAKO IVYOWEZA KUKUACHA NA ULEMAVU WA MAISHA.

Sindano ya matako ni moja ya sindano ambazo zinachomwa sana, sidhani kama kuna mtu ambaye hajawahi kukutana na sindano hii tangu amezaliwa.
sindano hii hutumika kuingiza dawa mbalimbali za kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo maumivu, magonjwa kama malaria, kaswende, kisonono na mengine mengi.
                                                                 
baadhi ya dawa kama diclofenac na benzathine penicilin hazichomwi kwenye mishipa ya damu na njia pekee ya kuchomwa sindano hizi ni matakoni tu.
bahati mbaya kuna madhara makubwa sana ambayo unaweza kuyapata iwapo ukichomwa vibaya sindano hii.

hali hii hutokea vipi?
mshipa wa fahamu mkubwa kuliko yote kitaalamu kama sciatic nerve unapita katikati ya tako la binadamu ukitokea mgongoni kwenye kipande cha L4 na S3, mshipa huo unafanya kazi kwanzia mgongoni,takoni, pajani na sehemu zote za miguu.
sasa wakati wa kuchoma sindano mchomaji lazima ahakikishe mshipa huu wa fahamu hauguswi na sindano na ikitokea umeuchoma mshipa huu kuna uwezekano mkubwa sana wa kua kilema maisha yako yote.                                                       
hivyo kwa kawaida sindano hii inatakiwa ichomwe upande wa juu wa kulia wa tako au upper outer quadrant.

chanzo ni nini?
kutotulia wakati wa kuchomwa; ukiwa unachomwa sindano ni vizuri kutulia hata kama maumivu ni makali kiasi gani, hii itamfanya mchomaji aweze kuchoma sehemu ambayo ni sahihi.
kuchomwa na mtu ambaye sio mtaalamu; huko mtaani kuna watu wengi ni manesi ambao hawajasoma vyuo vinavyotambulika lakini wanachoma watu sindano kila siku..hii ni hatari sana na inaweza ikaleta madhara makubwa.

dalili za kwamba mshipa wa fahamu umeumia.

  • kupata ngazi kali kwenye upande uliochomwa sindano.
  • mguu kuishiwa nguvu na kulegea.
  • mguu kupinda kuliko kawaida.
  • mguu kuanza kupungua ukubwa sababu hautumiki tena.

vipimo vinavyofanyika kugundua hali hii.

  • magnetic resonant imaging
  • electromyography
matibabu
mishipa ya fahamu ikishaharibika hua haiwezi kupona, mara nyingi matibabu ya kujaribu kusaidia tu ndio yanaweza kutumika..
kitengo cha mazoezi kitaalamu kama physiotherapy ndio kitengo pekee ambacho kinaweza kumpa mgonjwa nafuu japokua huwezi kupona kabisa,

                                                                      STAY ALIVE

                                             DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                            0769846183/0653095635

ZIFAHAMU DAWA KUU 6 ZINAZONENEPESHA SANA.

tunaishi kwenye ulimwengu wa magonjwa mengi sana yasiyotibika ambayo yanakuhitaji kutumia dawa kila siku ili uweze kuishi au kutumia dawa mara kwa mara kwa ajili ya kutibu tatizo fulani la kimwili.                         
                                                               
dawa hizi ni muhimu sana kwa afya yetu lakini bahati mbaya moja ya madhara yake ni kuongezeka unene kitu ambacho watu wengi hawakipendi na ni chanzo cha magonjwa mbalimbali ya kudumu kama moyo na kisukari.
sasa sijaandika makala hii kutishia watu lakini nimeandika makala hii ili watumiaji watumie huku wakijua kwamba dawa hizi zinaweza kuwanenepesha zaidi kama ifuatavyo.
dawa za uzazi wa mpango; karne ya 20 dawa ya kwanza ya kuzuia mimba iligundulika na kuleta mapinduzi makubwa kwenye vita ya kupambana na ongezeko la watu duniani..leo hii dawa hizi zinatumika na mamilioni ya watu duniani kwa matumizi ya kila siku au kwa matumizi ya kuzuia mimba pale wanaposhiriki tendo la ndoa siku za hatar.
bahati mbaya dawa hizi zina tabia ya kuongeza hamu ya kula na kukunenepesha watumiaji...na ukifanya utafiti utagundua wanawake wengi siku hizi ni wanene ukilinganisha na wanaume.
dawa za kutibu kisukari; mtu akigunduliwa na kisukari matibabu ya kwanza sio dawa, matibabu ya kwanza ni chakula na mazoezi..
lakini kwa bahati mbaya watu wengi hukimbilia dawa baada ya kugundulika.
kinachofanyika ni kwamba sukari ikiwa nyingi kwenye damu ukampa mtu dawa ya kuipunguza sukari ile, sukari hutolewa kwenye damu na kupelekwa kwenye seli na kua mafuta huko.
sasa unapoendelea kutumia dawa hizo mafuta mengi zaidi yanaendelea kutengenezwa na dozi yako ya kutumia dawa inazidi kuongezeka sababu ya kuongezeka uzito.
dawa za kutibu presha;  baadhi ya dawa za kutibu presha zimeonekana kuhusika sana na kuongeza uzito watumiaji, mfano wa dawa hizo ni kikundi cha beta blockers kama propanolol, atenolol, carviderol na kadhalika.
dawa hizi hufanya kazi kwa kupunguza kasi ya mapigo ya mwili hii hupunguza kasi ya mwili kuchoma mafuta kitaalamu kama metabolism.
steroids; hizi ni dawa zinazotumika sana kwa shida mbalimbali kama magonjwa ya mifupa, pumu na alleji mbalimbali.
dawa hizi zina tabia ya kuzuia maji mengi kutoka mwilini kwa njia ya mkojo na kuongeza hamu ya kula.
matumizi ya muda mrefu wa dawa hizi huongeza uzito na kupunguza kinga ya mwili kwa kuzuia mwili kupambana na magonjwa.
mfano wa dawa hizi ni dexamethasone, betamethasone, predinisole, triamnisolone na kadhalika.
dawa za msongo wa mawazo; dawa mbalimbali hutumika kwa watu ambao wanasumbuliwa sana na msongo wa mawazo, dawa hizi huongeza kiasi cha homoni ya serotonin ambayo humfanya mtu awe mchangamfu muda mwingi na kupunguza hali yake ya kua kwenye mawazo mengi.
tafiti zinaonyesha kwamba dawa hzi zitakupunguza uzito kwa muda mfupi lakini uzito wako utaongezeka mara dufu baada ya muda mrefu.
mfano wa dawa hizi ni amitriptyline, prozac.fluoxetine na paroxetine.
dawa za wagonjwa wa akili; baadhi ya dawa za magonjwa ya akili zilionekana ni tishio kwa kuongeza uzito kwa mara ya kwanza tu zilipoingia sokoni, dawa hizi zina madhara ya kufanya kazi kwenye ubongo na kukuongeza sana hamu ya kula na hii ndio chanzo kikuu cha unene kwani huwezi kuvumilia kula chakula kidogo.mfano chlropromazine.
mwisho; kama unatumia baadhi ya dawa hapo juu na unahisi ni chanzo cha wewe kunenepa basi ni vema ukaongea na daktari wako ili akutafutie mbadala wa dawa hizo, japokua baadhi ya dawa zinaweza zisiwe na mbadala sahihi sana.

                                                                 STAY ALIVE

                                         DR,KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

UKIWA NA MAGONJWA HAYA HUWEZI KUPUNGUA UZITO HATA UFANYE NINI.

watu wengi huongezeka uzito na kunenepa sana sababu wanakula chakula kingi kuliko kazi wanazofanya kila siku yaani calories au nguvu wanazokula ni nyingi kuliko wanazochoma kwenye shughuli zao za kila siku.
                                                               
lakini pamoja na sababu hiyo kuna baadhi ya magonjwa ambayo ikitokea yakashambulia mwili wa mtu husika basi hawezi kupungua hata afanye mazoezi gani au ale chakula kidogo kiasi gani.
kuna watu wana magonjwa haya na wamekua wakipambana sana kupungua uzito bila mafanikio na huenda leo wakisoma makala hiziwanaweza kwenda kufanya vipimo ili kuhakiki kama kweli wana magonjwa haya au hapana.
hypothyrodism; huu ni ugonjwa ambao unasababishwa na kupungua kwa homoni[thyroxine na triidothyranine] ambazo zinahusika na kuendesha mfumo wa mwili kitaalamu kama metabolism, homoni hizi zikipungua mwilini,  uwezo wa mwili kufanya kazi na kuchoma mafuta mwilini unapungua kiasi kwamba hata mtu akila chakula kiasi kidogo vipi ataendelea kua mnene.
ugonjwa huu hupata watu wa rika na jinsia zote lakini mara nyingi zaidi huonekana kwa akina mama watu wazima.
ugonjwa huu hupunguzwa makali kwa kumeza dawa za homoni ambazo zinafanana na hizo ambazo zinakua zimepungua mwilini mfano vidonge vya levothyroxine.
ukitaka kujua kama una ugonjwa huu unafanya kipimo kinaitwa thyroid function test.                            kisukari; wagonjwa wa kisukari hutumia dawa za insulini kama moja ya matibabu ya ugonjwa huu, sasa madhara ya dawa hii ambayo hufanya kazi ya kuufanya mwili utumie sukari iliyoko kwenye damu  kupeleka kwenye seli ili kukupa wewe ni nguvu ni kukufanya upate njaa.
sasa njaa ile humfanya mgonjwa kula mara kwa mara na matokeo yake huongezeka sana uzito na kua mnene.
ni vizuri kukaa vizuri na daktari wako ili kujua ni kiasi gani hasa cha dawa kitakufaa ili njaa hii isikupate mara kwa mara.
umri; misuli ya mwili hufanya kazi kubwa ya kuchoma mafuta mwilini, kwa bahati mbaya misuli hii hupungua ukubwa kadri mtu anavyozidi kua mtu mzima na matokeo yake kumfanya mtu huyo kunenepa..
kama umeongezeka unene sasa hivi utagundua kwamba chakula kile kile ulichokila ukiwa kijana mdogo wa miaka 17 ndio hichohicho kinachokunenepesha sasa hivi ukiwa na miaka zaidi ya 25.
hivyo unashauriwa kupunguza wingi wa chakula unachokula kadri unavyozidi kukua na kuongeza kasi ya mazoezi ili kujenga misuli.
cushing syndrome; huu ni ugonjwa ambao husababishwa na kuwepo kwa kiasi kikubwa sana cha homoni za cortisol.
hali hii husababishwa na matumizi ya muda mrefu wa dawa aina ya steroid ambayo hutumika kupunguza makali ya magonjwa mbalimbali kama pumu, aleji na maumivu ya mifupa lakini pia ugonjwa huu huweza kuanza wenyewe bila matumizi ya dawa yeyote kwa kuota kwa uvimbe ndani ya mwili kama saratani ambao hutengeneza homoni hizi za cortisol.
sasa homoni ya cortisol husababisha mafuta kusambaa sehemu mbalimbali za mwili kama kifuani, usoni na tumboni.
unene huu hauwezi kuisha bila kuacha hizi dawa au kufanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe ambao unakua unatengeneza homoni hizi mwilini.
polystic ovarian syndrome; huu ni ugonjwa ambao una athiri mfumo wa kazi wa ovari za mwanamke ambazo hufanya kazi ya kutengeneza mayai ya kike.
ugonjwa huu huleta viuvimbe vidogovidogo vingi ambavyo vinakua vina maji ndani yake karibu na ovari za mwanamke.
dalili za ugonjwa huu ni kuongezeka uzito, kua na manyoya mengi mwilini, kupata hedhi ambazo hazieleweki na kushindwa kubeba mimba.
chanzo halisi cha ugonjwa huu hakifahamiki japakua umehusishwa na kuwepo kiwango kikubwa cha homoni za testosterone na insulin.
mgonjwa huyu huongezeka unene maeneo ya tumboni,,,na kadri uzito unavyozidi kuongezeka mwili unatengeneza homoni nyingi za insulini na kuongezeka unene zaidi.
matumizi ya dawa za uzazi wa mpango husaidia kuziweka sawa homoni za uzazi na kupunguza chunusi, na hatari ya kupata saratani ya kizazi.
mwisho; kama kweli umefanya juhudi kubwa ya kupungua uzito bila mafanikio huenda una magonjwa haya, ni vizuri kwenda kuhakisha kwamba hauna matatizo yeyote ya kiafya ambayo yanakufanya uwe mnene kabla ya kuanza shughuli ya kupunguza unene.
ukigundulika na magonjwa haya na kuanza matibabu basi unaweza kupungua uzito.

                                                         STAY ALIVE

                               DR,KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                              0653095635/0769846183