data:post.body YAFAHAMU MADHARA YA KIAFYA YA KUVAA NGUO ZINAZOBANA SANA. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

YAFAHAMU MADHARA YA KIAFYA YA KUVAA NGUO ZINAZOBANA SANA.

je unajua?
pamoja na kwamba nguo zakubana sana sasa hivi na fasheni na ni chaguo kubwa la watu wengi sana hasa wanawake lakini nguo hizi ni hatari sana kiafya na ni chanzo cha matatizo mengine ya kiafya.unaweza kua unaona zimekupendeza na kukufanya uonekane vizuri zaidi lakini bado zinaweza kua tatizo kwako.
madhara haya ni makubwa zaidi hasa unapovaa nguo ngumu ambazo zinabana mwili kama jeans, na zingine za aina hiyo.
madhara hayo ni kama yafuatayo..
nguo za kubana zinazuia damu kurudi kwenye moyo; kurudisha damu kwenye moyo ni moja ya kazi muhimu sana za moyo, nguo zinapokuabana sana na damu kushindwa kurudi utajikuta unavimba miguu na baadhi ya sehemu za unyonya.
hivyo ili kupambana na hii basi moyo wako utajikuta unafanya kazi zaidi kitu ambacho sio kizuri kwa afya ya moyo.
husababisha kuonekana kwa mishipa ya vena[ varicose veins]; hii ni mishipa ambayo inavimba na kuonekana miguuni, homone ya progesterone inahusika sana kufanya mishipa hii ivimbe na kuonekana.
sasa hali hii inaweza kuongezwa makali kwa kuvaa nguo zinazobana sana, kutumia dawa za uzazi wa mpango na kusimama kwa muda mrefu.
hukufanya ushindwe kupumua vizuri; presha kubwa kwenye mapafu na koo la hewa huweza kukufanya ukashindwa kupumua, hii itakufanya ukose hewa ya kutosha na hii inaweza kufanya kitu kinaitwa oxidation ambacho kinafanya mtu aanze kuzeeka haraka. kiufupi nguo za kubana hazikufanyi uwe huru.
husababisha maumivu ya mgongo; unaweza kuhisi hivi vitu havina mahusiano lakini ukweli ni kwamba. ukivaa nguo za kubana sana miguu yako inashindwa kua free kufanya movements unazotaka, sasa hii inaufanya mgongo kufanya kazi ngumu zaidi ili wewe uweze kupata sapoti. mfano mtu aliyevaa nguo iliyobana sana hawezi kuruka shimo au ataruka kwa tabu sana na huu ni mzigo kwa mgongo.
hupunguza kasi ya mmengenyo wa chakula au digestion; ukiwa unakula tumbo linataka uhuru yaani liweze kupanuka sababu ya tindikali inayohitajika wakati wa kusaga chakula lakini kama umebanwa tumbo chakula haliwezi kupita vizuri hii huweza kusababisha kiungulia, maumivu ya tumbo, choo ngumu, chakula kukaa tumboni muda mrefu na kadhalika.
husababisha fangasi sehemu za siri; nguo zinazobana sana huleta joto na unyevunyevu sehemu za siri kitu ambacho husaidia ukuaji wa fangasi na bacteria kwa wakati mmoja, mtu huyu huweza kujikuta analalamika kuugua magonjwa ya sehemu za siri mara kwa mara.
kwa wanaume nguo hizi huathiri ubora wa mbegu za kiume na maumivu ya korodani.
matatizo ya ngozi; ngozi ianyobanwa sana haina afya njema kwani haipewi muda wa kupigwa na hewa safi sababu ya nguo ambazo sio kwamba ni ngumu tu lakini hazipitishi hata hewa kwenda ndani.
ngozi kuwasha, kua nyekundu, na nywele za ngozi kushindwa kuota vizuri ni moja ya matatizo ya nguo hizi.
huongeza kutokwa na jasho mwilini; harufu kali ya kwapa, miguu, na sehemu za siri ni moja ya vitu vinavyosababishwa na kuvaa nguo zinazobana sana sababu ya ngozi kubanwa sana.
kuharibu shepu ya mwili; nguo inayobana sana ni kama p.o.p au muhogo ambao wanafungwa watu waliovunjika...kama umechunguza sana, mkono uliovunjika ukitolewa p.o.p unakua mdogo sana kuliko mkono mwingine vivyo hivo nguo zinazobana sana zinahamisha mafuta ya muguni na mapajani kwenda tumboni na kumfanya mtu aonekane kama simba.
mwisho; kama unapenda nguo zinazobana sana basi achana na jeans, jaribu kuvaa ngu nyepesi kama skin tight ambazo unazivaa kirahisi sana, unakua huru kufanya unachotaka na miguu lakini pia hazikubani mwili wako.

                                                             STAY ALIVE

                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                     0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni