ukiangalia historia ya dunia kama miaka 100 iliyopita, dunia ilikua na wagonjwa wa saratani wachache sana ukilinganisha na hivi sasa.
ugonjwa wa saratani ni tishio tangu zamani lakini kwa sasa unaathiri watu wengi zaidi duniani na kuufanya kua tishio zaidi kuliko miaka ya zamani.
sisi wote tunafahamu kwamba ugonjwa wa saratani hutibika tu pale unapo onekana mapema sana na kwa sababu hauna dalili sio rahisi kuutambua mapema.
kitaalamu ugonjwa wa saratani unaonyesha dalili ukiwa umefika kwenye hatua za mwisho kabisa na watu wengi hufariki kwa kuchelewa kugunduliwa.
ukiwa ugonjwa wa pili duniani kwa kuua watu, kansa huua zaidi ya watu mililion 8 kila mwaka kwa takwimu za mwaka 2015.
70% ya vifo hivyo vilitokea kwa watu wa uchumi wa chini kabisa na wale wa uchumi wa kati na 22% ya kansa hizo zilitokana na uvutaji wa sigara.
kansa zinazoongoza kuua ni kansa ya mapafu, kansa ya maini, kansa ya utumbo mkubwa, kansa ya tumbo na kansa ya matiti.
saratani ni nini?
haya ni mabadiliko ya seli za binadamu kutoka zile za kwaida kwenda kwenye aina ya seli ambazo sio za kawaida ambazo mara nyingi hazifi ili kupisha zingine, matokeo yake hua nyingi sana na kuleta uvimbe au kansa..mabadiliko haya ya seli kitaalamu huitwa mutation.
kwanini kansa miaka ya hivi karibuni zimekua juu sana hivi karibuni?
vyakula; vyakula vingi vinavyoliwa sasa hivi na watu wengi sio vyakula asili yaani ni vya kiwandani au vya kukaangwa sana..hii husababisha vyakula hivi kukaa sana tumboni sababu havina nyuzinyuzi au fibres ambazo kitaalamu husaidia chakula kupita haraka sana tumboni.
sasa chakula kikikaa sana tumboni kinaanza kuharibu njia za utumbo na kuleta kansa ya utumbo. vyakula vya nyuzi nyuzi kama matunda na mboga za majani husaidia kukinga kansa hizi.
mfano mtu anayekula chips na kuku au chips na nyama kila siku bila mboga za majani yuko kwenye hatari kubwa sana ya kuugua kansa.
kuongezeka kwa umri wa kuishi; kimsingi kansa ni ugonjwa wa watu wenye umri mkubwa kwanzia miaka 40 na kwenda mbele[japokua hata watoto wanapata] sababu wameishi sana na miili yao imeshapata changamoto ya kemikali mbalimbali na kinga zao zimeanza kushuka. sasa hapo zamani wazee walikua wachache sana lakini sababu ya mabadiliko ya teknolojia na ubora wa huduma za afya sasa watu wanaishi miaka mingi kuliko zamani hasa nchi zilizoendelea.
ugunduzi wa dawa za uzazi wa mpango; mwaka 1960 kidonge cha kwanza kiliruhusiwa kuanza kutumiaka kwa ajili ya kuzuia mimba ambacho kina homoni ya oestrogen au progesterone, lakini kitaalamu ni kwamba hormone hii ya oestrogen imekua ikihusishwa sana na kuanza kwa kansa kwani kwa kawaida hufanya uzalishaji mwingi wa seli ndani ya mfuko wa uzazi wakati wa siku za hedhi kitaalamu kama hyperpalsia...uzalishaji huu ndio chanzo cha kansa hata kwa wanawake ambao hawatumii dawa hizi.
kuanzishwa kwa chanjo; chanjo ziligunduliwa baada ya binadamu kuteswa sana na magonjwa mbalimbali ambayo baadae walifanikiwa kuyaondoa kwa chanjo kama polio, surua, donda koo, pepopunda na kadhalika lakini baadae ilikuja kugundulika kwamba baadhi ya kemikali ambazo zinapatikana kwenye chanjo mfano formaldhyde zina mahusiano na kuanza kwa kansa kwenye mwili wa binadamu kitaalamu kama carcinogenic.
ongezeko kubwa la unywaji wa pombe; pombe ilianza kutumika tangu zamani lakini miaka ya hivi karibuni zimetokea pombe nyingi na pombe imekua moja ya starehe kuu, sasa pombe inaweza kuharibu maini moja kwa moja na kusababisha kansa ya ini..lakini pia ini likichoka linashindwa kuondoa sumu mbalimbali mwilini kitu ambacho huweza kuleta kansa.
mabadiliko ya mfumo wa maisha; baadhi ya vyanzo vikuu vya kansa ni kutofanya mazoezi kabisa, hapo zamani mfumo wa maisha ulitegemea sana kazi za nguvu kuliko akili..watu walikua wakimaliza kula asubuhi wanaenda kufanya kazi shambani mpaka jioni hivyo miili yao ilikua vizuri, lakini mfumo wa sasa wa kushinda ofisini au dukani siku nzima hufanya mwili kutokua na kinga kubwa ya mazoezi na kuugua kansa.
kuanza kushiriki tendo la ndoa mapema;miaka ya zamani kuanza tendo la ndoa ilikua ni kitu ambacho kinachelewa sana kuanza yaani lazima umeoa sasa kwa jamii za siku hizi kuanza ngono mapema kabla ya ndoa imekua kitu cha kawaida na hii huchangia maambukizi ya virusi vya human papailoma virus ambao ni moja ya chanzo kikuu cha saratani ya malango wa uzazi.
vipodozi; dunia ya sasa inaongozwa sana na urembo yaani sekta ya urembo kwa sasa inafanya biashara kubwa kuliko sekta nyingi sana, sasa huko kumevamiwa na vipodozi vingi sana ambavyo sio salama hasa hivi vya kujichubua ngozi ambavyo hupambana na sehemu muhimu ya ngozi inayotukinga na miale mikali ya jua.
serikali nyingi zimekua ikipiga marufuku vipodozi hivyo lakini ndio moja ya chanzo kikuu cha saratani ya ngozi.
kubeba chakula kwenye plastic; sababu ya ubize sana wa miaka hii ya karibuni watu wengi hufungiwa vyakula kwenye mifuko na kwenda kula hasa nyakati za mchana wanapokua makazini. lakini tafiti zinaonyesha kwamba mifuko ya plastic ikichemka hutoa gesi ambayo ikiingia kwenye chakula ni hatari na hata maji ya kunywa ambayo yanakua yamekaa kwenye jua au gari lenye joto na kuchemka hua yana hatari ya kusababisha saratani.
mwisho; kwa maisha ya sasa na teknolojia iliyopo ni vigumu sana kujikinga na hatari za kupata kansa au saratani mbalimbali hivyo kitu unachoweza kufanya ni kukaa mbali na vyanzo vya kansa kama kufanya mazoezi, kula mboga za majani na matunda, epuka sigara, epuka ulevi wa kupitiliza, kula vyakula asilia, tumia vipodozi asilia,usichemshe sana chakula na epuka ulaji mkubwa wa nyama hasa nyama nyekundu na kitu kingine cha msingi kufanya ni kufanya vipimo au check up ya mwili wote angalau mara moja kwa mwaka.
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0653095635/0769846183
0 maoni:
Chapisha Maoni