data:post.body LIFAHAMU TATIZO LA KUVIMBA KIZAZI NA MATIBABU YAKE.[UTERINE FIBROIDS] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

LIFAHAMU TATIZO LA KUVIMBA KIZAZI NA MATIBABU YAKE.[UTERINE FIBROIDS]

uterine fibroids ni nini?
huu ni uvimbe ambao unatokea kwenye kizazi cha mwanamke, inaweza kua ndani au nje ya kizazi, kwa jina lingine kama leiomyoma.
                                                               
huu ndio uvimbe unaowapata wanawake mara nyingi zaidi kuliko uvimbe wa aina yeyote wa kizazi, unawapata zaidi ya 25% ya wanawake wote ambao wako kwenye kipindi cha kuzaa na inatokea mara tisa zaidi kwa wanawake weusi kuliko wanawake weupe..kuna chembechembe za kurithi kwenye ugonjwa huu.

mambo hatarishi yanayoweza kumfanya mtu kuugua ugonjwa huu.

 • kua na umri zaidi ya miaka 30.
 • kuzaa watoto wachache sana
 • ugumba
 • unene
 • historia ya kua na ugonjwa kwenye ukoo.
kuna aina nne za uvimbe wa aina hii ya kizazi.
 • submucosal; hii ni ya aina ya uvimbe ambao unatokea ndani ya ukuta wa ndani kabisa wa kizazi kitaalamu kama endometrium.
 • intramural; huu ni uvimbe unaotokea ndani kabisa ya ukuta wa kizazi kitaalamu kama myometrium.
 • subserosal; huu ni uvimbe unaotokea juu ya ukuta wa ndani wa kizazi kitalamu kama endometrium
 • penduculated; huu ni uvimbe unaoota juu ya kizazi na kua na kamba ndefu za kuning'inia mpaka pembeni ya kizazi.
                                                                 
dalili za aina hizi za uvimbe wa kizazi
mara nyingi uvimbe huu wa kizazi hauna dalili lakini unaweza kutokea na dalili zifuatazo kwa mgonjwa mwenye uvimbe huo.
 • kutokwa na damu nyingi sana na nzito sehemu za siri.
 • upungufu wa damu.
 • kupata choo ngumu.
 • kubanwa na mkojo wa ghafla au kushidwa kutoa mkojo.
 • maumivu chini ya kitovu.
 • maumivu wakati wa tendo la ndoa na kutokwa na uchafu sehemu za siri.
vipimo vinavyofanyika...
 • picha ya utrasound kuangalia ndani ya kizazi.
 • picha ya x ray kwa baadhi ya kesi.
madhara ya uvimbe wa kizazi kwa watu wa kawaida..
 • kuishiwa damu sana
 • maumivu makali ya tumbo la uzazi
 • ugumba
 • kubadilika na kua saratani.
madhara ya uvimbe huu kwa wanawake wajawazito.
 • kuharibika kwa mimba
 • uchungu kuanza kabla ya wakati.
 • mtoto kutanguliza mkono au matako wakati wa kuzaliwa.
 • kutokwa na damu nyingi sana baada ya kuzaa.
 • mimba kutungwa nje ya kizazi.
matibabu ya uvimbe huu
kuwepo kwa ugonjwa huu haimaanishi kwamba unahitaji kutibiwa, uvimbe huu unaweza kuachwa kwa muda mrefu bila matatizo yeyote na usitibiwe kabisa..lakini kuna baadhi ya mazingira ambayo yanaweza kusababisha matibabu haya yafanyike kama ifuatavyo..
 • kutokwa na damu nyingi sana
 • kuendelea kuvimba sana kwa uvimbe.
 • kuendelea kuvimba baada ya mwanamke kufika miaka 60.
 • ugumba
 • mimba kuharibika mara kwa mara.
 • kuishiwa sana damu.
matibabu ya uvimbe huu.
 • upasuaji wa kuondoa sehemu ya uvimbe ya kizazi kitaalamu kama myomectomy hufanyika mara nyingi kwa wanawake ambao bado wanahitaji mtoto lakini kwa wanawake ambao bado hawahitaji kuzaa, kizazi hutolewa kabisa...hakuna dawa yeyote ya kienyeji au ya kisasa inayoweza kumaliza uvimbe huu bila upasuaji.
 • kwa wanawake ambao ni wazee sana au ambao hawako tayari kufanyiwa upasuji basi dawa za uzazi wa mpango huweza kuwasaidia.
                                                      STAY ALIVE
                             DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                               0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni