data:post.body HAYA NDIO MADHARA YA MIONZI YA X RAY NA CT SCAN KWENYE MWILI WA BINADAMU. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HAYA NDIO MADHARA YA MIONZI YA X RAY NA CT SCAN KWENYE MWILI WA BINADAMU.

mionzi hii ni ipi?
hii ni mionzi kitaalamu kama electromagnetic radiation ambayo huweza kupita katikati ya mifupa yake na kutoa picha za binadamu husika.
                                                             
mwili wa binadamu unavyonza mionzi hiyo na kwa hali moja au nyingine mionzi hiyo huweza kua hatari kwa mwili wa binadamu.

aina tatu za mionzi hii hospitali ni hii
radiography; ambayo hutoa picha za x ray
fluoroscopy; ambayo huonyesha picha zinazotembea kwenye mwili wa binadamu.
CT scan;hii hutoa picha zenye bora zaidi na rahisi kusomeka kuliko ct scan.

picha ipi kati ya hizo ni mionzi mikali?
picha moja ya ct scan ina mionzi mikali sana mara 100 au 1000 kuliko ile mionzi ya radiography and fkuoroscopy.

faida za mionzi hii ni nini?
kama tunavyofahamu wote mionzi hii hutumika sehemu hospital kugundua magonjwa mbalimbali ya mwili kama baridi yabisi[arthritis], kuvunjika mifupa, kugundua matatizo ya madonda ya tumbo, kugundua matatizo ya kuziba mirija ya uzazi, kuangalia matatizo ya meno, kupima kifua kikuu, kupima kupanuka kwa moyo,kupima saratani za matiti, kuangalia vitu vilivyomezwa ambavyo sio vya kawaida hasa wa watoto lakini pia hutumika kuangalia maendeleo ya mgonjwa hayo baada ya matibabu kuanza.

nini madhara ya mionzi hii?
mionzi hua ina madhara mbalimbali kwenye mwili wa binadamu yale ya kawaida na yale ya kutisha kabisa, madhara ya mionzi hutegemea kiasi cha mionzi ambayo imekupata kiasi kwamba kadri unavyozidi kufanyiwa vipimo zaidi ndio unazidi kuathirika zaidi na mionzi hii.
madhara hayo ni kama kuungua ngozi, utasa na ugumba, kupata kipara kichwani, mtoto wa jicho[cataract] na saratani za aina mbalimbali ambazo mara nyingi huua haraka sana.
saratani hutokea pale mionzi inapoharibu mfumo wa seli za binadamu kuzaana matokeo yake seli hizo huanza kuzaliana kwa wingi sana bila kufa na matokeo yake huleta uvimbe ambayo ndio dalili muhimu ya saratani.[DNA mutation]

je unatakiwa upige x ray au ct scan ngapi kwa mwaka?
kimsingi hakuna idadi kamili ya x ray za kupiga kwa mwaka kwani mara nyingi mpaka unaaandikiwa kupiga x ray daktari anakua ameshaona kwamba utapata faida kwa kupiga x ray kuliko ukisema usipige kabisa.
kikubwa cha kuzingatia ni kuhakikisha unapiga x ray chache zaidi na upige kweli pale zinapohitajika.

je kuna mbadala wa mionzi hii?
ndio vipimo kama mri na utrasound havina mionzi hivyo havina madhara kiafya na huweza kupima vitu vingi ambavyo vinapimwa kwa x ray na CT scan.

naweza kupigwa x ray au ct scan nikiwa mjamzito?
kiukweli x ray au ct scan haitakiwi kwa mama mjamzito kutokana na madhara makubwa ambayo yanaweza kumpata kiumbe ambaye yuko tumboni, na ukiona umeandikiwa x ray au ct scan ukiwa mjamzito basi ujue daktari ameona uko kwenye hatari kubwa na siku zote maisha ya mama ni muhimu zaidi kuliko maisha ya kile kichanga chake.

                                                             STAY ALIVE

                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                       0653095635/0769846183
                                                    

Maoni 5 :

  1. Je kwa mtu mwenye matatizo ya kusumbuliwa na mgongo apime kipimo gani?

    JibuFuta
    Majibu
    1. x ray, mri au ct scan.. inategemea na uzito wa tatizo

      Futa
  2. Kikohozi sugu cha zaidi ya miaka 15 hupimwa kwa x ray?

    JibuFuta
  3. ninasumbuliwa na mifupa ya kiuno upande wa kulia mifupa ilitenguka jenaweza kupima kipimo gani?

    JibuFuta
  4. Binafsi nimeenda hospital kumpima mama angu ajiwezi kuinuka hivyo wakanambia nimshike ili wapige x ray na wakapiga na wakarudia tena inaweza niletea matatizo???

    JibuFuta