data:post.body HAYA NDIO MADHARA YA KUVAA MIKANDA YA KUPUNGUZA TUMBO.[WAIST TRAINER BELT] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HAYA NDIO MADHARA YA KUVAA MIKANDA YA KUPUNGUZA TUMBO.[WAIST TRAINER BELT]

tangu kim karadashian alivyoonekana kwenye mitandao ya kijamii na kiuno chembamba sana sababu ya kuvaa waist training belt, basi ndio imkeua fasheni kubwa duniani kote kwa ujumla.
watu maarufu wengine pamoja na watu mbalimbali wamekua wakipiga picha wakiwa wamevaa mikanda hiyo.
                                                                     
sasa ni kweli kwamba mikanda hiyo ikivaliwa muda wa kutosha huonyesha matokeo mazuri kwa kufanya eneo la tumbo na kiuno kua dogo sana na mtu kuonekana mrembo zaidi lakini jamii ya wataalamu wa afya wameipinga njia hii na kuituhumu kwamba ina madhara makubwa ya kiafya hivyo kutoa onyo kwa watumiaji kwamba watumie lakini wajue kwamba kuna madhara makubwa ya kiafya ambayo yameonekana sana.
kimsingi ni kwamba mikanda hii sio mipya na iliwahi kuwepo zamani sana kwenye karne ya 16 lakini ilikua na mitindo tofauti lakini baadae ilipotea na sasa ndio imerudi kwa mtimdo tofauti.
nini madhara ya mikanda hii?
haipunguzi mafuta kama watu wanavyodhani; ukivaa mkanda ule ni kwamba mafuta yanabanwa na kuhama sehemu ya tumbo lakini hayatoki mwilini na baada ya muda mrefu ukiacha kutumia mkanda huo mafuta yatarudi palepale kama zamani yaani mwili utajirudisha kama zamani.
                                                     
haipunguzi uzito; tafiti zinaonyesha kwamba mkanda huo umetengenezwa na aina ya vitambaa ambavyo vinamfanya mtu atokwe jasho sana hasa wakati wa mazoezi, watu waliovaa mikanda hiyo wamekiri kutokwa jasho sana kuliko kawaida.
sasa kutokwa jasho kunafanya upunguze maji mwilini ambayo yakipungua MWILINI na uzito pia unapungua lakini kupungua uzito sababu ya kupungua maji hakuna faida yeyote kiafya zaidi ya hasara na ukinywa maji uzito uanrudi.
huweza kuhamisha viungo kitu ambacho ni hatari; ukivaa mkanda basi viungo vya juu huhamia juu zaidi na viungo vya chini huhamia chini zaidi, hii ina madhara sana kwani muhusika huanza kushindwa kula vyakula vya mafuta, kupata choo ngumu sana na kupata kiungulia sana, lakini pia katika hali isiyo ya kawaida huweza kuziba utumbo kabisa kwa kuukunja kitaalamu kama intestinal obstruction.
                                                               
huweza kuathiri misuli ya tumbo na mgongo;kuvaa mkanda wa waist training hufanya mwili kutegemea mkanda huo wakati mtu akiwa amekaa au anatembea na matokeo yake misuli hiyo inakua haifanyi kazi..
kutokufanya kazi huko matokeo yake misuli hiyo inaanza kupungua ukubwa na kua midogo kuliko mwanzoni.
humfanya mtu ashindwe kupumua vizuri; ili uweze kupumua vizuri lazima kifua na tumbo viweze kua huru kupanuka kwa kiwango chochote kile, sasa mkanda huu hukufanya kupumua juu juu hasa kipindi cha mazoezi ambapo unakua unahitaji hewa zaidi.
kukosa hewa ya kutosha humfanya mtu kuzeeka haraka na ngozi yake kutokua nzuri.
sio nzuri kwa vijana wanaokua; ikianza kutumika mapema kabla mtu hajakua vizuri yaani kabla ya miaka 18 huweza kuathiri ukuaji wa baadhi ya misuli moja kwa moja ambayo bado inakua, hivyo inashauriwa kutumia baada ya miaka 18 kuepueka madhara zaidi.
                                                         
madhara mengine ya kiafya; mkanda huu unaweza kusababisha madhara mengine ya kiafya kama shida ya mapafu, figo na ngozi bila kusahau kwamba mkanda huu unauma wakati mwingine na hata wanaotengeneza hawashauri kuvaliwa muda wote.
wataalamu wa afya hawakubaliani na mkanda huu; wataalamu wanasema kwamba mkanda huu una hasara nyingi kuliko faida, hivyo wanasema kwamba kama umeamua kuvaa basi vaa ukijua kwamba sio salama na una madhara mengi.
sio rahisi kuacha[addiction]; watumiaji wa mkanda huu wanasema kwamba ukishauzoea unakua mtumwa kwani huweze kuacha na muda wote utajikuta umevaa tu.
mwisho; pamoja na madhara yaliyoko hapo bado kuna watu ambao hawawezi kuacha kuvaa na wanashauriwa mabo yafuatayo vaa kwa muda mfupi kwa siku, epuka kufanya mazoezi ukiwa umeuvaa kwani mwili wako haupati hewa ya kutosha, usiukaze sana, usivae wakati bado unakua yaani kabla ya miaka 18, hakikisha unakunywa maji mengi sana kwani mkanda unakufanya utokwe jasho sana, lakini pia usiutumie kama mbadala wa mazoezi na diet kwani mkanda hauwezi kua na faida kama za mazoezi na diet.

                                                                       STAY ALIVE

Maoni 1 :