data:post.body Februari 2018 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

LIFAHAMU TATIZO LA KUVIMBA KIZAZI NA MATIBABU YAKE.[UTERINE FIBROIDS]

uterine fibroids ni nini?
huu ni uvimbe ambao unatokea kwenye kizazi cha mwanamke, inaweza kua ndani au nje ya kizazi, kwa jina lingine kama leiomyoma.
                                                               
huu ndio uvimbe unaowapata wanawake mara nyingi zaidi kuliko uvimbe wa aina yeyote wa kizazi, unawapata zaidi ya 25% ya wanawake wote ambao wako kwenye kipindi cha kuzaa na inatokea mara tisa zaidi kwa wanawake weusi kuliko wanawake weupe..kuna chembechembe za kurithi kwenye ugonjwa huu.

mambo hatarishi yanayoweza kumfanya mtu kuugua ugonjwa huu.

  • kua na umri zaidi ya miaka 30.
  • kuzaa watoto wachache sana
  • ugumba
  • unene
  • historia ya kua na ugonjwa kwenye ukoo.
kuna aina nne za uvimbe wa aina hii ya kizazi.
  • submucosal; hii ni ya aina ya uvimbe ambao unatokea ndani ya ukuta wa ndani kabisa wa kizazi kitaalamu kama endometrium.
  • intramural; huu ni uvimbe unaotokea ndani kabisa ya ukuta wa kizazi kitaalamu kama myometrium.
  • subserosal; huu ni uvimbe unaotokea juu ya ukuta wa ndani wa kizazi kitalamu kama endometrium
  • penduculated; huu ni uvimbe unaoota juu ya kizazi na kua na kamba ndefu za kuning'inia mpaka pembeni ya kizazi.
                                                                 
dalili za aina hizi za uvimbe wa kizazi
mara nyingi uvimbe huu wa kizazi hauna dalili lakini unaweza kutokea na dalili zifuatazo kwa mgonjwa mwenye uvimbe huo.
  • kutokwa na damu nyingi sana na nzito sehemu za siri.
  • upungufu wa damu.
  • kupata choo ngumu.
  • kubanwa na mkojo wa ghafla au kushidwa kutoa mkojo.
  • maumivu chini ya kitovu.
  • maumivu wakati wa tendo la ndoa na kutokwa na uchafu sehemu za siri.
vipimo vinavyofanyika...
  • picha ya utrasound kuangalia ndani ya kizazi.
  • picha ya x ray kwa baadhi ya kesi.
madhara ya uvimbe wa kizazi kwa watu wa kawaida..
  • kuishiwa damu sana
  • maumivu makali ya tumbo la uzazi
  • ugumba
  • kubadilika na kua saratani.
madhara ya uvimbe huu kwa wanawake wajawazito.
  • kuharibika kwa mimba
  • uchungu kuanza kabla ya wakati.
  • mtoto kutanguliza mkono au matako wakati wa kuzaliwa.
  • kutokwa na damu nyingi sana baada ya kuzaa.
  • mimba kutungwa nje ya kizazi.
matibabu ya uvimbe huu
kuwepo kwa ugonjwa huu haimaanishi kwamba unahitaji kutibiwa, uvimbe huu unaweza kuachwa kwa muda mrefu bila matatizo yeyote na usitibiwe kabisa..lakini kuna baadhi ya mazingira ambayo yanaweza kusababisha matibabu haya yafanyike kama ifuatavyo..
  • kutokwa na damu nyingi sana
  • kuendelea kuvimba sana kwa uvimbe.
  • kuendelea kuvimba baada ya mwanamke kufika miaka 60.
  • ugumba
  • mimba kuharibika mara kwa mara.
  • kuishiwa sana damu.
matibabu ya uvimbe huu.
  • upasuaji wa kuondoa sehemu ya uvimbe ya kizazi kitaalamu kama myomectomy hufanyika mara nyingi kwa wanawake ambao bado wanahitaji mtoto lakini kwa wanawake ambao bado hawahitaji kuzaa, kizazi hutolewa kabisa...hakuna dawa yeyote ya kienyeji au ya kisasa inayoweza kumaliza uvimbe huu bila upasuaji.
  • kwa wanawake ambao ni wazee sana au ambao hawako tayari kufanyiwa upasuji basi dawa za uzazi wa mpango huweza kuwasaidia.
                                                      STAY ALIVE
                             DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                               0653095635/0769846183

SABABU 10 ZA KUONGEZEKA KWA MAGONJWA YA SARATANI AU KANSA MIAKA HII YA KARIBUNI

                                                             
ukiangalia historia ya dunia kama miaka 100 iliyopita, dunia ilikua na wagonjwa wa saratani wachache sana ukilinganisha na hivi sasa.
ugonjwa wa saratani ni tishio tangu zamani lakini kwa sasa unaathiri watu wengi zaidi duniani na kuufanya kua tishio zaidi kuliko miaka ya zamani.
                                                                 
sisi wote tunafahamu kwamba ugonjwa wa saratani hutibika tu pale unapo onekana mapema sana na kwa sababu hauna dalili sio rahisi kuutambua mapema.
kitaalamu ugonjwa wa saratani unaonyesha dalili ukiwa umefika kwenye hatua za mwisho kabisa na watu wengi hufariki kwa kuchelewa kugunduliwa.
ukiwa ugonjwa wa pili duniani kwa kuua watu, kansa huua zaidi ya watu mililion 8 kila mwaka kwa takwimu za mwaka 2015.
70% ya vifo hivyo vilitokea kwa watu wa uchumi wa chini kabisa na wale wa uchumi wa kati na 22% ya kansa hizo zilitokana na uvutaji wa sigara.                                                                 
kansa zinazoongoza kuua ni kansa ya mapafu, kansa ya maini, kansa ya utumbo mkubwa, kansa ya tumbo na kansa ya matiti.
saratani ni nini?
haya ni mabadiliko ya seli za binadamu kutoka zile za kwaida kwenda kwenye aina ya seli ambazo sio za kawaida ambazo mara nyingi hazifi ili kupisha zingine, matokeo yake hua nyingi sana na kuleta uvimbe au kansa..mabadiliko haya ya seli kitaalamu huitwa mutation.
kwanini kansa miaka ya hivi karibuni zimekua juu sana hivi karibuni?
vyakula; vyakula vingi vinavyoliwa sasa hivi na watu wengi sio vyakula asili yaani ni vya kiwandani au vya kukaangwa sana..hii husababisha vyakula hivi kukaa sana tumboni sababu havina nyuzinyuzi au fibres ambazo kitaalamu husaidia chakula kupita haraka sana tumboni.
sasa chakula kikikaa sana tumboni kinaanza kuharibu njia za utumbo na kuleta kansa ya utumbo. vyakula vya nyuzi nyuzi kama matunda na mboga za majani husaidia kukinga kansa hizi.
mfano mtu anayekula chips na kuku au chips na nyama kila siku bila mboga za majani yuko kwenye hatari kubwa sana ya kuugua kansa.
kuongezeka kwa umri wa kuishi; kimsingi kansa ni ugonjwa wa watu wenye umri mkubwa kwanzia miaka 40 na kwenda mbele[japokua hata watoto wanapata]  sababu wameishi sana na miili yao imeshapata changamoto ya kemikali mbalimbali na kinga zao zimeanza kushuka. sasa hapo zamani wazee walikua wachache sana lakini sababu ya mabadiliko ya teknolojia na ubora wa huduma za afya  sasa watu wanaishi miaka mingi kuliko zamani hasa nchi zilizoendelea.
                 
ugunduzi wa dawa za uzazi wa mpango; mwaka 1960 kidonge cha kwanza kiliruhusiwa kuanza kutumiaka kwa ajili ya kuzuia mimba ambacho kina homoni ya oestrogen au progesterone, lakini kitaalamu ni kwamba hormone hii ya oestrogen imekua ikihusishwa sana na kuanza kwa kansa kwani kwa kawaida hufanya uzalishaji mwingi wa seli ndani ya mfuko wa uzazi wakati wa siku za hedhi kitaalamu kama hyperpalsia...uzalishaji huu ndio chanzo cha kansa hata kwa wanawake ambao hawatumii dawa hizi.
kuanzishwa kwa chanjo; chanjo ziligunduliwa baada ya binadamu kuteswa sana na magonjwa mbalimbali ambayo baadae walifanikiwa kuyaondoa kwa chanjo kama polio, surua, donda koo, pepopunda na kadhalika lakini baadae ilikuja kugundulika kwamba baadhi ya kemikali ambazo zinapatikana kwenye chanjo mfano formaldhyde zina mahusiano na kuanza kwa kansa kwenye mwili wa binadamu kitaalamu kama carcinogenic.
kuongezeka kwa teknolojia ya ugunduzi wa magonjwa; hapo zamani ilikua sio rahisi kujua kwamba mtu ameugua na kufa kwa kansa sababu ya teknolojia kidogo iliyokuwepo na hata kwa nchi za africa kwa sasa bado kuna watu wengi wanakufa vijijini baada ya kuugua sana na watu hawajui kwamba hao watu walikua wanaumwa nini lakini angalau teknolojia imekua na watu wengi sasa wanaweza kugunduliwa na magonjwa ya kansa.
ongezeko kubwa la unywaji wa pombe; pombe ilianza kutumika tangu zamani lakini miaka ya hivi karibuni zimetokea pombe nyingi na pombe imekua moja ya starehe kuu, sasa pombe inaweza kuharibu maini moja kwa moja na kusababisha kansa ya ini..lakini pia ini likichoka linashindwa kuondoa sumu mbalimbali mwilini kitu ambacho huweza kuleta kansa.
                                                   
mabadiliko ya mfumo wa maisha; baadhi ya vyanzo vikuu vya kansa ni kutofanya mazoezi kabisa, hapo zamani mfumo wa maisha ulitegemea sana kazi za nguvu kuliko akili..watu walikua wakimaliza kula asubuhi wanaenda kufanya kazi shambani mpaka jioni hivyo miili yao ilikua vizuri, lakini mfumo wa sasa wa kushinda ofisini au dukani siku nzima hufanya mwili kutokua na kinga kubwa ya mazoezi na kuugua kansa.
             
kuanza kushiriki tendo la ndoa mapema;miaka ya zamani kuanza tendo la ndoa ilikua ni kitu ambacho kinachelewa sana kuanza yaani lazima umeoa sasa kwa jamii za siku hizi kuanza ngono mapema kabla ya ndoa imekua kitu cha kawaida na hii huchangia maambukizi ya virusi vya human papailoma virus ambao ni moja ya chanzo kikuu cha saratani ya malango wa uzazi.
                                                           
vipodozi; dunia ya sasa inaongozwa sana na urembo yaani sekta ya urembo kwa sasa inafanya biashara kubwa kuliko sekta nyingi sana, sasa huko kumevamiwa na vipodozi vingi sana ambavyo sio salama hasa hivi vya kujichubua ngozi ambavyo hupambana na sehemu muhimu ya ngozi inayotukinga na miale mikali ya jua.
serikali nyingi zimekua ikipiga marufuku vipodozi hivyo lakini ndio moja ya chanzo kikuu cha saratani ya ngozi.                                                 
kubeba chakula kwenye plastic; sababu ya ubize sana wa miaka hii ya karibuni watu wengi hufungiwa vyakula kwenye mifuko na kwenda kula hasa nyakati za mchana wanapokua makazini. lakini tafiti zinaonyesha kwamba mifuko ya plastic ikichemka hutoa gesi ambayo ikiingia kwenye chakula ni hatari na hata maji ya kunywa ambayo yanakua yamekaa kwenye jua au gari lenye joto na kuchemka hua yana hatari ya kusababisha saratani.
mwisho; kwa maisha ya sasa na teknolojia iliyopo ni vigumu sana kujikinga na hatari za kupata kansa au saratani mbalimbali hivyo kitu unachoweza kufanya ni kukaa mbali na vyanzo vya kansa kama kufanya mazoezi, kula mboga za majani na matunda, epuka sigara, epuka ulevi wa kupitiliza, kula vyakula asilia, tumia vipodozi asilia,usichemshe sana chakula na epuka ulaji mkubwa wa nyama hasa nyama nyekundu na kitu kingine cha msingi kufanya ni kufanya vipimo au check up ya mwili wote angalau mara moja kwa mwaka.

                                                                STAY ALIVE

                                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                        0653095635/0769846183

HAYA NDIO MADHARA YA KUVAA MIKANDA YA KUPUNGUZA TUMBO.[WAIST TRAINER BELT]

tangu kim karadashian alivyoonekana kwenye mitandao ya kijamii na kiuno chembamba sana sababu ya kuvaa waist training belt, basi ndio imkeua fasheni kubwa duniani kote kwa ujumla.
watu maarufu wengine pamoja na watu mbalimbali wamekua wakipiga picha wakiwa wamevaa mikanda hiyo.
                                                                     
sasa ni kweli kwamba mikanda hiyo ikivaliwa muda wa kutosha huonyesha matokeo mazuri kwa kufanya eneo la tumbo na kiuno kua dogo sana na mtu kuonekana mrembo zaidi lakini jamii ya wataalamu wa afya wameipinga njia hii na kuituhumu kwamba ina madhara makubwa ya kiafya hivyo kutoa onyo kwa watumiaji kwamba watumie lakini wajue kwamba kuna madhara makubwa ya kiafya ambayo yameonekana sana.
kimsingi ni kwamba mikanda hii sio mipya na iliwahi kuwepo zamani sana kwenye karne ya 16 lakini ilikua na mitindo tofauti lakini baadae ilipotea na sasa ndio imerudi kwa mtimdo tofauti.
nini madhara ya mikanda hii?
haipunguzi mafuta kama watu wanavyodhani; ukivaa mkanda ule ni kwamba mafuta yanabanwa na kuhama sehemu ya tumbo lakini hayatoki mwilini na baada ya muda mrefu ukiacha kutumia mkanda huo mafuta yatarudi palepale kama zamani yaani mwili utajirudisha kama zamani.
                                                     
haipunguzi uzito; tafiti zinaonyesha kwamba mkanda huo umetengenezwa na aina ya vitambaa ambavyo vinamfanya mtu atokwe jasho sana hasa wakati wa mazoezi, watu waliovaa mikanda hiyo wamekiri kutokwa jasho sana kuliko kawaida.
sasa kutokwa jasho kunafanya upunguze maji mwilini ambayo yakipungua MWILINI na uzito pia unapungua lakini kupungua uzito sababu ya kupungua maji hakuna faida yeyote kiafya zaidi ya hasara na ukinywa maji uzito uanrudi.
huweza kuhamisha viungo kitu ambacho ni hatari; ukivaa mkanda basi viungo vya juu huhamia juu zaidi na viungo vya chini huhamia chini zaidi, hii ina madhara sana kwani muhusika huanza kushindwa kula vyakula vya mafuta, kupata choo ngumu sana na kupata kiungulia sana, lakini pia katika hali isiyo ya kawaida huweza kuziba utumbo kabisa kwa kuukunja kitaalamu kama intestinal obstruction.
                                                               
huweza kuathiri misuli ya tumbo na mgongo;kuvaa mkanda wa waist training hufanya mwili kutegemea mkanda huo wakati mtu akiwa amekaa au anatembea na matokeo yake misuli hiyo inakua haifanyi kazi..
kutokufanya kazi huko matokeo yake misuli hiyo inaanza kupungua ukubwa na kua midogo kuliko mwanzoni.
humfanya mtu ashindwe kupumua vizuri; ili uweze kupumua vizuri lazima kifua na tumbo viweze kua huru kupanuka kwa kiwango chochote kile, sasa mkanda huu hukufanya kupumua juu juu hasa kipindi cha mazoezi ambapo unakua unahitaji hewa zaidi.
kukosa hewa ya kutosha humfanya mtu kuzeeka haraka na ngozi yake kutokua nzuri.
sio nzuri kwa vijana wanaokua; ikianza kutumika mapema kabla mtu hajakua vizuri yaani kabla ya miaka 18 huweza kuathiri ukuaji wa baadhi ya misuli moja kwa moja ambayo bado inakua, hivyo inashauriwa kutumia baada ya miaka 18 kuepueka madhara zaidi.
                                                         
madhara mengine ya kiafya; mkanda huu unaweza kusababisha madhara mengine ya kiafya kama shida ya mapafu, figo na ngozi bila kusahau kwamba mkanda huu unauma wakati mwingine na hata wanaotengeneza hawashauri kuvaliwa muda wote.
wataalamu wa afya hawakubaliani na mkanda huu; wataalamu wanasema kwamba mkanda huu una hasara nyingi kuliko faida, hivyo wanasema kwamba kama umeamua kuvaa basi vaa ukijua kwamba sio salama na una madhara mengi.
sio rahisi kuacha[addiction]; watumiaji wa mkanda huu wanasema kwamba ukishauzoea unakua mtumwa kwani huweze kuacha na muda wote utajikuta umevaa tu.
mwisho; pamoja na madhara yaliyoko hapo bado kuna watu ambao hawawezi kuacha kuvaa na wanashauriwa mabo yafuatayo vaa kwa muda mfupi kwa siku, epuka kufanya mazoezi ukiwa umeuvaa kwani mwili wako haupati hewa ya kutosha, usiukaze sana, usivae wakati bado unakua yaani kabla ya miaka 18, hakikisha unakunywa maji mengi sana kwani mkanda unakufanya utokwe jasho sana, lakini pia usiutumie kama mbadala wa mazoezi na diet kwani mkanda hauwezi kua na faida kama za mazoezi na diet.

                                                                       STAY ALIVE

YAFAHAMU MADHARA YA KIAFYA YA KUVAA NGUO ZINAZOBANA SANA.

je unajua?
pamoja na kwamba nguo zakubana sana sasa hivi na fasheni na ni chaguo kubwa la watu wengi sana hasa wanawake lakini nguo hizi ni hatari sana kiafya na ni chanzo cha matatizo mengine ya kiafya.unaweza kua unaona zimekupendeza na kukufanya uonekane vizuri zaidi lakini bado zinaweza kua tatizo kwako.
madhara haya ni makubwa zaidi hasa unapovaa nguo ngumu ambazo zinabana mwili kama jeans, na zingine za aina hiyo.
madhara hayo ni kama yafuatayo..
nguo za kubana zinazuia damu kurudi kwenye moyo; kurudisha damu kwenye moyo ni moja ya kazi muhimu sana za moyo, nguo zinapokuabana sana na damu kushindwa kurudi utajikuta unavimba miguu na baadhi ya sehemu za unyonya.
hivyo ili kupambana na hii basi moyo wako utajikuta unafanya kazi zaidi kitu ambacho sio kizuri kwa afya ya moyo.
husababisha kuonekana kwa mishipa ya vena[ varicose veins]; hii ni mishipa ambayo inavimba na kuonekana miguuni, homone ya progesterone inahusika sana kufanya mishipa hii ivimbe na kuonekana.
sasa hali hii inaweza kuongezwa makali kwa kuvaa nguo zinazobana sana, kutumia dawa za uzazi wa mpango na kusimama kwa muda mrefu.
hukufanya ushindwe kupumua vizuri; presha kubwa kwenye mapafu na koo la hewa huweza kukufanya ukashindwa kupumua, hii itakufanya ukose hewa ya kutosha na hii inaweza kufanya kitu kinaitwa oxidation ambacho kinafanya mtu aanze kuzeeka haraka. kiufupi nguo za kubana hazikufanyi uwe huru.
husababisha maumivu ya mgongo; unaweza kuhisi hivi vitu havina mahusiano lakini ukweli ni kwamba. ukivaa nguo za kubana sana miguu yako inashindwa kua free kufanya movements unazotaka, sasa hii inaufanya mgongo kufanya kazi ngumu zaidi ili wewe uweze kupata sapoti. mfano mtu aliyevaa nguo iliyobana sana hawezi kuruka shimo au ataruka kwa tabu sana na huu ni mzigo kwa mgongo.
hupunguza kasi ya mmengenyo wa chakula au digestion; ukiwa unakula tumbo linataka uhuru yaani liweze kupanuka sababu ya tindikali inayohitajika wakati wa kusaga chakula lakini kama umebanwa tumbo chakula haliwezi kupita vizuri hii huweza kusababisha kiungulia, maumivu ya tumbo, choo ngumu, chakula kukaa tumboni muda mrefu na kadhalika.
husababisha fangasi sehemu za siri; nguo zinazobana sana huleta joto na unyevunyevu sehemu za siri kitu ambacho husaidia ukuaji wa fangasi na bacteria kwa wakati mmoja, mtu huyu huweza kujikuta analalamika kuugua magonjwa ya sehemu za siri mara kwa mara.
kwa wanaume nguo hizi huathiri ubora wa mbegu za kiume na maumivu ya korodani.
matatizo ya ngozi; ngozi ianyobanwa sana haina afya njema kwani haipewi muda wa kupigwa na hewa safi sababu ya nguo ambazo sio kwamba ni ngumu tu lakini hazipitishi hata hewa kwenda ndani.
ngozi kuwasha, kua nyekundu, na nywele za ngozi kushindwa kuota vizuri ni moja ya matatizo ya nguo hizi.
huongeza kutokwa na jasho mwilini; harufu kali ya kwapa, miguu, na sehemu za siri ni moja ya vitu vinavyosababishwa na kuvaa nguo zinazobana sana sababu ya ngozi kubanwa sana.
kuharibu shepu ya mwili; nguo inayobana sana ni kama p.o.p au muhogo ambao wanafungwa watu waliovunjika...kama umechunguza sana, mkono uliovunjika ukitolewa p.o.p unakua mdogo sana kuliko mkono mwingine vivyo hivo nguo zinazobana sana zinahamisha mafuta ya muguni na mapajani kwenda tumboni na kumfanya mtu aonekane kama simba.
mwisho; kama unapenda nguo zinazobana sana basi achana na jeans, jaribu kuvaa ngu nyepesi kama skin tight ambazo unazivaa kirahisi sana, unakua huru kufanya unachotaka na miguu lakini pia hazikubani mwili wako.

                                                             STAY ALIVE

                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                     0653095635/0769846183

HAYA NDIO MADHARA YA MIONZI YA X RAY NA CT SCAN KWENYE MWILI WA BINADAMU.

mionzi hii ni ipi?
hii ni mionzi kitaalamu kama electromagnetic radiation ambayo huweza kupita katikati ya mifupa yake na kutoa picha za binadamu husika.
                                                             
mwili wa binadamu unavyonza mionzi hiyo na kwa hali moja au nyingine mionzi hiyo huweza kua hatari kwa mwili wa binadamu.

aina tatu za mionzi hii hospitali ni hii
radiography; ambayo hutoa picha za x ray
fluoroscopy; ambayo huonyesha picha zinazotembea kwenye mwili wa binadamu.
CT scan;hii hutoa picha zenye bora zaidi na rahisi kusomeka kuliko ct scan.

picha ipi kati ya hizo ni mionzi mikali?
picha moja ya ct scan ina mionzi mikali sana mara 100 au 1000 kuliko ile mionzi ya radiography and fkuoroscopy.

faida za mionzi hii ni nini?
kama tunavyofahamu wote mionzi hii hutumika sehemu hospital kugundua magonjwa mbalimbali ya mwili kama baridi yabisi[arthritis], kuvunjika mifupa, kugundua matatizo ya madonda ya tumbo, kugundua matatizo ya kuziba mirija ya uzazi, kuangalia matatizo ya meno, kupima kifua kikuu, kupima kupanuka kwa moyo,kupima saratani za matiti, kuangalia vitu vilivyomezwa ambavyo sio vya kawaida hasa wa watoto lakini pia hutumika kuangalia maendeleo ya mgonjwa hayo baada ya matibabu kuanza.

nini madhara ya mionzi hii?
mionzi hua ina madhara mbalimbali kwenye mwili wa binadamu yale ya kawaida na yale ya kutisha kabisa, madhara ya mionzi hutegemea kiasi cha mionzi ambayo imekupata kiasi kwamba kadri unavyozidi kufanyiwa vipimo zaidi ndio unazidi kuathirika zaidi na mionzi hii.
madhara hayo ni kama kuungua ngozi, utasa na ugumba, kupata kipara kichwani, mtoto wa jicho[cataract] na saratani za aina mbalimbali ambazo mara nyingi huua haraka sana.
saratani hutokea pale mionzi inapoharibu mfumo wa seli za binadamu kuzaana matokeo yake seli hizo huanza kuzaliana kwa wingi sana bila kufa na matokeo yake huleta uvimbe ambayo ndio dalili muhimu ya saratani.[DNA mutation]

je unatakiwa upige x ray au ct scan ngapi kwa mwaka?
kimsingi hakuna idadi kamili ya x ray za kupiga kwa mwaka kwani mara nyingi mpaka unaaandikiwa kupiga x ray daktari anakua ameshaona kwamba utapata faida kwa kupiga x ray kuliko ukisema usipige kabisa.
kikubwa cha kuzingatia ni kuhakikisha unapiga x ray chache zaidi na upige kweli pale zinapohitajika.

je kuna mbadala wa mionzi hii?
ndio vipimo kama mri na utrasound havina mionzi hivyo havina madhara kiafya na huweza kupima vitu vingi ambavyo vinapimwa kwa x ray na CT scan.

naweza kupigwa x ray au ct scan nikiwa mjamzito?
kiukweli x ray au ct scan haitakiwi kwa mama mjamzito kutokana na madhara makubwa ambayo yanaweza kumpata kiumbe ambaye yuko tumboni, na ukiona umeandikiwa x ray au ct scan ukiwa mjamzito basi ujue daktari ameona uko kwenye hatari kubwa na siku zote maisha ya mama ni muhimu zaidi kuliko maisha ya kile kichanga chake.

                                                             STAY ALIVE

                              DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                       0653095635/0769846183
                                                    

JINSIA YA KIUME KUPOTEA KABISA DUNIANI.[TAFITI]

 chromosome Y ni vimelea vinavyohusika na kutoa jinsia ya kiume kwa viumbe vyote dunaini, yaani yenyewe ndio inafanya viumbe vya jinsia ya kiume kuendelea kuzaliwa na kuishi duniani.
lakini tafiti mpya zinaonyesha kwamba chromosome Y inapukutika au kupungua kwa kasi sana kiasi kwamba imeanza kuzua maswali ya uwepo wake miaka ya mbele.
                                                                     
                                                                     
makala iliyotolewa na chuo kikuu cha kent wiki iliyopita inasema kwamba japokua chromosome Y ndio inayohusika kuleta jinsia ya kiume sio muhimu kwa maisha ya binadamu ndio maana mwanamke anaishi na chromosome X bila shida yeyote.
binadamu wa kwanza alipoumbwa ukubwa au wingi wa chromsome X ambazo zinatoa mwanamke na chromosome Y ambazo zinatoa mwanamke zilikua zinalingana.
lakini muda unavyozidi kwenda chromosome Y za kiume zimekosa kitu kinaitwa genetic shuffling yaani kuzalishwa na kutengeneza upya chromosome Y.
                                                                 
hali hii imezifanya chromosome Y zianze kupungua na kubaki chromosome X za wanawake tu.
watafiti wanaongeza kwamba kama chromosome Y inayotoa jinsia za kiume ikiendelea kupungua kwa kasi hiyohiyo basi wanaume watapotea kabisa duniani baada ya miaka milioni nne na laki sita na kabla ya hapo wataendelea kupungua kwa kasi zaidi.
                                                                   
mtafiti Jenny Graves kutoaka chuo kikuu cha trobe huko Australia anasema panya aina ya spiny rats wanaopatiakana huko nchini japan wamepoteza kabisa chromosome Y na panya wote waliobaki ni wa kike kiasi kwamba kuzaliana kwao kumesimama na huenda wakapoea ulimwenguni.
teknolojia ya kutengeneza mbegu za kiume maabara ndio inategemewa kua tegemeo kubwa la panya hao kwa sasa.
                                                           STAY ALIVE