data:post.body LIFAHAMU TATIZO LA KUNUKA KIKWAPA NA MATIBABU YAKE... ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

LIFAHAMU TATIZO LA KUNUKA KIKWAPA NA MATIBABU YAKE...

kunuka kikwapa ni nini?
hii ni harufu kali inayotoka kwenye sehemu ya juu kabisa ya mkono kwa chini au kwa jina la kikwapa...                                                           

chanzo ni nini?
kimsingi harufu hii hutokana na bacteria kutumia jasho la binadamu na kutengeneza aina fulani ya tindikali ambayo hutoa harufu.
katika hali ya kawaida jasho binadamu hua halina harufu mpaka pale linapokutana na bacteria ambao hushambualia jasho lako.
mara nyingi binadamu huanza kutoka harufu sana akibalehe au kuvunja ungo ambapo manyoya huanza kuota kwenye kikwapa lakini pia watu wanene sana, wanaokula vyakula vyenye viungo vingi na wenye baadhi ya magonjwa kama kisukari.
harufu kwenye mwili wa binadamu ukiachana na makwapa pia hutoka sehemu za siri, miguuni, kwenye mikunjo ya nyama kwa wanene, nyuma ya masikio, sehemu ya haja kubwa, katikati ya mapaja, na kwenye nywele za sehemu za siri.
apocrine gland ni sehemu ya mwili ambayo inatengeneza jasho, huapatikana sehemu mbalimbali za mwili kama kwapa, ngozi, matiti,na kadhalika.

jinsi ya kuzuia harufu...
 • weka safi kwapa lako kwa kuosha na maji safi na sabuni ya kuua bacteria.
 • tumia deodorant na body spray, mara nyingi hupunguza wingi wa jasho na kukupa harufu nzuri.
 • oga kila siku angalau mara mbili asubuhi na jioni kwa maji ya moto kwani maji ya moto yanasaidia sana kuu bacteria walioko kwenye ngozi.
 • vaa nguo nyepesi ambazo zinakupa nafasi ya mwili kukausha joto kwa upepo, hivyo usivae nguo nzito sana.
 • usile vyakula vyenye viungo vingi sana kama kitunguu swaumu lakini pia utafiti umeonyesha kwamba ulaji mwingi wa nyama nyekundu huweza kuongezea harufu ya mwili.
 • kunywa maji mengi sana kwani yanasaidia kusafisha mwili wako.
 • nyoa manyoya ya kwapani kila yakiota kwani ni kihifadhi cha harufu kali.
matibabu.
 • upasuaji; wakati mwingine upasuaji kitaalamu kama endoscopic thoracic sympathectomy ambayo hufunga mishipa ya fahamu ambayo hufanya jasho litoke jingi hufanyika kutibu tatizo hili..
 • baadhi ya magonjwa ya figo, maini, fangasi, kufunga kwa hedhi kwa akina mama wa umri mkubwa huweza kusababisha hali hii hivyo muone daktari kwa vipimo zaidi na matibabu kama haupati nafuu.
ni wakati gani unatakiwa umuone daktari...?
 • kutokwa na jasho sana wakati wa usiku.
 • kutokwa jasho zaidi kuliko mwanzoni.
 • jasho linaanza kukuzuia na kazi zako za kawaida.
 • kutokwa na jasho sana wakati wa baridi.
 • kuwashwa sana na ngozi.
                                                                
                                                                   STAY ALIVE

                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0653095635/0769846183



0 maoni:

Chapisha Maoni