data:post.body HIZI NDIO DAWA 3 ZA KISASA ZINAZOSAIDIA WANAWAKE KUZAA BILA UCHUNGU KABISA. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HIZI NDIO DAWA 3 ZA KISASA ZINAZOSAIDIA WANAWAKE KUZAA BILA UCHUNGU KABISA.

dunia nzima inafahamu kwamba mwanamke atazaa kwa uchungu tu hata iweje, na vitabu vya dini vimeandikwa hivyo lakini kwa miaka ya hivi karibuni na mabadiliko ya tecnolojia hali hii imeanza kupotea kutokana na uwezekano mkubwa wa kumfanya mwanamke huyu kusubiri masaa yote ambayo mtoto anakua anshuka kutoka kwenye kizazi kwenda nje bila kusikia maumivu ya uchungu hata kidogo.
                                                             

kitaalamu maumivu ya uchungu huchukua masaa 8 mpaka 12 kwa mtoto wa kwanza na masaa 6 mpaka 8 kwa mtoto wa pili na kuendelea, kipindi hiki ni kigumu sana kwa mama.
huenda kwa nchi za kiafrika bado hatujaanza kutumia mfumo huu wa kuondoa maumivu ya uchungu  sababu ya ukomo wa bajeti na mila zetu lakini kwa nchi zilizoendelea au kwa hospitali binafsi hata hapa nchini inawezekana kabisa ukapata huduma hiii.
kimsingi maumivu ya kuzaa ni makali sana kiasi kwamba hufika hatua mama anaomba akapasuliwe kitu ambacho sio cha kawaida kuombwa kwa binadamu mwenye akili nzuri lakini pia ukitaka kujua uchungu ni mkali sana kuna wakati njia ya mwanamke inaongezwa kwa kukata sehemu ya uuke bila ganzi mwanamke haonekani kushtushwa kabisa na maumivu yale.
sasa zifuatazo ni njia ambazo hutumika kwenye wodi ya wazazi kuwapunguzia au kuwaondolea uchungu kabisa na kujikuta wanazaa bila kusikia kitu.
epidural block; hii ni njia inayotumiwa sana na wanawake wengi nchini marekani, ni njia ambayo sehemu ya ndani ya uti wa mgongo kitaalamu kama epidural space huingiziwa dawa ya ngazi ambayo imeandaliwa maalumu kwa kazi hiyo, mara nyingi dawa ya pubivacaine hutumika.
njia hii kwa hapa kwetu tanzania hutumika kabla ya kuwafanyia upasuaji wa kutoa mtoto wajawazito ambao wanakua wameshindwa kusukuma mtoto.
dawa ikishaingia maumivu ya uchungu huondoka kwa asilimia 90 mpk 100 na kumfanya mama kukaa akisubiri kusukuma mtoto bila maumivu hata kidogo.
baada ya dawa kuanza kufanya kazi hutaweza kuinua miguu yako wala hutaweza kuisikia miguu hata ikiguswa mpaka dawa itakapoisha, mara nyingi daktari huweka mpira[catheter] wa kuongeza dawa kila baada ya muda fulani kwani sindano moja ya kwanza haitoshi mpaka kujifungua.
kuna madhara ya njia hii? 
sio kila mtu anaweza kupewa dawa hii... kama ushafanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo, una tatizo la kuganda kwa damu au aleji ya dawa hizo huwezi kupewa.
madhara madogo madogo kama kichwa kuuma, presha ya mwili kushuka na kuwashwa kwa mgongo huweza kutokea.
opiods; hizi ni dawa za maumivu zenye nguvu sana ambazo hutumika kutuliza maumivu mbalimbali ya mwili lakini kwa sasa zinatumika kwenye uchungu pia, hazina nguvu sana kama nilizotaja hapo juu lakini huweza kuondoa maumivu ya uchungu kabisa kwa muda wa saa mbili, mara nyingi dawa hizi hutumika kwa mama ambaye amekaa kwenye maumivu ya uchungu kwa muda mrefu sasa anataka kupumzika au wakati uchungu ndio unaanza.
sindano kwa jina la morphine au pethidine huchomwa kwenye paja au tako na kukata maumivu kabisa.
madhara yake;
dawa hii inaweza ikaenda mpaka ndani ya mtoto na kumlevya hivyo hazitakiwi kutolewa pale ambapo mama anakua yuko anakaribia kusukuma mtoto kitaalamu kama second stage of labour lakini pia kichefuchefu na kutapika huweza kutokea.
nitrous oxide; hii ni dawa inayofahamika kwa utani kama laughing gas, hutolewa kwa njia ya maski ambapo mama mjamzito hupewa mask yenye mchanganyiko wa hewa ya oxygen na dawa hiyo, uzuri wa dawa hii haihitaji kufuatiliwa sana kwani mama mwenyewe anakua anaitumia mask ile akiona maumivu yamekua makali sana hivyo yeye ndio anakua anajiongoza.
dawa hii haina nguvu sana kama kama hizo nilizotaja mwanzo na baadhi ya wanawake huishia kuomba kuchomwa epidural ya mgngoni kama wakiona hawaridhiki na hiyo, japokua wapoa ambao huridhika nayo mpaka mwisho.
madhara ya dawa hii;
kizunguzungu, kichefuchefu na kucheka sana kwa mama huweza kujitokeza.
                                                                 
mwisho; kulingana na mila na sababu za kidini watu wengine hua hawataki kuzaa bila uchungu hasa afrika, hivyo ni maamuzi binafsi ya mtu kuamua kama kweli anahitaji huduma hii.
lakini pia ikumbukwe kutumia dawa hizi haimaanishi kukaamaa au na kuachia kwa misuli kitaalamu kama labour contractions zinaacha lakini ni kwamba zinaendelea bila wewe kusikia maumivu.
                                                            
                                                           STAY ALIVE

                                   DR,KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                  0653095635/0769846183

0 maoni:

Chapisha Maoni