data:post.body Januari 2018 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

HIKI NDIO CHANZO, DALILI NA MATIBABU YA MWANAUME KUMWAGA MBEGU KIDOGO.

mbegu kidogo ni zipi?
kwa kawaida mil moja au cc moja ya mbegu za kiume inatakiwa kua na mbegu million 20 na zaidi, mwanaume ambaye anatoa mbegu chini ya milioni 15 kwa kila cc huyo anahesabika ana upungufu mkubwa kiasi cha mbegu.
                                                       
kua na mbegu kidogo kuliko kawaida kunapunguza uwezekano wa mwanaume kumpa mimba mwanamke, japokua wakati mwingine unaweza kubahatisha na kumpa mimba mwanamke.

dalili za kua na mbegu kidogo ni zipi?
mara nyingi dalili kuu ni kushindwa kumpa mwanamke mimba, dalili zingine huweza kuja na kuonekana kulingana na chanzo husika kilichokufanya wewe mbegu zako zipungue lakini wingi wa manii unazomwaga haimaanishi na mbegu ni nyingi.
unaweza kumwaga kikombe kizima lakini ukipimwa hakuna hata mbegu moja iliyotoka.

sababu za mbegu kutolewa kidogo nini?
kemikali za viwandani; 
baadhi ya kemikali za viwandani tunazokutana nazo kutokana na mazingira tunayoishi na kazi tunazofanya huweza kusababisha mtu kuwa na kiwango kidogo sana cha mbegu...mfano kemikali za benzene, xylene,herbicides, dawa za kuua wadudu, dawa za kuua magugu shambani zote hizo zinahusika.
mionzi; mionzi kama ya x ray hupunguza wingi wa mbegu kutoakana na mara ngapi mionzi hii inakupata, kuendelea kupigwa mwanga kwa muda mrefu huweza kusababisha kupungua kabisa kwa kiwango cha mbegu kinachotolewa na muhusika.
joto sana kwenye korodani: mazingira yeyote ambayo yanachangia kiwango kikubwa cha joto kwenye korodani hupunguza kiwango cha mbegu,,,mfano kutumia laptop mapajani, kuvaa nguo nzito muda mwingi, kuoga na kukaa kwenye sink kubwa za maji ya moto, kuvaa tight zinazobana korodani kwenye mapaja na kadhalika.
kupiga punyeto; tabia za kupiga punyeto mara kwa mara hufanya kiwango cha mbegu kua chini sana kwani baadhi ya mbegu hutoka hata kabla hazijakomaa..hili ni tatizo kubwa kwa vijana wengi ambao wako kwenye umri wa kutafuta watoto.
matumizi ya dawa;
dawa aina ya anabolic steroids zinazotumika kujaza miili ya watu wanaofanya mazoezi ina tabia ya kupunguza ukubwa wa korodani na kusababisha kupungua utengenezaji wa mbegu lakini pia dawa za kulevya kama coacaine na bangi pia hupunguza ubora wa mbegu za kiume.
unywaji wa pombe na sigara; unywaji wa pombe kwa kiasi kikubwa unapunguza kiwango cha homoni za kiume kitaalamu kama testosterone ambazo huhusika kwenye utengenezaji wa mbegu pia sigara hupunguza kiwangi cha utengenezaji wa mbegu.
msongo mkali wa mawazo; msongo wa mawazo unaweza kufanya kuharibika kwa kiwango cha homoni mwilini, lakini pia mwanaume ambaye ana tatizo hili mawazo yake pia humfanya tatizo liwe kali zaidi,
unene; kiwango kikubwa cha unene huingilia utoaji wa mbegu kwa kuharibu mfumo mzima wa homoni zinazohusika na utoaju wa mbegu.
magonjwa mbalimbali ya mwili; magonjwa kama varicosele,magonjwa ya korodani, magonjwa ya zinaa kama gono, saratani za korodani, korodani ambazo hazijashuka chini vizuri, kuziba kwa mirija ya mbegu, matatizo ya njia za mbegu za kiume,baadhi ya magonjwa ya utumbo mkubwa huweza kusababisha ugumba.

 vipimo 
utrasound; kipimo cha utrasound hutumika sehemu mbalimbali kuangalia sehemu mbalimbali za korodani ikiwemo mirija kama iko sawa.
kiwango cha homoni; upimaji wa kiwango cha homoni mara nyingi hujaribu kuangalia kama kiwango cha homoni ya testosterone uko sawa.
post ejeculation analysis; kiwango kikubwa cha mbegu kwenye mkojo mara nyingi humaanisha kwamba mbegu zinatoka kwenye mirija na kwenda kuangukia kwenye kibofu cha mkojo badala ya kutoka nje kwenye uume.
genetic test; kipimo cha damu kwenye maabara zilizoendelea huweza kuonyesha matatizo ya kurithi au ya kuzaliwa nayo ambayo huweza kuathiri utoaji wa mbegu za kiume mfano tatizo la klenfelter syndrome.
ant sperm antibody test; kipimo hiki hupima aina ya askari wa mwili ambao hugeuka na kushambulia mbegu za mwanume kwa kudhani kwamba mbegu hizo ni adui kwa mwili.
sperm function test; kipimo hiki huangalia kama mbegu zinazotolewa na mwanaume zina kasi ya kutosha, ubora wa kutosha na muda gani zinaweza kuishi bila kufa baada ya kutoka nje ya korodani.
testicular biopsy; kipimo hiki hutumika kuchukua na kukata sehemu ya korodani na kuzipima kama utengenezaji wa mbegu uko sawa.


matibabu;
mara nyingi matibabu ya upungufu wa kiasi cha mbegu hutegemea zaidi chanzo husika cha tatizo, kama madaktari wakiweza kutambua chanzo au mgonjwa mwenyewe akiweza kutambua chanzo na kukiepuka basi anaweza akapata nafuu.
mfano wa matibabu hayo ni kama ifuatavyo.

kuepukana na vyanzo vya tatizo; kama umekutwa na tatizo hili ni vizuri ukaachana na utumiaji wa madawa au ulevi, mfano pombe, sigara, madawa ya kulevya, kupiga punyeto,kukaa mbali na mionzi na madawa mbalimbali ya wanyama na mimea.

upasuaji; magonjwa yote ambayo yanahusiana na kuziba kwa mirija, kuvimba kwa korodani, saratani za korodani, au varicose veins hutakiwa kufanyiwa upasuaji ili kuweza kulitatua tatizo.

matatizo ya tendo la ndoa; kwa wanaume ambao wanashindwa kusimamisha uume wakati wa tendo la ndoa ni vema wakatibiwa ili kuweza kuhimili tendo hilo na kutoa mbegu za kutosha.

matibabu ya homoni; baada ya vipimo vya homoni kama kuna ambazo zitaonekana zimepungua basi unaweza ukatibiwa kwa kupewa zile ambazo zimepungua.

kutibu magonjwa husika; magonjwa ya zinaa na mengine ambayo yanaonekana kushambulia njia ya uzazi na korodan zenyewe yanatakiwa yatibiwe.

fanya ngono siku hatari za mwanamke: kwa wale ambao mnatafuta mtoto ni vema ujifunza hesabu za siku za hatari ili mshiriki tendo siku hizo tu kwani mbegu za mwanaume zitakua kidogo zimekomaa na kuweza kumpa mwanamke mimba.

epuka vilainishi; baadhi ya vilainishi kama k-y gel, losheni na mafuta huweza kuzuia kasi ya mbegu za kiume hivyo jitahidi kutovitumia ili kujiweka salama wakati wa tendo la ndoa.

matumizi ya virutubisho; kuna virutubisho mbalimbali ambavyo hutumika sana kuongeza kiasi cha mbegu za mwanaume, binafsi nimeona ambavyo vimewasaidia ambao walikua na shida kama hizo..kwa dozi ya miezi mitatu mpaka sita mbegu huanza kuongezeka kama hakuna tatizo kubwa.
ukihitaji virutubisho hivi tuwasiliane.

mwisho; baadhi ya matatizo ya kutoa mbegu kidogo yanaweza yasitibike kabisa hata kwa kwenda kwenye hospitali kubwa sana, hivyo mgonjwa ni vizuri akubaliane na hali na ajue jinsi gani anaweza kuishi bila watoto au kulea watoto wa watu wengine.

UFAHAMU UGONJWA WA KUTOKWA JASHO SANA NA MATIBABU YAKE [hyperhidrosis]

hyperhidrosis ni nini?
hii ni hali ya kutokwa jasho jingi sana kuliko kawada, yaani kuliko watu wengine wanavyotokwa jasho..
jasho linalotoka ni jingi sana kuliko lile ambalo linahitajika na mwili wako kwa ajili ya kujipoza kipindi cha joto kali, hali hii huweza kusababisha msongo wa mawazo, na kukosa raha mbele za watu au mbele za watu ambao tunawapenda.
kutokwa jasho sana kunaweza kuathiri sehemu moja tu ya mwili kama viganja vya mikono, kikwapa, uso, nyayo, mgongo, na kadhalika au kuathiri mwili mzima.
mara nyingi likiathiri sehemu moja inakua sababu ya vitoa jasho au sweat glands kufanya kazi sana sehemu husika na ikitokea inaathiri mwili mzima mara nyingi linakua limesababishwa na magonjwa mengine.
lakini pia hali hii mtu anaweza kuzaliwa nayo au ikamuanza ukubwani.

chanzo ni nini?
tatazo la kutokwa jasho sana kwa mtu aliyezaliwa nalo ni chanzo chake mara nyingi hakifahamiki lakini kwa mtu ambaye anapata tatizo hili ukubwani basi kuna hali mbalimbali ambazo zinachangia sana yeye kupatwa sana na tatizo hili mfano matatizo ya ubongo[encephalitis], kisukari, mkanda wa jeshi, magonjwa ya tezi zinazotoa jasho, dawa kama adrenaline, amitriptyline, insulin, sertaline, magonjwa ya moyo, wasiwasi, umri mkubwa au menopause kwa wanawake.

jinsi ya kugundua ugonjwa huu.
mara nyingi ugonjwa wa kutokwa jasho wa kuzaliwa nao ni rahisi kuujua tangu mwanzoni, lakini ugonjwa wa kutokwa jasho sana ukubwani huweza kuathiri sana upande mmoja wa mwili.

matibabu;

  • anticholinergic drugs; dawa hizi hufanya kazi kwenye mishipa ya fahamu na kusababisha kupungua kwa utokaji wa jasho mwilini mfano benzatropine, propantheline, na oxybutinin..
  • body spray au perfum zenye kiwango kikubwa cha alluminium hydroxide pia huweza kutumika kukausha jasho kwa kujipulizia dakika chache baada ya kutoka kuoga,, maendeleo huanza kuonekana siku ya tano mpaka ya saba baada ya kuanza kutumia.
  • butolinum toxin; sindano hizi huchomwa sehemu husika na kukausha kiwango cha  jasho mwilini, hufanya kazi kwenye mishipa ya fahamu inayohusika na kutoa jasho.
  • upasuaji; hii ni hatua ya mwisho kabisa katika kazi ya matibabu ya kupunguza kiwango cha jasho mwilini, upasuaji hifanyika kuondoa tezi ambazo zinatoka jasho jingi.
  • mwisho kama tatizo lako limeonekana lina chanzo, hakikisha chanzo hicho kinatibiwa ili tatizo liweze kuondoka kabisa.

                                                                    STAY ALIVE

FAHAMU CHANZO NA JINSI YA KUTATUA TATIZO LA KUNUKA MIGUU.

kunuka miguu ni moja la tatizo sugu kwa wanaume wengi nje na ndani ya nchi, tatizo hili ni la aibu na humfanya mtu kukosa raha akiwa ugenini au akiwa faragha na mwenzake sababu ya harufu kali ya miguu ambayo inatoka miguuni.
                                                                     
chanzo ni nini?
chanzo kikuu cha kunuka miguu ni kutokwa na jasho sana la miguuni, kitaalamu miguu ni moja ya sehemu yenye vitoa jasho vingi au sweat glands kuliko sehemu zote za mwili.
jasho hili likinapotoka huliwa na  kuvunjwavunjwa na bacteria na kutoa harufu kali.
vitoa jasho au sweat gland kikawaida hupatikana mwili mzima kwa binadamu lakini miguuni hua nyingi zaidi na hutoa jasho wakati wote tofauti na zile za mwilini ambazo hutoa jasho wakati wa joto ili kuupoza mwili.

tabia zipi ambazo hufanya miguu ianze kunuka?

  • kuvaa viatu vilele kila siku kiasi kwamba leo vikiwa vimeloa jasho basi kesho yake unavivaa kabla havijakauka vizuri.
  • kutokua msafi wa kimwili yaani kutokuoga kila siku.
  • mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito na kuvunja ungo.
  • msongo wa mawazo
  • ugonjwa wa hyperhidrosis ambao humfanya mgonjwa kutokwa na jasho sana kuliko kawaida.
jinsi ya kupambana na miguu kunuka...
  • epuka kuvaa viatu mara mbili mfululizo kwani vinakua bado vina ubichi wa jasho la jana yake.
  • kua msafi kwa kuoga kila siku na kukausha miguu yako kabla ya kuvaa viatu.
  • vaa socks safi kila siku ambazo ni nzito, usivae socks nyembamba sana kwani hazina uwezo wa kunyonya jasho vizuri.
  • usivae viatu vya plastiki na hakikisha viatu unavyovaa vina manyoya ndani ambayo hunyonya jasho.
  • tumia body spray ambazo hutumika kwapani ili kukausha jasho kupuliza miguuni na kukausha jasho hilo.
matibabu ya hospitali
botox injection ; hizi ni sindano ambazo huchomwa kwenye sole ya mguu kwa chini ili kuzuia tatizo la kutokwa jasho jingi kutoka.
dawa za fangas; ugonjwa wa fangasi za miguu huweza kusababisha kunuka sana kwa miguu hivyo ukiona dalili za fangasi katikati ya vidole basi nunua dawa za kupaka au kumeza ujitibu mwenyewe.


                                                               STAY ALIVE
          
                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0653095635/0769846183  

LIFAHAMU TATIZO LA KUNUKA KIKWAPA NA MATIBABU YAKE...

kunuka kikwapa ni nini?
hii ni harufu kali inayotoka kwenye sehemu ya juu kabisa ya mkono kwa chini au kwa jina la kikwapa...                                                           

chanzo ni nini?
kimsingi harufu hii hutokana na bacteria kutumia jasho la binadamu na kutengeneza aina fulani ya tindikali ambayo hutoa harufu.
katika hali ya kawaida jasho binadamu hua halina harufu mpaka pale linapokutana na bacteria ambao hushambualia jasho lako.
mara nyingi binadamu huanza kutoka harufu sana akibalehe au kuvunja ungo ambapo manyoya huanza kuota kwenye kikwapa lakini pia watu wanene sana, wanaokula vyakula vyenye viungo vingi na wenye baadhi ya magonjwa kama kisukari.
harufu kwenye mwili wa binadamu ukiachana na makwapa pia hutoka sehemu za siri, miguuni, kwenye mikunjo ya nyama kwa wanene, nyuma ya masikio, sehemu ya haja kubwa, katikati ya mapaja, na kwenye nywele za sehemu za siri.
apocrine gland ni sehemu ya mwili ambayo inatengeneza jasho, huapatikana sehemu mbalimbali za mwili kama kwapa, ngozi, matiti,na kadhalika.

jinsi ya kuzuia harufu...
  • weka safi kwapa lako kwa kuosha na maji safi na sabuni ya kuua bacteria.
  • tumia deodorant na body spray, mara nyingi hupunguza wingi wa jasho na kukupa harufu nzuri.
  • oga kila siku angalau mara mbili asubuhi na jioni kwa maji ya moto kwani maji ya moto yanasaidia sana kuu bacteria walioko kwenye ngozi.
  • vaa nguo nyepesi ambazo zinakupa nafasi ya mwili kukausha joto kwa upepo, hivyo usivae nguo nzito sana.
  • usile vyakula vyenye viungo vingi sana kama kitunguu swaumu lakini pia utafiti umeonyesha kwamba ulaji mwingi wa nyama nyekundu huweza kuongezea harufu ya mwili.
  • kunywa maji mengi sana kwani yanasaidia kusafisha mwili wako.
  • nyoa manyoya ya kwapani kila yakiota kwani ni kihifadhi cha harufu kali.
matibabu.
  • upasuaji; wakati mwingine upasuaji kitaalamu kama endoscopic thoracic sympathectomy ambayo hufunga mishipa ya fahamu ambayo hufanya jasho litoke jingi hufanyika kutibu tatizo hili..
  • baadhi ya magonjwa ya figo, maini, fangasi, kufunga kwa hedhi kwa akina mama wa umri mkubwa huweza kusababisha hali hii hivyo muone daktari kwa vipimo zaidi na matibabu kama haupati nafuu.
ni wakati gani unatakiwa umuone daktari...?
  • kutokwa na jasho sana wakati wa usiku.
  • kutokwa jasho zaidi kuliko mwanzoni.
  • jasho linaanza kukuzuia na kazi zako za kawaida.
  • kutokwa na jasho sana wakati wa baridi.
  • kuwashwa sana na ngozi.
                                                                
                                                                   STAY ALIVE

                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0653095635/0769846183



UFAHAMU MPANGILIO BORA WA CHAKULA KUPUNGUA UZITO.[DIET]

kupungua uzito bado ni mtihani mkubwa kwa watu wengi, wengi wametumia mpaka madawa na virutubisho mbalimbali bila mafanikio lakini bado hawajafanikiwa kupungua na inshu inakuja kwamba nidhamu binafsi ya chakula na mazoezi ndio msingi mkuu wa kupungua uzito na kuishi maisha ya amani na furaha.
                                                                         
leo ntaenda kuwashirikisha mpangilio wa chakula ambao unaweza kukupa mafanikio ya kupungua uzito na kitambi iwapo tu ukijituma,  mfumo huu ni wa wanga kidogo na protini nyingi  na kama ifuatavyo.
chakula cha asubuhi;
kula slesi mbili za mkate wa brown, yai moja la kuchemshwa, na chai...lakini hapo kwenye chai usiweke sukari wala asali tafuta sukari ambazo ni sugar free....katikati ya chakula cha asubuhi na mchana kula nusu ya parachichi au tango... achana na maembe, ndizi na matunda yenye sukari nyingi.

chakula cha mchana; kula kuku robo aliyechunwa ngozi wa kuchemshwa au wa kuchoma, au kula samaki wa kuchemsha au wa kuchoma, mboga za majani, na  ugali au ndizi za kupika portion kidogo kama ile inayopimwa mahotelini.(pima ugali nusu ya kiganja chako)

chakula cha usiku; kula samaki au robo kuku ambaye ametolewa ngozi, ambao wamechomwa au kuchemshwa na mboga za majani.
hakikisha unakunywa maji mengi kama lita tatu kwa siku ili kusafisha na kuondoa sumu mwilini.

mwisho; uvumilivu na kutokata tamaa ndio nguzo kuu ya mafanikio, kama ikitokea umeanguka na kula vitu vya ajabu basi usikate tamaa wewe endela tu.
achana vyakula vya sukari nyingi na kukaangwa kama soda, biskuti,chocolate, maandazi, chapati, pipi, pombe na kadhalika.
kulingana na ubinadamu unaruhusiwa kula au kucheat kwa kula chakula unachokipendaga angalau mara moja kwa wiki.
mpango huu unaweza kukupunguza angalau kilo 2 mpaka 5  kwa mwezi.

                                                         STAY ALIVE

                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO


HIZI NDIO DAWA 3 ZA KISASA ZINAZOSAIDIA WANAWAKE KUZAA BILA UCHUNGU KABISA.

dunia nzima inafahamu kwamba mwanamke atazaa kwa uchungu tu hata iweje, na vitabu vya dini vimeandikwa hivyo lakini kwa miaka ya hivi karibuni na mabadiliko ya tecnolojia hali hii imeanza kupotea kutokana na uwezekano mkubwa wa kumfanya mwanamke huyu kusubiri masaa yote ambayo mtoto anakua anshuka kutoka kwenye kizazi kwenda nje bila kusikia maumivu ya uchungu hata kidogo.
                                                             

kitaalamu maumivu ya uchungu huchukua masaa 8 mpaka 12 kwa mtoto wa kwanza na masaa 6 mpaka 8 kwa mtoto wa pili na kuendelea, kipindi hiki ni kigumu sana kwa mama.
huenda kwa nchi za kiafrika bado hatujaanza kutumia mfumo huu wa kuondoa maumivu ya uchungu  sababu ya ukomo wa bajeti na mila zetu lakini kwa nchi zilizoendelea au kwa hospitali binafsi hata hapa nchini inawezekana kabisa ukapata huduma hiii.
kimsingi maumivu ya kuzaa ni makali sana kiasi kwamba hufika hatua mama anaomba akapasuliwe kitu ambacho sio cha kawaida kuombwa kwa binadamu mwenye akili nzuri lakini pia ukitaka kujua uchungu ni mkali sana kuna wakati njia ya mwanamke inaongezwa kwa kukata sehemu ya uuke bila ganzi mwanamke haonekani kushtushwa kabisa na maumivu yale.
sasa zifuatazo ni njia ambazo hutumika kwenye wodi ya wazazi kuwapunguzia au kuwaondolea uchungu kabisa na kujikuta wanazaa bila kusikia kitu.
epidural block; hii ni njia inayotumiwa sana na wanawake wengi nchini marekani, ni njia ambayo sehemu ya ndani ya uti wa mgongo kitaalamu kama epidural space huingiziwa dawa ya ngazi ambayo imeandaliwa maalumu kwa kazi hiyo, mara nyingi dawa ya pubivacaine hutumika.
njia hii kwa hapa kwetu tanzania hutumika kabla ya kuwafanyia upasuaji wa kutoa mtoto wajawazito ambao wanakua wameshindwa kusukuma mtoto.
dawa ikishaingia maumivu ya uchungu huondoka kwa asilimia 90 mpk 100 na kumfanya mama kukaa akisubiri kusukuma mtoto bila maumivu hata kidogo.
baada ya dawa kuanza kufanya kazi hutaweza kuinua miguu yako wala hutaweza kuisikia miguu hata ikiguswa mpaka dawa itakapoisha, mara nyingi daktari huweka mpira[catheter] wa kuongeza dawa kila baada ya muda fulani kwani sindano moja ya kwanza haitoshi mpaka kujifungua.
kuna madhara ya njia hii? 
sio kila mtu anaweza kupewa dawa hii... kama ushafanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo, una tatizo la kuganda kwa damu au aleji ya dawa hizo huwezi kupewa.
madhara madogo madogo kama kichwa kuuma, presha ya mwili kushuka na kuwashwa kwa mgongo huweza kutokea.
opiods; hizi ni dawa za maumivu zenye nguvu sana ambazo hutumika kutuliza maumivu mbalimbali ya mwili lakini kwa sasa zinatumika kwenye uchungu pia, hazina nguvu sana kama nilizotaja hapo juu lakini huweza kuondoa maumivu ya uchungu kabisa kwa muda wa saa mbili, mara nyingi dawa hizi hutumika kwa mama ambaye amekaa kwenye maumivu ya uchungu kwa muda mrefu sasa anataka kupumzika au wakati uchungu ndio unaanza.
sindano kwa jina la morphine au pethidine huchomwa kwenye paja au tako na kukata maumivu kabisa.
madhara yake;
dawa hii inaweza ikaenda mpaka ndani ya mtoto na kumlevya hivyo hazitakiwi kutolewa pale ambapo mama anakua yuko anakaribia kusukuma mtoto kitaalamu kama second stage of labour lakini pia kichefuchefu na kutapika huweza kutokea.
nitrous oxide; hii ni dawa inayofahamika kwa utani kama laughing gas, hutolewa kwa njia ya maski ambapo mama mjamzito hupewa mask yenye mchanganyiko wa hewa ya oxygen na dawa hiyo, uzuri wa dawa hii haihitaji kufuatiliwa sana kwani mama mwenyewe anakua anaitumia mask ile akiona maumivu yamekua makali sana hivyo yeye ndio anakua anajiongoza.
dawa hii haina nguvu sana kama kama hizo nilizotaja mwanzo na baadhi ya wanawake huishia kuomba kuchomwa epidural ya mgngoni kama wakiona hawaridhiki na hiyo, japokua wapoa ambao huridhika nayo mpaka mwisho.
madhara ya dawa hii;
kizunguzungu, kichefuchefu na kucheka sana kwa mama huweza kujitokeza.
                                                                 
mwisho; kulingana na mila na sababu za kidini watu wengine hua hawataki kuzaa bila uchungu hasa afrika, hivyo ni maamuzi binafsi ya mtu kuamua kama kweli anahitaji huduma hii.
lakini pia ikumbukwe kutumia dawa hizi haimaanishi kukaamaa au na kuachia kwa misuli kitaalamu kama labour contractions zinaacha lakini ni kwamba zinaendelea bila wewe kusikia maumivu.
                                                            
                                                           STAY ALIVE

                                   DR,KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                  0653095635/0769846183

LIFAHAMU TATIZO LA KUTEMBEA UKIWA USINGIZINI NA MATIBABU YAKE.[SLEEP WALKING]

noctambulism ni nini?
hii ni hali ambayo muhusika anakua katikati ya hali mbili yaani hali ya kusinzia na hali ya kua macho, katika hali hii muhusika anaweza kufanya mambo mengi akiwa usingizini kama kukaa kitandani, kutembea, kupika, kuendesha gari, kufanya usafi na hata kufanya mauaji.
                                                                         
                                                                                                                                                         
hali hii ya kufanya mambo akiwa amelala ni hatari sana na huweza kusababisha ajali mbalimbali ambazo zinaweza kuleta kifo au kulemaa kwa muhusika.

dalili za mtu ambaye anatembea usingizini ni zipi?
ni ngumu kidogo kuzitambua dalili za mtu ambaye anatembea huku amesinzia lakini ukiwa makini utaziona dalili kama kutanuka kwa sehemu nyeusi ya jicho au pupil, kuchanganyikiwa, kuongea vitu ambavyo havieleweki, na kusahau kabisa mambo aliyofanya jana usiku ukimuuliza kesho yake asubuhi.

chanzo cha kutembea usingizini ni nini?
tafiti zinaonyesha kwamba kukosa usingizi kwa muda mrefu, msongo mkubwa wa mawazo, kurithi kwenye ukoo, homa kali, baadhi ya madawa ya akili na msongo wa mawazo kama diazepam na amititryptline huweza kuchangia kwa hayo yote.

jinsi ya kugundua kwamba mgonjwa ana tatizo hilo
kwa sehemu ambazo hazina vipimo maalumu vya kugundua tatizo hili, maelezo kutoka kwa mpenzi, mke au wazazi yanaweza kujitosheleza kwani wao wanakua wameshuhuduia tatizo hili tayari.
kwa sehemu zilizoendelea kipimo cha polysomnography ambacho hutumika kupima maendeleo ya usingizi mtu akiwa amelala ndio kipimo pekee ambacho kinaweza kutumika kuwepo kwa tatizo hili.

matibabu
hakuna matibabu ya moja kwa moja ya tatizo hili, mambo kadhaa hutakiwa kufanyika ili kuweza kumsaida mtu mwenye tatizo hili kwa kuweka mbali silaha kama kisu, kioo, mkuki au bunduki...kuweka alarm kali mlango ukifunguliwa wakati wa usiku ili na yeye aweze kuamka usingizini.
baadhi ya dawa kama diazepam,amitriptyline na carbamazepine hutumika kuboresha usingizi lakini haziwez kutibu tatizo moja kwa moja.

kesi zilizofika mahakamani kwa tatizo hilo....

  • mwaka 2008 brain thomas alimuua mke wake akiwa usingizini wakiwa likizo huko walles na mahakama ilimuachia huru baada ya vipimo.
  • mwaka 1992 kijana ambaye anaitwa park alimuua mama mkwe wake na kujaribu kumuua baba mkwe wake lakini aliachiwa huru na mahakama ya canada.
  • mwaka 1991 kijana kwa jina la burgess alimpiga na chupa kichwani msichana wake na kumrekodi video lakini mahakama haikumkuta na hatia.
mwisho;tatizo hili linaweza kua utani kwenye jamii zetu lakini kwa hali moja linaweza kua hatari sana kwana kuna watu wamepoteza maisha kwa kua na tatizo hili au kwa kuishi na watu wenye tatizo hili.


                                                               STAY ALIVE

                                       DR, KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                 0653095635/0769846183