data:post.body 2018 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

JINSI YA KUONDOA KITU KILICHOKWAMA PUANI KWA MTOTO UKIWA NYUMBANI.

Mara nyingi watoto wadogo hua na tabia ya kujiingizia vitu puani wakati wa michezo, hii huleta taharuki sana kwa mama au walezi wa mtoto yule na kuwafanya waaache shughuli zao kukimbilia hospitali, kwa watu wazima hua ni bahati mbaya.

mara nyingi vitu ambavyo vinaingia kwenye pua la mtoto ni mbegu kama za maharage, njegere, au vyuma na plastiki za mduara mdogo.
mara nyingi sana pua moja ndio linaathirika kwani mtoto mwenyewe akishagundua hicho kitu hakitoki anaanza kulia au anabadilika ghafla.
dalili ni kama kupiga chafya sana. kutoka na kamasi nyingi au damu kidogo.

matibabu ya nyumbani.
hakikisha unakiona kitu kilichoingia, kama ni kitu chenye ncha kali basi hicho hakifai kutolewa nyumbani lakini kama sio kitu chenye ncha kali basi nunua kalamu yenye mrija, ondoa mrija wa ndani ubakize bomba.
sasa chukua bomba ingiza kidogo na upulize kwa nguvu kwenye lile pua ambalo halijaingiliwa na kitu, puliza kwa nguvu hata mara nne au mara tano.
inategemea na umbali kilipofika, ila kama kiko mwanzoni kitatoka mara moja na kama kipo juu kidogo kitakua kinashuka kila ukipuliza.
kwa mtu mzima anaweza kuziba pua zima na kupenga kamasi tu na kitu kikatoka lakini watoto hua hawawezi.
onyo; kama kitu kimeingia afu hakionekani usijaribu njia hii, nenda hospitali.

matibabu ya hospitali
kule kuna vifaa maalumu vya kuondoa vitu kama hivyo, mgonjwa atatolewa bila kumpa hata dawa ya usingizi.

jinsi ya kuzuia
kwa mtoto anayetambaa muweke mbali na kitu chochote ambacho unakiona kinaweza kupita puani kwake.
hata kama amefika umri wa kutembea muonye kutoweka kitu chochote mdomoni au puani ambacho sio chakula.

                                                                      STAY ALIVE

                                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                            0653095635/0769846183

FAHAMU CHANZO CHA KUOZA MENO NA MATIBABU YAKE.[DENTAL CARIES]

Kuoza meno ni nini?
hili ni tatizo ambalo husababishwa na bacteria kujificha ndani ya sehemu za meno kisha kumwaga tindikali ambayo huenda kuondoa madini ambayo yapo kwenye meno na kufanya meno kuanza kupungua ukubwa na kutoboka.
kitaalamu bacteria ambao wanaishi kwa kula sukari au wanga mdomoni ndio hutengeneza tindikali ambayo huharibu meno.
mdomoni mwa binadamu kuna kiwango cha tindikali{pH] kwanzia 6.2 mpaka 7 ambayo huongezeka pale mtu anapoanza kutumia sukari, soda, biskuti, chocolate au vyakula vya wanga kwani bacteria huanza kazi ya kutengeneza tindikali kila unapokula milo hiyo.
kiwango cha tindikali kikiwa kingi sana mdomoni basi tindikali huanza kutoboa matundu kwenye meno na hapo ndio chanzo cha meno kuanza kuharibika.
kama tatizo hili lisipowahiwa basi jino litashambuliwa mpaka kwenye mzizi na kitakacho baki itakua kuling'oa tu.

watu gani wako kwenye hatari ya kuharibika meno?
  • ulaji wa vyakula vya wanga
  • ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi.
  • kutopiga mswaki kwa wakati.
  • kurithi kwa wazazi.
dalili za ugonjwa huu ni kama ifuatavyo...

  • hatua ya kwanza ya ugonjwa; meno yanakua yametoboka kidogo sana na hapa hua hakuna dalili kabisa ambayo mgonjwa ataisikia.
  • hatua ya pili ya ugonjwa; hapa meno yanakua yametoboka zaidi na mgonjwa huanza kusikia dalili za maumivu kwa mbali sana hasa akila vyakula vyenye sukari sana.
  • hatua ya tatu ya ugonjwa; meno yanatoboka zaidi na kipindi hiki maumivu hua makali mgonjwa akila chakula cha moto sana au cha baridi sana.
  • hatua  ya nne ya ugonjwa;  jino kwa sasa limetoboka sana na maumivu hua ni makali mno kiasi kwamba ikifika usiku mtu hawezi kulala na hata akimeza dawa za maumivu hizi ndogo ndogo bado maumivu hayaishi.
  • hatua ya tano ya ugonjwa; hii ni hatua ambayo jino limekua limechimbika sana na kuleta jipu sehemu ya eneo la jino, maumivu ni makali sana na homa huwa juu.
matibabu

matibabu ya meno hutegemea sana hatua ya kuharibika ambayo meno yamefikia kama ifuatavyo.
hatua ya kwanza na ya pili; haihitaji matibabu lakini mgonjwa anashauriwa kuacha kutumia vyakula vyenye sukari na wanga sana kisha hushauriwa kupiga mswaki kila baada ya mlo ili kuonoda mabaki ya vyakula mdomoni.
hatua ya tatu; hii ni hatua ambayo jino limetoboka na na maumivu yanakua makali kwa kunywa maji ya baridi ya ya moto sana.
huu ni muda muafaka wa kuziba jino hili.
hatua ya nne; hii ni hatua ambayo maumivu ni makali sana hasa usiku na mgonjwa kushindwa kulala kitaalamu kama pulpitis.
matibabu pekee ni kuondoa sehemu ya ndani ya jino iliyoharibika kisha kuijaza kitaalamu kama root canal, lakini sababu sehemu nyingi hawafanyi matibabu haya ya root canal wengi huishia kung'olewa jino.
hatua ya tano; hii ni hatua ambayo mtu anapata jipu la kwenye jino, matibabu yanayohusika hapa ni kuliodoa jino na kufanya upasuaji mdogo kuondoa usaa.

jinsi ya kuzuia kuharibika kwa meno.

  • punguza ulaji wa sukari na vyakula vya wanga.
  • piga mwaki kila baada ya mlo.
  • muone daktari wa meno akuchunguze angalau mara nne kwa mwaka.

                                                  STAY ALIVE


                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                  0753095635/0769846183


,

HIZI NDIO NJIA KUMI ZA KUISHI NA UGONJWA WA PRESHA BILA KUTUMIA DAWA.

Wagonjwa wengi na baadhi ya madaktari huamini kwamba unapokutwa na ugonjwa wa shinikizo la damu au presha kitu cha kwanza ni kumeza dawa kisha mengine yatafuata, kitu ambacho sio kweli.
Mfumo wa maisha una mchango mkubwa sana kwenye tatizo la ugonjwa wa presha kuliko hata kumeza dawa.
                                                                           

ukiweza kuishi aina fulani ya maisha baada ya kuugua presha, basi unaweza usitumie dawa kabisa au ukachelewa kuanza dawa, cha msingi uwe na kipimo cha presha nyumbani kwako ili kila siku uhakikishe kweli presha iko sawa.
yafuatayo ni mambo muhimu ambayo unaweza kufanya na ukaishi bila kutumia dawa.
punguza uzito; kuongezeka kwa uzito hua kunaenda sambamba na kuongezeka kwa presha, tafiti zinaonyesha kwamba kila kilo unayopunguza inapungua na mmhg moja ya presha.
lakini sio uzito tu, angalia kiuno chako, hakikisha kiuno chako kinakua kwenye ukubwa sahihi kulingana na vipimo vya afya.
wanaume wana hatari ukubwa, kiuno kikizidi sentimita 102 na wanawake wana hatari ukubwa wa kiuno ukizidi sentimita 89.
fanya mazoezi mara kwa mara; kufanya mazoezi angalau nusu saa kwa siku tano za wiki itakuunguzia presha ya damu kwa kiasi kikubwa sana.
ni vizuri kua mvumilivu na kufuata ratiba yako kwa makini kwani kuacha mazoezi kutairudisha presha pale ilipokua mwanzo.
mazoezi kama kukimbia, kutembea na kuruka kamba ni muhimu sana kwa wagonjwa hawa.
kula vizuri; ulaji wa vyakula bora vya kiafya unaweza kupunguza presha kwa mpaka kwa 10mmhg.
hakikisha unakula mtunda, mboga za majani, vyakula asilia ambavyo havijakaangwa na mafuta mengi bila kusahau kupunguza au kuacha kabisa kula nyama nyekundu na maziwa yake.
punguza ulaji wa chumvi; kula chumvi kwa kiasi kidogo sana kunaweza kukupunguzia presha kwa 5 mpaka 6 mmhg kama presha yako iko juu.
epuka vyakula vya kusindikwa na kukaanga ambavyo huhifadhiwa kwa chumvi nyingi, epuka vyakula vya mahotelini ambavyo navyo hupikwa na chumvi nyingi.
pika vyakula nyumbani na uweke kiasi kidogo sana cha chumvi na kama huwezi tafuta chumvi maalumu kwa wagonjwa wa presha ambazo zinapatikana kwenye maduka ya madawa na supermarket.
punguza unywaji wa pombe; pombe inaweza kukupunguzia presha au kukuongezea presha kulingana na unywaji wako mwenyewe.
bia mbili kwa siku kwa mwanaume na moja kwa wanawake zenye kiwango cha kawaida cha ulevi au alcohol au mvinyo glasi moja kwa siku inaweza kua na faida sana na kupunguza presha.
lakini unywaji wa pombe mkubwa kupitiliza hapo unafanya presha ipande lakini pia huzuia dawa za presha kufanya kazi vizuri.
acha sigara; ukivuta sigara presha yako ya damu inaongezeka saa chache tu unapoanza kuvuta, na ukiacha kuvuta presha yako inashuka ndani ya muda mchache.
watu wanaoacha sigara huweza kuishi miaka mingi na kujizuia kuugua magonjwa ya moyo ukilinganisha na watu ambao hushindwa kuacha sigara.
achana na kawaha; kahawa ni kinywaji ambacho bado watafiti wanaamini kwamba kinaongeza presha ya damu, japokua inasemekana presha hiyo hupanda zaidi kwa watu ambao wanakunywa mara moja moja kuliko wanaokunywa kila siku.
lakini kama wewe ni mgonjwa wa presha, jaribu kunywa kikombe cha kahawa kisha pima presha baada ya nusu saa.
kama presha inapanda achana na kahawa.
epuka msongo wa mawazo; ni kweli kila binadamu ana msongo mkubwa wa mawazo hasa kwenye mambo ya mahusiano, fedha, kazi na familia.
kuwaza sana hakuwezi kubadilisha kabisa hali yako ya kifedha, kitu unachoweza kufanya ni kukubali kwamba changamoto za maisha ni kawaida na kukubaliana nazo.
ongeza juhudi kupambana na yale unayoweza kupambana nayo, yale usioyaweza achana nayo.
fuatilia presha yako; kama una uwezo nunua kipimo ukae nacho ndani, kama huna uwezo angalau uwe unapima mara mbili au mara tatu kwa wiki kwenye kituo chochote cha afya.
haya mambo niliyotaja hapo juu yakianza kufanya kazi presha itaanza kushuka sana hivyo ni vizuri kumuona daktari ili akupunguzie dozi au aukuahishe dawa kabisa chini ya uangalizi maalumu.
pata sapoti; hakikisha ndugu zako au watu wako wa karibu wana kukumbusha mambo yote muhimu ambayo yanahusika kama mazoezi, chakula na kadhalika.
kama hupati sapoti hii basi tafuta wagonjwa wa presha wakupe moyo na kukusaidia jinsi ya kumbana na hali hii.

                                                                    STAY ALIVE
                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                           
                                                          0653095635/0769846183

   



KWA MARA YA KWANZA MWANAMKE ALIYEWEKEWA KIZAZI CHA MAMA ALIYEFARIKI AJIFUNGUA

Huko nchini brazili katikati ya jiji la sao paul yametokea maajabu makubwa katika mapinduzi ya  sayansi kwa mara ya kwanza kabisa duniani.
                                                                   
katika majaribio 39 ambayo yameshawahi kufanyika ya kuchukua vizazi vya wanawake walioko hai na kuvipandikiza kwa wanawake wengine ambao wana matatizo ya uzazi, ni watoto 11 tu ambao walipatikana huku wengine 28 waliowekewa vizazi wakishindwa kabisa kupata watoto kwa mimba kushindwa kuingia kabisa au mimba kuharibika.
lakini pia kumekua na utafiti ambao wanawake 10 waliwekewa vizazi vya watu ambao ni wafu lakini wote hawakufanikiwa kupata watoto.
leo hii huko nchini brazili mtoto wa kwanza amezaliwa baada ya kizazi cha mwanamke ambaye alikua amefariki kupandikizwa kwa mwanamke mwingine.

kazi ilifanyika vipi?
mama mmoja mwenye umri wa miaka 40 ambaye alikua na watoto watatu alifariki baada ya kuvuja damu kwenye ubongo wake, ndani ya muda mfupi viungo vyake ikiwemo mfuko wa uzazi vilihifadhiwa,
mwanamke ambaye alizaliwa na tatizo la kizazi chake kushindwa kuumbika vizuri tangu utotoni alifanyiwa upasuaji na kuwekewa kizazi hichi cha mama mfu.
baadae mayai  ya mwanamke huyu mzima yalichukuliwa na kuchanganywa na mbegu za mme wake huko maabara kisha kuhifadhiwa vizuri.
baada ya wiki sita mwanamke huyu alianza kupata hedhi kama kawaida na alipofika wiki ya saba yai lake ambalo lilihifadhiwa, likiwa limeritubishwa tayari liliwekwa ndani ya kizazi chake.

matokeo
baada ya miezi tisa ya mimba kama kawaida, mtoto wa kike mwenye kilo mbili na nusu alizaliwa kwa upasuaji akiwa hai.
haya ni maendeleo mkubwa sana kwani katika viungo ambavyo ni ngumu kupata ni kizazi hasa kutoka kwa watu ambao wako hai.

                                                                 STAY ALIVE
                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                          
                                                    O769846183/0653095635

HAWA NDIO MAPACHA WASIOWEZA KUAMBUKIZWA UKIMWI, WANAOTENGENEZWA CHINA.

CRISPR ni nini?
hili ni neno la kibailogia linalomaanisha uwezo wa kubadili vinasasaba au gene ya viumbe hai vya aina yoyote kwa ajili ya lengo fulani la faida za kimaisha.
                                                                     
CRISPR iligunduliwa nchini marekani mwaka 2012 na mtaalamu wa bailojia profesa Jennifer Doudna ambaye alikua akifanya tafiti ya jinsi ambavyo bacteria wanaweza kujikinga na kushambukiwa na virusi.

nini kimetokea china?
Baada ya wataalamu hawa kuitangaza teknolojia hii, nchi nyingi duniani zimekua zikiitumia teknolojia hii kubadili vinasasaba vya wanyama na mimea mbalimbali kwa ajili ya kupata ubora mkubwa zaidi kuliko ule wa mwanzo.
Sasa huko nchini china wataalamu kwa mara ya kwanza wamefanya kitu hicho kwa mapacha ambao bado hawajazaliwa.

mtaalamu huyo kutoka china ameondoa vinasasaba kwa jina la CCR5 ambavyo hutumika na virusi vya ukimwi kama njia ya kuingia kwenye seli nyeupe za damu na kuushambulia mwili.
Kwa maana nyingine hata virusi vikiingia ndani ya mtu, vitashindwa kuingia ndani ya seli za damu kwa ajili ya kuushambulia mwili hivyo baada ya muda vitakufa kwa kukosa virutubisho.
hivyo tunategenegemea kwa mara ya kwanza kabisa kuzaliwa kwa binadamu ambao hawawezi kupata ukimwi kwa njia yeyote ile.
mpaka sasa hivi kuna wazazi zaidi wameshajitolea kubeba mimba kwajili ya utafiti huu.

kwanini dunia inampinga?
wataalamu mbalimbali duniani wamepinga sana teknolojia hii kutumika kwa binadamu kwani inaenda kinyume na makubaliano ya umoja wa mataifa ambayo hayaruhusu vinasasaba vya binadamu kuchezewa kwa aina yeyeote ile ili kutunza kizazi cha binadamu halisi.
Dunia ina hofu kwamba yeknolojia hii itaondoa usawa wa kibinadamu.
watu watakua wana uwezo wa kuamua kuzaa mtoto wa urefu wanaotaka, mwili wanaotaka, na rangi wanayotaka.
Mwisho wa siku hata magonjwa ya aina fulani yatakua hayawahusu binadamu wengine.
Hii italeta aina mpya ya binadamu ambao hawajawahi kutokea na wengine watatumika vitani kama silaha kwa nchi zilizoendelea.
Teknolojia hii italeta watu wakubwa au giants ambao siku za usoni wanaweza wakatubadilikia wakaangamiza vizazi halisi vya binadamu.
Historia ya dunia kibiblia inaonyesha kwamba waliwahi kutokea binadamu wakubwa sana ambao walileta shida sana duniani lakini baadae waliangamizwa wakati wa nuhu na inasemekana mpaka leo kuna mabaki ya binadamu waliowahi kua wakubwa sana.

                                
nini faida ya teknolojia hii?
Teknolojia hii ikitumika vizuri inaweza kuondoa magonjwa yote ya kurithi kwenye ukoo, magonjwa ya saratani, kuzuia unene, na magonjwa yote ambaukizi ambayo yamekosa dawa, kwani wanasayansi watakua na uwezo wa kutengeneza binadamu imara yaani kama ku update version za binadamu mpya.
tatizo ni kwamba, teknolojia hii haitaweza kudhibitiwa na itaweza kuleta maafa makubwa duniani au kuleta magonjwa mapya ambayo yalikua yanazuiliwa na vinasasaba ambavyo tunaviondoa sasa hivi.


                                                                STAY ALIVE 

                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0653095635/0769846183

HIZI NDIO SABABU ZINAZOPELEKEA MWANAUME KUA SHOGA.

Swala la ushoga limeleta mijadiliano mikali sana kwenye nchi mbalimbali huku nchi zingine zikiwaunga mkono mashoga, wakati huo huo nchi zenye misimamo mikali ya kidini zikiwapa adhabu kali za vifungo vya gerezani.
                                                                 
mashoga hupingwa sana na dini mbalimbali za kikikristo na kiislam, dini hizo zikidai kwamba wanachokifanya ni chukizo mbele za mungu na wataishia motoni.
lakini pia mashoga hupingwa sana na kwenye nchi za afrika ambazo zina maadili yao amabyao hayaamini kwenye ushoga tofauti na nchi zilizoendelea ambazo ubaguzi wa mashoga hauna nguvu sana.
baadhi ya nchi zilizoendelea mashoga ni kundi maaalumu ambalo hupewa vipaumbele hata kwenye ufadhili wa kusoma vyuo vikuu.

msimamo wa kitaalamu kuhusu mashoga ukoje?
kitengo cha madaktari wa akili huko nchini marekani kinachofahamika kama THE AMERICAN PSYCHIATRIC  ASSOCIATION ilikua ikiwatambua mashoga wote au watu wote wenye mahusiano na jinsia moja kama wagonjwa wa akili.
lakini mwaka 1970 kitengo hichi kiliacha kuwatambua watu hawa kama wagonjwa wa akili sababu waliweza kuendelea na shughuli zao za kikazi kama kawaida kama watu wengine bila msaada wowote hivyo waliona hakuna haja ya kuwatambua watu hawa kama wagonjwa wa akili.
lakini bado swali linakuja, je kwanini mtu anaamua kua shoga? tafiti mbalimbali zilizofanyika zilikuja na majibu yafuatayo.
Genetics; mwaka 1990 utafiti ulifanyika na ambao ulikuja na majibu kwamba chromosome X ambayo inatoka kwa mama kwenda kwa mtoto wa kiume hua inakua imebeba vinasasaba tofauti tofauti ambavyo vinaweza kumfanya mtoto huyu wa kiume akawa shoga.
tafiti hii iligundua kuwepo kwa vinasasaba hivi kwenye asilimia hamsini mpaka sitini ya mashoga waliofanyiwa utafiti.
sababu kibailojia;  tafiti zingingine mpya zinasema kwamba kuna mabadiliko ya homoni ambayo yanatokea kwenye mfuko wa uzazi wa mama kabla mtoto hajazaliwa.
mabadiliko haya huathiri ubongo wa mtoto kwa njia ambayo haijafahamika na kumfanya atoke akiwa na tabia hizi za kushiriki mapenzi ya jinsia moja.
kitaalamu mwanaume akiwa kwenye mfuko wa uzazi anakua na vinasasaba vya kiume yaani XY lakini anakua na maumbile ya kike mpaka wiki sita ambapo homoni za kiume huingilia kati na kuanza kumtengenezea maumbile ya kiume, lakini homoni hii ikipata shida kidogo mtu anaweza akatoka na maumbile ya kiume lakini hajakamikika.
ushahidi kwamba mwanaume alikuwa mwanamke kabla ni uwepo wa matiti kwa mwanaume ambayo hayana kazi, na kufanana sana kwa kazi kati ya kinembe na uume.
mazingira; baadhi ya tafiti zinaamini kwamba mazingira ambayo mtoto anakuziwa yanaweza kumfanya awe shoga.
yaani kutunzwa na mama muda mwingi na kua na baba mkali ambaye hana muda na mtoto, kuishi na dada zake tu bila kuwepo watoto wengine wa kiume, kuanza kuingiliwa kinyume na maumbile akiwa mtoto mdogo, kuona swala la ushoga kwenye TV na kulichukulia kawaida, kutokemewa kwa tabia za kishoga akiaanza kuzionyesha utotoni na  umaskini wa kipato.
lakini pia baadhi ya watu hua mashoga sababu ya kuiga mambo au kujaribu kila kitu ujanani.
kuna watu ambao ukiwaona mtaani hawana dalili hata moja ya ushoga kimuonekano lakini ni mashoga.
mfano ukiangalia soko la mitindo au modeling Tanzania lina watu wengi sana wa mapenzi ya  jinsia moja ambao kwa hali ya kawiada ni rahisi kujua kwamba hawa watu wanafanya mambo haya kama kwa kuigana au kulazimika kufanya hivyo sababu ya shida sio kwamba walizaliwa hivo.
lakini pia baadhi ya tafiti zilikuja kupinga hoja kwamba watoto waliozaliwa kwenye mazingira ya kishoga hua mashoga kwani kuna watu wengi ambao wamelelewa na wapenzi wa jinsia moja lakini wakakua na kutojihusisha na mambo hayo ya ushoga na pia kuna wazazi ambao wamezaa watoto mashoga japokua wao sio jinsia moja.
baadhi ya mashoga walihojiwa wanasema kwamba wao walizaliwa wa kiume japokua moyoni walijihisi wa kike.
walipambana sana ili wasiingie kwenye tabia hiyo ya jinsia moja kwa kutafuta wapenzi wa kike na hata kujaribu kushiriki tendo la ndoa na wanawake lakini hawakupata hisia zozote huko na baadae walaiamua kukubaliana na hali zao za jinsia moja.
mwisho; wataalamu wanaamini kwamba asilimia kubwa ya watu ambao ni mashoga hawakua vile kwa kuamua lakini kwa kuwepo kwa sababu mbalimbali za kibailojia, mabadiliko ya homoni, na mazingira waliyokulia.
japokua baadhi ya tabia za kishoga kwa baadhi ya mashoga zingeweza kuzuiliwa kwa kuzikemea tabia hizi, hasa zinazosababishwa na mazingira.

                                                               STAY ALIVE...

                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                  0769846183/0653095635

TAFITI MPYA:KUNYWA MAJI YA BARIDI SANA KUNASAIDIA KUPUNGUZA UZITO NA KITAMBI.

Ni wazi kwamba watu wengi sana wanafahamu kwamba kunywa maji ya uvuguvugu hasa wakati wa asubuhi kunasaidia sana kupunguza uzito kwa kuongeza joto la mwili na kuongeza kasi ya uchomaji wa mafuta mwilini.
                                                               
na hii njia imekua ikitumika kwa miaka mingi sana na baadhi ya watu wamekua wakiongeza na limao ili kupata matokeo zaidi.
lakini pia watu walikua wakiyaogopa maji ya baridi sana kwa kuamini kwamba yanagandisha mafuta tumboni na kuongeza kitambi.
lakini tafiti mpya hivi karibuni zimeonyesha tofauti na watu walivyokua wanafikiria mwanzo.

tafiti mpya zinasemaje?
maji ya baridi sana au yenye barafu kabisa yanasaidia kupunguza uzito zaidi kwani maji yakiingia tumboni yakiwa ya baridi sana, mwili unalazimika kutumia nguvu za ziada kuyachemsha yawe katika kiwango kinachohitajika na mwili kabla ya kuanza kuyatumia.
sio kwamba maji ya uvuguvugu hayasaidii tena lakini tafiti zinaonyesha maji ya baridi sana ni bora zaidi kuliko ya uvuguvugu.
lakini pia tafiti hizo zinaongeza kwamba sio kwenye kunywa tu lakini hata utafiti uliofanyika kwa watu wanao ogelea kwenye maji ya baridi sana huweza kupungua uzito haraka kutokana na njia hiyo hiyo.

nini cha kufanya?
hii ni habari njema hasa kwa watu ambao wanashi maeneo ya joto, kwani walikua wakilia sana kunywa maji ya uvuguvugu kipindi cha joto kali.
sasa hivi wanaweza kunywa maji ya baridi sana bila wasiwasi wa kuhisi kwamba watanenepa zaidi.

                                                                     STAY ALIVE

                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                          0769846183/0653095635  

HIZI NDIO NJIA ZINAZOTUMIKA KUBADILI JINSIA (TRANSGENDER)

Watu wengi duniani ambao ni wa jinsia fulani hua wanahisi kwamba walizaliwa na jinsia ile kimakosa hivyo wanatamani wangezaliwa na jinsia tofauti.
                                                     
           
Baadhi yao hukubaliana na hali yao lakini wengine huamua kuchukua hatua ya kujibadilisha jinsia ili wawe tofauti na mwanzo.
Inakadiriwa kwamba zaidi ya watu laki saba nchini marekani walibadilisha jinsia baada ya kutoridhika na jinsia zao za mwanzo.
Ukishabadilisha jinsia, unaruhusiwa kubadilisha jina na jinsia yako kwenye vyeti vyako vya kuzaliwa na vitambulisho vyako vyote.
zifuatazo ni hatua za kitaalamu zinazofuata kubadilisha jinsia.

hatua ya kwanza; kupimwa akili.
kabla ya kuanza hatua za kitatbibu za kubadilisha jinsia, madaktari bingwa wa mambo ya akili na saikolojia hukaa na mgonjwa ili kujua kweli kwamba ana tatizo la kisaikolojia ambalo linamfanya ahisi kwamba yeye hafai kua jinsia fulani.
kitaalamu ugonjwa huu unaitwa gender dysphoria.
baada ya hapo wataalamu hawa watakwambia hatua ambazo utapitia ili ubadilishe jinsia yaani kwanzia dawa mpaka upasuaji wa kubadilisha viungo vya uzazi.
watakwambia madhara yote ambayo huambatana na hatua utakazo pitia ili kufika huko lakini mwisho watahitaji kujua watu ambao watakua pamoja na wewe na kusapoti mabadiliko hayo kwani kila mtu akikupinga utaishi kwa shida sana.

hatua ya pili; matibabu ya homoni
homoni hizi ndio hatua ya kwanza kabisa ya kubadilisha maumbile ya mtu,  hubadilisha maumbile ya kike kua ya kiume au maumbile ya kiume kua ya kike.
wanawake ambao wanataka kua wanaume huanza kutumia homoni za kiume kitaalamu kama adrogens ambazo ndio huanza kuwabadilisha kua wanaume kwa kufanya yafuatayo.

  • huongeza misuli
  • kuleta sauti nzito
  • kuleta manyonya kwenye ngozi
  • kuongeza ukubwa wa kinembe.
wanaume ambao wanataka kubadilisha jinsia na kua wanaume hutumia homone za kike ambazo zinaweza kubadilisha maumbile yao yakawa ya kike mfano oestrogen.
dawa hizo 
  • hupunguza homoni za kiume aina ya testosterone mwilini.
  • hupunguza manyoya kwenye ngozi.
  • kuongeza matiti.
  • kugawanya mafuta ya mwili.
mabadiliko huanza mapema ndani ya mwezi mmoja na huweza kufika hatua ya mwisho kabisa ndani ya miaka mitano.
mfano mwanaume anayaetaka kua mwanaumke mpaka matiti yatokee  huchukua miaka mitatu mpaka mitano.
matumizi ya dawa hizi yana madhara mbalimbali kama magonjwa ya moyo, ugumba, damu kuganda, na kadhalika hivyo ni vizuri kufanya vipimo mbalimbali wakati wa kuanza dawa ilikuona kama mwili unaenda vizuri na dawa hizo.
wakati mwingine watumiaji wa dawa hupata msongo wa mawazo kutokana na kutokua na uhakika wa kitu ambacho wameamua hivyo ni vizuri kutembelea wataalamu wa ushauri.

hatua ya tatu; upasuaji
Hii ni hatua ya  mwisho kabisa wa kubadilisha baadhi ya viungo ambavyo haviwezi kubadilika kwa matumizi ya homoni tu.
Lakini asilimia sabini na tano ya watu ambao hujibadilisha jinsia zao hawapendi kufanya upasuaji kutokana na gharama kubwa sana pamoja na madhara ambayo hayawezi kubadilika baada ya kutoa maamuzi.
viungo kama matiti ya wanawake, uume kwa wanaume, korodani, kizazi na mirija ya uzazi ya kike huweza kuondolewa.
wanaume hufanyiwa upasuaji na kuwekewa uke lakini pia wanawake hufanyiwa upasuaji na kuwekewa uume.
upasuaji wa kuweka uke hua una matokeo mazuri lakini upasuaji wa kuweka uuume mpya kitaalamu kama phalloplasty hauna matokeo mazuri sana ndio maana wanawake wengi wanaotaka kua wanaume hawapendi kufanya upasuaji huo.

je unaweza kurudi kwenye jinsia yako ya zamani baada ya kubadilika?
baadhi ya watu waliojibadilisha jinsia hujutia maamuzi yao hivyo huamua kurudi kwenye jinsia zao za zamani.
mabadiliko ambayo yanafanywa na homoni mara nyingi yanaweza kurudi kama mwanzo iwapo ukiacha dawa japokua tafiti zinaonyesha kuna mabadiliko ambayo huletwa na homoni za kiume kwa wanawake yanaweza yasirudi kama mwanzo.
baadhi ya watu wamefanikiwa kurudi katika hali zao za zamani japo sio kwa asilimia mia moja.
Mabadiliko ya upasuaji hayawezi kurudi kama mwanzo.

                                                                
                                                          STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                             0769846183/0653095635

                                      

VYAKULA 7 MUHIMU SANA KWA WAGONJWA WA SHINIKIZO LA DAMU AU PRESHA.

Kama tayari wewe ni mgonjwa wa presha huenda tayari unafahamu kwamba ugonjwa wako ni wa kudumu yaani hakuna dawa ambayo itakuponywa moja kwa moja ila kuna uwezekano mkubwa ukameza dawa miasha yako yote.
ugonjwa wa shinikizo la damu ni ugonjwa unao ongeza msukumo wa damu kwenye kuta za mishipa ya damu na kusababisha madhara kwenye moyo, figo na mishipa ya damu. kama unataka kujua zaidi kuhusu ugonjwa wa presha soma hapa.......http://www.sirizaafyabora.info/2015/07/ufahamu-ugonjwa-wa-presha-ya-kupanda-na.html
katika matibabu ya ugonjwa wowote vyakula ni muhimu sana kwani ndio vinaujenga mwili wetu.. kimsingi muonekano wa miili yetu huchangiwa sana na chakula tunachokula.
vifuatavyo ni vyakula ambavyo ni muhimu sana kutumika na wagonjwa wa presha ili kupunguza presha hiyo ya damu.
mboga za majani; uwepo wa chumvi nyingi au sodium kwenye damu ni moja ya vyanzo vikuu vya presha kua juu kwa wagonjwa hawa wa presha.
potassium husaidia sana kuondoa kiasi kingi cha sodium mwilini au chumvi na kupunguza presha.
mboga za majani zenye potassium nyingi ni kama bamia, chainisi, spinachi, na mchicha ni nzuri sana kwa wagonjwa hawa.

berries; haya ni aina ya matunda ambayo yana kemikali inayoitwa flavonoids ambayo imethibitika  kuzuia ugonjwa wa shinikizo la damu na kushusha presha kwa wagonjwa hawa.
Mara nyingi hupatikana sana kwenye super market kubwa hapa nchini.
                                                                 

samaki; samaki ni chanzo kizuri cha protini kwenye mwili wa binadamu, samaki wa aina ya salmon kama anavyoonekana kwenye picha hapo chini ni chanzo kizuri cha kemikali ya omega 3 ambayo husaidia kushusha shinikizo la damu kwa kupunguza lehemu au cholestrol, na kuponya mishipa ya damu.              
                                   
mbegu; mbegu ni chanzo kizuri cha madini ya pottasium na magnesium ambayo husaidia kupunguza kiasi kikubwa cha chumvi mwilini na kupunguza presha.
Mbegu za maboga na alizeti ni nzuri zikiliwa na wagonjwa hawa.
                                             

vitunguu swaumu; hivi vina kiasi kikubwa cha kemikali ya nitric acid ambayo inafanya kazi ya kupanua mishipa ya damu, hii huongeza nafasi kubwa kwa ajili ya kupitisha damu vizuri kwenda sehemu mbalimbali za mwili bila kuongeza shinikizo la damu.
                                                               

ndizi mbivu; kama ilivyo kwa mboga za majani, ndizi mbivu ni muhimu sana kwani zina kiwango kikubwa cha potassium ambayo hutumika kuondoa chumvi nyingi mwilini ambayo husababisha presha kupanda.                        

                                               
tangawizi; hii hufanya kazi ya kulainisha damu kwa kupunguza uzito wake(blood thinner), na kupunguza shinikizo la damu kwa kiasi kikubwa sana.
unaweza kutumia unga wa tangawizi kwenye chai yako kila siku badala ya kutumia majani ya chai ambayo tunajua hayana faida yeyote.
                                                     


mwisho; kama wewe ni mgonjwa wa presha usipuuze kabisa ugonjwa wako, hakikisha unafuata maelekezo yote ya wataalamu uweze kuishi maisha salama.

                                                                 STAY ALIVE 
                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                           
                                                     0769846183/0653095635

HIVI NDIO VYAKULA 5 MUHIMU ZAIDI KWA WAGONJWA WA SIKO SELI.

katika matibabu ya ugonjwa wa siko seli, mara nyingi nguvu nyingi zinawekwa kuhakikasha mgonjwa hapungukiwi na damu wala hapati maumivu makali ya mara kwa mara kwani hivyo ndio vyanzo vikuu vinavyosababisha vifo kwa wagonjwa hawa kwa kusababisha kufeli kwa baadhi ya viungo muhimu kama vigo, maini, mapafu na ubongo.
sasa kama wewe ni mama au baba una mgonjwa huyu ndani basi vyakula vifuatavyo visikose nyumbani kwako.
5.nyama nyekundu; nyama hii ina kiwango kikubwa sana cha madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa mgonjwa wa huyu kwa ajili ya kuongeza kiasi cha damu mwilini.
kimsingi nyama nyekundu ina madini ya chuma mengi zaidi kuliko nyama  ya samaki na kuku. ule weupe wa nyama ya kuku na samaki ni taarifa ya kiasi kidogo cha madini ya chuma kilichomo.
Sijasema asile kuku wala samaki lakini nyama nyekundu ya ngombe na mbuzi ni muhimu zaidi.
Hivyo hakikisha hakosi nyama nyekundu angalau mara mbili kwa wiki huku ukimchanganyia na samaki na kuku siku zingine.
                                                     

4.matembele; hii ni mboga ya majani inayopatikana sehemu mbalimbali nchini kwetu, mboga hii ina kijani nzito kuliko mboga nyingi..
ukijani huu unaonyesha wingi wa madini ya folic acid ndani yake. Mboga zote za rangi ya kijani kama mchicha, chinese, kisamvu zina madini haya lakini matembele ndio kiboko yao.
folic acid ni muhimu sana kwa mgonjwa huyu kwani huungana na madini ya chuma kutengeneza seli nyekundu za damu ambazo ni muhimu sana kwa mgonjwa lakini pia ni husaidia kupunguza kiasi cha lehemu au cholestrol kinachopatikana kwenye ulaji nyama nyekundu.
                                                   
3.machungwa; haya ni jamii ya matunda ambayo yana kiasi kikubwa sana cha vitamin C. kazi ya vitamin hii ni kuusaidia mwili kuchukua madini ya chuma ambayo yanapatikana kwenye nyama unayokula.Hivyo hata ukimpa mtoto nyama  nyingi kiasi gani bila matunda unapoteza muda tu.
lakini pia matunda haya yana kemikali kitaalamu kama ant oxidant ambazo ni kinga ya mwili hasa kuzuia madhara ya ambatanayo na ulaji wa nyama nyekundu kama saratani, magonjwa nyemelezi na magonjwa ya moyo.

2.dagaa; dagaa zina kiasi kikubwa sana cha madini ya kashiamu kuliko kiwango kinachopatikana kwenye samaki.
sababu kubwa ni kwamba ukila dagaa unakula na mifupa yake ambayo ina kashiumu nyingi sana kuliko ukila samaki kwani sio rahisi kula samaki na mifupa yake.
wagonjwa hawa wanahitaji kashium nyingi kwa ajili ya kuimarisha mifupa yao, kusaidia mishipa ya fahamu na husaidia kuganda kwa damu haraka pale unapopata kidonda lakini pia dagaa zina madini ya chuma na huweza kua mbadala kwa watu ambao kununua nyama ni ngumu kwao.
kumbuka, kuvuja damu kidogo tu kwa mgonjwa huyu ni hatari na huweza kuleta kifo.
                                                      
        
 1.maji ya kunywa; asilimia sabini ya mwili wa binadamu ni maji tu, ni bora mgonjwa wa siko seli ashinde na kulala njaa kuliko kushinda na kulala bila kunywa maji.
maji ni muhimu sana kwa wagonjwa hawa kwani husaidia kusambaza seli zake sehemu mbalimbali za mwili bila kukwama.
mgonjwa huyu akikosa maji ya kutosha, seli za damu hukwama kwenye mishipa ya damu na kuanzisha maumivu makali sana au sickle cell crisis.
hivyo mgonjwa huyu akishinda na kulala bila kunywa maji basi majibu yake utayaona hapohapo kuliko kushinda na kulala njaa kwani damu haiwezi kupungua ghafla.
                                                                           

5.mwisho; kama mzazi wa mgonjwa wa siko seli basi ni vizuri ukawekeza kwenye elimu kujifunza kuhusu wagonjwa hawa ili uwe na elimu ya kutosha na kuweza kuwasaidia.
mgonjwa huyu anaweza kuishi maisha marefu kama watu wengine na tafit zinaonyesha mwanaume anaweza kuishi mpaka miaka 60 wakati mwanamke anaweza kuishi miaka 68.


                                                              STAY ALIVE
                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                             0653095635/0769846183
                              







HIZI NDIO NJIA TISA ZA KUONDOA TATTOO KWENYE NGOZI.

Wakati mwingine katika maisha watu hufanya maamuzi ambayo huja kuyajutia baadae, moja ya maamuzi hayo ni kuchora tattoo ambayo baadae unaweza kujuta kwasababu huenda uliweka jina la mpenzi wako wa zamani au ulichora tattoo nyingi sana kiasi kwamba sasa zinakuathiri kupata baadhi ya fursa ambazo zinajitokeza.

Tattoo kikawaida hua haitoki lakini kutokana na ongezeko la watu ambao wanahitaji kuziondoa tattoo zao basi kuna njia mbalimbali ambazo zimeanzishwa za kuondoa tattoo japokua nyingi ni gharama sana au zinauma sana kama ifuatavyo.
laser; hii ni njia ya kutumia aina fulani ya mionzi kuondoa michoro ya tattoo kwenye ngozi, njia hii inauma na ni gharama sana kutumia.
huchukua muda mrefu kufuta kulingana na ukubwa wa tattoo yako lakini sio kazi ya siku moja hivyo utakua unaenda kila baada ya muda fulani.
gharama ni kama laki mbili na nusu kwa saa.
                                                               

kufunika na tatoo nyingine; wakati mwingine tattoo sio tatizo kwako lakini maneno uliyoandika ndio yanakukwaza.
Unaweza kuchora tattoo nyingine na kuifunika kwa maneno mengine ile tattoo ya kwanza ili iweze kupoteza maana yake ya zamani.
                                               

mafuta ya kutoa tattoo; kuna mafuta yamegunduliwa ya kuondoa tattoo lakini yanachukua muda mrefu sana kuifuta na ni gharama kutumia.
Uzuri wa mafuta haya hayana gharama sana lakini lazima uwe mvumilivu kwani itachukua muda mrefu na gharama kubwa.
ukiagiza mtandaoni chupa moja ni shilingi laki tatu.(amazon)
                                                                 

upasuaji; hii ni njia ya haraka ya kuondoa tattoo bila maumivu lakini gharama yake iko juu kidogo, ninachofanyika ni kwamba ngozi moja ya mwili wako hutumika kufunika sehemu ya ngozi ambayo imepakwa tattoo.
                                                             

kuisugua tattoo na chumvi; hii ni njia ambayo sio gharama ambayo unaisugua tattoo yako na chumvi kama mtu anayefanya scrubbing lakini kua makini usijiumize.
inachukua muda mrefu na baadhi ya madhara yake ni kuharibu muonekano wa ngozi.
                                                                 

limao: limao ni rahisi sana kupata kwenye mazingira yetu ya nyumbani, sio gharama kutumia lakini inataka uvumilivu na muda.
chukua maji ya uvuguvugu kisha osha sehemu yenye tattoo,baada ya hapo chukua limao na sugua sehemu yenye tatoo na usubiri mpaka pakauke.
baada ya hapo unaweza kuosha tena kwa maji ya uvuguvugu, fanya hivyo angalau mara moja kila siku.                                                  

asali;moja ya vitu bora kabisa kutumia kuondoa tattoo kwenye ngozi ni matumizi ya asali, jinsi ya kutumia;chukua kimiminika cha aloe vera, changanya na asali, maziwa ya mgando, na chumvi.
kisha changanya kimiminika hiki paka kwenye tattoo na uache mpaka ikauke.
kabla ya kupaka hakikisha umepaosha na maji ya uvuguvugu.
                                                                 

cream za kuondoa tattoo; kulingana na uhitaj mkubwa wa watu wengi kutaka kuondoa tattoo sasa hivi kuna makampuni mengi sana ya kutengeneza tattoo hizi, hivyo unaweza kuagiza tattoo mtandaoni kupitia amazon na ukazitumia kuondoa tattoo zako. bonyeza hapa  kuagiza.https://amzn.to/3vfeQpU
                                      


                                                      STAY ALIVE
                                DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                           0769846183/0653095635

VIPIMO FEKI VYA UKIMWI NI JANGA LA AFRIKA

Katika vita dhidi ya ukimwi hapa Afrika, kumekua na changamoto nyingi ikiwemo watu kupuuzia elimu ya kujikinga na ukimwi, kutokuwepo kwa dawa za kutosha za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi na watu kutojitokeza kabisa kupima ukimwi.
                                                                       

kulingana na muongozo wa shirika la afya duniani(WHO), mgonjwa hatakiwi kupewa majibu ya kua ameathirika na ukimwi mpaka apimwe na vipimo vya aina tofauti ambavyo vinahakikisha kweli ana maambukizi ya ukimwi.
shirika la doctor without borders(MSF) lilifanya utafiti  na kugundua kwamba vipimo havifanani nguvu hivyo kuleta makosa katika utoaji wa majibu na msisitizo mkubwa ukiwa katika watu ambao wanapewa majibu kwamba wameathirika wakati hawajaathirika kitaalamu kama false positive.
Ni kweli kuna baadhi ya watu ambao wanaweza kua na ukimwi vipimo vikaoneyesha hawana kitaalamu kama false negative lakini ni asilimia ndogo sana.

mtu kupewa majibu ya ukimwi kwamba ameathirika wakati hajaathirika huweza kuleta msongo mkubwa wa mawazo, maumivu ya kihisia na kuvunjika kwa mahusiano.

ushahidi wa hili ni upi?
Damu ilikusanywa kutoka kwa wagonjwa 2785 wa ukimwi ambao walikua wanahudhuria katika kliniki  mbalimbali za nchini kenya, uganda, congo, guinea na cameroon.
damu hiyo ilihifadhiwa vizuri na kutumwa ubeligiji kwa ajili ya vipimo vya ukimwi ili kuweza kuhakiki kama kweli wale watu ni wagonjwa wa ukimwi.
kati ya watu 2785 ambao damu zao zilichukuliwa, watu 1474 walikua hawana ukimwi na  watu 1306 pekee ndio walikua na virusi vya ukimwi kweli.
kwa maana nyingine hawa watu 1474 wamekua wakimeza dawa za ukimwi kwa muda wote huo kimakosa.

nchini Tanzania hali ikoje?
Hakuna tafiti kama hii iliyofanyika na kutangazwa rasmi nchini kwetu kuhusu hili lakini nitoe rai kwa wizara ya afya na wadau wengine wa afya kuliangalia swala hili kwa makini sana sababu kenya na uganda ni majirani zetu na sidhani kama teknolojia tunazotumia zimeachana mbali sana na teknolojia za kwao.
huenda na sisi tunatoa dawa kwa watu ambao sio wagonjwa.

                                                               STAY ALIVE
                                               DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                       0769846183/0653095635

HAYA NDIO MAKOSA WANAYOFANYA WATU WANAOJIPIMA UKIMWI NYUMBANI.

Watu wengi siku hizi wanapenda kujipima ukimwi wenyewe bila kwenda hospitali, ni kitu ambacho hata serikali sasa hivi imeanza kuunga mkono kampeni hizi ili kupata wagonjwa zaidi wa kuanza matibabu.
sababu kuu ya kujipima ni hofu ya kujulikana iwapo mtu atapima na mpenzi kwa wakati mmoja na wengine hupenda kupima na wapenzi wao wapya kabla hawajaanza kushiriki tendo la ndoa.
vipimo ambavyo vinapatikana kwa sasa nchi nzima ni vile vya damu japokua sasa hivi vipo vya kutumia mate lakini bado havipatikani nchi nzima.
kuna vipimo vikuu vitatu vya  kupima ukimwi hapa nchini kwetu kwa majina ya SD BIOLINE,UNIGOLD, na DETERMINE.

jinsi ya kupima ukimwi nyumbani.
1.chukua spirit futa kwenye kidole ambacho unataka kutoa damu
2.choma sindano toa damu kidogo kisha weka kwenye kipimo ambacho unacho.
3.mimina tone moja au mbili za damu kwenye kipimo.
4.weka tone moja au mbili ya dawa ya kupimia.
5.subiri dakika tano kisha soma majibu.

jinsi ya kusoma majibu
  • kipimo kitakisoma mstari mmoja wa controll kama hujaathirika.
  • kipimo kitasoma mistari miwili kama umeathirika na aina moja ya virusi vya ukimwi.
  • kipimo kitasoma mistari mitatu kama kama umeathiriwa na aina mbili ya virusi vya ukimwi.

makosa ambayo yanafanyika wakati wa kujipima ukimwi.
kukubali majibu ya vipimo vya mwanzo;  vipimo pekee ambavyo vinaruhusiwa kutoa majibu ya ukimwi ni kipimo cha UNIGOLD, kama ukipima ukimwi na kipimo cha bioline au determine kisha majibu yakasoma umeathirika inabidi ukahakikishe na kipimo cha UNIGOLD.
lakini kama umepima na vipimo vya determine na bioline ikaonekana huna ukimwi basi huhitaji kuendelea na vipimo zaidi.
kusoma majibu baada ya dakika tano; majibu ya ukimwi yanatakiwa yasomwe ndani ya dakika tano tu, ukikaa na kipimo muda mrefu kitaonyesha mstari wa pili, kitu ambacho kinaweza kumfanya muhusika aanze kupaniki akidhani kaathirika lakini hajaathirika.
kupima mara moja; mkiwa wapenzi wapya ni vizuri kupima tena baada ya miezi mitatu kuhakikisha kweli kwamba mko salama kabla ya kuvua kondom.
kuanza kufanya ngono nzembe baada ya kipimo kimoja ni hatari kwani mwenza wako anaweza kua ameshaathirika lakini vipimo bado havijaanza kusoma majibu yake.


                                                       STAY ALIVE

                                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                             0769846183/0653095635

HIVI NDIO MAITI INAVYOWEZA KUMPA MWANAMKE MIMBA.

Hii habari unaweza kua umeshaisikia lakini mpaka leo hujaamini kwasababu haiingii alikini hata kidogo kwa maiti ya kiume kushiriki tendo la ndoa.
                                                                           

Historia ya dunia inaonyesha kwamba askari wengi ambao walikua wakirudisha miili ya marehemu kutoka vitani kwenda nyumbani walishiriki nazo tendo la ndoa.
tendo hili la ndoa lilihusisha miili ya jinsia zote yaani wanawake na wanaume.
hii ilifikia hatua kwamba baadhi ya wafalme na viongozi wakubwa walikua wana tabia ya kuuweka mwili wa marehemu kwa siku nne ndio uharibike  wawape watu wa kuzika.

necrophilia ni nini?
hii ni hali ambayo sio ya kawaida ambayo mtu ambaye yuko hai anavutiwa sana na kulala na wafu, mtu huyu anaweza hata kumchukua mwanamke au mwanaume ambaye yuko hai kisha akamuua wakati wa tendo la ndoa kwa kumkaba au kumnyima hewa kisha ashiriki naye tendo la ndoa baada ya kifo.
kwa mwili wa mwanamke kuingiliwa na mwanaume inaeleweka kabisa kwamba inawezekana kwa hali ya kawaida hata kama mwanamke amekufa.

je mwananaume mfu anaweza kushiriki vipi tendo la ndoa?
sisi wote tunafahamu kwamba uume hauwezi kusimama baaada ya kifo kwenye miili mingi, lakini hua kuna wanaume tofauti kidogo katika hili.
katika hali isiyo ya kawaida mwanaume anaweza anaweza akafa na uume ukabaki umesimama.
hali hii hutokea pale sehemu ya ubongo kwa jina ya celeberum inapokua imekandamizwa wakati wa kifo.
vyanzo vya vifo ambavyo uume huendelea kusimama ni kupigwa risasi ya kichwa, kunyongwa, kupewa sumu na kifo kinachosababishwa na kumeza dozi kubwa ya viagra.(dawa za kuongeza nguvu za kiume)
hali kama hii ikitokea ndipo mwanamke ambaye anapenda kulala na marehemu anapoamua kujiridhisha kwa kulala na mwili huu wa mwanaume.

je mwanaume mfu anaweza kumpa mtu mimba?
baada ya kifo mbegu za mwanaume hukaa masaa 24 kabla hazijaharibika, lakini mbegu hizi haziwezi kumpa mimba mwanamke kwa njia ya kawaida ya tendo la ndoa mpaka mbegu zile zichukuliwe na ziingizwe ndani ya kizazi cha mwanamke kitaalamu.
historia inaonyesha kwamba mtoto wa kwanza kuzaliwa kwa kutumia mbegu za mwanaume mfu alipatikana duniani mwaka 1999 na kazi hii ilifanyika nchini marekani.

                                                        STAY ALIVE

                                  DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                            0653095635/0769846183
                                                                               

JE BINADAMU ANAWEZA KUISHI MUDA GANI BILA KULA WA KUNYWA?

Binadamu anahitaji maji na chakula iliaweze kuishi, 60% ya mwili wa binadamu ni maji matupu na vingine vilivyobaki ndio misuli, mafuta, mifupa na viungo mbalimbali.
kumekua na ubishani mwingi ni muda gani binadamu anaweza kuishi bila kula na kumekua na majibu ya tafiti mbalimbali kutoka kwa uzoefu wa watu walikofa sababu ya kutokula.
                                                                   

Mahatma Gadhi aliyekua mwanaharakati wa India wakati wa kudai uhuru aliwahi kukaa wiki tatu bila kula huku akinywa maji lakini hii haimaanishi kwamba yeye ndio kipimo sahihi cha watu wote.

ukweli ni upi?
tafiti nyingi zinaamini kwamba binadamu mwenye afya ya kawaida akipewa maji tu anaweza kuishi wiki nne mpaka nane bila kufa lakini pia binadamu ambaye ni mnene sana akipewa maji anaweza kuishi mpaka miezi 6 huku mwili wake ukichoma mafuta na kutumia kama chanzo cha nguvu.
lakini kwa jinsi watu wengi wasivyotarajia, binadamu akipewa chakula akanyimwa maji basi ana uwezo wa kuishi siku nne mpaka siku saba tu kwani maji ni muhimu sana kwa binadamu kuliko hata chakula.

kitu gani husababisha kifo mtu akikosa chakula?
binadamu akikosa chakula kwa muda fulani mwili huanza kutumia mafuta kutengeneza nguvu kwa ajili ya kutumia, baadae mafuta yakiisha mwili huanza kutumia misuli kutengeneza nguvu na hapa ndipo viungo maalumu kama moyo hushindwa kuendelea na kazi na kusimama.

                                                            STAY ALIVE
                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                           0769846183/0653095635

                                    
 
 

HII NDIO SABABU BAADHI YA WATU WANAKULA SANA LAKINI HAWANENEPI.

Kila mtu hua ana ushahidi wa kua na rafiki yake ambaye hata ale chakula kiasi gani hawezi kunenepa, lakini wewe binafsi unahisi ukila kidogo tu unanenepa kupindukia na unashindwa kuelewa ni kitu gani kinasababisha hivyo.
Kimsingi ni kwamba asilimia 60 mpaka 70  ya unene au wembamba wa mtu unategemea urithi wa kibailojia kutoka kwa wazazi na mababu zake.(genetics)
lakini pia watafiti wanaongeza kwamba mambo mengine kama mazoezi na chakula tunachokula kinachangia uzito au muonekano wa miili yetu kwa asilimia 30 mpaka 40.
hivyo ukiwa unafanya mazoezi na kufanya diet kumbuka kwamba unapambana na asilimia 30 mpaka 40 tu, na zingine zilizobaki zinaamuliwa na genes zako.
watafiti wameshagundua genes ambazo zinaamua ukubwa wa miili yetu lakini mpaka leo hawaelewi genes hizo zinafanya kazi vipi, kama ukichunguza vizuri utagundua kuna baadhi ya ukoo watu ni wanene watupu wakati koo zingine ni wembamba watupu.

chanzo ni nini?
mwili wa binadamu una aina mbili za mafuta yaani mafuta meupe na mafuta ya kahawia, kimsingi mafuta ya kahawia ambayo yanapatikana shingoni na mgongoni kwa juu yana kiasi kikubwa cha mitochondria[sehemu ya mwili inayochuma chakula kutengeneza nguvu].
sasa kwa tabia hii ya mafuta kuchoma chakula kutengeneza nguvu hufanya watu ambao wana mafuta haya kuendelea kua wembamba na kuonekana vijana miaka yote.
hivyo kitaalamu mafuta haya tunaita mafuta mazuri  kwani husaidia kuchoma chakula badala ya kuhifadhi mafuta.
mtoto akiwa mdogo anakua na mafuta ya kahawia mengi sana na ndio maana watoto wadogo huweza kula sana bila kunenepa na mafuta haya yanaendelea kupungua kadri mtoto anavyozidi kukua LAKINI mafuta meupe au white adipose tissue hayana uwezo kama mafuta ya kawahia.
mafuta meupe yana mitochondria kidogo na hufanya kazi ya kuhifadhi zaidi kuliko kuchoma, mafuta haya yanakua mengi zaidi mtu anavyokua mtu mzima na hayasaidii kuchoma chakula ili kupunguza uzito.
mafuta haya hupatikana karibia sehemu zote za mwili wa binadamu kama tumboni, makalioni, hips na sehemu mbalimbali.
watu weye mafuta meupe mengi hua wanene sana kutokana na asili ya mafuta haya kutochoma chakula sana kutengeneza joto.
sasa baadhi ya watu wana mafuta ya kahawia mengi zaidi kuliko meupe, watu hawa hawanenepi hata wale nini kwani miili yao huchoma chakula sana kutengeneza nguvu na joto.
watu wenye hii bahati ya kuzaliwa na mafuta mengi ya kahawia hua hawangaiki na swala la uzito kwenye maisha yao.

jinsi gani unaweza kuongeza mafuta ya kahawia mwilini? 
kama unaona watu wengi kwenye ukoo wenu ni wanene, inawezekana kwenu kuna asili ya unene hivyo una mafuta mengi meupe.

mafuta ya kahawia yanaweza kuongezwa kwa kufanya mazoezi, kukaa sehemu yenye baridi kali ili kuulazimisha mwili kutengeneza joto, kula matunda ya apple, kupata usingizi wa kutosha, na kutojishindisha njaa kwa kula kwa kiasi.

                                                                  STAY ALIVE     
                                               
                                           DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0769846183/0653095635



FAHAMU KIFO CHA MAJI KINAVYOTOKEA NA JINSI YA KUJIOKOA.[IMMERSION DEATH]

Vifo vya maji sio vigeni kuviona au kuvisikia kwenye maisha yetu, vifo hivi ni moja ya vifo vibaya sana ambavyo mwanadamu yeyote asingependa kuvipitia kwenye maisha yake.
                                                                   

sio kila mtu anayekutwa kwenye maji anakua alikufa sababu ya maji, kuna wengine walikufa kabla hawajatumbukia kwenye maji na wengine waliuawa na magonjwa ambayo walikua nayo tangu zamani hasa magonjwa ya moyo.
ukiwa na tatizo la  moyo ukatumbukia kwenye maji ule uchovu mdogo tu wa kupambana na maji utasababisha moyo kusimama.

mtu anakufaje akiingia kwenye maji?
mtu akitumbukia kwenye maji anazama kidogo sababu ya uzito wake pamoja na kasi ya mvutano kitaalamu kama force of gravity lakini baada ya sekunde chache hurudi juu ya maji sababu ya uasili wa mwili kuelea.(boyancy).
kama akitumbukia kwenye maji ya baridi sana atavuta hewa kwa nguvu sababu ya mshtuko wa mwili ambao unatokea.(reflex from skin stimulation).
mtu huyu anaweza kushikilia pumzi kwa dakika chache lakini baada ya muda hewa ya carbondioxide itamzidia mwilini mwake na atajikuta anaanza kupumua na kuvuta maji kwenye mapafu yake.
kadri mtu huyu anavyozidi kulia kuomba msaada na kupambana ndio anavyozidi kuvuta maji mengi zaidi.
anaweza kutapika lakini anavyozidi kupambana ndio anazidi kuzama zaidi kwenye maji.
kuzama na kuibuka kwenye maji huendelea mpaka mtu anapata degedege na kupoteza fahamu ndani ya maji.
mtu akishapoteza fahamu hawezi kujiokoa tena na kifo kitamkuta hapa.
mara nyingi watu hupoteza fahamu kwanzia dakika ya tatu mpaka ya kumi ambapo ubongo hukosa hewa kiasi kwamba hauwez kupona hata mtu akikolewa muda huo.(irrevesible brain damage).

kifo kwenye maji ya yasiyo na chumvi.
maji ya mtoni na ziwani hua na chumvi kidogo kama 0.6% hivi, mtu akifa huvuta maji haya kwa kiasi kikubwa na kupitia mapafu huingia ndani ya damu.
ndani ya dakika moja damu inakua imeshachanganyikana na damu zaidi ya lita mbili na nusu, baada ya dakika tatu maji huzidi zaidi.
hii hufanya moyo kuzidiwa na kushindwa kusukuma kiasi kikubwa cha maji kilichoingia.
hii husababisha moyo kusimama na kuleta kifo.
                                                               


kifo kwenye maji ya chumvi.
kiasi kikubwa cha chumvi iliyoko kwenye maji huingia kwenye damu kupitia mapafu, muhanga hufariki kwa kukosa hewa safi ya oxygen.

nini cha kufanya?
jukumu la kulinda maisha lipo mikononi mwako, kama una shughuli zako ambazo zinakufanya upite kwenye maji hakikisha unamiliki life jacket yako kwenye begi ambayo utaivaa kila siku wakati wa kupita kwenye chombo hicho.
ukitumbukia kwenye maji na life jacket kitakachoweza kukuua na wanyama wa majini au njaa kitu ambacho sio rahisi.
kumbuka ukitumbukia kwenye maji ya baridi kali sana unaweza ukafa kwa sababu ya baridi kama jinsi watu wengi walivyokufa baada ya meli ya TITANIC kuzama.
wengi wao walikua na life jackets lakini bahari ya atlantic kazikazini ni baridi sana kiasi kwamba ukitumbukia unakufa ndani ya dakika 30.

                                                                      STAY ALIVE

                                                   DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                         0769846183/0653095635


                                                       

HUU NDIO UMRI AMBAO NGUVU ZA KIUME ZINAANZA KUPUNGUA KWA MWANAUME.

Tafiti mpya zinaonyesha kwamba kadri umri unavyozidi kwenda mbele lazima kila mwanaume atakutana uso kwa uso na tatizo la kuishiwa nguvu za kiume.
                                                                               

Tafiti hii iliwekwa wazi mwaka 2003 kwenye jarida la issue of Annals of Internal Medicine, ilionyesha kwamba tatizo hili lipo sana kwa watu wazima sana ukilinganisha na umri mdogo na nguvu za kiume hupungua ghafla baada ya miaka 50 na kuendelea kupungua zaidi na zaidi.

kuishiwa nguvu za kiume ni nini?
kuishiwa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kuusimamisha uume wako vizuri na kwa muda mrefu ili kuweza kushiriki tendo la ndoa na kuridhika wewe na mpenzi wako.
mwanzoni madaktari walidhani ni tatizo la kisaikolojia tu na msongo wa mawazo lakini tafiti hizo zinaonyesha kwamba asilimia 90 ya wahannga ni zaidi ya miaka 50.

utafiti ulifanyika wa watu gani?
utafiti huu ulifanyika kwa wataalamu wa afya 31000 wenye umri wa miaka 53 mpaka 90 ambao walijitolea kufanyiwa utafiti huu na waliambiwa waseme nguvu zao za kiume kama ni nzuri, mbaya au mbaya sana.
lakini pia watafiti waliangalia vigezo vingine kama unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara na mazoezi.

majibu ya utafiti yako vipi?
majibu yalionyeshwa kwamba asilimia kubwa ya wanaume zaidi ya miaka 50 walionyesha kupungukiwa nguvu za kiume huku asilimia kidogo sana ya watu wenye umri huu wakionyesha kua na nguvu zao za kiume kama kawaida.
wanaume  wenye umri mkubwa ambao hufanya mazoezi, ambao sio wanene na kutovuta sigara walionekana kupungukiwa na hatari hii kwa asilimia 30.
nchini marekani tu zaidi ya watu milion 20 walionekana kuishiwa nguvu za kiume kitu ambacho hupunguza uwezo wa kujiamini kwa wanaume wengi.

                                                                     STAY ALIVE


 

HUU NDIO UMRI AMBAO MBEGU ZA KIUME ZINAANZA KUPOTEZA UBORA WAKE.

Inafahamika kwamba mwanaume anaweza kuzalisha mwanamke kwa kipindi chote cha maisha yake kwani mwanaume aliyerekodiwa kumpa mwanamke mimba akiwa na umri mkubwa kabisa alikua na miaka 96.                                                    

Lakini linapokuja swala la kubeba mimba salama na kuzaa watoto salama umri wa mwanaume ni muhimu sana kama jinsi umri wa mwanamke ulivyo muhimu, kama una mpango wa kuzaa ni vizuri kuzaa mapema sana ili kuepuka matatizo ambayo yanatokana na umri mkubwa.
baadhi ya magonjwa ya watoto kama kua bubu, magonjwa ya akili na baadhi ya saratani husababishwa na mwanaume kua na umri mkubwa.

ubora wa mbegu unapungua mtu akiwa na miaka mingapi?
Kadri umri unavyozidi kua mkubwa uwezo wa mwanaume kumpa mwanamke mimba unazidi kupungua, mwanaume akifikisha miaka 40 uwezo wa kumpa mwanamke mimba ndio unaanza kupungua rasmi.
kipindi hiki mwanaume humpa mwanamke mimba kwa shida sana na hata akifanikiwa uwezekano wa mimba kuharibika hua mkubwa sana.
sio kwamba wanaume wote wenye umri zaidi ya miaka 40 watapata shida hizi lakini hichi ni kipindi cha bahati nasibu sana hivyo kama una mpango wa kubeba mimba na kuzaa basi hakikisha unafanya maamuzi mapema.

nini cha kufanya?
kuna baadhi ya wanaume huchelewa kuoa kwasababu mbalimbali ambazo zinakua nje ya uwezo wao lakini kumbuka hakuna mahusiano kati ya ndoa na kuzaa kwenye dunia ya sasa.
unaweza kuanza uzazi hata kama huna uwezo wa kugharamia harusi au hauko tayari kwa sasa kuingia kweye majukumu hayo lakini ukafuga ndoa baadae lakini mtoto hasubiri.
lakini pia kama tayari ndio umri sahihi wa kuzaa umeshakutupa mkono na una nia ya kupata watoto basi ni vizuri mimba hiyo ifuatiliwe kwa makini sana huku ikifanyiwa vipimo mbalimbali ili kujua kama mtoto mtarajiwa ana tatizo lolote na kama tatizo likionekana basi hatua ichukuliwe mapema.

                                                                        STAY ALIVE

                                                        DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO\
                                                                     0653095635/0769846183