data:post.body UFAHAMU UGONJWA MWINGINE AMBAO KWA SASA NI HATARI KULIKO UKIMWI.[HEPATITIS B] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

UFAHAMU UGONJWA MWINGINE AMBAO KWA SASA NI HATARI KULIKO UKIMWI.[HEPATITIS B]

hapatitis B ni ugonjwa hatari wa virusi vinavyoshambulia maini ya binadamu, ugonjwa huu ni tatizo la dunia kwani mpaka sasa hivi watu milioni 257 wana ugonjwa huo yaani wengi kuliko milioni 50 ambao wanaishi na virusi vya ukimwi duniani.
                                                           
ugonjwa huu uko sana maeneo ya pacific na africa ambapo watu zaidi ya 6.2% wameathrika na ugonjwa huu,
tafiti za hivi karibuni zinaonyesha jiji la dar es laam pia lina wagonjwa wengi zaidi kuliko hata mikoani kulingana na muingiliano mkubwa wa watu.
mwaka 2015 watu zaidi ya laki nane walikufa kwa ugonjwa hepatitis ambayo mara nyingi husababisha saratani ya maini, makovu ya kwenye maini au maini kushindwa kufanya kazi ghafla.
kuna aina mbili za hepatitis.
acute hepatitis B; hii ni aina ya hepatitis b ambayo humshambulia mtu sio zaidi ya miezi sita.
chronic hepatitis B; ni aina ya hepatits b humshambulia mtu zaidi ya miezi sita.

ugonjwa huu unaambukizwa vipi?
kama ilivyo ukimwi, ugonjwa wa hepatitis b huambukizwa kwa njia ya kushiriki tendo la ndoa, kuchangia vifaa vyenye ncha kali, maambukizi kutokwa kwa mama mpaka kwa mtoto lakini tofauti kidogo na virusi vya ukimwi...virusi vya hepatitis b vina ambukizwa kirahisi sana kuliko virusi vya ukimwi.
tafiti zinaonyesha kwamba watu 1000 wakijichoma na vifaa vyenye ncha kali VYENYE VIRUSI VYA UKIMWI basi 10 wataambukiza na virusi vya ukimwi wakati watu 1000 wakichomwa na ncha kali yenye virusi ya hepatitis B basi  300 wataambukizwa na virusi vya hepatitis b.

dalili za ugonjwa huu zikoje?
mgonjwa huweza kuchukua siku 30 mpaka 180 bila kuonyesha dalili yeyote ile baada ya kupata maambukizi ya virusi vya hepatitis...
                                                               
baadhi wa watu hawana dalili kabisa lakini wengine huanza na dalili ya kua na macho ya njano, mkojo mweusi sana, kuchoka sana, kichefu chefu, maumivu ya tumbo, kutapika sana na kadhalika.
baaadhi ya watu wenye ugonjwa wa hepatitis huweza kupata tatizo la maini kushindwa kufanya kazi na kufariki ndani ya wiki chache baada ya kuugua.
watu wengine hujikuta wameathirika na magonjwa yote mawili yaani virusi vya ukimwi na virusi vya hepatitis kitu ambacho hufanya mgonjwa awe kwemye hatari kubwa zaidi.

jinsi ya kutambua muathirika wa ugonjwa huu.
sasa hivi kuna vipimo vya damu ambavyo vipo kama vile vya ukimwi kitalamu kama antibody test, mgonjwa hupimwa na kupewa majibu yake ndani ya muda mfupi.

matibabu ya ugonjwa wa hepatitis;
matibabu ya hepatitis hutegemea na aina ya hepatitis.
acute hepatitis; hii huweza kupona yenyewe bila matibabu yeyote.
chronic hepatitis; kama ulivyo ugonjwa wa ukimwi, ugonjwa wa chronic hepatitis B hauna  dawa ya kuutibu kabisa, mgonjwa kulingana na hali yake ataanzishiwa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huu na kutumia kwa miaka yote.
ugonjwa hepatitis hushambulia maini zaidi, hivyo wagonjwa wengi watapata saratani ya maini na maini kushidwa kufanya kazi kabisa.
kwa nchi ambazo zimeendelea matibabu kama kubadilisha maini, dawa za saratani  na mionzi yamechangia sana kusogeza siku za wagonjwa mbele na kuishi miaka mingi zaidi.
kwa nchi ambazo ni maskini kama afrika na zingine mgonjwa akishapata kansa ya maini  ambayo mara nyingi hugunduliwa kwenye hatua ya mwisho kabisa hapa aftiaca, hataweza kuishi zaidi ya miezi sita kabla ya kufariki.

jinsi ya kuzia ugonjwa huu
bahati nzuri chanjo ya ugonjwa huu iligunduliwa mwaka 1982 na inaweza kuzuia ugonjwa huu kwa zaidi ya silimia 95%,
kuna changamoto kadhaa za kuipata chanjo hii hapa tanzania sababu ya kua adimu sana na gharama yake kua juu kidogo hasa wa watu wazima lakini ukipata nafasi basi choma chanjo hii.
watoto wadogo chini ya miaka mitano hupata chanjo hii bure kipindi cha mahudhurio ya kliniki.
njia zingine ni kuepuka ngono zembe, kupima kabla ya kupata ujauzito, kuepuka kuchangia vifaa vya ncha kali na kua na mpenzi mmoja aliyepimwa.

                                                              STAY ALIVE

                                 DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0653095635/0769846183

Maoni 2 :

 1. Ahsante sana Dr.Kwa maelezo yako mazuriii.

  Kiukweli umenipa mwanga sana!

  Ninao ugonjwa huu haujaonyesha dalili kabisaaa...

  Niliugundua pale nilipoenda kumtolea mtu damu nikabainika kuwa nina ugonjwa huu kabla hata dalili hazijaonekana.

  Kwa Ushauri wa Daktari amenishauri na kunipa Dawa za Kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi.

  Ambavyo nameza kila siku usiku kabla ya kuingia kulala.

  Na kwa mujibu wa maelezo yako ni kwamba kwenye hatua ya Acute yaani kwa wenye ugonjwa huu kwa chini ya miezi sita..

  Wao wanapona kabisa bila kutumia Dawa yoyote ile.

  Lakini je,mtu anawezaje kufika hatua ya Chronic kama kwa Mwenye hatua ya Acute anapona kabisa bila Dawa yoyote?

  Lakini pia inakuaje kwa ambaye tayari wameanzishiwa Huduma ya Dawa ilihali bado wako kwenye acute?

  JibuFuta
  Majibu
  1. pole sana, ugonjwa huu unaweza kupona bila dawa kabisa, sio vizuri kuanza kutumiadawa bila kuhakikisha ugonjwa upo kwenye hatua gani.

   Futa