data:post.body Desemba 2017 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

LIFAHAMU TATIZO LA KUVUNJIKA UUME NA MATIBABU YAKE[PENILE FRACTURE]

kuvunjika kwa uume ni pale ambapo nyama ngumu au tendoni zinazoshika uume zinachanika kwa nguvu na kuacha uume kama umevunjika.
                                                           
hali hii husababishwa na nguvu nyingi kutumika kwenye uume hasa wakati wa tendo la ndoa pale mwanamke anapokua juu au mwanaume anapojichua kwa nguvu sana.
tatizo hili pia husababisha kuchanika kwa mishipa ya fahamu, mishipa ya damu na hata njia ya mkojo.

dalili za kuvunjika kwa uume..
sauti ya kuvunjika kitu wakati wa tendo la ndoa likiaambatana na maumivu makali, kuvimba kwa uume na uume kulala ghafla ni dalili kuu kwamba uume umevunjika na unahitaji matibabu.

chanzo ni nini?
karibia wagonjwa wote waliofikishwa hospitali walikua wanashiriki tendo la ndoa kabla ya hali hiyo kutokea,
mwanamke anapokua juu ya uume yeye ndio anakua kama kiongozi wa tendo la ndoa na uzito wote wa mwili wake unakua unaishia juu ya uume wa mwanaume husika,  hivyo asipokua makini atajikuta anaukalia vibaya uume na kuuvunja.

vipimo vinavyofanyika..
vipimo vya utrasound na MRI ndio hutumika zaidi kuhakikisha kweli tatizo hili limetokea na kwa kiasi gani tatizo hili limetokea, pia vipimo hivi vitasaidia katika hatua zifuatazo za matibabu.

matibabu yake
upasuaji ndio njia pekee ya kutibu tatizo la kuvunjika kwa uume na mgonjwa huweza kupona kabisa, kutokufanya upasuaji huweza kusababisha maumivu makali wakati wa tendo la ndoa, kuishiwa nguvu za kiume, uume kupinda milele na kadhalika.

                                                         STAY ALIVE

                                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0653095635/0769846183

UFAHAMU UGONJWA MWINGINE AMBAO KWA SASA NI HATARI KULIKO UKIMWI.[HEPATITIS B]

hapatitis B ni ugonjwa hatari wa virusi vinavyoshambulia maini ya binadamu, ugonjwa huu ni tatizo la dunia kwani mpaka sasa hivi watu milioni 257 wana ugonjwa huo yaani wengi kuliko milioni 50 ambao wanaishi na virusi vya ukimwi duniani.
                                                           
ugonjwa huu uko sana maeneo ya pacific na africa ambapo watu zaidi ya 6.2% wameathrika na ugonjwa huu,
tafiti za hivi karibuni zinaonyesha jiji la dar es laam pia lina wagonjwa wengi zaidi kuliko hata mikoani kulingana na muingiliano mkubwa wa watu.
mwaka 2015 watu zaidi ya laki nane walikufa kwa ugonjwa hepatitis ambayo mara nyingi husababisha saratani ya maini, makovu ya kwenye maini au maini kushindwa kufanya kazi ghafla.
kuna aina mbili za hepatitis.
acute hepatitis B; hii ni aina ya hepatitis b ambayo humshambulia mtu sio zaidi ya miezi sita.
chronic hepatitis B; ni aina ya hepatits b humshambulia mtu zaidi ya miezi sita.

ugonjwa huu unaambukizwa vipi?
kama ilivyo ukimwi, ugonjwa wa hepatitis b huambukizwa kwa njia ya kushiriki tendo la ndoa, kuchangia vifaa vyenye ncha kali, maambukizi kutokwa kwa mama mpaka kwa mtoto lakini tofauti kidogo na virusi vya ukimwi...virusi vya hepatitis b vina ambukizwa kirahisi sana kuliko virusi vya ukimwi.
tafiti zinaonyesha kwamba watu 1000 wakijichoma na vifaa vyenye ncha kali VYENYE VIRUSI VYA UKIMWI basi 10 wataambukiza na virusi vya ukimwi wakati watu 1000 wakichomwa na ncha kali yenye virusi ya hepatitis B basi  300 wataambukizwa na virusi vya hepatitis b.

dalili za ugonjwa huu zikoje?
mgonjwa huweza kuchukua siku 30 mpaka 180 bila kuonyesha dalili yeyote ile baada ya kupata maambukizi ya virusi vya hepatitis...
                                                               
baadhi wa watu hawana dalili kabisa lakini wengine huanza na dalili ya kua na macho ya njano, mkojo mweusi sana, kuchoka sana, kichefu chefu, maumivu ya tumbo, kutapika sana na kadhalika.
baaadhi ya watu wenye ugonjwa wa hepatitis huweza kupata tatizo la maini kushindwa kufanya kazi na kufariki ndani ya wiki chache baada ya kuugua.
watu wengine hujikuta wameathirika na magonjwa yote mawili yaani virusi vya ukimwi na virusi vya hepatitis kitu ambacho hufanya mgonjwa awe kwemye hatari kubwa zaidi.

jinsi ya kutambua muathirika wa ugonjwa huu.
sasa hivi kuna vipimo vya damu ambavyo vipo kama vile vya ukimwi kitalamu kama antibody test, mgonjwa hupimwa na kupewa majibu yake ndani ya muda mfupi.

matibabu ya ugonjwa wa hepatitis;
matibabu ya hepatitis hutegemea na aina ya hepatitis.
acute hepatitis; hii huweza kupona yenyewe bila matibabu yeyote.
chronic hepatitis; kama ulivyo ugonjwa wa ukimwi, ugonjwa wa chronic hepatitis B hauna  dawa ya kuutibu kabisa, mgonjwa kulingana na hali yake ataanzishiwa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huu na kutumia kwa miaka yote.
ugonjwa hepatitis hushambulia maini zaidi, hivyo wagonjwa wengi watapata saratani ya maini na maini kushidwa kufanya kazi kabisa.
kwa nchi ambazo zimeendelea matibabu kama kubadilisha maini, dawa za saratani  na mionzi yamechangia sana kusogeza siku za wagonjwa mbele na kuishi miaka mingi zaidi.
kwa nchi ambazo ni maskini kama afrika na zingine mgonjwa akishapata kansa ya maini  ambayo mara nyingi hugunduliwa kwenye hatua ya mwisho kabisa hapa aftiaca, hataweza kuishi zaidi ya miezi sita kabla ya kufariki.

jinsi ya kuzia ugonjwa huu
bahati nzuri chanjo ya ugonjwa huu iligunduliwa mwaka 1982 na inaweza kuzuia ugonjwa huu kwa zaidi ya silimia 95%,
kuna changamoto kadhaa za kuipata chanjo hii hapa tanzania sababu ya kua adimu sana na gharama yake kua juu kidogo hasa wa watu wazima lakini ukipata nafasi basi choma chanjo hii.
watoto wadogo chini ya miaka mitano hupata chanjo hii bure kipindi cha mahudhurio ya kliniki.
njia zingine ni kuepuka ngono zembe, kupima kabla ya kupata ujauzito, kuepuka kuchangia vifaa vya ncha kali na kua na mpenzi mmoja aliyepimwa.

                                                              STAY ALIVE

                                 DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                   0653095635/0769846183

HIZI NDIZO SUMU 10 KALI ZAIDI ZINAZOTUMIKA KUUA DUNIANI.

tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia, binadamu wamekua wakitafuta njia mbalimbali za kuua watu au wamekuwa wakiuawa bila kujua kwa sumu mbalimbali.
lakini wataalamu wamefanya tafiti na kugundua sumu ambzo ni kali sana na huweza kufanya maangamizi ya kutisha kwa taifa zima au mtu mmoja mmoja.
mashirika ya kijasusi yamekua yakitumia sumu hizi kuwaua watu ambao ni hatari kwa maslahi yao fulani.
                                                                           
                                                           
sumu nyingi ni hatari sana na hata mtumiaji anayetaka kuua asipokua makini na yeye anaweza kujikuta anauawa na sumu hizo.
hebu tuangalie list hii ya sumu za kutisha zaidi duniani.
10.arsenic 
hii ni sumu inayopatikana nyumbani kwani huchanganywa kwenye rangi za kupaka ukutani au picha za ukutani, ikitokea mtu amekula au kuguswa na sumu hii dalili za kwanza ni kuota vipele na kua na macho ya njano, kiasi kikiwa kikubwa mtu huumwa tumbo kutapika. baadae hupoteza fahamu degedege na kufariki.
9. mustard gas
sumu hii inayokua na harufu ya kitunguu swaumu, ilitumika vitani kuwaua askari kipindi cha vita ya kwanza ya dunia, ikiwa na rangi ya njano moshi wa sumu hii huchoma moto kila kitu ambacho hukutana nacho, huunguza sehemu mbalimbali za mwili na hata ikikupata kidogo basi kuna hatari kubwa ya kuugua ugonjwa saratani baadae.
8.cyanide; hii ni sumu maarufu sana tangu kipindi cha vita ya kwanza na pili ya dunia, ikiwa kwenye mfumo wa vidonge hupendwa kubebwa sana na askari wa kijajusi kuua watu fulani fulani, sumu hii huua haraka sana ndani ya dakika moja au mbili kwa kuzuia mfumo wa upumuaji na kumuacha mtu akitapatapa kwa kukosa hewa. wakati wa vita ya pili ya dunia dikteta Adrof Hittler aliitumia kuwaua sana waisrael kwa sumu hii.
7.strychinine; hii ni sumu inayopatikana kwenye mmea wa dog button plant, mmea huu unatoa sumu kali ambayo hufanya misuli yote ya mwili wa binadamu kukakamaa sana na kufa baada ya masaa mwawili mpka matatu. baadhi yawatu hutumia sumu hii kuua panya.
                                                   
6.ricin; hii ni aina ya sumu inayobatikana kwenye aina ya maharage yanayoitwa castrol beans, sumu yenye ukubwa wa punje moja ya chumvi huweza kumuua mtu mzima hapo hapo. sumu hii haiwezi kuua kwa kula ila kwa kunusa au kuchomwa kama sindano.
sumu hii hufanya kazi kwa kuzuia mfumo wa seli kutengeneza protini mwilini na ulaji wa punje hizo tano tu za maharage ambayo sumu hiyo hupatikana unaweza kumuua mtu.
5.sarin; hii ni sumu ambayo inapatikana kwenye kikundi cha dawa za organophosphate yaani kama zile zinazotumika mashambani kuua wadudu kwenye mimea.
sumu hii ni kali sana na hufanya kazi kwa kuzuia ufanyaji kazi wa mishipa ya fahamu.
mgonjwa hupata dalili kama kutoka mate mengi, kukojoa sana na kutapika sana na baadae hupata degedege, kupoteza fahamu na kufa.
4.vx; sumu hii iligunduliwa na waingereza, inatengenezwa maabara moja kwa moja wala sio sumu inyopatikana kwenye mimea au wanyama.
sumu hii hushambulia mishipa ya fahamu na kumuua mtu ndani ya muda mfupi hasa kwa kushindwa kupumua.
mwaka 1993 ilipigwa marufuku ikiwa tayari imehifadhiwa vya kutosha na wamerekani na urusi hivyo ilibidi imwagwe yote.
3.batrachotoxin; hii ni aina ya sumu inayopatikana kwenye aina fulani ya chura ambao wana rangi ya dhahabu, sumu ya chura huyu hutumika na wawindaji huko india kwa kuwekwa kwenye mishale yao wakati wa kuwinda.
chura mdogo tu anayelingana na kidole gumba chako ana uwezo wa kuua watu kumi.
2.polonium; hii ni sumu kali sana ambayo iko kwenye mfumo wa kemikali za mionzi kitaalamu kama radiaoctive substances.
gram moja ya polinium ina uwezo wa kuuwa watu milioni kumi, sumu hii haiwezi kupita kwnye ngozi lakini ikinuswa au kuliwa basi ina uwezo wa kufanya uharibifu mkubwa kwenye mifumo ya mwili ya mwanadamu, na kama ukibahatika kupona basi itakuacha na kansa baada ya muda fulani
sumu huu inasemekana kumuua kiongoizi wa wapelestina maarufu kama yYesser alafati.
                                                               
1.botulinum toxin; hii ni sumu kali zaidi ambayo haijawahi kutokea duniani, sumu hii hutengenezwa na bacteria kwa jina la clostridium butoni...
inakadiriwa kwamba kijiko kimoja kinaweza kuua watu bilioni moja kwa mpigo yaani mara mbili ya wachina wote wanaoishi duniani.
sumu huu imeua watu wengi duniani sana hasa kwa kula vyakula ambavyo vimeingiliwa na bacteria ha wa na bahati mbaya au kwa kuwekewa na watu makusudi.
majasusi wanadai kwamba kipindi cha utawala wa Sadamu Hussein alimiliki sumu ya kuweza kuua mara tatu ya watu wote duniani.

                                                                   STAY ALIVE





YAFAHAMU MADHARA 4 YA KUTISHA YA KUSAFISHA UKE.[douching]

asilimia 20% mpaka 40%  ya wanawake duniani wenye umri kati ya miaka 15 mpaka 44 kwa sasa wanajisafisha sehemu za za siri wakidai kwamba wanaondoa harufu sehemu za siri, wanajizuia na magonjwa ya zinaa, wanaondoa damu ya hedhi baada ya hedhi kuisha, na kuzuia mimba baada ya ngono.                                                                       
                                                       
wataalamu wa afya wanalipinga hili na kusema kwamba hakuna ushahidi kwamba kusafisha sehemu za siri kuna faida hizo na kuonya kwamba sehemu za siri za mwanamke hazitakiwi kuguswa kabisa, hata wakati wa kuoga haitakiwi kuingiza vidole huko ndani kwani sehemu hizo zina mfumo maalumu wa kujisafisha wenyewe.
nani ameshawahi kuingiza vidole ndani ya sehemu za haja kubwa kujisafisha? mbona hakutoi harufu? basi sehemu za uke pia hazitakiwi kuguswa.

douching ni nini?
hii ni njia ya kusafisha uke kwa kutumia maji na vinegar au maji tu, nchi zilizoendelea kuna mafuta maalumu kabisa kwa ajili ya kazi hiyo,
wanawake waliohojiwa walidai kwamba hujisikia safi na salama kwa kusafisha sehemu zao za siri.

tafiti zinasemaje? 
kitaalamu uke hautakiwi kusafishwa kabisa kwani unajisafisha wenyewe na hata wakati wa kuoga ni marufuku kuingiza hata vidole ndani ya uke na kusafisha na maji kwani kuna usumbufu unaoletwa huko ndani na vidole ambao unaweza kukuletea matatizo makubwa mno.
yafuatayo ni madhara ya kujisafisha kwa vidole
magonjwa ya uke; ndani ya uke kuna bacteria maalumu na hali ya hewa maalumu ambayo kazi yake ni kupambana na magonjwa yanayoshambulia uke, hivyo kuosha uke husababisha kufa kwa bacteria hao walinzi..magonjwa ya fangas za uke mara kwa mara kwa wanawake wanao osha sehemu za siri ni kawaida sana.
magonjwa ya mifuko ya uzazi; haya ni magonjwa ambayo hushambulia mirija ya uzazi, kizazi na mayai ya mwanamke...wanawake wanao osha sehemu zao za siri wana nafasi kubwa sana ya kupata magonjwa haya sababu ya kuingiza bacteria wengine wakati wa kazi hii, hii  ni moja ya vyanzo vikuu vya ugumba kwa wanawake wengi sana duniani.
mimba kutunga nje ya kizazi; wanawake wanaojisafisha sana uke hupata shida sana kupata watoto sababu mazingira ya nyeti zao hayasaidii safari ya mbegu za kiume kuelekea kwenye kizazi hivyo hata ikitokea wakapata mimba basi mimba hiyo huenda nje ya kizazi.
saratani ya mlango wa uzazi; kusafisha uke mara kwa mara kumehusishwa sana na kuongezeka kwa uwezekano wa wa kupata saratani ya mlango wa uzazi kwa asilimia kubwa ukilinganisha na wale ambao hawafanyi hivyo.
mwisho; kwa hali ya kawaida uke hua una harufu yake japokua haitakiwi iwe kali sana, hivyo usitumie njia yeyote kusafisha uke wako kwani hua unajisafisha wenyewe na hata wakati wa kuoga usiingize hata vidole ukeni na kuingiza maji kwa madai eti unasafisha.
madhara yake ni makubwa na huweza kukunyima mtoto baadae.

                                                                   STAY ALIVE

                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO