data:post.body FAHAMU CHANZO, DALILI NA MATIBABU YA MTOTO ALIYEFIA TUMBONI. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

FAHAMU CHANZO, DALILI NA MATIBABU YA MTOTO ALIYEFIA TUMBONI.

kufia tumboni kwa mtoto nini?
huhesabika pale mtoto anapofia tumboni wiki ya 20 mpaka 28, kabla ya wiki ya 20 huitwa mimba kuharibika.
                                                   
kufia kwa mtoto tumboni hua kuna madhara makubwa sana ya kisaikolojia hasa kwa mama ambaye anatarajia kupata mtoto na ameshajiandaa, baada ya hali hii mama anahitaji kukaa na mshauri wa afya ili aweze kupata ushauri wa kutosha kuondoa maumivu yake makali ya kihisia.

chanzo ni nini?
mara nyingi chanzo cha mtoto kufia tumboni hakifahamiki lakini vitu kama kifafa cha mimba, mtoto mwenye matatizo ya kimaumbile, matatizo ya kondo la nyuma, ajari, ugonjwa wa malaria na kaswende , kupewa sumu, kutumia dawa za kuua mtoto kwa makusudi, tofauti ya makundi ya damu kati ya mama na mtoto  huchangia sana na lakini pia mtoto huweza kufia tumboni ghafla tu bila kujua hata chanzo.

watu gani wako kwenye hatari ya kupata shida kama hizi?
watu wanaobeba mimba za kwanza
umri kwanzia miaka 35 kwenda mbele
matumizi ya madawa kipindi cha ujauzito
wagonjwa wa presha na kisukari
wanywaji wa pombe na wavuta sigara
magonjwa ya utumbo
mimba kupitiliza siku zake za matarajio

utajuaje kama mtoto wako amefia tumboni?
dalili ya kwanza kabisa na kuu ni pale mtoto anapoacha kucheza ghafla tumboni, hii hutokea pale mtoto ambaye siku zote alikua bize anaruka ruka lakini ghafla ameacha.

vipimo gani hufanyika?
picha ya utrasound hupigwa kuhakikisha kama kweli mtoto amefia tumboni, daktari mara nyingi huangalia mapigo ya moyo ya mtoto na akiona moyo wa mtoto umesimama anahakikisha kwamba ni kweli kifo cha mtoto kimetokea.
kabla ya hapo wakunga hutumia kifaa kwa jina la featoscope kusikiliza mapigo ya moyo na kama hawayasikii watamshauri mama kwenda kupiga picha kuhakikisha.
                                                                             
                                                         
matibabu ya mtoto aliyefia tumboni
hakuna madhara anayopata mama kama mtoto akifia tumboni, baada ya wiki mbili uchungu utaanza wenyewe na mama atamzaa mtoto huyo mfu, lakini kama baada ya wili mbili uchungu haujaanza ataanzishiwa dawa za uchungu kwani mama anaweza kupata mdhara kama kuganda kwa damu yake.
wakati mwingine mama huchagua kupewa dawa ya uchungu hapo hapo kwani inaumiza sana kihisia kuendelea kusubiri wakati ukiwa na mtoto mfu tumboni.
upasuaji hufanyika pale mtoto anaposhindwa kuzaliwa kwa njia ya kawaida lakini madaktari hujitahidi sana kuhakikisha mtoto anatoka kwa njia ya kawaida kwani inauma sana kubaki na makovu ya mtoto mfu.

                                                              STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                               0653095635/0769846183     

Maoni 6 :

 1. Ata mm nilijisikia vibaya 4/9/2019 baada mke wangu kuambiwa ana tatizo ilo ila alijifungua kwa njia salama na dactar alisema mama yuko vizuri

  JibuFuta
 2. Mtoto akifia tumboni akiwa na wiki4 utajuaje na kama hamna damu inayotoka

  JibuFuta
 3. Nashukuru mialifia tumboni miez 8

  JibuFuta
 4. Ila ametolewa leo ni mwezi Sasa ila inaniumašŸ˜­ namuomba mungu azidi kunipa nguvu

  JibuFuta
 5. Je mtoto akifia tumbon ukijifungua unahitaji kisafishwa? Maana mimi mwanangu alipo fia tumbon hawakunijali nilijifungua mwenyew kitandani ila baada ya pale nilifutwa na kupew vidonge tu ila mpaka leo sikubahatika tena lakin mzunguko uko vizur na sijatumia dawa yoyote ya kukinga mimba lakin damu ya hedhi inatoka katk hali ya mabonge naomba ushaur nimezunguka hospital wana sema nipo sawa nitapata mimba

  JibuFuta