data:post.body Novemba 2017 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

ZIFAHAMU NJIA 7 ZA UZAZI WA MPANGO AMBAZO HAZINENEPESHI NA SALAMA.

karne ya 20 kidonge cha kwanza kwa ajili ya kuzuia mimba kiligunduliwa hapa duniani, hii ilikua moja ya mapinduzi makubwa kabisa kwenye sekta ya afya kwani wanawake walikua wanakumbwa sana na tatizo la kubeba mimba bila kutarajia, kuzaa watoto wengi, vifo kwa kujaribu kutoa mimba na kadhalika.
baadae kwa kupitia kidonge hicho njia zingine ambazo zinafanana na kidonge hicho yaani zinatumia homoni kufanya kazi kama sindano, vijiti, dawa za kumeza baada ya tendo ziligundulika pia.
lakini pamoja na faida ambazo zilipatikana, changamoto nyingi sana zimekua zikiambata na dawa hizo ikiwemo mdhara madogo madogo kama kichefuchefu, kutokwa damu nyingi sana, kutokwa na damu kila siku na kushindwa kufurahia tendo la ndoa,  na kadhalika pia madhara makubwa makubwa kama kunenepa sana na kua kwenye hatari ya magonjwa kama kisukari na presha, kuganda kwa damu hali ambayo ni hatari sana na hatari ya kupata saratani mbalimbali za mwili.
kwa kuliona hilo leo nimekuja na njia zingine ambazo unaweza kuzitumia kuzuia mimba ambazo hazina kemikali za homoni ambazo kimsingi ni hatari kwa bainadamu kama ifuatavyo.
                                                                     
njia ya kitanzi; hii ni njia ambayo kifaa kidogo huingizwa ukeni na kuzuia mbegu za mwanaume kukutana na mayai ya mama, kitanzi hichi hakina kemikali za homoni na huweza kukaa hapo hata miaka kumi, kitanzi hichi hakinenepeshi, hakina hatari ya kansa..baadhi ya vitanzi vina homoni hivyo ni vizuri ukienda hospitali useme nataka kitanzi cha copper ambacho hakina vichocheo vya homoni.
kwa mara ya kwanza kikiwekwa damu huweza kutoka nyingi sana lakini baadae huacha, kitaalamu ni njia salama sana kiafya kuliko kijiti, vidonge na sindano ambavyo vina kemikali nyingi za homoni.
dawa za kuua mbegu; hizi ni dawa ambazo kazi yake ni kuua mbegu za mwanaume wakati anapomwaga ndani, hufanya kazi vizuri sana na hazina madhara ya kimwili kama nilivyotaja hapo juu..huuzwa kama cream, au vidonge ambavyo hupachikwa muda mchache kabla ya tendo la ndoa.     mfuniko wa mfuko wa uzazi; huu ni mfuniko ambao unatumika kufunika sehemu ya mlango wa uzazi ili mbegu zisipite, ni moja ya njia salama sana na huzuia mimba kwa kiasi kikubwa sana, changamoto ni kwamba unahitaji kujifunza vizuri jinsi ya kutumia kwani ukiweka vibaya njia hii inaweza kushindwa,
njia ya calenda; hii ni moja ya njia salama sana ya kuzuia mimba, watu wengi hawajui jinsi ya kuitumia sio kwasababu ni ngumu hapana, ila watu wengi hua hawako serious linapokuja swala hili na wengine hujikuta wamefanya ngono zembe baada ya kulewa au kushawishiwa sana wakiwa kwenye siku za hatari.
matumizi ya kondomu; japokua watu wengi hawependi kuzitumia kwa madai hazina ladha lakini kama una nidhamu ya maisha ni moja ya njia bora sana ya kuzuia mimba na magonjwa ya zinaa ikiwemo ukimwi.
kwa kijana ambaye hujaoa au kuolewa hata kama una mpenzi ni vizuri kujizoesha kutumia hizi kinga kwani uaminifu siku hizi ni mdogo sana na watu wengi wana wapenzi tofauti tofauti.
kuna kondom nzuri ambazo laini sana kiasi kwamba ukivaa unaweza kuhisi hujavaa kitu mfano rough riders.
unaweza kuona kwamba kutumia kondomu ni mzigo lakini kama huna ukimwi unatakiwa utumie kondom kuzuia ukimwi, ukishapata ukimwi unatakiwa uvae kondomu kuzuia maambukizi mapya hivyo ni bora kuzivaa mapema.
kukata mirija ya uzazi; mirija ya uzazi hasa kwa wale wanawake na wanaume ambao tayari wana watoto wakubwa na hawategemei kuzaa kwa namna yeyeote ile hakuna haja ya kuendelea kuteseka na vidonge au kemikali mbali mbali, cha msingi ongea na daktari na huduma hii ya kukata mirija hiyo hufanika bure kwa jinsia zote.
kumwaga mbegu nje; hii ni moja ya njia bora sana kama wewe na mpenzi wako mkielewana, nawafahamu watu waliotumia njia hii kwa muda mrefu sana na mafanikio makubwa sana, kikubwa ni nidhamu tu na kuhakikisha mwanaume unachomoa uume kwa wakati muafaka.

                                                                       
                                                                    STAY ALIVE
                                                                           

FAHAMU JINSI MWANAMKE ANAVYOWEZA KUBEBA MIMBA YA MAPACHA WA WANAUME WAWILI TOFAUTI.

katika hali ya kawaida mwanamke anatakiwa kubeba mimba ya baba mmoja, haijalishi kama anazaa mapacha au mtoto mmoja..
hii ni kwasababu kila mwezi yai moja pekee la mama ndio linashuka kutoka kwenye mirija ya uzazi na kurutubishwa na mbegu za kiume  ili mtoto apatikane.
huko new jersey nchini marekani kesi ilifika mahakamani baada ya kuonekana kwamba watoto wawili mapacha waliozaliwa sio wa baba mmoja na mahakama iliamua kwamba kila mtoto ahudumiwe na baba yake ilimkuepusha usumbufu ambao ulikua umeanza kujitokeza.
vipimo vya DNA vilivyopimwa vilionyesha kwamba watoto wale ni wa baba tofauti na mama yao alikiri kua na mahusiano na mwanaume mwingine.

hali hii inatokea vipi?
hali hii kitaalamu inaitwa heteroparental superfecundation, ni hali ambayo sio ya kawaida ambayo mwanamke anatoa mayai mawili kwenye siku yake ya hatari na kisha kulala na wanaume wawili tofauti siku hiyo hiyo, matokeo yake ni kwamba  yai la kwanza linashuka na kurutubishwa na mbegu za mwanaume wa kwanza  kisha la pili linashuka na kurutubishwa na mbegu za mwanaume wa pili pia.
kitaalamu baada ya yai moja kurutubishwa taarifa inatakiwa itumwe ili yai lingine lisishuke lakini kutokana na mawasiliano ya kimwili kua mabovu yai lingine pia hushuka.

nini hutokea baada ya hapo?
mayai mawili yakisharutubishwa yatakua kwenye mifuko miwili tofauti ndani ya mfuko wa uzazi na kutoa mapacha wawili wasiofanana, kwa hali ya kawaida usipokua makini unaweza ukahisi ni kawaida tu lakini vipimo vikifanyika vya DNA vitaonyesha kwamba mapacha hao ni wa baba wawili tofauti.
                                                                         
                                                                            STAY ALIVE

HIZI NDIO NJIA TANO ZA KUTAMBUA NYAMA ILIYOHARIBIKA BUCHANI.

katika nchi zetu za afrika swala la utunzaji wa nyama hua haliko katika ubora wa 100% kutokana na wauzaji wenyewe kutokua waaminifu pamoja na mazingira ya kuchinja mifugo hiyo.
wakati mwingine nyama inaweza kukaa buchani muda mrefu na kuanza kuharibika lakini wauzaji wataendelea kuuza hivyohivyo bila kujali afya za walaji.
                                                         
kwa nchi zilizoendelea hitu kama hivi havipo labda nyama iharibike mikononi mwa mlaji baada ya kukaa nayo nyumbani kwa muda mrefu.
ulaji wa nyama iliyoharibika ni hatari sana kwani huweza kusababisha magonjwa hatari ambayo yanaweza kukuua ndani ya muda mfupi kitaalamu kama food poisoning.
ukiwa kama mtumizi wa nyama ni vizuri kuzingatia yafuatayo ukienda buchani kununua au kabla ya kupika nyama yako ya nyumbani ambayo ulikua umeihifadhi.
rangi ya nyama; katika hali ya kawaida nyama iliyo salama ina rangi ya papo na ikipata hewa ya oxygen inakua nyekundu kabisa, hivyo ukienda buchani ukakuta nyama ina rangi ya kijivu, ukijani kwa mbali au brown basi ujue nyama hiyo imeanza kuharibika na haifai kwa matumizi ya binadamu.
                         
harufu ya nyama; sisi wote tunafahamu harufu ya nyama ambayo imetoka kuchinjwa hapo hapo na ndio harufu unatakiwa uipate muda wote unapoenda kununua nyama, ukisikia harufu ya tofauti ujue nyama hiyo imeharibika na mara nyingi nyama huanza kua na harufu kama ya samaki.
                                                           
iguse nyama; nyama ambayo ni salama hua ni ngumu ukiigusa lakini nyama ikisha haribika inaanza kunata na ukiigusa inaanza kuacha matundu... hii ni dalili kwamba bacteria hameanza kuzaliana kwenye nyama hiyo na huweza kuleta shida iwapo ikiliwa.
                                                                     
iweke nje ya friji; kama nyama ilikua na rangi ya kijivu ndani ya friji ukiiweka pembeni baada ya dakika kumi na tano inatakiwa ianza kubadilika rangi na kua nyekundu, kama haibadiliki rangi ujue imekwisha haribika.
angalia tarehe ya matumizi; baadhi ya watu wananunua nyama supermarket zikiwa zimefungwa tayari, hakikisha unaangalia ilihifadhiwa lini na inatakiwa itumike mwisho lini.
mwisho; ukigundua nyama imeharibika kwa namna yeyote ili usikate kipande kilichoharibika na kukitupa bali tuma nyama yote na ukanunue nyingine.
kuwa makini ili uweze kuitunza familia yako na jamaa zako.
                                                 
                                                                     STAY ALIVE

                                                          kalegamyehinyuye@gmail.com
                                                              0653095635/0769846183

FAHAMU CHANZO, DALILI NA MATIBABU YA MTOTO ALIYEFIA TUMBONI.

kufia tumboni kwa mtoto nini?
huhesabika pale mtoto anapofia tumboni wiki ya 20 mpaka 28, kabla ya wiki ya 20 huitwa mimba kuharibika.
                                                   
kufia kwa mtoto tumboni hua kuna madhara makubwa sana ya kisaikolojia hasa kwa mama ambaye anatarajia kupata mtoto na ameshajiandaa, baada ya hali hii mama anahitaji kukaa na mshauri wa afya ili aweze kupata ushauri wa kutosha kuondoa maumivu yake makali ya kihisia.

chanzo ni nini?
mara nyingi chanzo cha mtoto kufia tumboni hakifahamiki lakini vitu kama kifafa cha mimba, mtoto mwenye matatizo ya kimaumbile, matatizo ya kondo la nyuma, ajari, ugonjwa wa malaria na kaswende , kupewa sumu, kutumia dawa za kuua mtoto kwa makusudi, tofauti ya makundi ya damu kati ya mama na mtoto  huchangia sana na lakini pia mtoto huweza kufia tumboni ghafla tu bila kujua hata chanzo.

watu gani wako kwenye hatari ya kupata shida kama hizi?
watu wanaobeba mimba za kwanza
umri kwanzia miaka 35 kwenda mbele
matumizi ya madawa kipindi cha ujauzito
wagonjwa wa presha na kisukari
wanywaji wa pombe na wavuta sigara
magonjwa ya utumbo
mimba kupitiliza siku zake za matarajio

utajuaje kama mtoto wako amefia tumboni?
dalili ya kwanza kabisa na kuu ni pale mtoto anapoacha kucheza ghafla tumboni, hii hutokea pale mtoto ambaye siku zote alikua bize anaruka ruka lakini ghafla ameacha.

vipimo gani hufanyika?
picha ya utrasound hupigwa kuhakikisha kama kweli mtoto amefia tumboni, daktari mara nyingi huangalia mapigo ya moyo ya mtoto na akiona moyo wa mtoto umesimama anahakikisha kwamba ni kweli kifo cha mtoto kimetokea.
kabla ya hapo wakunga hutumia kifaa kwa jina la featoscope kusikiliza mapigo ya moyo na kama hawayasikii watamshauri mama kwenda kupiga picha kuhakikisha.
                                                                             
                                                         
matibabu ya mtoto aliyefia tumboni
hakuna madhara anayopata mama kama mtoto akifia tumboni, baada ya wiki mbili uchungu utaanza wenyewe na mama atamzaa mtoto huyo mfu, lakini kama baada ya wili mbili uchungu haujaanza ataanzishiwa dawa za uchungu kwani mama anaweza kupata mdhara kama kuganda kwa damu yake.
wakati mwingine mama huchagua kupewa dawa ya uchungu hapo hapo kwani inaumiza sana kihisia kuendelea kusubiri wakati ukiwa na mtoto mfu tumboni.
upasuaji hufanyika pale mtoto anaposhindwa kuzaliwa kwa njia ya kawaida lakini madaktari hujitahidi sana kuhakikisha mtoto anatoka kwa njia ya kawaida kwani inauma sana kubaki na makovu ya mtoto mfu.

                                                              STAY ALIVE

                                     DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                               0653095635/0769846183     

HAYA NDIO MADHARA 9 YA KUVAA VIATU VIREFU.

viatu virefu ni mtindo mpya au fashion kwa wadada wengi wa siku hizi wanaopenda mambo ya urembo, lakini pia hupendelewa sana na wasichana wafupi ili nao waonekane warefu.
                                                         

kuna madhara mengi yatokanayo na uvaaji wa viatu hivi virefu na usipokua makini unaweza kudhani labda ni magonjwa mengine tu yanakuandama kumbe mchawi wako ni viatu vyako mwenyewe. hebu tuyaone madhara hayo kwa kirefu.
maumivu ya mgongo; katika hali ya kutembea na viatu virefu sana mtumiaji hukosa balance yaani uzito wa mwili wake unashindwa kubalance kati ya upande wa kushoto na kulia wa mwili wake hivyo hupata maumivu makali sana ya mgongo na kuhisi dalili za kutoneshwa akiguswa hasa sehemu za mgongo wa chini.
ugumba; kama nilivyosema kwenye pointi ya kwanza kukosa kwa balance ya mwili husababisha kupotea balance ya kwenye nyonga pia, hali hii hufanya mfuko wa uzazi kukaa vibaya na kua katika sehemu ambayo sio sahihi. hali hii huweza kumnyima mama mtoto na huambatana na dalili kama maumivu wakati wa tendo la ndoa, kushindwa kuzuia mkojo, na kushindwa kubeba mimba.
                                                                   
maumivu ya misuli ya nyuma ya miguu; viatu virefu huleta maumivu makali ya nyama za nyuma ya mguu litaalamu kama calf muscles na ukiwachunguza vizuri watu wengi wanaovaa viatu hivyo hawawezi kusimama kwa muda mrefu yaani wataomba kiti wakae kila sehemu sababu ya maumivu makali, lakini pia mishipa huchomoza kwenye mishipa hiyo na kuleta maumivu inapoguswa.
                                         
kubadilika kwa muonekano wa vidole; kutokana na kidole gumba kushindwa kuhimili mgandamizo unaopata kutoka kwenye mwili mzima, kidole hicho hujikuta kinapinda na kuleta shepu ambayo sio ya kawaida, hii sio nzuri sana kwa urembo na huweza kuleta maumivu.
                                                   
mishipa ya damu kukunjika; mguu unaovishwa kiatu kirefu mara nyingi hujilazimisha kuingia kwenye kiatu kirefu na chembamba hii hufanya mishipa ya damu kujikunja sana na kua midogo sana na katika hali mbaya sana mishipa ya damu huweza kukatika.
maumivu ya joint ya mguu; presha kubwa kwenye joint ya mguu kitaalamu kama knee joint husababisha maumivu makali  ya joint hiyo na kua kama chanzo cha ugonjwa wa kuvimba na kuumwa joint kitaalamu kama osteoarthritis.

kupinda kwa mgongo; kukosa kwa balance ya mwili wakati wa kutembea humfanya mtu kijaribu kupinda kidogo ili kupata balance, baada ya muda mrefu mgongo huanza kuzoea hali ile na kuleta maumivu makali yakiambatana na kupinda kwa eneo la juu na enoe la chini la mgongo.
 kuvunjika mifupa; baadhi ya watu wamewahi kupata ajali kwa kushindwa kuvihimili viatu virefu na kuanguka navyo, baadhi yao waliweza kuvunjika mifupa ya kisigino au mifupa ya vidole kama picha hapo chini inavyoonyesha.

maumivu ya unyayo; katika matembezi ya kutumia viatu virefu kwa muda mrefu mgonjwa husikia maumivu makali ya kisigino, unyayo kwa chini na vidole kwa mbele, hii huweza kumnyima raha na kupunguza ufanisi wa shughuli zake za kila siku.
 
                                                          STAY ALIVE