data:post.body UFAHAMU UGONJWA WA KUZIBA SIKIO NA MATIBABU YAKE.[CERUMEN IMPACTION] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

UFAHAMU UGONJWA WA KUZIBA SIKIO NA MATIBABU YAKE.[CERUMEN IMPACTION]

katika hali ya kawaida sikio la binadamu hutengeneza utando unaovutika kama asali, utando huu huzuia uchafu kuingia ndani ya sikio, kulainisha sikio na kukamata wadudu wanaoingia ndani ya sikio..utando huu hutengenezwa kwa kiasi kidogo sana kwa siku ili kukizi mahitaji ya sikio kwa siku lakini katika hali isiyo ya kawaida utando huu unaweza kua mwingi sana na kuziba sikio na kumfanya mtu ashidwe kusikia vizuri.
                                                         
sio hivyo tu kuna sababu zingine mbalimbali ambazo zinaweza kuziba sikio la mtu na kulifanya lishindwe kusikia kama ifuatavyo..

  • matumizi ya vitu vya kuchokonoa sikio kama viberiti, kalama au pamba za masikioni.
  • kuziba kwa nywele ambazo hupatikana ndani ya sikio.
  • kuishi sehemu yenye vumbi sana
  • matatizo ya mirija ya masikio kitaalamu kama auditory canal
dalili za kuziba kwa sikio
  • maumivu makali sikioni
  • kushindwa kusikia
  • kuwashwa sikioni
  • kusikia kama sauti za kengere sikioni.
  • kizunguzungu
vipimo vipi hufanyika?
kwa kifaa maalumu kwa jina la otoscope daktari ataweza kuchunguza sikio na kuona kitu kilichoziba na kuweka mpango wa kukiondoa.
                                                     
 matibabu
dawa ya sodium carbonate au mafuta huanza kutumika na mgonjwa kwa kuweka matone mawili kwenye sikio husika kwa siku tatu mpaka tano ili kulainisha uchafu ulioganda sikioni kisha mgonjwa hutolewa uchafu huo kwa bomba maalumu hospitali.
angalizo; sikio kwa ndani ni laini sana, ukipata shida ya sikio usilete ujanja wowote wa kujitibu mwenyewe kwani unaweza kuitoboa kabisa ngoma ya sikio, kumbuka hata pamba maalumu zinazouzwa kwa jaili ya masikio hazikubaliki kitaalamu na ni moja ya vyanzo vya kuziba masikio.

                                                                             STAY ALIVE

0 maoni:

Chapisha Maoni